Apostle Victor Herbert

Apostle Victor Herbert Welcome to Apostle Victor H Page ,Founder of The Miracle church of God Ministry, found in Mbezi beach Dar es salaam Tanzania. Prayer line +255784814200

05/03/2024

Apostle Victor Herbert unaalifiwa Kuwasiliana Na Ndugu Prophet Dr. Richard Godwin Magenge Kwa haraka Sana Kuhusu Ukurasa Wako Huu Wa Wa Facebook
+255620285763

16/01/2019

NENO :

ZAKARIA 8:5-8

Na hizo njia za mji zitajaa wavulana, na wasichana, wakicheza katika njia zake.

BWANA wa majeshi asema hivi, Ingawa hili ni neno lililo gumu mbele ya macho ya mabaki ya watu hawa katika siku hizo, je! Liwe neno gumu mbele ya macho yangu? Asema BWANA wa majeshi.

BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaokoa watu wangu toka nchi ya mashariki, na toka nchi ya magharibi;

nami nitawaleta, nao watakaa katikati ya Yerusalemu; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, katika kweli na katika haki.

Apostle Victor H

17/08/2018
Ni jambo gani unataka  mwaka 2018 Mungu akutendee?Kumbuka Musa alipanda Mlimani kutafuta uso  wa Mungu tena siku 40!Je W...
22/12/2017

Ni jambo gani unataka mwaka 2018 Mungu akutendee?

Kumbuka Musa alipanda Mlimani kutafuta uso wa Mungu tena siku 40!

Je Wewe unashindwa kuutafuta uso wa Mungu wako usiku huu ili unacho kihitaji mwaka 2018 akujibu?

Leo ni wakati wako mhimu kufanya Maombi maalumu kwa Bwana na hakika mwaka kesho utakuwa wa kwanza kushuhudia matendo ma kubwa ya Mungu aliyo kutendea.

Nina ona mtu mmoja Leo atakaye tii neno hili la kinabii kila kicho kuwa kime kufa katika maisha yako Bwana anasema kina kwenda kuzaa ,huu ni mwaka wa wewe kuongezeka yani kuzaa yawezekana katika biashara,ndoa,kazi,Huduma yako,au katika elimu yako.
Pokea katika jina la Yesu Kristo.

Yohana 15:16

16 Hamkunichagua, bali mimi nimewachagua ninyi na nimewatuma mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu, ili lo lote mtakalomwomba Baba katika jina langu, awatimizie.

Apostle Victor H

09/11/2017
HIVYO ULIVYO NI KWA KUSUDI LA MUNGU*1 SAMWELI 8: 20**"...ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu at...
11/10/2017

HIVYO ULIVYO NI KWA KUSUDI LA MUNGU

*1 SAMWELI 8: 20*

*"...ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu."*

Mungu amemuumba kila mtu kwa upekee wake, na kila taifa kwa namna yake.

Haya yote aliyafanya kwa mpango wake mzuri kwa kila mmoja wetu.

Hoja ya Israeli kumkataa MUNGU kuwa mfalme, kigezo ilikuwa ni ili wafanane na mataifa mengine.

Kwa tafsiri yangu, *walifika mahali wakazoea na kuuchoka upekee wao* wakataka kufanana na wengine, hata pale walipoelimishwa juu ya madhara ya kufanana na wengine, walichagua madhara kuliko kuendelea kuwa wa pekee.

Mpendwa, inawezekana, nawe umefika mahali pa kujitathmini na kujilinganisha na wengine kimaisha, huoni k**a ni sawa ulivyo, hali uliyo nayo imekuchosha, unaona k**a vile MUNGU hajakutendea haki kuwa ulivyo sasa, nafsi imeinama na kuanza manung'uniko au kuanza juhudi nje ya mpango wa MUNGU kuelekea mabadiliko ili ufanane na uliotamani kufanana nao.

Mpendwa nakusihi, tulia, litafute kusudi la MUNGU la wewe kuwa ulivyo, na ikiwa ipo sababu ya mabadiliko, itake kwa MUNGU ambaye ndiye asili ya uwepo wako.

Mungu akiruhusu mabadiliko katika mfumo wa maisha yako, hutayajutia mabadiliko hayo.

Apostle Victor H

LEO NI SIKU YAKO YA KUTOKA KABURINI.LUKA 8:26-29Yawezekana kaburi lako ni*Kukosa Kazi*Uchumba wako kuvunjika*Ndoa yako h...
28/09/2017

LEO NI SIKU YAKO YA KUTOKA KABURINI.

LUKA 8:26-29

Yawezekana kaburi lako ni
*Kukosa Kazi
*Uchumba wako kuvunjika
*Ndoa yako haina Amani
*Biashara haziendi
*Kuchekwa kwa hayo Mapito.

Tunaona Yesu alipo kutana na mtu mwenye mapepo huko pwani ya inchi ya Wagerase inayo kabiliana na Galilaya,mtu mmoja aliye kuwa amepagawa na mapepo hakuwa amevaa nguo,wala hakuwa anaishi nyumbani bali Makaburini,alipo mwona Yesu alijitupa chini na kumwambia nakusihi usinitese japo pepo huyo mchafu alikuwa ana mvamia huyo mtu Mara nyingi.

Basi Yesu akamuuliza "Jina lako nani " Yeye akajibu ,Jina langu ni jeshi"kwa sababu pepo wengi walikuwa wame mpagaa .

Hapo pepo wakamsihi asiwapeleke kwenye shimo Juu ambapo kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha Mlimani hao pepo waka msihi wawaruhusu wawaingie, naye Yesu akawapa ruhusa.

Ulisha jiuliza kwa nini hayo yote yanakupata Wewe tu?

Umevuliwa nguo na mapepo umekuwa wa kukataliwa kila mahali.

Ndoa yako kila siku imekuwa ni vikao tu kuinusulu.

Biashara zako hazifanikiwi

Hata mahusiano yako yamekuwa ni ya kuishia njiani tu.

K**a mtumishi wa Mungu nina sema Leo kila pepo alie kuvua nguo au kuzika kwenye makaburi hayo Leo nina waruhusu hao mapepo wote wakamuingie yeye aliye kutumia na uzao wake .

Kila kaburi ulilo kuwa umewekwa ninakuchomoa kwa jina lenye mamlaka kuliko majina yote jina la Yesu .

K**a nawe upo katika kaburi la aina yako andika neno Amen&Share ilikuchomoka katika makaburi hayo.

Apostle Victor H

Address

255
Dar Es Salam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Apostle Victor Herbert posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share