Dr Thabit-Uislam Dini Yangu

Dr Thabit-Uislam Dini Yangu When people hate you for no reason, remember Allah loves you for no reason, Allah knows best

05/09/2025
23/05/2024
04/04/2021

INASISIMUA ILA MAISHA NDO HAYA,.

HEBU SOMA SIMULIZI HII YA KWELI.

Mwanaume wa miaka 78 alianguka ghafla na kuwahishwa hospitali.

Alipokelewa na madaktari na kuwekewa oksijeni iweze kumsaidia kwa masaa 24, .

Baada ya muda, alirejea kwenye hali yake ya kawaida, daktari waliponwona kuwa amerejea kwenye hali yake ya kawaida, walimpa (MUSWADA) bili ya tshs milion 2 na nusu na alipoona muswada huo, akaanza kulia,😥😥😭

Daktari akamwambia asilie kwa sababu ya muswada huo.

Lakini yule mtu akasema, "Silii kwa sababu ya pesa, naweza kulipa pesa zote.

Ninalia kwa sababu kwa masaa 24 tu ya kutumia oksijeni, lazima nitumie kwa gharama kubwa kiasi hicho, million 2 na nus, lakini nimekuwa nikipumua hewa ya bure ya Mungu kwa miaka 78.

Sijawahi kulipa chochote, unajua ni deni gani anayo juu yako?

Daktari alishusha kichwa chake na kutokwa na machozi.

Sasa, kwako wewe unayesoma hii, unapumua hewa bure ya Mungu bila bei yoyote ya kulipa kwa miaka sasa, tafadhali chukua sekunde 2 za wakati wako na utume hii hata kwa watu 5 kuwakumbusha kusema kila wakati Asante " Allah" kwa huduma za kuishi na kutujalia kuvuta hewa safi, na kutambua thamani uliyo tujalia kuwa nayo duniani,.

Usipuuze kushirikisha watu hata 5 na andika asante sana Mwenyezi Mungu kwa pumzi ya uhai

*MAELEKEZO YA MAISHA KTK QUR'AN**1_Usizungumze kwa ukali (3:159)**2_Jizuie na hasira (3:134)**3_Kuwa mwema kwa wengine (...
21/03/2021

*MAELEKEZO YA MAISHA KTK QUR'AN*

*1_Usizungumze kwa ukali (3:159)*

*2_Jizuie na hasira (3:134)*

*3_Kuwa mwema kwa wengine (4:36)*

*4_Usiwe mwenye kiburi(7:13)*

*5_Samehe wanaokukosea (7:199)*

*6_Zungumza na watu kwa upole (20:44)*

*7 _Shusha sauti yako (31:19)*

*8_ Usiwakejeli wengine (49:11)*

*9_Watendee wema wazazi wako (17:23)*

*10 _Usiseme maneno ya kuwakosea adabu wazazi wako (17:23)*

*11_ Usiingie chumba cha wazazi wako bila kuomba idhini (24:58)*

*12_Andikishianeni mnapokopeshana (2:282)*

*13Usifuate rai ya yeyote kibubusa (2:170)*

*14_Muongezee unayemdai muda wa kulipa deni k**a ana hali ngumu (2:280)*

*15_ Usile riba (2:275)*

*16_ Usijihusishe na rushwa (2:188)*

*17_ Usivunje ahadi (2:177)*

*18_Tunza amana (2:283)*

*19_ Usiufiche ukweli unaoujua (2:42)*

*20_ Wahukumu watu kwa haki (4:58)*

*21_Simamia haki (4:135)*

*22_Mali za marehemu zigawiwe kwa warithi wao (4:7)*

*23_Wanawake pia wana haki yakurithi (4:7)*

*24_Usile Mali ya yatima (4:10)*

*25_ Watunze yatima (2:220)*

*26_Msiliane Mali zenu kwa dhuluma (4:29)*

*27_Patanisheni miongoni mwa wanaogombana (49:9)*

*28_Jiepushe nakuwajengea watu Dhana mbaya (49:12)*

*29_ Msipelelezane na msisengenyane (2:283)*

*30_Msipelelezane au msisengenyane (49:12)*

*31_ Toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu (56:7)*

*32_Jihimizeni kuwalisha maskini (107:7)*

*33_ Watafuteni wenye kuhitaji muwasaidie (2:283)*

*34_Usitumie ovyo pesa zako (17:29)*

*35_Msiharibu sadaka zenu kwa masimulizi (2:264)*

*36_ Wakirimu wageni (51:26)*

*37._Waamrishe watu kutenda mema baada ya wewe mwenyewe kuyatenda (2:44)*

*38_Msifanye uharibifu katika Ardhi (2:60)*

*39_Msiwazue watu kuingia misikitini (2:114)*

*40_Piganeni na wale wanaowapigeni tu (2:190)*

*Pendelea kukumbusha Uislam ndio njia mfumo wa maisha yetu

Indeed, we are all servants of AlmightyGod (Allah), we are made of clay and dust we will return. Your leadership has lef...
18/03/2021

Indeed, we are all servants of AlmightyGod (Allah), we are made of clay and dust we will return. Your leadership has left a big mark, not only in Tanzania, but in the whole of East Africa and the whole world as well. You have left when we still need you more my Father, my President. The nation of Tanzania In general we are very sad, we loved you, we love you, and we will continue to remember with great love my President. We will weep for you and remember your goodness to Tanzanians especially the weak and poor Tanzanians. May God Rest you In Peace.

KHUTBA YA KUAGA YA MTUME MUHAMMAD Rehema Za Allah ziwe juu yake Pamoja na amani (HIJJAH TUL-WADAAAH)Khutba hii ilitolewa...
27/02/2021

KHUTBA YA KUAGA YA MTUME MUHAMMAD Rehema Za Allah ziwe juu yake Pamoja na amani (HIJJAH TUL-WADAAAH)

Khutba hii ilitolewa na Mtume Muhammad Rehema Za Allah ziwe juu yake Pamoja na amani tarehe 09 Dhul
Hijja mwaka wa 10 Hijriya kwenye Mlima Arafah.

1 Enyi watu! Nisikilizeni maneno yangu vizuri , kwani sidhani
k**a baada ya mwaka huu nitakuwa pamoja nanyi. Hivyo sikilizeni
kwa makini nitakayoyasema na (maneno haya ) mfikishieni kila
asiekuwepo hapa leo.

2."Enyi watu! Hakika damu zenu na mali zenu ni takatifu kwenu
k**a mlivyoufanya mwezi huu kuwa mtakatifu na mji huu kuwa
mtukufu”
Rudisheni amana mlizokabidhiwa kwa wenyewe wanaostahiki.
Msimdhuru yeyote ili nanyi msije mkadhuriwa. Kumbukeni mtakuja
kukutana na mola wenu naye atahesabu amali zenu. Allah Subhana Wataala
amekukatazeni kula riba . Hivyo riba zote zimeondoshwa na mna
haki ya kubaki na rasilmali (mitaji) yenu . Hamna haki ya
kudhulumu wala kudhulumiwa . Allah Subhana Wataala ameharamisha riba na
Kila haki ya kisasi iliyekuwepo enzi za Ujahiliya imefutwa!

3 "Enyi watu! washirikina wanajaribu kuakhirisha (kuchelewesha)
kalenda ili wafanye kuwa sawa idadi ya ile (miezi) aliyo
itukuza Allah na kulifanya halali jambo ambalo Allah Subhana Wataala ameliharamisha
na kulikataza jambo ambalo Allah Subhana Wataala ameliruhusu Miezi kwa Allah Subhana Wataala ni
kumi na miwili . Minne kati yao ni mitakatifu, mitatu ikiambatana (Dhul Qaadah, Dhul Hijjah na Muharram) na mmoja (Rajab) uko kati ya Jumada (ya mwanzo na ya mwisho) na Shaaban.

4 "Jiepusheni na shetani kwa ajili ya kuilinda dini yenu . Tayari
(shetani ) amekata tamaa kwamba hataweza kuabudiwa katika ardhi
hii milele lakini bado ana mikakati ya kukupotezeni hivyo
tahadharini nae katika mambo mengine ."

5 "Enyi watu ! ni kweli mna haki juu ya wanawake na wao pia wana
haki juu yenu . Kumbukeni mmewachukua kuwafanya wake zenu kwa
amana ya Allah Subhana Wataala na mmehalalishiwa (kustarehe) nao

6 "Nnakuusieni kuwatendea wema wanawake na kuwa na huruma kwao
kwani ni wake zenu ni wasaidizi wenu .

7 " Enyi watu, nisikilizeni kwa utulivu , mcheni Allah Subhana Wataala ,
msali sala tano kila siku, fungeni katika mfungo wa Ramadhan na
toeni Zakah. Tekelezeni ibada ya Hijjah ikiwa mna uwezo."

8 Binadamu wote wametokana na Adam na Hawaa , hakuna mbora kati
ya mwarabu na asiyekuwa mwarabu , wala asiekuwa mwarabu kwa
mwarabu , wala mweupe kwa mweusi au mweusi kwa mweupe
isipokuwa kwa Taqwa( kumcha Allah).*

9"Enyi watu Eleweni * kila muislamu ni ndugu kwa muislamu na waislamu wote
ni ndugu. Hatohalalishiwa muislamu kitu chochote isipokuwa kile
alichopewa kwa ridhaa na ndugu yake . Wala msidhulumu nafsi
zenu . Na msisahau kwamba kuna siku mtakutana na mola wenu na
mtahesabiwa amali zenu. Hivyo tahadharini msije mkapotea baada
yangu"

10 "Enyi watu ! Hakuna tena Mtume baada yangu na hakuna dini
nyengine itakayokuja. Ninakuachieni vitu viwili ambavyo
mkishik**ana navyo hamtopotea milele navyo ni QURAAN na SUNNA

11 "Wale wote walionisikiliza waufikishe ujumbe huu kwa wengine
na wengine waufikishe kwa watakaofuatia na inawezekana hawa wa mwisho wakayafahamu vyema maneno yangu kuliko hawa walionisikiliza moja kwa moja."
"Ewe mola shuhudia kwamba nimefikisha ujumbe kwa watu wako"
**
Inshaallah kila atakaepata ujumbe huu ahakikishe anamfikishia mwengine
k**a tulivyoagizwa na Al Habib Mustafa Rehema Za Allah ziwe juu yake Pamoja na amani na inawezekana miongoni mwetu kuwapata Watakao msikilza Mtume Rehema Za Allah ziwe juu yake Pamoja na amani na kumfahamu vyema na hivyo kuufuata mwenendo wake . Tumuombe Allah Subhana Wataala atujaalie miongoni mwao.
Amin.

*MAELEKEZO YA MAISHA KTK QUR'AN**1_Usizungumze kwa ukali (3:159)**2_Jizuie na hasira (3:134)**3_Kuwa mwema kwa wengine (...
13/02/2021

*MAELEKEZO YA MAISHA KTK QUR'AN*

*1_Usizungumze kwa ukali (3:159)*

*2_Jizuie na hasira (3:134)*

*3_Kuwa mwema kwa wengine (4:36)*

*4_Usiwe mwenye kiburi(7:13)*

*5_Samehe wanaokukosea (7:199)*

*6_Zungumza na watu kwa upole (20:44)*

*7 _Shusha sauti yako (31:19)*

*8_ Usiwakejeli wengine (49:11)*

*9_Watendee wema wazazi wako (17:23)*

*10 _Usiseme maneno ya kuwakosea adabu wazazi wako (17:23)*

*11_ Usiingie chumba cha wazazi wako bila kuomba idhini (24:58)*

*12_Andikishianeni mnapokopeshana (2:282)*

*13Usifuate rai ya yeyote kibubusa (2:170)*

*14_Muongezee unayemdai muda wa kulipa deni k**a ana hali ngumu (2:280)*

*15_ Usile riba (2:275)*

*16_ Usijihusishe na rushwa (2:188)*

*17_ Usivunje ahadi (2:177)*

*18_Tunza amana (2:283)*

*19_ Usiufiche ukweli unaoujua (2:42)*

*20_ Wahukumu watu kwa haki (4:58)*

*21_Simamia haki (4:135)*

*22_Mali za marehemu zigawiwe kwa warithi wao (4:7)*

*23_Wanawake pia wana haki yakurithi (4:7)*

*24_Usile Mali ya yatima (4:10)*

*25_ Watunze yatima (2:220)*

*26_Msiliane Mali zenu kwa dhuluma (4:29)*

*27_Patanisheni miongoni mwa wanaogombana (49:9)*

*28_Jiepushe nakuwajengea watu Dhana mbaya (49:12)*

*29_ Msipelelezane na msisengenyane (2:283)*

*30_Msipelelezane au msisengenyane (49:12)*

*31_ Toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu (56:7)*

*32_Jihimizeni kuwalisha maskini (107:7)*

*33_ Watafuteni wenye kuhitaji muwasaidie (2:283)*

*34_Usitumie ovyo pesa zako (17:29)*

*35_Msiharibu sadaka zenu kwa masimulizi (2:264)*

*36_ Wakirimu wageni (51:26)*

*37._Waamrishe watu kutenda mema baada ya wewe mwenyewe kuyatenda (2:44)*

*38_Msifanye uharibifu katika Ardhi (2:60)*

*39_Msiwazue watu kuingia misikitini (2:114)*

*40_Piganeni na wale wanaowapigeni tu (2:190)*

*Pendelea kukumbusha Uislam ndio njia mfumo wa maisha yetu

Address

Mbezi Beach Jogoo
Dar Es Salaam
14128

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dr Thabit-Uislam Dini Yangu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share