Evangelist Grace kaondo

Evangelist Grace kaondo JESUS IS A TRUE WAY AND LIFE.

01/08/2024
02/06/2023

"HII NI COPY AND PASTE K**A ILIVYO",

Leo watoto wamefunga shule, kwenye group la WhatsApp la Darasa, Mwalimu ametutumia ujumbe huu, nikaona unaweza kuwa msaada kwa wengi 👇

Wapendwa Wazazi na Walezi ,Mungu ni mwema.

Imefikia tena Wakati Watoto Wetu wananakiwa Warudi nyumbani tar 31/05/2023 kwa Mapumziko.

Nakuomba Sana:-

1. Simamia Mwanao afanye kazi zake zote alizopewa na Waalimu.

2. Mpangie kufanya kazi ndogo ndogo za bustani, kufua, kuku,mifugo nk usimlelee k**a yai!

Labda k**a una bima ya kuishi nae milele.

Mfundishe ajitegemee siku ukiondoka ghafla asitaabike sana kujua la kufanya.

3. Ongea na mtoto wako juu ya matumizi ya simu na TV mwambie huko ulaya watoto wengi hawapotezi muda, kila sekunde yao ina shughuli.

Movies na simu asilimia kubwa ni kumpoteza mwafrika na mtu mjinga.

Huwezi kufuatilia Series 400 ukawa timamu lazima kuna shida mahali katika Ubongo.

Waambie kuwa dk 1 ya jana alopoteza haitajirudia milele na kuwa kuna wakati watautamani muda wa leo na hautarudi.

4. Ongea na Mwanao juu ya masomo na malengo yake ya mbele na je yatafikiwa!

Muulize juu ya aina za marafiki zake, mwelekeze kwa upendo.

5. Mwambie mwanao dunia imevua utu na ubinadamu, mweleze juu ya Ushoga athari zake, hata na Upuuzi wa Elon Musk ili ajue achague nini duniani humu.

Mfundishe Mwanao kupika hata ugali wa mchicha wengi ni tatizo.

Mwisho mfanye mwanao awe rafiki, we ni polisi, mwanajeshi, mkuu wa shule, mkuu mkuu mkuu yeyote usipeleke ukuu/ cheo, utajiri nyumbani.

Watoto wanayo mengi wanataka kuwashirikisha tafadhali wapeni muda.

Waeleze pia k**a haupo kesho unapendelea waishije au waweje.

Wafundishe matendo ya huruma hebu wapeleke vituo vya yatima,

Wazee hata waliopo jirani na Sukari kg 1 tu waongee nao utaona mabadiliko watakayokuwa nayo katika kuwaza na kutenda baada ya hapo.

Kumbuka hao watoto ni wako kwa jina ila Mungu amewapitisha kwako ili wakuzwe kuhudumia watu wengine, hata wewe unahudumia wengine katika kazi yako.

Mungu awabariki na Kuwalinda Taifa la Mungu.

Amen.

31/05/2023
28/04/2022

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255762440731

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Evangelist Grace kaondo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share