23/07/2016
Bwana Yesu asifiwe.
Tafakari ya leo Zaburi 37: 23-24
"Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA,
Naye aipenda njia yake.
Ajapojikwaa hata anguka chini,
BWANA humshika mkono na kumtegemeza.
Mengi magumu hupitia katika maisha yetu,lakini Mungu hutuimarisha zaidi na zaidi. Katika kila hatua tunayopiga fikiria ulikuwa mtoto mchanga mwenye kulishwa chakula na leo umekuwa k**a ulivyo. Ni hatua ngapi umepitia amini bila Mungu usingalikuwa ulivyo, Mungu ni mwaminifu usijali changamoto unazopitia jua Mungu anakuimarisha kwa kusudi lake.
Usiogope jipe moyo ni siku mpya nawe upate kibali mbele za Mungu katika yote uyatendayo kwa Jina la YESU.
Kuwa na maandalizi mazuri ya ibada ya kesho na karibu sana Kijitonyama lutheran church, tutahudumu ibada ya kwanza. Njoo tumsifu na kumwabudu Mungu pamoja.
Amen.