YESU NI Mshindi

YESU NI Mshindi Yesu mpendwa, Asante kwa kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu. Tafadhali nisamehe kwa mambo yote Watu hawa wamefungwa kwenye magereza na Ibilisi.
(1)

Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaidia familia yako. Biblia inapozungumza habari ya watu waliofungwa wapate kufunguliwa, hii ina maana ya kuwa kuna watu wamefungwa chini ya utawala wa nguvu za giza katika ulimwengu wa Roho. Tutambue ya kuwa Yesu aliposema amekuja kutuokoa hii inamaanisha kwamba ku

na mahali ambako tusingeweza kujikwamua wenyewe bila nguvu yake yeye mwenywe kuingia kati yetu. MAOMBI YA KUMTEKETEZA SHETANI:

Baba katika Jina la Yesu:

1. Ninayaharibu na kuyateketeza mamlaka yote aliyopewa shetani na mababu/ mababa, ndugu zangu katika Jina la Yesu.
2. Nina zilaani na kuziteketeza kwa damu ya Yesu roho zote zinazoendelea kutilia mkazo hayo maagano katika maisha yangu na naziteketeza na kuzivunavunja kwa Jina la Yesu.
3. Kitu chochote kilichoingizwa kwenye maisha yangu,kwa mkono wa kipepo, au majini ninakiamuru kiachie kwa JIna la Yesu.
4. Kila aina ya sumu iliyopenyezwa kwenye maisha yangu nina iamuru itoke nje sasa, katika jina la Yesu, nina sukuma nje kwa damu ya Yesu.
5. Ee Bwana Yesu, shusha moto juu ya kila roho ya mauti na kuzimu, iliyoandaliwa kwa ajili yangu, katika jina la Yesu
6. Nina ponda kichwa na kukanyaga kila mkia wa majoka ya kiroho, katika jina la Yesu
7. Upanga wa moto, na uanze kukata kila kifungo walichokifunga wazazi, katika jina la Yesu
8. Ee Bwana, nifunulie agano lolote la siri ambalo shetani amefunga na nafsi yangu au anataka kufunga na nafsi yangu, katika jina la Yesu.
9. Kila pando,ambalo baba yangu wa mbinguni hakulipanda katika maisha yangu, nina kungo’a katika jina la Yesu.

𝐀𝐦𝐞𝐞𝐧�

09/06/2024

BWANA YESU ASIFIWE

27/04/2024

BADO NAFASI YAKO IPO WEE NJOO TU

Shalom. Leo nakuletea ujumbe mfupi kupitia story ya kijana mmoja. Yupo kijana mmoja alikua anampenda Mungu sana, na alikua na bidii kubwa katika kazi yake. Kazi hiyo aliipata katika kampuni fulani inayojihusisha na madini

Akiwa kazini alikua kijana mzuri tu, alikua mchapakazi na wengi walimpenda kwa bidii, nidhamu na weledi wake kazini. Miaka kadhaa ikapita, kijana yule alianza kubadilika ghafla akaanza ku-behave vibaya tofauti na alivyokua. Kuifanya story hii ndefu iwe fupi, ni kwamba kijana alikua ameshapata kazi sehemu nyingine ambayo mshahara ni mkubwa zaidi ya pale. Alianza vituko pale ili afukuzwe na mwisho wa siku akaondolewa pale

Alipondoka akaenda kwenye kampuni mpya yenye mshahara mkubwa. Akafanya kwa muda mfupi akagundua wanalipa kwa kuchelewa, hana uhuru, pamoja na mambo mengine mabaya tofauti na kule kwa mwanzo. Alianza kujuta kwanini alitoka kule. Akaanza kuwaza amtafute boss wake wa zamani arudi

Akamtumia boss wake wa zamani message kuwa anaomba kurudi kwani alifanya makosa kuondoka. Boss akamjibu kwamba "BADO NAFASI YAKO IPO WEE NJOO TU"

Jambo gani hapa Mungu anataka kusema na sisi? Nafasi yako wewe uliyemuacha Mungu kwa sababu ya dunia bado ipo. Yesu anasema na wewe kwamba nafasi yako hakuna mwingine ameichukua, rudi nyumbani atakupokea

Hata k**a kwa boss wako wa zamani umetoka vibaya, ulimtukana sana boss, ukamchafulia jina na kusababisha hasara kubwa... Boss wako huyo wa zamani anasema wewe njoo tu nafasi yako bado ipo

Naam, ni sauti ya Roho Mtakatifu kukuita. Hakuna sehemu nyingine salama zaidi ya kwake. Hakuna usalama nje ya Mungu, rudi na utapokelewa. Mungu akubariki sana

By Mathias
0766246830

13/04/2024

HAYA NDIO MAMBO ADUI HUFANYA UNAPOKUA UNAOMBA

1. Kukuaminisha kuwa hakitafanyika au hakitawezekana. Atakuonesha muda wote ukubwa wa hilo jambo na kukuambia kuwa hilo haliwezekani. Atakuonesha watu waliowahi kujaribu k**a wewe wakashindwa. Atakuonesha namna ulivyodhaifu au kukuonesha madhaifu yako. Hataweza kukuonesha namna Mungu alivyo mkubwa na muweza yote. Yeye mission yake hapa ni kukukatisha tamaa ili uone unachofanya ni kazi bure, uombee vingine. Kuna changamoto unaweza ukawa unapitia, ni kubwa mno kiasi kwamba unaona kabisa haiwezekani. Umefika hatua huamini k**a Mungu anaweza kuingilia kati na kuitatua. Ukifika hatua hii, hata ukianza kuomba adui atatumia hiyohiyo k**a njia ya kukuzuia usiombe ipasavyo. Kila ukianza kuomba tu, unakumbuka kwamba bado siku tatu kodi yako iishe na mpaka sasa huna na wala huoni dalili ya kupata. Utajikuta unaacha kuomba halafu unaanza kuwaza nifanye nini? Niende wapi? Nimtafute nani? Ndugu yangu hebu jiulize, kwani hakuna muda mwingine wa kuwaza hayo hadi wakati ukiwa unaomba ndio mawazo hayo huja tena kwa kasi? Usikubali! Hizo ni hila za adui. Kila siku jaza Neno la Mungu ndani yako, omba pia ili hata ukiwa unaomba umuone Mungu na si tatizo lako au madhaifu yako

2. Kukuondolea focus, utajikuta wakati mwingine unaacha kukiombea kitu hiko na kuombea vingine au kukufanya uache kuomba na kuanza kuwaza mambo mengine kabisa

3. Kukuondolea nguvu ya kuendelea kukiombea. Hata baada ya maombi yako, atajitahidi ukishamaliza kuomba hutaweza kuomba tena. Ndio maana watu wengi wakianza kuombea kitu fulani, siku inayofuata hawaombi tena au wataomba kikawaida sana. Adui huinuka na kuua nguvu yako ya kuendelea kukiombea kitu hiko. Usikubali hii ikupate, moto ulioanzisha uendeleze kila siku

4. Kukukumbusha dhambi ambazo ulishasamehewa na kuanza kukuhukumu kupitia hizo kuwa zinakuzuia. Inawezekana unaomba upate mtoto, na pengine zamani umewahi kutoa mimba ukatubu na kusamehewa. Kila utakaposimama kuomba kwa ajili hiyo, atakuletea Kumbukumbu hizo tu ili ujione hufai wala hustahili. Pazia la hekalu lilipasuka kumaanisha kwamba sasa tunaweza kumsogelea Mungu mwenyewe aliye Kuhani Mkuu(Ebr 9:12).Usikubali kuamini kuhusu hilo, Mungu akishasamehe haendelei kukuhukumu, wewe sasa ni kiumbe kipya kabisa. Simama kwa ujasiri uombe na usikate tamaa, atakujibu siku moja Warumi 8:1

5. Adui anaweza kukufanya ujione wewe unajitosheleza, umekamilika, kwahiyo hata usipoomba bado mambo yako yatakua sawa. Wakati mwingine unaweza kweli ukaona upo vizuri, huwa unaomba, huwa unasoma Neno, uchumi wako umekaa vizuri, ndoa yako ina amani na furaha nk. Kwahiyo wewe mwenyewe ukiona hivyo unaona ya nini kujitesa kuomba kila siku? Ya nini kufunga? Usikubali kufika huko, uwe navyo usiwe navyo bado unahitaji kuomba na kujenga mahusiano mazuri na Baba yako wa Mbinguni

Ubarikiwe

By Mathias
0766246830

18/11/2022

BWANA YESU ASIFIWE??

09/11/2022
Baba wa Mbinguni, mimi ni mtumishi wako mnyenyekevu, ninakuja mbele zako leo nikihitaji tumaini. Kuna wakati nilianguka ...
09/11/2022

Baba wa Mbinguni, mimi ni mtumishi wako mnyenyekevu, ninakuja mbele zako leo nikihitaji tumaini.
Kuna wakati nilianguka hoi,
Kuna wakati najihisi mnyonge.
Ninaomba kwa matumaini.
Nahitaji tumaini la maisha bora ya baadaye. Nahitaji matumaini ya maisha bora.
Nahitaji tumaini la upendo na fadhili.
Wengine husema kwamba anga kuna giza zaidi kabla ya mwanga. Ninaomba kwamba hii ni kweli, kwa maana yote yanaonekana giza. Nahitaji nuru yako, Bwana, kwa kila njia. Ninaomba kujazwa nuru yako kuanzia kichwani hadi miguuni. Ili kufurahiya utukufu wako. Kujua kuwa kila kitu kiko sawa ulimwenguni, k**a ulivyopanga, na vile unavyotaka iwe. Nisaidie kutembea katika nuru yako, na kuishi maisha yangu katika imani na utukufu ninaomba. Amina.

09/11/2022

Bwana Nisaidie nitembee katika nuru yako na kuishi maisha yangu katika imani na utukufu wako Amina.

Baba wa Mbinguni, tafadhali nipe amani ya akili na utulize moyo wangu wenye matatizo. Nafsi yangu ni k**a bahari iliyoch...
09/11/2022

Baba wa Mbinguni, tafadhali nipe amani ya akili na utulize moyo wangu wenye matatizo. Nafsi yangu ni k**a bahari iliyochafuka. Siwezi kupata usawa wangu kwa hivyo ninajikwaa na kuwa na wasiwasi kila wakati. Nipe nguvu na uwazi wa akili kupata kusudi langu na kutembea katika njia uliyoniwekea. Ninakuamin Mungu wa Upendo, na najua kuwa utaponya mkazo huu. K**a vile jua linachomoza kila siku dhidi ya giza la usiku. Tafadhali niletee uwazi kwa nuru Yako Mungu. Kwa jina lako naomba, Amina.

Ee Mungu Tunakubariki kwa ajili ya maisha yetu tunakupa sifa kwa ajili ya rehema zako nyingi na neema tunayopokea. Tunak...
09/11/2022

Ee Mungu Tunakubariki kwa ajili ya maisha yetu tunakupa sifa kwa ajili ya rehema zako nyingi na neema tunayopokea. Tunakushukuru kwa uaminifu wako ingawa sisi sio waaminifu kwako. tunakuomba utupe amani pande zote katika akili, mwili, nafsi na roho. Tunakuomba uondoe kila kitu kinachosababisha dhiki, huzuni na huzuni katika maisha yetu. Tafadhali ongoza njia yetu katika maisha na uwafanye maadui zetu wawe na amani nasi. Acha amani yako itawale katika familia zetu, mahali petu pa kazi, biashara na kila kitu tunachoweka mikono yetu. Waache malaika wako wa amani watutangulie tunapotoka na wakae kando yetu tunaporudi. Katika jina la Yesu, Amen

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when YESU NI Mshindi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to YESU NI Mshindi:

Share