City center Interdenominational Bible Fellowship

City center Interdenominational Bible Fellowship This is an Interdenominational Bible fellowship for all Christians around the city of Dar es salaam. service is on fridays @ Posta Hidery plaza building

This is an interdenomination Bible fellowship, design for all people around Dar es salaam city center,

Easter Conference 2024, Save the Dates.
19/03/2024

Easter Conference 2024, Save the Dates.

20/06/2022

Alhamis wiki ijayo ni majira ya kukutana na Bwana katika Kongamano kubwa la Penuel 2022.
Nakusihi mwana wa Mungu panga kuhudhuria, mahudumio ya Bwana kupitia watumishi wake yatakuwa makubwa!

12/05/2022
22/05/2021
03/05/2021
30/04/2021
30/04/2021

Kila jumapili kuanzia saa 1:30 asubuhi. Usikose

18/04/2021

SOMO:
MNENAJI : Apostle Lillian Ndegi


13:11 [11]Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema k**a mtoto mchanga, nalifahamu k**a mtoto mchanga, nalifikiri k**a mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.

Kukua kiroho ni lazima kwa mwamini kwa maana ni katika ukuaji wa kiroho pekee ndipo kuna kukua katika mambo mengine yote.


Kukua ni kuwa zaidi ya ulivyo kuwa awali, ni kupanda daraja , ama kuwa bora zaidi ya awali.

Tazama kutokukua ni mzigo, tena ni mzigo unaoumiza. Tazama mzazi anavyofurahia ukuwaji wa mwanae katika kila hatua kutoka kutokujiweza kabisa mpaka kuanza kukaa kutambaa na kutembea. Umeshawai jiuliza inakuwaje pale mzazi anapikuwa na mtoto halafu hakui?, yani mathalani miezi tisa imepita lakini mtoto hakai, wala hatambai wala kuongezeka uzito yuko vile vile k**a alivyozaliwa, hii hali ni teso kwa mzazi. Tazama hivi inawezekana kwa mtu kuwa na umri wa miaka 20 bado awe anavalishwa nepi? Sasa kwa sisi wa amini inakuaje tukubali kuwa watoto kiroho japo kuwa tulikwisha zaliwa mara ya pili na mbegu usiyoharibika? Umeshawai jiuliza Mungu anajisikiaje kuwa na watoto wasiokuwa?

?
2:1 [1]Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote. Pale unapotembea kwenye tabia za mwilini ni uthibitisho tosha kuwa bado unatembea k**a mtoto

3:1-3 [1]Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi k**a na watu wenye tabia ya rohoni, bali k**a na watu wenye tabia ya mwilini, k**a na watoto wachanga katika Kristo.[2]Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi,[3]kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?

Tazama unapokua mtoto maana yake pia unakua tegemzi na kuwa k**a mtumwa tu. Ukiwa mtoto utayumbishwa na mawimbi ya kila aina. Lakini ukikua unaindikana na hizi adha.


Maamuzi ya kukua
Kukua sio ajali, ni jambo ambalo linategemea maamuzi yako ya moyo wako nje na hapo kukua kiroho hakuwezekani


Tazama bila ya kuwa na kiu hutayanywa. Sikiliza, adui kitu anacho pambana kuiiba kutoka kwako ni kiu yako juu ya Neno la Mungu. Tazama ni kwenye kiu ya Neno Pekee ndiko kuna kusoma Neno kwa mwendelezo na hapo ndipo kwenye kukua kiroho. Kiu ndio fedha pekee ndani ya Ufalme wa Mungu ili uweze kununua aliyokuwanayo baba bure. Tazama Yeye anasema huwapa wote wenye kiu maji ya Uzima bure.

4:1-2 [1]Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, ingawa ni bwana wa yote;[2]bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba. Hakuna maombi ya kuondoa utoto isipokua kwa kukua pekee. Usije ukasema utafunga ufanye maombi ya kuukemea utoto wa kiroho. Unaitaji tu kukua, kunatokana na kujifunza Neno la MUNGU kwa mwendelezo ili upate badiliko la kweli la ndani.

Tazama lazima ukue mpaka ufike katika kiwango cha kuliishi kusudi lako. Mtoto hawezi tu kuliishi kusudi tu, hata kulijua kusudi lake.Tazama ni kwenye wajibu pekee ndipo kulipo na mahudumio ya kiungu na hii ndio upelekea kufunguliwa kweli kweli.

Barikiwa sana

Address

Haidery Plaza Kisutu Street, McHafukonge, Dar Es Salaam
Dar Es Salam
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when City center Interdenominational Bible Fellowship posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share