El-Shaddai Christian Center

El-Shaddai Christian Center We exist to train believers to be Christ's ambassadors.

K**A WEWE NI KIJANA HII SI YAKUKOSA
28/03/2024

K**A WEWE NI KIJANA HII SI YAKUKOSA

Karibu ujifunze namna ya kuomba Mungu akushindie vita ya kubadilisha  kwa kubofya link hiii
21/02/2024

Karibu ujifunze namna ya kuomba Mungu akushindie vita ya kubadilisha kwa kubofya link hiii

Karibu katika ibada ya maombi ya Mfungo wa siku tatu za maombi ya Mungu kutushindia vita ya kubadilisha maisha

https://youtu.be/J46s2dIkgcA
18/02/2024

https://youtu.be/J46s2dIkgcA

Karibu katika ibada ya Ijumaa hapa ECC Mbezi Luis inayoongozwa na Mchungaji Kiongozi Reuben Njereka

Naisikia sauti na msisitizo mkubwa sana unaotangaza KUKUBALI NA KUAMUA KUANZA UPYA! Mungu ni Mungu wa mianzo mipya! Kuna...
26/11/2022

Naisikia sauti na msisitizo mkubwa sana unaotangaza KUKUBALI NA KUAMUA KUANZA UPYA! Mungu ni Mungu wa mianzo mipya! Kuna eneo umekaa muda mrefu mno. Na huwezi ukaenda kiwango na hatua nyingine mpaka UKUBALI KUANZA UPYA! Kuna BARAKA NA MIUZIJA HUPATIKANA ‘MTAA WA KUKUBALI NA KUAMUA KUANZA KWA UPYA’ TU.

Halafu kuna vitu huwaga haviwezi kutokea mpaka mtu AAMUE KUANZA UPYA!

Ungana nasi Jumapili hii-27/21/2022.

NOVEMBER Tarehe MPYA, Wiki mpya, mwezi MPYA; umezawadiwa tena na MUNGU wa Mbinguni! Wakati wote Mungu anapoleta siku, wi...
01/11/2022

NOVEMBER

Tarehe MPYA, Wiki mpya, mwezi MPYA; umezawadiwa tena na MUNGU wa Mbinguni! Wakati wote Mungu anapoleta siku, wiki au mwezi mpya anataka: -

1. Kukupa nafasi ya KUTENGENEZA NA KUJIWEKA SAWA MAHALI AMBAPO HAUKO SAWA. Unakuwa umepewa nafasi nyingine ya kurejea kwenye ushirika na MUNGU wako wa mbinguni ili UANZE KUISHI MAISHA YALIYOKUSUDIWA KWA AJILI YAKO kwa sababu kila mtu ana aina ya maisha ambayo aliandaliwa na MUNGU hata kabla yajazaliwa duniani!

2. UKAMILISHE KAZI ILIYO MBELE YAKO. Lengo la MUNGU ni kuhakikisha kila mtu anakalisha kazi yake aliyopewa na MUNGU wake. Mungu anataka kila mtu anapoondoka duniani awe amekamilisha “assignments” zake zote. Tunaongezewa siku kwa sababu bado HATUJAMALIZA KAZI ZETU! Tuna viporo vya kazi!

3. UPOKEE MUUJIZA WAKO! Kila siku, kila wiki, au mwezi huja vikiwa vimebebeshwa na zile baraka za majira husika KUTOKA KWA MUNGU! Kwa hiyo, kuna nyakati MUNGU hutupa siku, wiki, au mwezi kwa lengo la kutufikisha mahali pa miujiza yetu!

Nakuombea KUTIMIZA WAJIBU WAKO KIKAMILIFU NA KISHA UPOKEE BARAKA ZAKO ZOTE ZA NOVEMBER KWA JINA LA YESU!

24/12/2021

Unaposherekea Christmas hii jitahidi sana, usiishie katika kumwona Yesu katika hatua ya utoto wake, HIYO HAIWEZI KUKUSAIDIA!

Badala yake, toka hapo, safiri ukipita kwa speed mpaka mtaa wa useremala wake, ukifika hapo hamia mtaa wa utumishi wake ambao, “of course,” utakuwa na watu wanaoshuhudia miujiza na matendo yake ya kimbingu! Hata hivyo, USIISHIE HAPO! Kwa sababu wanaoshuhudia ni WAO SIYO WEWE!

So, tembea, kaza mwendo nenda NAYE mpaka msalabani, kisha KUFA NAYE kwa habari ya dhambi (mwone anateseka na kufa ili kukomesha nguvu ya dhambi ndani yako) na kisha fufuka naye kwa habari ya MAMBO YA KIUNGU!

Then, PAA Naye mpaka katika ulimwengu wa roho na kisha KETI NAYE huko huko! Bakia huko huko katika ukimwengu wa roho wa Kristo! Ili UISHI MAISHA DUNIANI KUTOKEA HUKO ULIKOKETISHWA NA KRISTO. Hakikisha LOLOTE UNALOLIFANYA HAPA UNALIFANYIA UKIWA UNAJIONA KULE PAMOJA NA KRISTO au ukiwa NDANI YA KRISTO NA KRISTO NDANI YAKO!

Usisahau KUWA UENYEJI WAKO BAADA YA KUOKOKA NI MBINGUNI!

Merry Christmas everybody!

Mtunzwe sana!

Mungu ni Mungu wa MIUJIZA! Ukiwa NDANI YAKE kwa njia ya KRISTO, UNA NJIA ZA KIUNGU ZA KUKUTIMILIZIA AHADI ZAKE na kukupa...
13/11/2020

Mungu ni Mungu wa MIUJIZA! Ukiwa NDANI YAKE kwa njia ya KRISTO, UNA NJIA ZA KIUNGU ZA KUKUTIMILIZIA AHADI ZAKE na kukupatia mahitaji yako hata mahali ambapo njia tegemewa za kibinadamu zimeshindwa!

Huwezi ukawa na YESU NDANI YAKO, kisha ukafurahia mwanadamu mwenzako kupitia mateso! Wokovu wetu ni WA KULIA NA WANAOLIA...
10/11/2020

Huwezi ukawa na YESU NDANI YAKO, kisha ukafurahia mwanadamu mwenzako kupitia mateso! Wokovu wetu ni WA KULIA NA WANAOLIA! Ukishindwa kuona na kuguswa na mateso na dhiki ya mwanadamu mwezako, basi ujue MUNGU ALIYE PENDO na wa HURUMA HAKAI NDANI YAKO.

KATAA KUZAMAKuna vitu katika maisha havimwachiagi mtu mpaka aamue kuvikataa! Kuna nguvu ya ajabu sana katika kukataa yal...
23/09/2020

KATAA KUZAMA

Kuna vitu katika maisha havimwachiagi mtu mpaka aamue kuvikataa! Kuna nguvu ya ajabu sana katika kukataa yale yasiyopatana na Neno la Mungu! Chochote unachojua siyo fungu lako kwa mujibu wa neno la Mungu unapaswa kukikataa!

Jumapili ya wiki hii tutahitimisha kwa maombi na maombezi somo la KUKATAA KUZAMA! Ni kujua mbinu za ushindi na kukataa KUZAMA ndo kutakuokoa na kuishiwa, mateso ya adui Shetani, ukame, dhambi, kufilisika, kupoa kiroho, magonjwa na yote YASIYO FUNGU LAKO!

Ukijihurumia hushindi! Ukideka hushindi! Ukisusa hutoboi! Ukienda kawaida imekula kwako! Ukilala unazama! Ukileta story huvuki! Ukijipendekeza kwa shetani na mawakala wake ili wasikuonee, ndo unazama mazima! Dawa? Ni kuchukua mbinu za ushindi na KUKATAA KUZAMA KWA NGUVU ZAKO ZOTE!

KUTOKEZA LAZIMA! Karibu Jumapili hii!

Ni KESHO! Ndani ya ECC!
06/07/2019

Ni KESHO! Ndani ya ECC!

Address

P. O. BOX 53634
Dar Es Salaam
255

Telephone

255714514363

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when El-Shaddai Christian Center posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share