Free Jesus Gospel

Free Jesus Gospel Free Gospel for all Nation Free Jesus Gospel For All Nation

MAVAZI? SURUALI? SKETI? 😀😀Biblia inafundisha kuvaa kwa kujisitiri na kwa heshima.. (modest dressing) wala haifundishi va...
15/09/2024

MAVAZI? SURUALI? SKETI? 😀😀

Biblia inafundisha kuvaa kwa kujisitiri na kwa heshima.. (modest dressing) wala haifundishi vazi gani livaliwe.

Kujisitiri ni swala la utamaduni..
Tafsiri ya kujisitiri kwa wamasai na Wachaga hazifanani. Kwa Wahadzabe na Wahaya hazifanani. Kwa wazungu na Waafrika hazifanani.

Kwa waafrika wengine kutoa "maziwa" na kumnyonyesha mtoto kwenye daladala ni jambo la kawaida... kwa wazungu ni "taboo" ni jambo la aibu sana. Lakini kibongobongo mtu anatoa "maziwa" yake kwenye daladala na kumnyonyesha mtoto na hakuna kinyaa wala mtu anawaza ujinga.. tunaona tu mtoto anapata dinner yake.

Lakini nchi za Magharibi hiyo ni issue kubwa.
Ndiyo maana ni ngumu kuona filamu za kizungu wanaonyesha mtoto anaponyonya waziwazi. Ni jambo la kukosesha heshima kabisa... lakini watu hao hao watavaa "bikini" na kujisambaza bustanini wakati wa "summer".. au kiangazi..

Na bado asilimia ya ubakaji (r**e) ikawa kidogo kuliko wale wanaojifunika "gubigubi"... hii isiwe tabu sana.. tuendelee..

Kile ambacho mmasai anaita nguo ya heshima sicho anachokiita mnyakyusa.

Tafsiri ya kujisitiri pia inategemea umbo la mtu..
Usipigilie mavazi mpaka kila mtu anatokwa na mate mdomoni. Unatafuta nini?
😀

Mtu mmoja kwa speed atanukuu 👉🏽Kumbukumbu la Torati 22:5
[5]Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.
Hapa kuna ugonjwa mkubwa wa kunyofoa mistari nje ya muktadha ili mtu alazimishe iseme kile anataka.. NI UOVU WA KIWANGO CHA PhD..

Lakini mtu huyo hatasoma Mistari inayofuata k**a ataweza kuyatendea kazi.

Okay hii hapa vipi? Kumbukumbu la Torati 22:9
[9]Usipande shamba lako la mizabibu aina mbili za mbegu; yasije yakaondolewa matunda yote, mbegu ulizopanda na maongeo ya mizabibu yako.

Unafanyia kazi?

Unachanganya mazao shambani? Unafanya "mixed cropping"?

Vipi kuhusu hii?

Kumbukumbu la Torati 22:10
[10]Usilime kwa ng’ombe na punda wakikokota jembe pamoja.

Hapa kwenye kuchanganya nguo na vishada?
Kumbukumbu la Torati 22:11-12
[11]Usivae nguo iliyochanganyikana sufu na kitani pamoja.
[12]Ujifanyizie vishada katika pembe nne za mavazi yako ya kujifunika.

Hapa wote tungevaa makanzu tu hahaha.

Nimechukua tu baadhi ila watu wanapenda sana kukazia mstari wa 5 ila sura ya 22 yote wanajua hawawezi kutendea kazi.
Ili uweze kutendea kazi inabidi mambo yafuatayo.
1. Aina za sheria za Musa.
2. Lengo la sheria za Musa.

Usipojua utapata tabu sana.

Wakati Musa anawapa sheria hii.. hawakuwa na sketi na suruali k**a mavazi yao rasmi.
Nguo zao ni makanzu au jamii ya nguo za kufunika juu mpaka chini. Ni rahisi kabisa mwanamke kujivalia vazi la mwanaume. Siku hizi kuna mbwembwe zimewekwa kutofautisha.. lakini ilikuwa ngumu kuzitofautisha. Kiasi kwamba mwanaume akichukua nguo za mwanamke (akiwa kwenye siku zake) anakuwa NAJISI.. akaingia nayo kwenye HEMA YA KUKUTANIA ujue anaenda kufa. 😀
Njia rahisi ya kuwasaidia.. WASIVALIANE.

Leo ukienda umasaini.. Rubega ya k**e na ya kiume haipo..

Huo mstari wa Kumb 22:5 utautumiaje?

Maana kinachotofautisha ya "kiume" na ya "k**e" siyo mavazi.. bali namna atakavyofunga hiyo rubega (nguo iko k**a shuka tu).

Vipi kuhusu suruali kutajwa kwenye Biblia.. Oh ipo na imetajwa kwenye Biblia ya Kiswahili Standard Union Version mara 7 kwenye Agano la Kale.. tena kitabu cha KUTOKA, MAMBO YA WALAWI, EZEKIELI na DANIELI.

Maelezo ya nguo hiyo yako.. kwenye Kutoka peke yake na ilikuwa spesho kwa haruni..

Angalia.. Kutoka 28:42
[42]Nawe wafanyie SURUALI za nguo ya kitani, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani;
And thou shalt make them linen BREECHES to cover their nakedness; from the loins even unto the thighs they shall reach:
HIZI NI NGUO ZA KUTOKA KUNONI HADI MAPAJANI.. Actually ni nguo ya ndani ya KUHANI MKUU (enzi hizo Haruni). Haruni akivaa mavazi ya KIKUHANI nguo hiyo haionekani. 😀😀
Inakuwa UNDERWEAR.. (Picha na maelezo ninazo)..

Hili vazi "BREECHES" kwa lugha ya siku hizi ni suruali fulani wanavaa watu wanaopanda farasi ambapo wanakuwa wamevaa viatu fulani vinakuja mpaka magotini.

Google: breeches.

Sasa mavazi ni jambo la utamaduni..
NCHI YA FIJI, Raisi na Waziri mkuu anavaa sketi inaitwa KILN.. tena kwenye sherehe maalumu anatokeza na sketi.. 😀 baadhi ya nchi askari wanavaa sketi k**a baadhi ya askari Scotland..
Askari wa Kirumi walikuwa wanavaa nini? 🤷🏽‍♂️

Ukiacha kufikiri kidini na kimapokeo hili jambo.

Sasa k**a kwenu suruali inawakwaza... katazeni tu lakini acheni kusema Biblia imesema..😎 SEMA HAYA NI MAPOKEO YETU na watu wenu WATAYAPOKEA k**a mapokeo yenu ikiwa ni lazima kufanya hivyo na k**a kuna sababu za msingi..

The bottomline is...
VAA, PENDEZA, HESHIMIKA KULINGANA NA MAZINGIRA YAKO.

Katika mazingira yako yote... LENGA KUMTUKUZA BABA YETU (MUNGU) NA KUHAKIKISHA HAUWI KWAZO LA INJILI KWENYE MAZINGIRA HAYO..
Nikienda umasaini na hawawezi kupokea Injili nikiwa nimevaa suruali.. nitavaa nguo zao.

Anyway. Wakati tunabishana juu ya suruali na sketi kuna ndugu (WAMISIONARI) wako mbigani huko wamevua nguo zao.. wamevaa majani na kufunika sehemu fulani tu ili wahubiri Injili... maana kuna makabila huwezi kuwafikia huko porini ukiwa na sketi au suruali..

Nimepita tu!.

Ap Shemeji Melayeki
Global Family Gatherings
"God's Standards"

SITETEI SURUALI KWA MABINTI SITETEI SKETI FUPI WALA SKIN TIGHT SITETEI MAPAJA KUWA NJE AU MATITI KUWA WAZI SITETEI MIPAS...
12/07/2024

SITETEI SURUALI KWA MABINTI
SITETEI SKETI FUPI WALA SKIN TIGHT
SITETEI MAPAJA KUWA NJE AU MATITI KUWA WAZI
SITETEI MIPASUO KWA MABINTI HASA WA MAKANISA

ILA
Nasema na wewe kijana au Mtumishi ambaye ukiona hayo mapaja unadata

✍️Moja ya kitu kinadhihirisha kuwa haujaokoka ni kuona kivutio Cha dhambi alafu ukashake kiroho au kikakupa shida

Hii imekuwa tatizo sana kwa makanisa ya sasa
Vijana wengi na watumishi wengi pamoja na wababa wamekuwa wakijificha na dhambi Yao ya tamaa kwa kigezo Cha mavazi ya dada zetu
🔸Sikiliza wewe
Wewe ni mzinzi tu k**a wazinzi wengine
Mtu aliyeokoka hatikiswi na kivutio Cha dhambi
K**a ukiwa kanisani unashake inakuwaje unapokuwa nje ya kanisa na uko peke yako

✍️“Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana?”
— Ayubu 31:1 (Biblia Takatifu)

Maana yake Ayubu hapa alikuwa anazungumza kwa Habari ya kumtazama mwanamke jinsi alivyo na kumtamani

Anasema yeye aliweka agano na macho yake hawezi kumtazama msichana bila kujali ana kimini au hana

Mtu aliyeokoka anaichukia dhambi ila anawahurumia inayowatesa
Hivyo huwaombea au kuwapelekea habari za Yesu Kristo au habari za ukombozi

K**a hujashinda tamaa yako Huwezi kuingia mbinguni

Na shetani amekuwekea mtego hapo
Kila ukiangalia unakwepesha macho na kuwaza
"Hivi huyu dada hajui anatuharibia ibada watu wengine"

Wewe na nani mzinzi mkubwa wewe sema unaniharibia ibada
Maana nimekuja kupunguza Dhambi yangu ya tamaa hapa

Na kwa taarifa yako tu Huwezi ingia mbinguni na tamaa zako

“WENYE MACHO YAJAAYO UZINZI, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;”
— 2 Petro 2:14 (Biblia Takatifu)

“Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye KUTAMANI au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.”
— 1 Wakorintho 5:11 (Biblia Takatifu

Zingatia usishake kwasababu ya mwanamke kavaaje
Omba Mungu akupe misuli na uimara rohoni ili ushinde tamaa

SITETEI NGUO ZA HOVYO MAKANISANI
Ila ikitokea ndio wapo sasa itakuwaje maana yake sket za watu zitakunyima mbingu!?

Shtuka wewe
Shida sio hizo skin shida ni wewe baba

UMEBARIKIWA SANA NA BWANA

By Pst Elias Jonh

Free Jesus Gospel

MTU MMOJA ALISEMA "WALIOOKOKA WANAKUWA MASIKINI KWASABABU WANAFANYA MAOMBI BADALA YA KUTUMIA AKILI"Nililazimika kujibu k...
04/07/2024

MTU MMOJA ALISEMA "WALIOOKOKA WANAKUWA MASIKINI KWASABABU WANAFANYA MAOMBI BADALA YA KUTUMIA AKILI"

Nililazimika kujibu kwa namna nyepesi ambayo na yeye anaweza kuelewa, unaweza kujifunza pia;

[ SASA NAOMBA MWENYE AKILI ASOME HII YOTE......]

Kuhusu kauli ya "TUACHANE NA MAOMBI TUTUMIE AKILI"

■Kwanza,Maombi sio mbadala ya kutokutumia akili aliyotupa Mungu k**a ambavyo Kutumia akili sio mbadala wa kutokuomba.(maombi).

Akili ya mwanadamu pekee haitoshi ndiyo maana neno la Mungu limetutaka "tusizitegemee akili zetu pekee"

"Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,
Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;" Mithali 3:5

•Pia,zaidi ni kwamba watu wanaomtegemea Mungu na wanakaa kwenye Neno la Mungu na Kuomba ni watu wenye akili nyingi na ya juu zaidi kuliko mtu anayefikiri akili yake pekee inatosha na haitaji kuomba.

"Anakuwa tu "mjinga" anayejiona ana "akili" kumbe ni mjinga asiyejijua kwasababu ujinga umepufusha macho yake!

■John Knox alikuwa mtumishi wa Mungu huko Scotland,mwanatheolojia wa matengenezo, msomi na mwandishi ambaye alikuwa kiongozi wa Matengenezo ya nchi. Alikuwa mwanzilishi wa Kanisa la Presbyterian la Scotland. (Hakuwa mwafrika huyu na Bado alikwa mwombaji"

Kiasi kwamba ,MATOKEO ya MAOMBI yake yalimfanya Malkia Mary wa Scotland kusema "kwamba aliogopa maombi ya John Knox zaidi ya kuogopa majeshi yote ya Scotland."

■ John Wesley aliomba, na uamsho ukaja Uingereza (sio Afrika), na kuliepusha taifa hilo na maovu ya Mapinduzi ya Ufaransa.

■ Jonathan Edwards aliomba, na uamsho ukaenea katika makoloni yote ya Marekani. Historia imebadilishwa muda baada ya muda kwa sababu ya maombi.

Hawa wote niliowataja hawatoki kwa khoikhoi au Hadzabe, ni Wazungu wa Uingereza na waliomba! Walijua Nguvu ya Maombi! Usifikirie kwamba Ni Afrika tu ndiyo "WANAOMBA"

■K**a haujui Maombi ni nini unaweza "kupuuza neno maombi" lakini sio "maombi", Ni kwasababu Lugha haina maneno yakutosha kutaja "Maombi" !

Maombi kwetu tu kulia lia k**a wengi wanavyofikiri, sio kulalamika njaa , ni zaidi ya kupeleka mahitaji, ni mazungumzo yetu na Mungu! Yaani tukiomba ni sawa na tumekaa kikao na Mungu aliyeumba Mbingu na Nchi! Tunaongea naye!! Wewe mwenye akili umewahi kukaa hata jopo la wanasanyansi? Pengine umewahi, hongera ! Ila umewahi kukaa ukaongea na Mungu? Hautawahi mpaka ujue umuhimu wa Maombi!

■WANAOMJUA MUNGU,WANAOMBA NA WANAAKILI NYINGI!

Maandiko yanasema "Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote." 2 Timotheo 2:7
"Insight and understanding in everything"

Ndani ya Kristo Tunaakili Nyingi sio tu kwa mambo ya rohoni bali katika mambo yote! Tuna hekima iliyotukuka kuliko hekima yeyote ile!

■NJOO AFRIKA BASI Tuone k**a Maombi ni Ujinga,
Mtumishi wa Mungu, Mchungaji Enock Adeboye kutoka nchini Nigeria , huyu ni Baba wa wengi katika Kristo, ni mwombaji na mhubiri wa utakatifu.

Anaweza kutumia hata masaa 12,

Hata hivyo, amesoma na Elimu ya juu ambayo "haijamfanya adharau Kuomba" Alipata Shahada ya Kwanza katika Hisabati kutoka Chuo Kikuu cha Ife, Nigeria mwaka wa 1967 l.

Alipata Shahada ya Uzamili katika Hydrodynamics kutoka Chuo Kikuu cha Lagos, Nigeria mwaka wa 1969 Desemba 18, 1998, alipoandaa Kongamano la kwanza kabisa la Holy Ghost Congress (mkutano wa wazi) huko Lekki, Lagos, Nigeria na mahudhurio ya zaidi ya watu milioni 7 k**a ilivyoripotiwa na CNN na BBC.

Inajumuisha uhamasishaji mkubwa zaidi wa watu katika sehemu moja juu ya uso wa dunia, jambo ambalo halijawahi kurekodiwa.

[Sijajua wasioomba wanotumia Akili wameripotiwa nini na CNN au BCC?]

■Nenda katafute habari za Folorunsho Alakija , Mwanamama TAJIRI SANA nchini Nigeria, ambaye alitajwa na FORBES mwaka 2020 k**a mwanamke tajiri sana na Bilionea kwa Nigeria na wa pili kwa Afrika nzima,

Huyu mwana mama pamoja na umaarufu alionao, utajiri alio nao, huwa anaingia mtaani "kuhubiri injili na kuleta watu kwa Yesu"

Pamoja na kutoa sadaka , kusapoti yatima, wajane na maskini, lakini bado anafanya kazi ya kuhubiri injili na kuleta watu kwa Yesu.Anaandaa makusanyiko ya maombi ya wanawake.

•Wewe ni maarufu kiasi gani ? Wewe ni Bilionea wa net worth ya dolar kiasi gani? Hata Usiombe? Hata Upuuze habari za Yesu Kristo?

Mungu aturehemu!

■Kupitia haya MAOMBI kuna Wasomi madaktari ambao kwa Udaktari walishindwa kushinda Zinaa! Walishindwa kutoka kwenye ulevi uliopindukia! Kitaalumu walijua madhara ya ulevi, lakini "elimu na taaluma yao haikuweza kuwasaidia"

Hizi sio hadhithi! Ni shuhuda tulizonazo kwenye huduma hii, kwa maombi na mafundisho ya Neno haya haya!

Maprofesa wanaponea huku!
Wasomi wa dunia wanaponea huku!

Maombi sio ya waafrika au Wazungu tu , ni ya watu wote wanaomjua Mungu!

●Watu wanaomba na Bado wanafanya kazi pia! Sio kwamba tunaomba halafu tunakuwa "omba omba"

●Kwenye makanisa yenu tuna wasomi wa elimu ya Duniani! Tuna waalimu! Tuna ma-engineer! Tuna viongozi wa serikali! Tuna wakufunzi wa vyuo vikuu! Tuna madaktari! Tuna wafanya biashara! Na bado TUNAOMBA! NA WAO WANAFUNGA NA KUOMBA!

●Hata sisi wachungaji tumesoma Hiyo elimu ya duniani, hatujivunii! Tunajivunia kwamba tumempata Kristo Yesu! Tunazo biashara ! Tunazo kampuni! Tunafanya kazi! Na bado TUNAOMBA!!!

"Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa." Luka 18:1

"Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;" 1 Timotheo 2:1

USIACHE KUOMBA!

Free Jesus Gospel
"Neema ya Mungu Inatutosha"

Prophet AllenGrace
RGG Ministries International

Haki sawa ni mfumo wa kishetani 😬😬K**a wanawake tusiposimama kumuinua, kumlinda, na kumtetea mwanaume tunaua kizazi hiki...
30/06/2024

Haki sawa ni mfumo wa kishetani 😬😬

K**a wanawake tusiposimama kumuinua, kumlinda, na kumtetea mwanaume tunaua kizazi hiki😭 mwanaume yeyote ni mfalme, vyovyote alivyo mwanaume ndani yake ana ufalme, lakini huu ufalme ili ufanye kazi au uonekene lazima awepo mwanamke atakaye msapoti

Naomba wanawake tuondoke kwenye viti vya wanaume,tuwapishe wanaume wakae kwenye viti vya KIFALME

Tunaendelea na kungamano hapa Tabata ..

Free Jesus Gospel

Mtumishi Leah Ndabila

MAMBO 10 AMBAYO YASIPOJADILIWA WAKATI WA UCHUMBA LAZIMA NDOA IWE NA MIGOGORO ISiYOISHA1. MTAISHI WAPI BAADA YA NDOA? Kwa...
27/06/2024

MAMBO 10 AMBAYO YASIPOJADILIWA WAKATI WA UCHUMBA LAZIMA NDOA IWE NA MIGOGORO ISiYOISHA

1. MTAISHI WAPI BAADA YA NDOA?
Kwao? Kwenu? Kwako? Mtapanga nyumba ? Ya aina gani na wapi?

2. JE MTAKUWA NA WATOTO BAADA TU NDOA AU MTASUBIRI KWANZA?
Mngependa kuwa na watoto wangapi k**a Mungu atawajalia? Na k**a mtasubiri je mtatumia njia gani za uzazi wa mpango?

3. NANI ATALIPA BILI MBALIMBALI
Nani atalipa kodi ya nyumba kati yenu je mke, mume au mtachanga nusu kwa nusu? Chakula nani atanunua? Ada za shule, Luku, bili za hospitali na gharama zingine nani atalipa? Je mshahara mtaweka mezani mpange matumizi pamoja au kila mtu atakuwa ananunua k**a anavyojisikia?

4. KUNA NDUGU YOYOTE MTAISHI NAYE MARA BAADA YA KUFUNGA NDOA?
Jadilini nani na nani watakaa na ninyi mtakapotoka honeymoon na kuanza maisha yenu mapya, kwanini na kwa muda gani watakaa nanyi? Ukiachana na hao watakaokaa kwenu ni ndugu gani wengine wa kuwasaidia wakiwa huko huko walipo? Wekeni mkakati unaoleweka k**a kuna wa kulipiwa ada, mkakati wa kutunza wazazi n.k.

5. JE, MKE ATAFANYA KAZI AU ATAKAA NYUMBANI?
Kuna wanaume hawapendi wake zao wafanye kazi za kuajiriwa au biashara. Hayo myaongee na kukubaliana wakati wa uchumba sio umemkuta dada wa watu na kazi yake unaanza kumwambia akae nyumbani sababu ya wivu wako.
Na wale wenye kazi za utata mfano unaingia shifti za usiku au mfano msanii unaigiza na wake au waume za watu, kazi yako itafanya muda mwingi uwe mbali na familia, n.k ambianeni mapemaaaa.

6. UNA MAONO GANI?
Una maono yoyote makubwa ambayo mbeleni yatahitaji sapoti ya mwenzi wako jaribu kulisema mapema ikiwezekana.

7. KILA MWEZI MTAWEKA AKIBA ASILIMIA NGAPI YA MAPATO YENU?
Mkishaonana lazima muweke akiba kwa ajili ya maendeleo ya familia na dharula mbalimbali. Je itakuwa asilimia ngapi ya mapato.yenu? Je mtakuwa na akaunti ya pamoja au kila mtu na akaunti yake? Jadilini

8. MTAABUDU WAPI?
Je mtaabudu anapoabudu mume? Au anapoabudu mke? Mtahama dhehebu au mtaabudu wapi? Ongeeni mapema.

9. WEWE NI NANI?
Jieleze undani wako. Wewe ni nani hasa? Una mapungufu yoyote ya kimaumbile sema mapema. Una watoto usimfiche mwenzio. Una historia ambayo mwenzi wako akiiisikia baadae itaathiri mahusiano yenu? Mwambie. Kuna jambo lolote kwako au kwenye familia yenu ambalo linaweza kuathiri ndoa yenu sema mapema.

Free Jesus Gospel

10..........? ONGEZA

Cc:
Daudi Richard

FUNGU LA KUMIKUTOA NI MUHIMU SANA ILA SIO KWA KULAZIMISHWA AU KWA KUTISHIWA. UKIMPENDA MUNGU HUTAHUBIRIWA KUTOA ILA UTAK...
19/06/2024

FUNGU LA KUMI

KUTOA NI MUHIMU SANA ILA SIO KWA KULAZIMISHWA AU KWA KUTISHIWA.

UKIMPENDA MUNGU HUTAHUBIRIWA KUTOA ILA UTAKUA UNATOA MWENYEWE. NA UKIONA UNATOA ALAFU HAUPATI MATOKEO YA UTOAJI WAKO MAANA YAKE NI KWAMBA KUNA MAMBO HAYAKO SAWA.
1. MADHABAHU UNAYO TOLEA SIO SAHIHI
2. UNATOA KWA LENGO LA KUPATA NA SIO KWA UPENDO
3. UMETOA KWASABABU UMEONA ALIE TOA AMEBARIKIWA NA WEWE HUNA UPENDO NA MUNGU ILA NI K**A UNA MHONGA MUNGU.
MAISHA YAKO HAYANA UTAKATIFU NDANI NA BADALA YA KUWA MTAKATIFU UPATE BARAKA ZA UTAKATIFU WEWE UMEKIMBILIA KUTOA KWASABABU ULIAMBIWA TOA UPATE.

4. SWALA LA KUTOA NI SWALA LA UPENDO NA SIO SHERIA KILA ANAYE MPENDA MUNGU LAZMA ATATOA NA HATAISHIA FUNGU LA KUMI ATATOA NA ZAIDI.

NB. TUWAFUNDISHE WATU KUMPENDA MUNGU KISHA WAO WATAIFANYA KAZI YAKE KWA FEDHA ZAO WENYEWE.

NITAWAJIA TENA NA SOMO TIMILIFU.

Free Jesus Gospel

Nabii Denis Tanzania 🇹🇿
Call 0747-807523
WhatsApp 0655 548 679

SOMA USHUHUDA HUU MPAKA MWISHO ...Akiwa kwenye huduma ya siku 10 nchini Marekani Askofu Benson idahosa, ikamfikia taarif...
16/06/2024

SOMA USHUHUDA HUU MPAKA MWISHO ...

Akiwa kwenye huduma ya siku 10 nchini Marekani Askofu Benson idahosa, ikamfikia taarifa kwamba mama yake kafariki. Yeye alichowajibu ni kwamba hapana mama hajafariki, wakamsisitiza kwamba ni kweli kafariki maana majibu ya madaktari yametoka hivyo na hana pumzi hata kidogo.... Benny akawaambia Mungu na kumwambia k**a atamchukua mamaye, kwasababu hiyo haikubali hata kidogo, akawaambia wafungue mlango wa chumba chake (maana mama alikuwa anakaa kwa mwanaye) akawaambia waulaze mwili wake kitandani pake.

Wale ndugu wakamuuliza kwani yeye anarudi lini? Akawaambia siku 10 mbele, wakasema sasa haoni k**a mwili utaharibika na kunuka sana? Akawajibu "hicho ni chumba changu hata k**a akinuka ni chumba changu nyie muwekeni humo kitandani pangu"

Basi wakamuweka humo ndani.... Muujiza wa kwanza ni kwamba mwili wa mama Benny kwa siku zote hizo 10 ulibadilika na kuwa wa kijivu yaani k**a majivu rangi inayoonekana kwa maiti ya siku nyingi... Ila haukuwahi kutoa harufu wala kuharibika.

Free Jesus Gospel

Siku ile anaporudi benson wakampokea Airport, alipofika nyumbani akaongoza moja kwa moja chumbani ulimo mwili wa mama, akiwa mlangoni akamwita "Mama naomba nipe maji ya kunywa" Mama akaitika na kusema haya njoo... Akafungua mlango na kumkuta mama kaamka kitandani.

Benson idahosa alifufua maiti nyingi na huyu mama ni mmojawapo tu wa wale waliofufuliwa.

Kwa kusema haya, chochote kilichokufa maishani mwako Bwana akakifufue kwa jina lake Amen!

GHARAMA UNAYOLIPA1. Inaamua UMBALI utakaokwenda kwenye jambo unalofanya au kimaishaAnayelipa shilingi mia tano kwenye ba...
11/06/2024

GHARAMA UNAYOLIPA

1. Inaamua UMBALI utakaokwenda kwenye jambo unalofanya au kimaisha

Anayelipa shilingi mia tano kwenye bajaj au daladala anakwenda tu vituo kadhaa mbele, anayelipa 16,000 anaelekea Mkoa mwingine jirani, anayelipa zaidi anaelekea zaidi!
KUKWEPA KULIPA GHARAMA NI KUAMUA KUISHIA NJIANI NA KUTOKWENDA MBALI

2. Inaamua KASI utakayokwenda nayo kuelekea unakokwenda kwenye jambo ufanyalo kwenye maisha,

Anayelipa 75,000 kuelekea Mwanza kutokea Dar Es Salaam kwa basi la abiria atatumia masaa 18, na mtu mwingine akilipa laki kadhaa kwenye ndege atatumia saa 1 tu kuwa Mwanza!
Mmoja AMEKWEPA GHARAMA KUBWA katumia muda mrefu, mmoja AMELIPA GHARAMA KUBWA katumia muda mfupi zaidi kufika eneo lile lile!

3. Inaamua UHAKIKA WA KUFIKA au kutofika kwa mhusika anapokwenda au kuishia njiani

Aliyepanda basi na kulipa nauli kiduchu kuelekea Mwanza, akifika Dodoma akachoka kukaa na mgongo unamuuma anaweza kughairisha safari na kushukia njiani, LAKINI aliyelipa nauli ya ndege hata angetamani kushuka na ndege nzima yeye ni abiria pekee HAIWEZEKANI lazima afikishwe mwisho wa safari kwanza!

Kwenye huduma hautakuwa zaidi ya gharama unazolipa sirini na wazi,

Kwenye biashara hautakuwa zaidi ya gharama unazolipa,

Kwenye ndoa na familia hautakuwa na ndoa au familia zaidi ya gharama unazolipa,

MAISHA YA MTU YATAKUWA BORA AU OVYO KUTEGEMEA NA UTAYARI WAKE KULIPA GHARAMA,

Free Jesus Gospel

Askofu Dickson Cornel Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI
11.06.2024

11/06/2024

MWANAUME NI NANI KATIKA JAMII?

o Mwanaume ni kiongozi wa familia

o Mwanaume ni mlinzi wa mwanamke pamoja na familia

o Mwanaume ni mfano wa kuigwa na jamii

o Mwanaume ni mrithi wa Mungu

MWANAUME MWENYE ASILI YA MUNGU (MWENYE MAADILI MAZURI)

o Ni mnyenyekevu wakati wote

o Ni mvumilivu wakati wote

o Yupo tayari kusuluhisha kesi yake na kuanza upya

o Ni mwepesi kusamehe na kusahau

o Ni mtu mwenye utu na anathamini utu wa mtu

o Anajali watoto na mke wake pia

o Hatak**a atakuwa si muaminifu hujitahidi sana mke wake asijue

MWANAUME MWENYE ASILI YA DUNIA (ASIYE NA MAADILI MAZURI)

o Ni mkorofi kupindukia

o Hana utu wala kujali

o Ni mtu wa lawama wakati wote

o Hana hofu kwa chochote anachokifanya

o Huhesabu makosa wakati wote

o Hana maneno ya faraja kila wakati hulaani tu

o Hana moyo wa kusamehe, siyo rahisi kesi yake imalizike kwa amani

v Kundi la kwanza linamtambulisha mwanaume mwenye anayefuata muongozo mzuri wa malezi kutoka kwa wazazi wake na pia sheria za dini ambazo zinamuandaa kuwa mwanaume mwenye majukumu ya mke na familia. Hivyo anapokutana na mwanamke asiye na maadili inamuwia vigumu sana kumbadilisha tabia na k**a Mungu asipoingilia kati mahusiano haya kunaweza kumfanya mwanaume huyu asitamani tena kuoa au kuwa katika mahusiano maana huwaza kupenda na endapo atapata mwanamke mwenye maadili ndoa yao itakuwa nzuri sana kutokana na asili yao.

v Kundi la pili linamtambulisha mwanaume asiye na malezi na asiye jua nini wajibu wake k**a mwanaume. Mwanaume huyu anakuwa katika hali k**a hii endapo kwa upande mmoja wazazi wake walichangia katika malezi mabovu au wazazi walijitahidi sana kumfundisha lakini hakufundishika, Mwanaume huyu anapokutana na mwanamke mwenye maadili au aliyefundishwa vizuri tangu mwanzo kuwa ipo siku moja atakuwa mke wa mtu itamuwia vigumu mke huyu kuchukuliana na huyu mwanaume na atahangaika sana kutaka kumbalisha lakini haitawezekana kwa kipindi kifupi tu. Itamlazimu kulipa gharama ya muda mrefu na kumtafuta Mungu zaidi kuliko kutumia akili zake mwenyewe.

v Katika makundi yote haya tunaweza kuona mwanaume uliyenae wewe yupo katika kundi gani na asili gani ili unapoanza kushugulika na kasoro unazoziona katika ndoa au mahusiano yako utambue mwanaume huyo asili yake ni nini na jinsi gani utaweza kusaidiana naye katika safari hii ya mahusiano au ndoa yenu.

MWANAMKE NI NANI KATIKA JAMII?

o Mwanamke ni msaidizi wa mwanaume

o Mwanamke ni taji ya mwanaume

o Mwanamke ni mjenzi wa mji wake na nyumba yake

o Mwanamke ni kipenzi cha watoto na mume

o Mwanamke ni mwalimu wa familia

o Mwanamke ni mshawishi wa tabia njema kwa jamii inayomzunguka

MWANAMKE MWENYE ASILI YA MUNGU (MWANAMKE MWENYE MAADILI)

o Hana haraka ya mambo

o Mvumilivu, mnyenyekevu, mtiifu, mkweli, anaheshima, anajituma, ana utu

o Yupo tayari kufanya suluhu na kusahau

o Yupo tayari kujifunza kutokana na makosa

o Ana mapenzi ya dhati nay a ukweli

o Anajali watoto na mume wake pia pamoja na jamii yote inayomzunguka

o Hayupo tayari kumsaliti mume wake hata k**a sababu zote anazo.

MWANAMKE MWENYE ASILI YA DUNIA (ASIYE NA MAADILI)

o Ni mkorofi

o Hasira zake huwa karibu na za wazi wazi sana

o Kinywa chake hutoa matusi na lawama wakati wote

o Hukusanya makosa ya mume wake wakati wote

o Huwa na upendo wa mtego, hana upendo wa dhati

o Hupenda kupokea zaidi ya kutoa

o Hulazimisha mambo yafanyike hata k**a haiwezekani kwa wakati huo.

v Katika kundi la kwanza tunamuona mwanamke mwenye asili ya mungu ambaye hutambulika k**a mwanamke shujaa mwenye maadili ya kuwa mke mwema na aliye andaliwa vizuri kuwa mke bora kwa mume na familia nzima, Mwanamke huyu anapokutana na mwanaume mwenye asili ya dunia hujuta sana kwanini ameingia katika mahusiano na mtu huyu, inamuwia vigumu kuikabili tabia ya mwanaume huyu na kuona wanaume wote ni maadui na k**a ikishindikana kupata msaada wa kumtoa katika eneo hilo basi hujikuta akibaki mnyonge na mwenye kilio wakati wote hatimae kutokuwa katika mahusiano tena. Anapobahatika kukutana na mwanaume ambaye ana maadili mahusiano yao huwa ya amani sana na hata ndoa yao huwa inadumu kwa kiasi kikubwa sana.

v Kundi la pili linamtambulisha mwanamke asiye na malezi na asiye jua nini wajibu wake k**a mwanamke. Mwanamke huyu anakuwa katika hali k**a hii endapo kwa upande mmoja wazazi wake walichangia katika malezi mabovu au wazazi walijitahidi sana kumfundisha lakini hakufundishika, Mwanamke huyu anapokutana na mwanaume mwenye maadili au aliyefundishwa vizuri tangu mwanzo kuwa ipo siku moja atakuwa mume wa mtu itamuwia vigumu mume huyu kuchukuliana na huyu mwanamke na atahangaika sana kutaka kumbalisha lakini haitawezekana kwa kipindi kifupi tu. Itamlazimu kulipa gharama ya muda mrefu na kumtafuta Mungu zaidi kuliko kutumia akili zake mwenyewe.

v Katika makundi yote haya tunaweza kuona mwanaume uliyenae wewe yupo katika kundi gani na asili gani ili unapoanza kushugulika na kasoro unazoziona katika ndoa au mahusiano yako utambue mwanaume huyo asili yake ni nini na jinsi gani utaweza kusaidiana naye katika safari hii ya mahusiano au ndoa yenu.

MAPENZI NI NINI?

Kutokana na tafsiri mbali mbali na mijadala mbali mbali inaonesha mapenzi ni ‘’ mkusanyiko wa hisia za binadamu zinazopelekea kujenga urafiki wa kudumu kati ya mwanamke na mwanaume au mtu na mtu mwingine.’’

MPENZI NI NANI?

o Ni binadamu aliyejitoa kwa ajili yako, kusaidiana na wewe katika shida na raha

o Ni mtu yeyote aliyetayari kuumizwa kwa ajili yako

o Ni binadamu aliye tayari kushauriana na wewe pale anapoona umekosea

o Ni binadamu aliyetayari kuona unafanikiwa badala ya kuangauka

o Ni binadamu aliyetayari kushirikisha hisia zake za kimapenzi na wewe bila kificho

KUFANYA MAPENZI NI NINI?

o Kuonesha hisia zako za kimapenzi kwa vitendo

o Kufanya vitendo vya upendo kwa wale wote walio shirikiana na wewe ktika shida au raha

o Kujitoa kwa jamii nzima zaidi ya kusubiri kupokea zaidi

KUSUDI LA KUFANYA MAPENZI NI NINI?

o Kumfurahisha mpenzi wako

o Kufurahisha mwili wako na nafsi yako

o Kupata watoto/ kuanzisha familia kwa kupata watoto

o Kujenga ushirikiano wa kudumu baina yako na mwenzi wako/ jamii inayokuzunguka

o Kuonesha hisia za mapenzi kwa vitendo na kufanya suluhu ya matatizo yenu.

MAPENZI YANABEBWA NA VITU VIWILI VIKUBWA AMBAVYO NI:
UPENDO NA HISIA ZA MAPENZI.

UPENDO NI NINI?

v Ni tendo la hiari kutoka moyoni mwa mtu analo kusudia kulifanya kupitia vitendo vya ukarimu, upendo siyo kujivuna, siyo kujisikia wewe ni bora kuliko wengine, siyo kulipiza kisasi, siyo kulaani bali kubariki n.k

v Upendo ni kusaidiana katika raha na shida pia kutoa shukurani kwa Mungu na jamii nzima pale unapokuwa umeshirikiana nao katika jambo lako lolote.

v Upendo husaidia kumaliza ugomvi na kufanya jamii nzima iwe na amani

v Upendo mara nyingi unapokuwa ni wa dhati hauwezi kupotea kamwe kwani kila sku vitendo vya upendo husaidia kuongeza ladha ya mahusiano. Hivyo unapoona vitendo vya upendo vinapungua katika nyumba yako ujue ni rahisi kupoteza amani iliyomo humo ndani.

v JUKUMU LAKO K**A MWANAUME AU MWANAMKE ULIYE KATIKA MAHUSIANO NI KUPENDA KWA DHATI ILI KUFANYA VITENDO VYA UPENDO VIZAE AMANI KATIKA NYUMBA YENU NA MAHUSIANO YENU.

HISIA ZA MAPENZI NI NINI?

o Hapa kila mmoja wetu atakuwa na jibu lake kuhusu swali hili lakini hebu na tuziangalie hisia za penzi ni nini maana yake.

o Hisia za mapenzi ni ile hali isyo kifani, msisimko, shauku, kujiskia raha mara zote unapoona mwenzi wako anarudi kutoka katika shughuli za kila siku, au anarudi kutoka safari, au anapokuwa karibu na wewe.

o Hisia za mapenzi ni tendo linalonesha mapenzi ya dhati kati ya wewe na mpenzi wako jinsi mlivyoshibana.

o Hisia za mapenzi ni nzuri kupindukia ndo maana mamilioni ya wasanii wa muziki duniani kote wamekuwa wakiimba nyimbo zinazolenga mapenzi na wapenzi.

o Wengi wetu tumeshapatwa na hisia za mapenzi kali sana kiasi kwamba tumebaki tukijilaumu na kufikia hatua ya kujiua au kuwaua wale wanaoingilia mapenzi yetu. Hisia za mapenzi zaweza kujenga undugu wa kudumu na waliokaribu yako au kubomoa/kuvunja undugu na waliokaribu yako.

UKWELI KUHUSU HISIA ZA MAPENZI UPOJE?

o Hisia za mapenzi hujengwa na vitendo vya upendo

o Hisia za mapenzi huweza kutoweka na kuhamia mahali popote pale penye upenyo ambapo vitendo vya upendo hupatikana kwa urahisi.

o Hisia za mapenzi huweza kurudisha mapenzi yaliyoharibiwa vibaya kwa kupata vitendo vya upendo wa dhati mara dufu ya ilivyokuwa mwanzo.

v Tatizo ulilonalo leo katika NDOA yako au mahusiano yako ni vyema ukalifanyia uchunguzi mapema ili kujuwa k**a limetokana na kushuka kwa kiwango cha UPENDO hivyo kupelekea HISIA ZA MAPENZI kupotea na kuvunja amani yako na mpenzi wako.

· FANYA TATHIMINI YA MAHUSIANO YAKO, NA UJIHOJI MASWALI YAFUATAYO!

(i) Unauhakika kuwa unafahamu hisia za mapenzi, na unajuwa zinachochewa na vitedo vya upendo?

(ii) Unafahamu gharama ya kupoteza vitendo vya upendo?

(iii) Upo tayari kupoteza NDOA/MAHUSIANO kutokana na kutokuwa mtafiti wa mbinu mbali mbali za kudumisha mahusiano au ndoa yako?

(iv) Ulishawahi kumpenda mume / mke wako kwa vitendo?

(v) Unatarajia nini kutoka kwa mume/ mke wako unapofanya vitendo vya upendo? (b) Unatarajia kupokea zaidi au kutoa zaidi?

(vi) Wewe ni muaminifu kwa kila jambo katika mahusiano uliyopo? (b) Unauwezo gani wa kusimamia uaminifu wako na mwenzi wako linapokuja tatizo la KUKOSA UAMINIFU?

(vii) Upo tayari kusamehe na kusahau? (b) Je upo tayari kucheza vizuri katika nafasi yako?

(viii) Upo tayari kupanga mambo yako upya? (b) Upo tayari kuangalia mazuri ya mwenzako na kukumbuka mazuri aliyokutendea kuliko kuangalia mabaya na makosa madogo madogo anayokosea eidha kwa kujuwa au kutokujuwa k**a kwako ni makosa?

MAMBO YA KUANGALIA NA KUZINGATIA KATIKA SWALA LA MAPENZI!
(i) Kumbuka kuwa penzi ni kitendo, kitendo cha kumjali na kumfikiria mwenzi wako na kuwa mpole,
muungwana, mwenye subira, na kuelewa kuwa huyo mpenzi wako ana uhuru wa kuweza kuchagua kukupenda au kutokukupenda milele bila kuangalia hasara zitakazopatikana.

(ii) Kumbuka kuwa hisia za penzi ni hisia tu, zinaweza kuja kwa wingi au zinaweza kutoweka kabisa.

(iii) Endapo utaona hisia za penzi zimeanza kutoweka unaweza kufanya jitihada kuzirudisha kwa kufanya matendo ya upendo bila kujali faida au hasara zitakazotokea, unachohitaji hapa ni kurudisha penzi lako katika mstari ulionyooka!

v Ili kudumisha NDOA yenu au mahusiano yenu itakutegemea wewe k**a wewe eidha ni mwanamke / mwanaume. Kwa upande wa mwanamke ana paswa kuonesha upendo zaidi kuliko kupokea, isipokuwa pale ambapo mwanaume ameshindwa kabisa kupokea upendo wako.

Chanzo: Mitandao ya Kijamii

Address

2029
Dar Es Salaam
255

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Telephone

+255684892369

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Free Jesus Gospel posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Free Jesus Gospel:

Share