12/08/2026
NENO LA SIKU
NA MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA – KANISA LA EFATHA
TAREHE 12/08/2026
SOMO: NENO LA MUNGU LINAKUPA KUWA HODARI
Waefeso 6:10 “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.”
Je! Unakuwaje hodari? Tunakuwa hodari kwa kulijua Neno la Mungu, hauwi hodari kwa sababu unaomba sana, la! Yesu alimshinda ibilisi siyo kwa maombi bali kwa Neno la Mungu, hivyo unahitaji kuelewa kuwa kinachokufanya wewe uwe hodari siyo maombi, maombi yana sehemu yake na Neno lina sehemu yake pia.
Yohana 1:1-5 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.” Unapolijua Neno la Mungu unakuwa hodari na hata adui akija kukushambulia anashindwa kwa maana wewe unakuwa k**a mti uliopandwa kando kando ya vijito vya maji, adui akija kukusukuma anashindwa, kwa nini? Kwa sababu umepandwa katika Neno hivyo unakuwa imara.
Kwa namna unavyolielewa Neno ndivyo unavyostawi, haustawi kwa kunena kwa lugha, kufunga na kuomba, la! Bali kwa kupitia Neno ulilonalo. Neno la Mungu lipo ili kuwezesha akili yako. Neno linapokuja linakaa moyoni na ndipo sasa linaweza kutumiwa na akili yako, k**a akili yako ikitafuta Neno ndani yako na ikakosa ndipo sasa inaanza kutumia neno la ulimwengu huu maana akili kamwe haiwezi kuwa tupu. Hivyo tamani kulijua Neno la Mungu ili likupe kuishi sawa sawa na ahadi zake katika maisha yako.