23/05/2020
NAWAPA HESHIMA YENU WANAWAKE!
Nawapongeza kwa kuwa wepesi wa kuamini. Nawapongeza WANAWAKE wale waliokuwa wepesi wa kuisiki INJIL ya Mungu, wakaamini. Wanaume huwa na moyo mgumu kidogo.
Hebu tulinganishe
MWANAUME Zakaria alipoambiwa atamzaa Yohana Mbatizaji na kusudi la kuzaliwa mtoto huyo, akamwambia malaika, Jambo hili haliwezekani kwa kuwa Mimi na more wangu tu wazee, tumeshapitisha muda was kuzaa, huyo huyo aliyewafundisha waisrael kuwa baba yao Ibrahim aliwazaa wao akiwa na miaka Mia, na mkewe tisini na, na kwa sababu ya kutokuamini kwake akatiwa ububu, mpaka Mungu alipompa mtoto K**a alivyosema (Luke 1:8-20).
Lakini MWANAMKE Mariamu alipoambiwa na malaika yuleyule aliyemwambia Zekaria, alipomwambia juu ya kumzaa Messiah, aliuliza tu itakuwaje pasipo kungiliana na mwansmume, alipoambiwa mpango wa Mungu, alinyenyekea na kusema tu, Mungu atanye K**a alivyosema, Luke 1:28-38.
WANAUME, Mitume wa Yesu, walipokuwa wakivua usiku kucha nz kuambulia patupu, aliposema nao hawakumtambua Bwana wao, japo walikuwa naye Kila siku, Yohana 21:5-14; WANAUME Mitume hawakuwahi kaburini mara sabato ilipoisha, na hata walipoambiwa na mwanamke wamemtoa Yesu kaburini, walienda tu wachungulia ndani ya kaburi, halafu hao wakaondoka zao Yohana 20:1-10; WANAUME wanafunzi wawili wa Yesu Kutoka Emausi, Yesu alipowatokea njiani, akaongea nao kwa muda mrefu wasimtambue kwa njia ya sauti yake, mpaka walipomtambua kwa kumega mkate Luka 13:13-35; Lakini, MWANAMKE MARIAMU Magdalena aliamka asubuhi na mapema, alipoona Bwana wake hayupo, akarudi kuwapasha habari Mitume, akarudi nao Tena kaburini, mbiombio, walipoondoka, Yeye akabaki kuendelea na msako wake wa kumtafuta, Bwana, na matokeo yake yakamfanya kukutana na BWANA, ambaye alimtambua kwa sauti moja tu, pale alipomwambia jina lake, "MARIAMU" YOHANA 20.
Unajifunza Nini hapo?