Mahanaim Genuine Christian Mgct.

Mahanaim Genuine Christian Mgct. KANISA LA MGCT YOMBO MALAWI DAR ES SALAAM, LINAKUKARIBISHA KUSHIRIKI IBADA ZAO. JUMAPILI SAA 2:00 ASUBUHI HADI SAA 7: 00 SIMU 0755528965

USIACHE KUTAZAMA SOMO HILI YOUTUBE. KISHA SHEA KWA UWAPENDAO, PIA NIKUOMBE K**A HUJA SUBSCRIBE CHANEL YANGU PLZ SUBSRIBE...
13/09/2022

USIACHE KUTAZAMA SOMO HILI YOUTUBE. KISHA SHEA KWA UWAPENDAO, PIA NIKUOMBE K**A HUJA SUBSCRIBE CHANEL YANGU PLZ SUBSRIBE, LIKE, BOFYA ALAMA YA KENGELE.

MAOMBI YA KUUSHINDA UCHAWI - PRAYER TO OVERCOME WITCHCRAFT -Je! Uchawi upo kweli? - Does magic really exist? Waefeso 6:12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si ...

24/05/2022

like

06/05/2022
26/01/2021

VITABU VYA LION A MANGOLE NI K**A IFUATAVYO.
1. KUWA NA UWEZO MKUBWA KIAKILI, KWA AJILI YA WATU WOTE PAMOJA NA WANAFUNZI WANAOPENDA KUFAULU MASOMO YAO. Sh 20,000
2. Sumu ya Ukuaji wa Kanisa. Chenye masomo ya kuujenga ushirika. Sh 10,000
3. Huduma ya Mchungaji, chenye mwongozo wa ibada maalumu k**a maziko, ubatizo, ndoa, kubariki watoto nk. Sh 10,000
4. Vita katika Madhabahu. Sh 10,000
5. Wajibu wa Mama Mchungaji na Wake wa viongozi wa Kanisa. Sh 5000
6. Ufunguo wa kuzungumza na Waislamu, kina aya 323 za Quran pamoja na majibu ya maswali tata. Sh 7000
7. Kinga na dawa ya mapenzi kinachofundisha
uchumba hadi ndoa. Sh 5000
8 . Uchumi huru usiokuwa na majuto. Kinachofundisha
uchumi na ujasiriamali. Sh 10,000
9 Kuchinja ni haki ya nani?. Sh 2000
10 Omba k**a Tai Maombi ya upenyo, Kina aina kumi za maimbi. . Sh 4000
11. Ufunguo wa kuzungumza na Waislamu Toleo maalumu namba 1. 5000
12. Chochote kinaweza kuwa k**a dhahabu. Sh 3000
13. Nguvu ya Agano. Sh 3000
14. Jifunze ukweli kuhusu mavazi. Sh 4000
15. Biashara isiyododa. Sh 3000
16. Kanuni bora za kufanya maombezi (kitabu cha kiongozi &muumini ). Sh 5000
17. Kuwatunza Wazee na Vikongwe. Sh 5000
18 Wamachinga. Sh 4000
19. Sababu 11 za kumuombea Mchungaji wako Sh 4000
20. Maombi ya kuushinda uchawi. Sh 10,000.
21. Kuwa Tajiri kwa Mbinu rahisi. Sh 4000.

Kwa manunuzi ya jumla au rejareja popote ulipo na pia tunatuma mikoani kwa njia ya basi au posta wasiliana nasi kwa 0717528272/0788170367/0755528965 Tupo Dae es salaam Nyantira Kitunda na Yombo Kwalimboa. Hautajutia kununua vitabu hivi mwandishi anauzoefu wa miaka 18 ya uandishi wake.

06/06/2020

Somo: Nidhamu ya maombi / ibada Kanisani.

Maelezo: Ni vema utambue kuwa, nidhamu ya maombi, au
utaratibu wa kuwa katika maombi ni jambo moja muhimu
sana. Unapoingia Kanisani ni lazima uelewe mambo ya
muhimu ya kuzingatia au kujua umuhimu wa nidhamu katika
nyumba ya Mungu au maombi.
Mambo ya kuzingatia katika nidhamu ya Maombi (au Kanisani)

k**a ifuatavyo.
1. Mavazi unayovaa. Kuvaa kwako unapokuja Kanisani au
unapokuwa katika maombi. Hakikisha unavaa mavazi ya
heshima au adabu kwani nyumba ya Mungu ni mahali pa
kuheshimika sana kuliko sehemu yoyote ile. Hivyo ni vema
mavazi yetu yawe ya heshima.

2. Zima simu, ondoa mlio wa simu, lakini hata ikiita usitoke
nje kupokea hadi umalize ibada. Unapotoka nje kupokea simu
na kuacha maombi au kuacha ibada ni kumdharau Mungu na
ni dhambi. 1 Sam. ....Kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu

3. Ukichelewa kufika ibadani, unapoingia Kanisani usiburuze
miguu au viatu ukawapigia watu kelele, na k**a una
viatu vya koo koko, vua au nyata visipige kelele.

4. Unapochelewa na umewakuta watu kwenye maombi au
kuabudu, unapotaka kukaa kiti cha ndani ya mstari, ikiwa na
maana, ili ukae ni lazima umpite mtu mmoja au wawili, unashauriwa usiingie kukaa hadi wamalize maombi ili usiwasumbue na kuwatoa katika uwepo wa Mungu. 1 Kor. 14:40 Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.

5. Iwapo mtu yupo kwenye maombi nyumbani chumbani
nk. Usiingie hadi amalize kuomba au k**a utaingia basi
iwe ni kwa lengo la kuungana naye katika maombi. Aidha
mwombaji iwapo utatumia chumba chenye matumizi ya
watu wengi ni vema uwajulishe wenzako kuwa utakuwa na
maombi kwa muda fulani ili wawe na taarifa.

6. Kila kinachoagizwa au unachotakiwa ufanye wakati wa
maombi ya pamoja k**a Kanisani nk. Hakikisha unafanya
pamoja na wenzako. Kwa mfano, kiongozi anaposema tusimame basi na wewe simama, au tuimbe, tuombe nk ufanye k**a wenzako wote wanavyofanya usifanye kinyume na kiongozi wa ibada anavyokuelekeza.

Tunapoona mtu huwa hataki kufanya sawa na waumini weningine Kanisani inatosha kujua huyo mtu ana roho nyingine tofauti na waumini wengine. Biblia imeagiza kuwa tuwe na nia moja na roho moja na mapenzi mamoja. Wafilipi 2:2.3 ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.

1 Yohona 4:1. Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo
roho, kwamba zimetokana na Mungu;

Matendo 4: 24.31. Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti
zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu,
ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;........................ Hata walipokwisha kumwomba Mungu, Mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.

Hapo tunaona umuhimuwa kuwa na nia moja katika maombi
au nguvu ya umoja katika maombi. Aidha kutokugawanyika
katika maombi. Kufanya kila kitu kwa pamoja. Kiongozi wa
maombi au Mchungaji awe makini sana na watu ambao wanaotofautiana na utaratibu wa maombi awasaidie au awakemee kwani mtu anayejibagua bagua mara nyingi huwa anatumiwa na adui shetani kuvuruga uwepo wa maombi.

Somo hili limetoka katika kitabu changu Kiitwacho "Omaba k**a Tai, Maombi ya Upenyo" Iwapo utahitaji kitabu hiki wasiliana na Mwandishi kwa+255717528272

Address

Yombo Malawi Hospitali
Dar Es Salaam

Telephone

+255755528965

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mahanaim Genuine Christian Mgct. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share