17/11/2025
Bwana Yesu asifiwe wapendwa wa Mungu!Nawakumbusha kwamba leo tarehe 17 November, tutaanza challenge yetu ya Maswali ya Biblia. Saa ya kupost ni saa 3 na nusu (saa tatu na dk 30 usiku) kutokana na mapendekezo yenu, wengi mtakuwa mmetulia majumbani mda huo,
Nitapost hapa kwenye page yetu ya Facebook https://www.facebook.com/profile.php?id=61572840240114 # namba ya swali kutoka maswali ya kitabu cha Mwanzo. Maswali yote ni kwa lugha ya Kiswahili.
Unachopaswa kufanya: Ingia kwenye maswali nenda kwenye namba ya swali nililoandika click jibu sahihi, andika swali linasemaje na jibu lake, upost k**a reply ya post yangu ya namba ya swali. Screenshot inaruhusiwa pia. Post yangu nitaipost na kuipin hapa https://www.facebook.com/profile.php?id=61572840240114 #
Mtu wa kwanza kupost reply ya swali na jibu lake atakuwa ndie mshindi wa siku, ataniandikia inbox email yake, user name na tarehe aliyojisajili kwenye Nurukuu Maswali ya Biblia, na namba ya simu ya kupokelea zawadi yake ya Tsh 20,000
Kila siku nitapost namba ya swali Facebook, challenge yetu itakuwa kwa siku 5, yaani tarehe 17 hadi 21 November. Lengo la challenge yetu ni kuhamasisha usomaji wa Biblia. Kwa wasio na ujuzi wa neno la Mungu, msihofu, maswali ni ya kuchagua na ukichagua jibu lisilo sahihi utaonyeshwa jibu sahihi papo hapo. Andika Swali na jibu lake sahihi , au screenshot, utume k**a reply kwenye post yangu ya namba ya swali, ukiwa wa kwanza kureply utakuwa mshindi wa challenge ya siku.
karibuni sana.
Kwa wanaotaka kufanya challenge lakini hawajajiunga na NuruKuu Maswali ya Biblia, nashauri wajiunge mapema na kujaribu kuyafikia maswali ili k**a kuna shida yoyote waweze kupata msaada kabla ya challenge kuanza.
Kwa waliojiunga tayari ingia hapa https://nurukuu.com/my-account/ scroll chini kwenye kitufe cha kijani "Anza maswali ya Biblia" , k**a uli logout page ya ku login itatokea, login kwa kutumia username na password uliyotumia kujisajili, itakupeleka moja kwa moja kwenye maswali
Yeyote mwenye swali kuhusu Challenge inayoanza leo anione inbox.
Karibuni sana wapendwa