Shining Light Church Dar Es Salaam

Shining Light Church Dar Es Salaam Maono yetu ni Kuangaza nuru ya Injili katika Ulimwengu Mzima

Karibu uwe na familia ya
30/03/2026

Karibu uwe na familia ya

27/03/2026
20/03/2026
  katika   .   na
03/01/2026

katika . na

10/05/2025

katika

08/05/2025

22/04/2025

pasaka vibe

  Semina! Semina!Semina ya neno la Mungu kuhusu Uponyaji.Karibu kwenye Group la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/Jr940...
18/04/2025

Semina! Semina!

Semina ya neno la Mungu kuhusu Uponyaji.

Karibu kwenye Group la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/Jr940ugCUWXAOrDyG0TUjx la mafundisho ya Neno la Mungu kwa njia ya sauti, chini ya huduma ya Mchungaji William Mayemba

Kupitia mafundisho haya, utajengwa kiroho, kufundishwa kweli ya Neno, na kuimarishwa katika imani.

Jiunge sasa ili usikose kile ambacho Mungu ameandaa kwa ajili ya maisha yako.

Leo Mchungaji alianza utangulizi huu Waebrania 14:12

"Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hapana mtu atakayemuona Bwana , asipokuwa nao. Angalia, hajasema hautamwona Mungu kwa kukosa ibada. Sawa Kukosa ibada inasababisha vitu vingine ambavyo vinasababisha usimuone. Lakini amesema hakuna mtu atakayemuona Mungu k**a hana amani na watu wengine, pili si mtakatifu. Inawezekana mahusiano yangu mimi na Mungu ni ya kujitenga na uchafu na ubaya na uovu. Lakini anasema amani na watu wote niitafute kwa bidii Sitamuona Mungu k**a sina amani na watu wengine. Amina. ndiyo hivyo hivyo, haleluya.

Haitawezekana nimuone Mungu, haitawezekana niingie mbinguni, haitawezekana haleluya nikakae na Yeye k**a kuna mtu sina amani naye kwa sababu yoyote. Ndio maana anasema, kwa upande wangu, kuwa na amani na watu wote. Amina.

Hata kwenye kitabu kile cha Wafilipi, anasema usijisumbue kwa neno lolote ila kwa kila neno kwa kuomba, kusali, pamoja na kushukuru, haja zenu zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu ipitayo akili itawalinda nia zenu na mioyo yenu katika Kristo Yesu. Hallelujah.

Sasa angalia, anasema usisumbuke. Kwa hiyo, katikati ya masumbufu, Yeye anasema sio kwamba hataondoa masumbufu tu, ambao ni kweli yataondoka. lakini anasema atakacho kupatia sio kuondoa masumbuko tu , sio ile haja tu. Yaani masumbuko yakiondoka, bado hujapata jibu. Haleluya. Haja yako ikitimizwa, bado hujapata jibu lenyewe. Jibu lenyewe Ni nini? Amani ipitayo. Haleluya, wapendwa,

Amen.

Katiki ya masumbufu, wasiwasi, majonzi, misiba, mahangaiko, sintofahamu, magumu, matatizo—yawe yamesababishwa na watu, yamesababishwa na mazingira, yamesababishwa na maamuzi yako mwenyewe. Bwana anasema usisumbuke na jambo lolote.

Bwana asifiwe!

Usisumbuke na jambo lolote. Bwana Yesu alisema, usisumbukie maisha, ule nini, uvae nini. Hayo hata watu wa mataifa wanayosumbukia. Tafuta kwanza wewe ufalme wa Mungu na haki yake, na mengine yote mtazidishiwa.

Tunajua kitabu cha Warumi 14 anasema ufalme wa Mungu sio kula na kunywa tu bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.

Kwa hiyo unaona kumbe amani ni nini: alama ya uwepo wa ufalme wa Mungu.

Kukosekana kwa amani ni alama ya uwepo wa ufalme wa Shetani.

Neno la Mungu linasema kitabu cha Yakobo, palipo na machafuko ndipo pana magumu na kila tendo la kuwa. Hekima hiyo itokayo juu ni ya kidunia, ya Shetani, na ya mwili, tena ni ya upole, tena ni ya amani. Bwana Yesu asifiwe, haleluya.

Tunda la haki inapandwa na walio na imani wanaotafuta amani, ndiyo kuna kuwa na tunda la haki hapo.

Bwana anasema amani ya Kristo na iamue mioyoni mwenu. Hiyo ndiyo kitu kikubwa sana kwenye maisha yetu. Bwana asifiwe! Amani, ndio Mungu anataka kila mmoja awe nayo.

Unajua, wakati mwingine mtu anaweza akawa anaomba mpaka anaomba mpaka tatizo fulani liondoke. Akiona lile tatizo limeisha, basi, au anaomba apate haja fulani, labda anaomba apate pesa. Akishapata pesa, basi kumbe Mungu anasema yeye sio yule jambo kuisha ni kitu kimoja, haja ikitimizwa ni kitu kingine. Mungu anataka amani yake. Bwana asifiwe.

Kwa sababu ukishakuwa na amani, ndio Mungu anaonekana. Tunajua Ayubu alisema umjue sana Mungu utakuwa na amani na ndipo mema yatakapokuja. Haleluya, amen. Ni amani mbele ya sababu ya Mungu ya kukosekana kwa amani ndio kunasababishwa ya Shetani. Ni jambo tu la muhimu kwa kila mmoja wetu kukaa katika amani. Biblia inasema iweni na amani katika kuamini. Mara nyingi tunamwamini Mungu lakini mtu anakosa amani katika kile anachokiamini. Ndio maana anakuwa na mahangaiko. Lakini ukianza kuwa na amani katika kile unachokiamini, yaani unamwamini Mungu labda kwa ajili ya uponyaji, utakuwa na amani ajabu. Haleluya.

K**a bado hujapata amani, endelea, k**a ni neno, endelea kutafakari neno, endelea, yaani, endelea kuwajibika ipaswavyo mpaka kwanza upate amani.

Bwana asifiwe!.

Ukishakuwa na amani, kila kitu cha Mungu kinakuja.

Haleluya!.

Yesu alikuwa anatumia amani k**a silaha dhidi ya kila shambulizi la Shetani. Hata alipokuwa akiona upepo mkali unapiga chombo, aliuambia iwe amani, tulia na kunakuwa shwari. Safari ikaendelea.

Haleluya!

Amani inajumuisha pia kustawi, usalama, na mzima.
*Ndio maana Yesu anaitwa Mfalme wa Amani. Bwana Yesu asifiwe.*

K**a afya yako imechafuka, yeye anatuliza; k**a tabia zako zimechafuka, yeye anatuliza dhoruba; k**a mtazamo wako umeharibika, yeye anatuliza dhoruba.
....tunapoenda kuhubiri popote, cha kwanza tunasema hivi: 'Amani iwe kwenu'.

Haleluya!

Uponyaji ni sehemu ya kazi ya mfalme wa amani. *Unamporuhusu mfalme wa amani kutawala maisha yako, kitu kimojawapo anachokupa ni uponyaji wa mwili*, uponyaji wa akili, zaidi sana uponyaji wa roho. Bwana asifiwe. Anakupatia uzima katika roho, anakupa uzima katika akili, na anakupa uzima katika mwili.

*Semina yetu itahusu uponyaji wa mwili huu wa damu na nyama. Bwana asifiwe.*

Hata k**a kuakuwa pia na uponyaji wa nafsi na roho au vyote. Lakini tusiche, cha kwanza ambacho tunaanza kukiangalia leo ni haya magonjwa makubwa.

Magonjwa Yamekujaje?

Yaani yametokeaje huku duniani?

Na yanafikaje sasa kwenye maisha yetu, kwenye ratiba zetu, kwenye familia zetu, kwenye jamii zetu?

Kwa sababu tumeingia duniani kwenye mazingira ambayo tulikuwa tunaona magonjwa ni sehemu ya maisha yetu, na tunaona kila mmoja anategemea kupata magonjwa. Lakini mimi nilikuwa nikiambiwa kwanza kwamba magonjwa yanatoka kwa Mungu.

Pili, je magonjwa yananifundisha kunyenyekea au la. Tatu, mtu k**a haumwi atapata ugonjwa mara moja na atakufa.

Je ni lazima ujiandae kuumwa?
Au usipoumwa unajicheki na kujishangaa mbona siumwi?

Na kulikuwa na mambo mengi sana yalikuwa yanakuja pamoja na hayo magonjwa. Watu wanasema eti "huyu anaumwa ugonjwa wa Mungu". Eti Mtu amekufa kwa sababu alikuwepo na ugonjwa wa Mungu. Ni lugha rahisi lakini zilikuwa zinaharibu sana mtazamo wetu kuhusiana na Mungu na ilituzuilia kabisa tusiweze kufikia kile Mungu alichonacho kwa ajili yetu.

Bwana asifiwe!

Lakini Mungu Baba yetu, kwa sababu utupenda, ameamua atufunulie kweli yote.

Tunajua kitabu kile cha Isaya sura ya tano. Tutauangalia kitu ambacho tunachojifinza sasa, ule mstari wa kumi na mbili,

'Na kinubi na zeze na matari na filimbi na mvinyo zote zipo katika karamu zao, lakini hawaiangalii kazi ya Bwana wala kuyafikiri matendo ya mikono yake. Kwa sababu hiyo, watu wangu wamechukuliwa mateka kwa kukosa kuwa na maarifa na watu wao wenye cheo wana njaa na wengi wao wanaona kiu sana. Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, umefunua kinywa chake bila kiasi na utukufu wao, na wingi wao, na ngazi yao nao pia afurahie miongoni mwao kushuka na kuingia humo'.

Angalia kwa mambo ameyataja ameyasema hapa k**a ni k**a kundi la vitu vitatu au vinne. Kundi la kwanza, amesema hivi: watu wanashughulika na mambo mengi sana —zeze, mathari, filimbi, mvinyo—vyote hivyo vipo katika karamu zao.

Tunafanya hayo yote tunaimba, tunafanya nini, kusherekea, tunashughulika na mengi. Tunakaribia Pasaka sasa, watu wanaandaa nguo kwa ajili ya Pasaka, ndio. Lakini kumbe Pasaka haihusiki na nguo. Amina.

Watu wanaandaa chakula kwa ajili ya Pasaka, ni vizuri, lakini kumbe *Pasaka haihusiki na chakula. Bwana asifiwe.*

Watu wanaandaa nyimbo mbalimbali, haleluya.

* *Pasaka tangu mwanzo wake ilikuwa inahusika na kuzuiliwa kwa mauti* iliyokuwa inasababishwa na Shetani na kuwatoa watu wa Mungu mikononi mwa utumwa, tangu mwanzo.

Haleluya!

Hata vyakula vilivyokuwa vinaliwa vilikuwa sio kufurahia tu chakula, lakini ni kukumbuka ile kazi ambayo Mungu aliifanya,
*Kuzuia uonezi wa Shetani kwenye maisha yao* na
*kuwatoa mikononi mwa adui.*
* Bwana asifiwe. ""

Amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu.

Jiunge nasi, zama ndani upate fahamu sawasawa na kweli ya neno.







































WhatsApp Group Invite

08/04/2025

Malaika wanakutamani

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 06:00 - 07:15
13:00 - 14:00
Tuesday 06:00 - 07:00
13:00 - 14:00
Wednesday 06:00 - 07:15
13:00 - 14:00
Thursday 06:00 - 07:15
13:00 - 14:00
Friday 06:00 - 07:15
13:00 - 14:00
Saturday 06:00 - 07:15
13:00 - 14:00
Sunday 08:00 - 18:15

Telephone

+255715750120

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Shining Light Church Dar Es Salaam posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category