NENO La KWELI

NENO La KWELI NENO LA KWELI

hii page inahusika na kujifunza neno la MUNGU kiuhalisia wake na msingi mkuu wa hii page umejengwa katika BIBLIA TAKATIFU inaongozwa na mtumishi wa Mungu Jackobo Mbwaga {Bro Jackobo}

KUJIKA NDANI YA KRISTO YESU (Sehemu  ya tatu Final)Utakuwa nami mpendwa katika kristo yesuName: Bro JackoboPhone: 0766 9...
20/12/2025

KUJIKA NDANI YA KRISTO YESU (Sehemu ya tatu Final)

Utakuwa nami mpendwa katika kristo yesu
Name: Bro Jackobo
Phone: 0766 944 441
Email; [email protected]

Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu?? Karibu Tena kwenye sehemu hii ya tatu na ya mwisho ambapo ni muendelezo wa somo la Kujikana ndani ya Yesu ambapo tuliona maana ya kujikana ndani ya Yesu kristo, Tuliona nani alikuwa mwanzilishi wa kujikana tangu asili ambaye ni mfano wetu wa kuigwa tukaona na maeneo muhimu mawili ambayo mwamini anapaswa kuonyesha na kuthibitisha kuwa amejikana ndani ya Yesu kristo Yesu katika sehemu ya kwanza halafu tukasoma sehemu ya pili ambapo tuliangalia vipingamizi katika kujikana kwa mwamini mbele ya Mungu wake. K**a hujayasoma masomo hayo naomba uende uyasome ili upate mtiririko mzuri.
Leo Tutaanzia kwenye kipengele cha madhara kwa kanisa kushindwa kujikana kikamilifu kwaajili ya kristo Yesu.

5. MADHARA KWA KANISA KUSHINDWA KUJIKANA KWAAJILI YA YESU KRISTO.
Mungu wetu ni wa utaratibu sana amabaye hawezi kumlazimisha mtu kumfuata bali anatamani kila mtu amfuate kwakuwa amependa kumfuata japo yeye Mungu sio k**a mwanadamu ambaye ameweka uongozi wake usiwe wa mfumo wa kidemokrasia tu bali ameuweka uongozi wake wa theoklasia (Theocracy) ambapo ana utaratibu wake anaotaka tuufuate ambao una maelekezo ya kila kitu tunachotakiwa kukifanya na akaweka kwamba tusipofuata kuna madhara yatakayo tokea.

Sasa kanisa lazima likubali kufuata taratibu zake mwenyewe lasivyo madhara yatatupata k**a ifuatavyo hapa chiniπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

A. Kutokujibiwa kwa maombi yetu
B. Kukosekana kwa matendo makuu ya Mungu
C. Kupotea kwa kibali na heshima mbele za Mungu

A. KUTOKUJIBIWA MAOMBI
Maombi ni mawasiliano ya pande mbili ambapo huwa mwamini anamuelezea yule anayemuamini juu ya yale yanamsibu na muaminiwa kutoa majibu kwa anayemuamini juu ya kile alichokiweka mezani. Kwahiyo maombi ni mchakato wa njia mbili ambapo lazima pande zote zipate muitikio kutoka kwa upande mwingine juu ya hoja moja inayowaunganisha ili kujenga uhusiano wa karibu sana "Intimacy".
Kwasababu ya kanisa kutokuwa na uhusiano mzuri na Mungu yani kushindwa kujitoa kikamilifu kwaajili ya Yesu kristo, mambo mengi yamemfanya Mungu azibe sikio lake lisiweze kusikia yale ambayo wanahitaji kwasababu hakuna lengo moja linalowaunganisha la kimahusiano. Sasa Mungu ndio maana anataka watu wake wote wajitoe kikamilifu na k**a hawatajitoa wanakuwa wameikataa sheria yake na ndio maana anakuja kusema ya kwambaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mithali 28:9 "Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo."

Pia ukifuatilia biblia utagundua wana wa Israel pale walipokosea mara nyingi waliingia katika mikono ya adui hata kupewa adhabu na Mungu mwenyewe. Sasa kipindi cha nabii Amosi wana wa Israel walikuwa wamekosea kiasi wakawa wanaabudu mpaka sanamu huku bado wakitaka kutaka kumfanyia Mungu ibada huku hawajajikabidhi kwa Mungu kikamilifu mpaka ikafika Mungu. Anakuja kufoka na kuwaambia maneno hayaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Amosi 5:22-23 "Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona. Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu."

Kutoa kwao sadaka na kumfanyia Mungu nyimbo za shangwe za kuoyesha furaha yao kwa Mungu hakukuwa na maana kabisa mpaka Mungu akawa anawaambia wamuondolee nyimbo zao maana zimekuwa kelele kwakuwa mioyo yao haikuwa kwake kamili. Kwahiyo ukitaka Mungu akusikie lazima ujitoe kikamilifu mbele zake lasivyo utakuwa unajidanganya na utakuwa unapoteza muda wako. Hii inakuja kuthibitisha kile Mungu anataka kiuhalisia wakeπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yohana 9:31 "Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo."

Sasa lazima pia uwe na moyo wa kutafakari kikamilifu sana na kwaakili ambayo imetulia sana kuelewa hili. Mungu amesema mwenyewe kabisa kwenye maandiko yake kuwa pale ambapo mtu anachagua kuishi katika dhambi huwa dhambi inamfarakanisha na Mungu na hata yale mambo anayokuwa anayaomba Mungu hawezi kuyajibu wala Mungu hawezi kuwaokoa maana dhambi inakuwa ni kiambaza kinacho watenganisha nyie na Mungu wenuπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Isaya 59:1-2 "Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; ]lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia."

B.. KUKOSEKANA KWA MATENDO MAKUU YA MUNGU.
Kanisa inapaswa kuwa ni sehemu ambapo madhihirisho makubwa ya uwezo wa Mungu kwa matendo makuu kuonekana lakini kwasasa imekuwa nii kitu ambacho ni adimu sana kwasababu watu wengi hawako thabiti sana mbele zake ili na yeye aweze kuyaonyesha matendo yake kwa kanisa. Kizazi hiki kimekuwa kina ukaidi sana hakiko tayari kabisa kujitoa kikamilifu kwaajili ya kristo kitu ambacho kinaleta mapooza ndani ya Nyumba ya Mungu na Mungu kumfanya anyamaze kabisa. Yesu alizungumza wazi kabisa kuwa kizazi hiki kitatafuta ishara lakini hakitapata kwasababu ya movu yao katika maandiko kadhhaa πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mathayo 16:4 "Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake."
Mathayo 12:38-39. "Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona."

Sasa ukitaka kuelewa vizuri unaweza ukarudi nyuma ukaona namna Gideoni alivyokuwa anashangaa kwamba walisimuliwa matendo makuu ya Mungu lakini kipindi chao hakuona yale matendo makuu ya Mungu ila ameona namna ambavyo taifa la Israel likiwa liko chini ya kongwa la utumwa wa wamidiani mpakka akawa anajiuliza wewe Mungu ikoje hapa lakini hakuwa amezingiatia kuwa taifa la Israel lilikuwa limeingia katika dhambi ndicho kitu kikawafanya wasiyaone matendo makuu ya Mungu.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Waamuzi 6:1,13 "Kisha wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA; BWANA akawatia mikononi mwa Midiani muda wa miaka saba. Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani."

(Unaweza ukasoma pia waamuzi 2:10-15)
Kwahiyo mlango mkuu wa kanisa kutokuona matendo makuu ya Mungu ni kuto kujitoa kikamilifu kwa Yesu mwenyewe maana yeye ndiye mwenye matendo makuu, lazima tukubali kumfuata na kuacha yote kwaajili ya Yesu kristo Yesu.

C. KUPOTEA KWA KIBALI NA HESHIMA MBELE ZA MUNGU.

Mungu anapo liona kanisa lake likiwa limepoteza mwelekeo anaoutaka kwa kutokujitoa kwake mbele zake huwa anacho kifanya anaondoa mambo makuu mawili ambayo ni muhimu sana ambayo ni
A. Heshima
B. Kibali

Ufunuo wa Yohana 2:5 "Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu."
Ukisoma hapo juu unaona Yesu anazungumza kupitia kinywa cha Yohana kuwa lazima ukumbuke ulipoanguka ili utubu na usipofanya hivyo anakuja kuondoa kinara (Kibali na heshima) ambayo alikuwa amekupatia ili ubaki wewe mwenyewe maana haujafuata njia zake. K**a alivyokuwa ametaka. Hii kitu ndiyo ilimfanya pia hata petro kusema hiki kituπŸ‘‡πŸ‘‡

1 Petro 5:6 "Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;"

Kifupi ni kuwa k**a ukinyenyekea (Umejitoa kikamilifu mbele za Mungu) yeye atakuinua kwa wakati wake( Yani atakupa Heshima). Kiufupi k**a usipofanya hivyo uwe na uhakika atakupa aibu kabisa kwakuwa mkono wake hautakuwa juu yako na shetani atakuwa na uhalali wa kufanya kile anachokitaka kwenye maisha yako ya kila siku.

Naomba tuangalie japo kwa kifupi juu ya kibali ili kuweza kuelewa uzuri wa kuwa nacho kutoka kwa Mungu.
KIBALI
Mithali 8:35-36 "Maana yeye anionaye mimi aona uzima, naye atapata kibali kwa BWANA. Bali anikosaye hujidhuru nafsi yake mwenyewe, nao wanichukiao hupenda mauti."

Mambo muhimu kuhusu kibali
β€’ Hii ni hali ya kupokelewa au kukubaliwa kufanya jambo au kupewa ruhusa ambayo sio watu wote wanapewa bali ni kwa wale waliochaguliwa tu.
β€’ Pia, Kibali humaanisha kuonyeshwa wema, Yani Mungu anakutendea mema ambayo hata wengine huwa wanatamani k**a wangeyapata lakini wameyakosa kwasababu ya namna Mungu ametaka mwenyewe.
β€’ Pia hii ni hali ya kupewa upendeleo na Mungu
Mithali 12:2 "Mtu mwema atapata upendeleo kwa BWANA; Bali mtu wa hila atahukumiwa naye"

Lazima uelewe kuwa kibali huwa kinatafutwa na huwa kinatunzwa kwahiyo kwa kujitoa kwako kikamilifu mbele zako mbele za Mungu kutakufanya upate hicho kibali cha Mungu lakini k**a hautafuata matakwa yake utakipoteza kabisa.

MAMBO YA KUKUSAIDIA KUTUNZA KIBALI CHAKO KWA MUNGU
A. Jifunze kuwa na nia safi kabisa ndani yako kila inapoitwa leo
Wakolosai 3:17 "Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye."
1 Wakorintho 10:31 "Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. "

B. Jitahidi kufanya Mema mbele za Mungu
Mwanzo 4:5-7 "bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? K**a ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde."

C.Okoka kwa kumaanisha kwelikweli
D. Kuwa mtu wa Ibada.
Matendo ya Mitume 16:25-26 "Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa."

6. MAMBO YA KUFANYA ILI KULISAIDIA KANISA KUMAANISHA KUJITOA KWAKE.
Mungu wetu ni mwaminifu sana ambaye ametupa maarifa ya kuweza kutusaidia kumaanisha kujitoa kwetu. Kwahiyo kuna baadhi ya mambo ambayo yanaweza kutusaidia kumaanisha kujitoa kwetu kwa Mungu wetu. Mambo yenyewe ni k**a ifuatavyo
A. Kumjua Mungu
B.kuwa rafiki wa Neno la Mungu
C. Kumpenda Mungu na mambo yake yote
D. Kuchagua uaminifu na utii
E. Kuwa mtu wa Ibada, Maombi na kutenga muda wa maana na Mungu wako.

A. KUMJUA MUNGU
Moja ya jambo la kumsaidia mwamini kuweza kumaanisha kujitoa kwake ni kumjua Mungu vizuri ili kwamba kwenye kuamua kwake kujitoa anaelewa kwanini ameamua kuambatana naye. Kiufupi nguvu ya kujua inauwezo ndani yake wa kuambatanisha. Huwezi kuambatana na mtu usiye mjua wala huwezi kumuamini kwahiyo ukimjua Mungu utaambatana naye na utamuamini kwakuwa unaelewa kila kitu chake.

Ayubu 22:21 "Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia."

Mtu anapomjua Mungu huwa amani kwake sio kitu cha kuuliza wala kufikiria maana wakati wote anakuwa ana uelewa wa nini anakifanya. Kwahiyo hata k**a akiamua kuambatana na Mungu hata yakija magumu hayawezi kumtoa kwenye msitari wa kuendelea kuambatana na Mungu wake na ndio maana Daudi anasema πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Zaburi 119:165 "Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza."

Sasa ukimuangalia mtumishi wa Mungu paulo anaeleza namna ambavyo amejitoa kwa kristo Yesu na kuyaona mengine yote kuwa k**a mavi, lakini anatamani kumfahamu Mungu wake vizuri kwa kutokutumia haki yake mwenyewe bali kwa imani ipatikanayo katika kristo Yesu kitu kitakachomfanya aweze kumshika Mungu wa mbinguni kiukwelikweli na kuweza kuambatana naye siku zote.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Wafilipi 3:9-10 "tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;"

B. URAFIKI WA KWELI NA NENO LA MUNGU
Neno La Mungu huwa linatoa mwongozo wa namna ya kuishi katika maisha ya kila siku. Mtu anapokuwa rafiki wa Neno la Mungu kila hatua atakayokuwa anaiamua Neno litampa mwongozo na kumfanya aweze kuamua kikamilifu kujitoa kwaajili ya Yesu kristo.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Zaburi 119:105 "Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu."

Mungu ndiye pumnzi na uhai wetu na ndio maana hata kipindi cha Yoshua alimsisitiza kuishika sheria yake kila wakati ili kupitia hiyo imuongoze kwenye maamuzi kwakuwa toka asili Neno la Mungu ndio msingi wa ki maongozi kwa mtu yeyote ambaye amekubali kumfuata MunguπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana."

Mungu siku zote anachokitaka kwa kanisa lake ni ule moyo wa kuwa tayari kusikiliza Maneno yake na kuyatenda na kuhakikisha tunaishi katika hayo. Katika Neno ya Mungu tunapata kuwa salama na ndio maana hata Suleiman alipokuwa ameandika mithali kuna sehemu alisema hiviπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mithali 4:20-22 "Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu. Zisiondoke machoni pako;
Uzihifadhi ndani ya moyo wako. Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote."

Ukijiuliza ni kwanini mtumishi wa Mungu huyu alisema jambo k**a hili unagundua kwamba alikuwa akitamani watu wasikilize mahusia ya Mungu (Neno La Mungu) ambalo hilo unakuwa unamzungumzia Yesu kristo mwenyewe (Yohana 1:1-5) ambapo anatamani tumshike yeye yaani tujitoe kikamlifu kwaajili ya Mungu wetu maana katika yeye tutakuwa hai ikiwa tutamkimbilia. Unaweza ona namna ambavyo hata paulo alisema na watu wa Athene alipowakuta wakiabudu kwa Mungu asiyejulikana na akawatambulisha Mungu anayejulikana na kuwaambia kuwaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Matendo ya Mitume 17:28 "Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. K**a vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.

Ikiwa Uhai unapatikana kupitia Yesu kristo kwahiyo lazima tuwe na urafiki na Neno la Mungu ndipo tutaweza kujikuta tumeweza kulishika Neno La Mungu kikamilifu kabisa na kujikana kwaajili ya kristo Yesu. Jambo lingine mambo mengi tunayaweza kwasababu tumekaa ndani ya Yesu kikamilifu kwahiyo nguvu ya uwezesho wa kujitoa na kujikana kwetu huwa mara nyingi tunapewa k**a zawadi tu na Mungu mwenyewe kupitia Kristo Yesu. Ndio maana hata Yesu alizungumza na wanafunzi juu ya kukaa ndani yake ili waweze kuzaa matunda yani kiufupi uwezo wako wa kujikana kikamilifu kwaajili ya kristo Yesu unatokana na Yesu mwenyewe (Urafiki wa kweli na Neno la Mungu).πŸ‘‡πŸ‘‡

Yohana 15:5-6 "Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje k**a tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea"

C. KUMPENDA MUNGU NA MAMBO YAKE YOTE.
Mambo mengi huwa tunaweza kuyafanya ni kwasababu Mungu ametuwezesha lasivyo vitu vingi tungeshindwa kuvifanya (Wafilipi 4:13, 2timotheo 4:17). Sasa kwasababu mambo yote tunawezeshwa na yeye ni jambo moja Mungu analolitafuta kwetu ambalo kila wakati aangetamani tuweze kuishi katika njia hiyo ambayo ni Upendo na ndio maana katika kuzitaja amri yeye alitupatia amri moja kuu inayobeba kila kitu ambayo ni upendo.

Mathayo 22:36-40 "Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako k**a nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii."
Nimekuambia kuwa unapaswa kumpenda Mungu na mambo yake yote kwasababu kupitia Upendo ndipo utaweza kufanya maamuzi yaliyo sahihi ya kuamua kuambatana na Mungu kwenye maisha yako na kujikataa mwenyewe kabisa, hii ndio sababu hata ukiingia kusoma agano jipya ndipo unaona msisitizo wa mitume ulikuwa juu ya kufanya vitu kwa upendo mfano kwa habati ya utoaji (2wakorintho 9:7). Pia pale utakapo kuwa umempenda Mungu hata k**a utapitia magumu hautakata tamaa kumuishia Mungu utajikuta kila kitu kwako ni amani maana yupo Mungu akupaye amani.

Zaburi 119:165 "Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza."

D. CHAGUA UAMINIFU NA UTII
Uaminifu ni hali ya kitabia ambapo mtu anachagua kusimama katika makubaliano, ahadi, wajibu na mahusiano pasina kuangalia upande wa pili hata k**a yale mambo yanamuumiza.
Wakati
Utii ni kitendo cha kusikiliza, kukubali na kutenda kulingana na maagizo, sheria au mapenzi ya mamlaka halali, kwa hiari na heshima.

Sasa haya mambo mawili yaani uamini na utii lazima ukubali kuambatana navyo maana katika hivyo Ndipo kuna ufunguo wa kubaki katika mshik**ano. Kuna wakati lazima wewe uweke dhamira ya ndani ya kutaka kujikataa kwaajili ya Kristo Yesu ili Mungu aweze kukupa hiyo neema ya kuweza kujidhabihu kweli kweli na ndio maana samweli alimwambia sauli kuwaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

1 Samweli 15:22-23 "Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni k**a dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni k**a ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme."

E. IBADA, MAOMBI NA MUDA WA MAANA NA MUNGU.
Maana Ya Ibada
Neno Ibada linaweza kutafsirika kwa namna mbili ukitumia maneno ya kigiriki cha biblia(Kiyunani) ambayo ni "Proskuneo" na neno "Latreia"

"Latreia": humaanisha Huduma ya ibada, kumtumikia Mungu ambpo sasa Huhusisha maisha ya kujitoa kwa Mungu, si matendo ya nje tu bali mpaka utu wako wa ndani kabisa.πŸ‘‡πŸ‘‡

Warumi 12:1 "Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana."

"Proskuneo": humaanisha Kusujudu, kuinama kwa heshima na unyenyekevu. Hii Inaonyesha mtazamo wa moyo na mwili mbele za Mungu.πŸ‘‡πŸ‘‡

Yohana 4:24 "Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."

Pale kanisa/mwamini anapochagua kuwa chombo cha ibada huwa wakati wote Mungu anakuwa anafanya kazi pamoja naye, kitu kitakachomsaidia yeye mwenyewe kuendelea kujitoa kwa Mungu wake aliye muita na kumuokoa. Ibada siku zote inakuwa inaambatana na Maombi ambapo lazima utafute mda mzuri wa kuzungumza na Mungu wako ili akupe maelekezo ya namana ya kuishi kitu kitakachokusaidia kuwa salama na kujitoa kikamilifu mbele zake.
Jambo ambalo lilimfanya Yesu aweze kujitoa kikamilifu mbele za Mungu ni ule utayari wake aliokuwa anamfanyia Mungu ibada, pia alikuwa ni mtu wa maombi na alitafuta muda wa maana usiokuwa na vurugu za aina yeyote ambapo na sisi tunapaswa kufuata msingi huo lasivyo tutapotea pasina kujua.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Marko 1:35 "Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko."

Luka 22:39 "Akatoka akaenda mpaka mlima wa Mizeituni k**a ilivyokuwa desturi yake; wanafunzi wake nao wakafuatana naye."

Mungu akubariki kwa kuambatana nami katika mfululizo wote wa tatu katika somo hili Mungu aliliweka ndani yangu

K**a una swali au sehemu hujaelewa unaweza ukawasiliana nami kupitia mawasiliano hapo chini.

Ulikuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Number: 0766 944 441
Email: [email protected]

KUJIKANA NDANI YA KRISTO YESU (sehemu ya pili)Utakuwa nami mpendwa katika kristo yesuName: Bro JackoboPhone: +2557669444...
17/12/2025

KUJIKANA NDANI YA KRISTO YESU (sehemu ya pili)

Utakuwa nami mpendwa katika kristo yesu
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email; [email protected]

Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu?? Karibu Tena kwenye sehemu hii ya pili ambapo ni muendelezo wa somo la Kujikana ndani ya Kristo Yesu ambapo tuliona maana ya kujikana ndani ya Yesu kristo, Tuliona nani alikuwa mwanzilishi wa kujikana tangu asili ambaye ni mfano wetu wa kuigwa tuk**alizia na maeneo muhimu mawili ambayo mwamini anapaswa kuonyesha na kuthibitisha kuwa amejikana ndani ya kristo Yesu. K**a hujalisoma somo hilo naomba uende usome sehemu ya kwanza kwa kubonyeza hapa SEHEMU YA KWANZA.
Leo tutaanzia kwenye kipengele cha vipingamizi katika kujikana ndani ya Kristo Yesu.

4. VIPINGAMIZI KATIKA KUJIKANA KWA MWAMINI NDANI YA KRISTO YESU.
Tunapozungumza juu ya Vipingamizi tunaangalia juu ya mambo au vitu ambavyo vinaweza kuleta shida kwa mtu huyu ambaye anataka kujitoa kwa ajili ya kristo vinakuwa vinamrudisha nyuma licha ya yeye kutaka kusonga mbele kwenye kujitoa kwaajili ya Yesu wake aliye muaamini. Watu wamejikuta wanakumbana na vikwazo vingi sana vinavyowafanya washindwe kujidhabihu vizuri katika eneo la utumishi na Utakatifu na utaua.

Vikwazo hivyo ni k**a ifuatavyo
A). Upinzani wa ndani ya nyumba ya Mungu/kanisa
B). Upinzani wa nje ya nyumba ya Mungu/kanisa
C). Fedha
D). Msimamo wa kiuaminifu katika mahusiano baina ya jinsia mbili
E). Vyakula
F). Uelewa mdogo wa Mungu unayemuabudu
G). Vyeo vya kiuongozi

A. UPINZANI WA NDANI YA NYUMBA YA MUNGU/KANISA
Hivi vizuizi vinakuwa vinatokana na mazingira ya ndani kwenye nyumba ya Mungu ambayo yanamfanya huyu mtumishi wa Mungu ashindwe kuishi ule utayari wake wa kumtumikia Mungu ambapo ndio kujikana halisi kwa mwamini.

Mathayo 16:21-23
"Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu."

Ukiangalia hapo juu utaona Yesu alikuwa akikemewa na petro kwamba hata pitia mateso lakini Yesu hakumsikiliza Petro bali aliangalia mbele ili kutimiza kusudi lake lililomleta. Tulitegemea kwamba Petro asiwe kikwazo au kumvunja moyo Yesu kutimiza kusudi japo kwa akili ya kibinadamu ilikuwa ni ngumu sana kuelewa ule utumishi ambao ilitakiwa Yesu kuupitia. Hii ndio inatufanya hata nasi k**a waamini lazima tuelewe vizuri ni kwa namna gani Mungu ametuita ili tuweze kumtumikia na k**a tusipoelewa ndio tunajikuta sasa tunaishia kuvunjwa moyo na watu watu wa karibu au ndani ya nyumba ya Mungu.

Unaweza ukavunjwa moyo na watumishi wa Mungu mfano Mwalimu, mchungaji, mzee n.k lakini usiache kufanya kazi ya Mungu. Wewe hakikisha unamtazama kristo tu k**a kielelezo chako katika kumtumikia Yeye.

Kwa namna gani upinzani wa ndani unaweza kuwafanya waamini wakate tamaa??
1. Kuzuiliwa katika huduma na kiongozi wako wa kiroho; usiaangalie ni kwa namna gani kiongozi wako kakuambia au kukukataza kutumika kikubwa jihakikishe uhusiano wako na Mungu halafu uendelee kumuomba Mungu ili akupe namna ya kutumika.
2. Maisha ya dhambi kwa viongozi wa kiroho wanaosimama mbele ya madhabahu; watu wengi wanaosimama mbele ya madhabahu wamekuwa wakiwavunja moyo watumishi wengine kutumika kwa kuwa na maisha mabovu sana. Japo usimfanye mwanadamu akawa ni kielelezo chako kwenye kumtumikia Mungu maana wanadamu watakukatisha tamaa lakini wewe mtazame Yesu na umfuate na sio vinginevyo.
NOTE: HUU UPINZANI WENGI UNAWAINGIZA KWENYE MTEGO KWASABABU YA KUTO KUMUELEWA MUNGU WANAYEMTUMIKIA PAMOJA NA KUSUDI WALILOLIBEBA NDANI YAO.

B). UPINZANI WA NJE YA NYUMBA YA MUNGU/KANISA (WATU WASIO AMINI)
Hapo mwanzoni tumeona upinzani unaopatikana ndani ya nyumba ya Mungu na kumfanya huyu mtu akashindwa kujikana kwaajili ya kristo Yesu, lakini hapa tutaona mambo yanayoweza toka nje ya ya nyumba ya Mungu (wasio Waamini) na kumfanya huyu mtu akarudi nyuma.

Yohana 16:1-3
"Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi."

Yesu aliamua kuwaambia wanafunzi wake juu ya changamoto na upinzani watakao upata kutoka kwa watu wa dini ya kiyaudi ili kwamba wasije vunjika moyo hata siku moja. Na aliwaambia hivyo maana alijua wapo watakao fanya k**a kuwaua kabisa wakijua ya kwamba wanamtumikia Mungu lakini kiuhalisia hawako kumtumikia Mungu bali wanafanya kazi ya shetani.
Pale ambapo ukikutana na watu wanakupiga vita juu ya kumtumikia Mungu huko nje usije ukaacha kumtumikia Mungu hata siku moja wewe fanya kazi ya Mungu tu hata k**a mazingira ni magumu sana.
Kuna watu huwa wanakataliwa na ndugu na kutengwa na familia kabisa kisa wamemkubali Yesu, sasa hata k**a yakikutokea hayo jua tu kuwa ni upinzani wa nje unaotaka kukukwamisha usimuishie Mungu wako uliyekubali kujikataa kwaajili yake, Fanyauwezavyo usiingie katika huu mtego utakuwa salama sana yani.

Note: Watu wamekuwa na urafiki usiokuwa na mipaka kiasi kwamba hawawezi tena hata kuwaambia watu wengine juu ya utumishi wao walio nao. Kwahiyo watu wako wa nje na nyumba ya Mungu lazima uishi nao kwa kwa akili sana ili usije ukapoteza lengo la kuishi. Hakikisha maisha yako mwenyewe ni ushuhuda tosha kwa ajili ya kukurahisisha kuweza kuwahudumia wale walioko nje waujilie ule upendo wa Kristo Yesu.

C. FEDHA
Fedha na dhahabu vyote hivi ni mali ya Mungu mwenyewe (Hagai 2:8) hivi vyote Mungu amempa mwanadamu awe ni wakili juu yake kwahiyo hata kwenye matumizi yake yanahitaji neema ya Mungu sana ili mtu asitoke katika msingi wa Neno lake. Sasa katika kanisa letu la leo tumehama kabisa kutoka kwenye uwakili wa hizo mali tumepewa na Mungu kiasi kwamba tumechagua kuiweka mioyo yetu kwenye mali zetu kwa kuzipa kipaumbele kuliko hata kumpa Mungu nafasi ya kutuongoza. Hapa tunapewa maonyo na mtumishi wa Mungu juu ya fedha.

1 Timotheo 6:10 "Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi"

2 Timotheo 3:1-2 "Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi"

Sasa ukisoma hapo unaona ya kwamba kuwa na pesa sio kitu kibaya ila kuuhamishia moyo wako kwenye pesa na kuzipenda kunakuwa ni mzizi wa mambo mengi mabaya kuweza kutokea maana ukiwa katika hali hiyo unaweza kufanya jambo lolote pasipo hata kufikilia mara mbili juu ya madhara yanayoweza kutokea kwa maamuzi yako.

Ukiwa mtu wa kupenda sana fedha ni ngumu sana kumuabudu Bwana na ndio maana hata maandiko yanatuonyesha kuwepo kwa mabwana wawili ambao ni Fedha na Mungu ambapo haiwezekani ukavitumikia vyote kwahiyo lazima uchague kimoja cha kwenda nacho ndipo utakuwa salama.

Mathayo 6:24 "Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashik**ana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali."

Hii inatuonyesha namna pesa ilivyo na nguvu sana ya kuteka mioyo ya watu k**a hawataangalia na kukaa vizuri kwenye nafasi zao. Kwasababu ya fedha kuwa na nguvu ya kushika mioyo ya watu, watu wengi wametupilia mbali ule ujasiri wao na kujikana kwao kwaajili ya kristo Yesu wameanza kutafuta tu pesa. Watu wengi wameacha mambo ya ki Mungu kabisa mfano Kuhubiri injili, kuwepo kwenye makusanyiko ya ki imani wako busy na mambo ya kutafuta fedha na ndio maana ukienda makanisani siku za jumapili utakuta watu wengi sana lakini siku za katikati huwezi kuwakuta watu kwasababu wengi wao wako busy kutafuta pesa wameacha nafasi ya Mungu na hata ndani ya mioyo yao hawajihisi hata Hatia au kukosea kwakuwa fedha zimekuwa Bwana kwao. Mungu atusaidie sana kwenye eneo hili tusije kutekwa mazima tukapotea

NAMNA GANI FEDHA IMEKUWA KIKWAZO KWA WATU KWENYE KUJIKANA KWAAJILI YA KRISTO YESU??
1. Watumishi kuwashikilia watu wenye Fedha kwenye uongozi ingali wanafanya maovu; Hii imekuwa kikwazo sana maana wachungaji wengine wamejikuta wakilitukanisha jina la Mungu kwasababu hiyo maana wanakuwa wameyachagua matumbo yao badala ya kumchagua Mungu wa ibada za kweli.

2. Watu wanadanganya ili wapate fedha: Kitendo cha kukubali kudanganya na kupata fedha ni dhahiri kabisa kuwa umeuacha upendo wa Mungu na kuushika mwenendo usiokuonyesha kujitoa kwako kwa Mungu. Mfano Gehazi alikubali kudanganya ili apate fedha (2wafalme5:21-23).

3. Kuanguka kwenye zinaa (Uasherati na uzinzi) ili kupata fedha: Dunia ya leo imejaa Zinaa sana kiasi kila utakapopita kwenye mitandao ya kijamii mbalimbali masuala ya ngono yanapewa matangazo makubwa sana kiasi kinawafanya wengi kuanguka kwenye mtego kirahisi lakini wengine wanaingia huko ili wapate fedha ambapo ni jambo la kutisha sana tena sana.

4. Watumishi wengine wanatumia nguvu za giza kwenye huduma zao ili wapate washirika wengi lengo ikiwa ni kupata fedha kutoka kwao:

Wito wangu naomba usikubali fedha ikakutoa kwenye mpango wa Mungu aliokuitia hakikisha unaupa ufalme wa Mungu kipaumbele kwanza kabla ya hizo mali na uchumi unao utafuta na Mungu katika hayo atakuzidishia sana tena sana.

D. MAHUSIANO BAINA YA JINSIA MBILI TOFAUTI
Moja ya maeneo yamekuwa ni changamoto sana kwenye kizazi cha leo ambacho Mungu mwenyewe alikiita kizazi cha zinaa (Mathayo 12:36, 16:4) ni kuwa na uaminifu kwenye uhusiano wanao kuwa nao baina ya jinsi mbili yani mwanamke na mwanaume. Watu wengi wako makanisani lakini uasherati na uzinzi ni kitu cha kawaida sana kwao na wala hata hawaogopi kabisa wanaona tu ni kawaida yani wameizoelea neema ya Mungu kiasi kwamba hata wanapoonywa hawawezi kumtii Roho wa Mungu.

Mungu anataka watu wasiingie kwenye huu mtego wa zinaa kwa namna yeyote lazima wayajue mapenzi ya Mungu ndipo wataweza kushinda lasivyo wataanguka kwa mtego wa adui na ndio maana Suleiman anaseme kwenye Mithali mambo haya hapa

Mithali 6:25-26 "Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake. Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate;
Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani"

Mithali 5:15-20 (15-16) "Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu?

Baada ya Mungu kusema na vijana wasio na ndoa na kuwaonya juu ya kuwa na uaminifu kwenye eneo hili anasema pia juu ya wanandoa kubaki kwenye kiapo chao na kuwa waaminifu kwa kutokutoka nje ya ndoa zao (Kunywa maji ya birika lako mwenyewe) hii itakufanya kuwa mtu ambaye umejikana kikamilifu sana mbele za Mungu wako lakini isipokuwa hivyo utakuwa wewe haujajikana mbele za Mungu hata k**a unaingia nyumbani mwa Mungu".

Unaweza ukasoma maandiko haya kwa faida yako zaidi (1WAKORINTHO 6:9, WAGALATIA 6:7-8).

E. VYAKULA
Watu wanaweza wakashangaa kwa namna gani chakula kinaweza kikamfanya mtu akashibdwa kujikana vizuri mbele za Mungu!! Ila naomba fuatana nami, watu wengi huwa wanajikwaa sana katika eneo la chakula mfano akikosa chakula yuko tayari kumuacha Mungu wake ili alishibishe tumbo lake, wengine wametoa hata rushwa ili wapate chakula chao cha kila siku, wengine walifika wakamnung'unikia Mungu kwasababu ya kukosa chakula

Kutoka 16:2-3 "Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawanung’unikia Musa na Haruni, huko barani; wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa BWANA katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote."

Wana wa Israeli walikuwa wanafikiria chakula walichokiacha misri na kuacha kumtazama Mungu mpaka wakawa wanamlaumu Mungu kwanini aliwatoa misri wakasahau mateso waliyokuwa wanayapata mpaka wakawa wanamlilia Mungu. Kwahiyo kukosa chakula kusikufanye ukamkosea Mungu au ukamtukana Mungu wako hata siku moja bali chagua kumuheshimu Mungu wako.

Tumekuwa na masherehe mbalimbali kwenye kizazi chetu lazima uchague kumtukuza Mungu tu kwenye eneo hili, wengine wameingia kwenye mtego wa kushiriki hata vyakyula vilivyotolewa kwa sanamu/ vyakyula ambavyo vinaleta machukizo mbele za Mungu mfano Pombe n.k. lazima tujifunze kwa mtumishi wa Mungu Danieli namna alivyo azimia moyoni mwake na akapata kibali na kumtukuza Mungu wake kupitia hiloπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Danieli 1:8 "Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi."

F. UELEWA MDOGO WA MUNGU WAKO UNAYEMUABUDU
Moja ya msingi mkubwa wa upotovu kwa maisha ya mwamini ni uelewa mdogo juu ya Mungu wako, haiwezekani kujitoa kikamilifu hata siku moja kwa Mungu usiyemjua kikamilifu lasivyo utakuwa unapapasapapasa tu kitu kitakacho kupoteza kwenye ramani ya ki Mungu.

Kutoka 32:1-6(1)
Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.

Wana wa Israel walikuwa hawamjui Mungu wao ambaye amewatoa nchi ya utumwa bali walimjua M***a na ndio maana baada ya M***a kuchelewa waliamua kuchonga sanamu kitu kilicho mchukiza sana Mungu kwakuwa hawakumpa heshima aliyokuwa amestahili. Watu wengi hawamfahamu vizuri Mungu wanaye Muabudu na ndio maana wanaweza kufanya mambo ya ajabu ajabu tu mbele zake na wengi wapo kwa nyumba ya Mungu lakini hawawezi kujitoa kikamilifu mbele zake.

G. VYEO VYA KIUONGOZI
Kanisa Tulilo nalo kwasasa limekuwa na changamoto sana kwenye eneo hili yani wachungaji wamekuwa wakifanyiana hata mambo ya ajabu, washirika wamekuwa wanachafuana lengo ni kuweza kupata nafasi za kiuongozi kitu ambacho kimewapelekea wengine kutenda dhambi kitu kinachowafanya wawe hawajajitoa kikamilifu mbele za Mungu k**a ambavyo anataka Mungu wetu.
Herode alitaka kumuua Yesu kwasababu ya kuhofia kupoteza nafasi yake ya kiuongozi kitu kilicho mfanya akaamua kuangamiza watoto wote chini ya miaka miwili (MATHAYO2:1-18). Jambo k**a hili halifai kuonekana kabisa kwa mtu ambaye amekubali kumuamini Yesu kristo kwahiyo jifunze kuondoa wivu utakuwa salama. Ona hapa namna sauli pia alivyoharibikiwa.

1 Samweli 18:6-9 "Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake. Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme? Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile."

Ukisoma utaona namna Sauli alivyojaa wivu kwasababu ya kuutaka uongozi kiasi alikuwa tayari kumuua Daudi ili asiwe na mpinzani wa aina yeyote kwenye nafasi ya ufalme, Ndugu yangu usije ukaingia kwenye mtego wa kutaka kuwa kiongozi na ukamtukanisha Mungu wako kwakufanya mambo ya ajabu, Rizika na mahali Mungu amekuweka ukae na cheo alichokupa ili jina la Mungu litukuzwe na akuinue kwa wakati wake anaoona kwake unafaa kwako.

Mungu akubariki kwakuwa nami Sehemu hii ya pili ya mfululizo huu. Wa Somo letu hili Zuri, naomba usiache kufuatilia muendelezo wa sehemu ya tatu na ya mwisho kwenye somo letu hili, naamini utapata kitu cha kukupa hatua ya kiroho zaidi

Ulikuwa nami mpendwa na mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Namba: +255766944441
Email: [email protected]
Blog: jackobombwaga.blogspot.com

Address

KIMARA STOP OVER
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NENO La KWELI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to NENO La KWELI:

Share