05/01/2024
Hata k**a nitunge nyimbo za kukusifu Ee uliyewangu naona bado sitamaliza kuusifia uzuri wako kwani hata karatasi hazitoshi na peni zitaisha wino wote na mkono wangu utazidiwa na nguvu za upendo wako kwangu, maana naona kukumbatiwa na wewe saa zote, muda wote na hali zote, udhaifu wako ndiyo kituo Cha nguvu zangu. Leo hii nafurahia sana kukutaja na kukusifu hadharani eeh uliyewangu sijutii kuwa na wewe mywangu...sijisikii kufungwa au nipo gerezani hapana najiona niko huru kwa sababu wewe upo, halafu nilisahau kukuambia wewe ni mwanzo na mwisho wa raha zangu my, tabasamu lako Ni nuru yangu kicheko chako ni bahari safi ya kuogelea na maneno yako mazuri ni taulo safi lakunifutia wakati umetoka kuniogesha...sijasahau uliponitoa mywangu nakupenda halafu nakulove......
Jamani tujifunze kuwakubali wapenzi wetu na kuwasifia hata K**a hakuna maokoto 🤣🤣🤣