Tmcs lita morogoro

Tmcs lita morogoro Official Facebook account for TMCS LITA MOROGORO

Tmcs lita morogoro inawakaribisha wote kwenye mahafali ya 19. Ni hapo kesho Tumaini hall ๐Ÿฅ‚๐ŸŽ‚๐Ÿพ
04/07/2025

Tmcs lita morogoro inawakaribisha wote kwenye mahafali ya 19. Ni hapo kesho Tumaini hall ๐Ÿฅ‚๐ŸŽ‚๐Ÿพ

Rest in peace ๐Ÿ•Š๏ธ
21/04/2025

Rest in peace ๐Ÿ•Š๏ธ

BABA MTAKATIFU FRANCISKO AMEFARIKI DUNIA (1936-2025)
Taarifa kutoka Vatican zinathibitisha kuwa Baba Mtakatifu Francisko amefariki dunia Kardinali Farrell, alitangaza kwa masikitiko kifo cha Baba Mtakatifu Francisko, kwa maneno haya: "kaka na dada wapendwa ni kwa huzuni kubwa kwamba sina budi kutangaza kifo cha Baba yetu Mtakatifu Francisko. Saa 01.35 asubuhi ya leo, (Jumatatu 21 Aprili 2025),Askofu wa Roma, Francisko, alirejea nyumbani kwa Baba.
www.radiomaria.co.tz

12/02/2025

SALAMU MALKIA:
Salamu Malkia Mama mwenye huruma; uzima, tulizo na matumaini yetu, salamu. Tunakusihi ugenini hapa sisi wana wa Eva. Tunakulilia tukilalamika bondeni huku kwenye machozi. Haya basi muombezi wetu, utuangalie kwa macho yako yenye huruma. Na mwisho wa ugeni, utuonyeshe Yesu, mzao mbarikiwa watumbo lako.
Ee mpole, ee mwema, ee mpendelevu, Bikira Maria.
www.radiomaria.co.tz

02/01/2025

ZAWADI NYINGINE YA MTAKATIFU WA LEO, MTAKATIFU GREGORI wa NAZIANZE (390) ASKOFU na MWALIMU WA KANISA

Mtakatifu Gregori alizaliwa Kapadoki (Uturuki) na wazazi bora wanaoheshimiwa na Kanisa k**a Watakatifu. Alizaliwa karibu na mji wa Nazianze mwaka 330. Alipokuwa mkubwa ya kutosha alipelekwa Atene (Ugiriki) akasome. Huko alikutana na Basili.
Walifanya urafiki kwa kusaidiana na kuendelea katika Utakatifu.
Kila jambo walilifanya pamoja, kuzungumza, kujifunza na kusali.

Walipomaliza masomo yao hapo Atene, Basili alikwenda zake ili apate kujitenga na malimwengu. Gregori alibaki papo hapo akifundisha lafudhi.
Baba yake Mzee Gregori alipokuwa mtu wa makamo alibatizwa pamoja na mke wake. Baadaye, alipata upadre na alikuwa Askofu wa Nazianze kwa Muda wa miaka 45.

Alipokuwa na umri wa miaka 80, Askofu Mzee Gregori alimwita mtoto wake akamfanya Padre ili amsaidie kulitawala Kanisa. Hatimaye, Gregori huyo mdogo aliwekwa kuwa Askofu wa Nazianze. Aliwapinga kwa uhodari wazushi wafuasi wa Arios.

Mji wa Konstantinopoli (Uturuki) ulikuwa ukishambuliwa pia na wazushi hao na Wakristo wengi walidanganywa. Wakuu wa Konstantinopoli walipoona vurugu hiyo, walimwita Gregori aje kuwaongoza.
Kwa sababu ya uvumilivu na upole wake, Gregori alifaulu kutuliza hasira za watu, kuwafundisha na kuwaongoa wazushi wengi katika dini ya kweli.

Baadaye ulitokea ugomvi kati ya wakuu wa Konstantinopoli. Gregori alijaribu kuwatuliza na kuwapatanisha, asiweze.
Alipoona hawamsikii, alijiuzulu uaskofu wa Konstantinopoli akaenda kukaa Nazianze.

Alikufa mwaka 390.
Maiti yake ilihamishiwa Roma, na sasa hivi kaburi lake limo katika kanisa la Mtakatifu Petro huko Roma.

MTAKATIFU GREGORI wa NAZIANZE, ASKOFU na MWALIMU WA KANISA
UTUOMBEE

03/12/2024

LEO DISEMBA 3 TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU FRANSISKO KSAVERI, PADRE(1552)

Fransisko Ksaveri alizaliwa Hispania Mwaka 1506 na Wazazi wa Ukoo bora.
K**a angalitaka angaliwaza kujipatia ukuu mbele za watu lakini siku moja, alipokuwa akisoma huko Paris (Ufaransa) Mtakatifu Inyasi wa Loyola (tunayemkumbuka 31 Julai) alimwambia Ksaveri, Ksaveri, yafaa nini kwa mtu kupata ulimwengu wote akipoteza roho yake?.

Baada ya siku za Mafungo Ksaveri na Mtakatifu Inyasi pamoja na wenzake watano Wayesuiti wakafunga Nadhiri ya kwenda katika nchi Takatifu ili kuwatunza Wakristo waliokuwa wakilalama utumwani wa Waislamu, kwa kuwa hawakufaulu kwenda huko badala yake walisafiri kwenda Roma (Italia) wakaonane na Papa ili afanye nao jinsi apendavyo pale Italia, Ksaveri alipewa Upadre Mwaka 1537.

Mwaka 1540, Inyasi na Ksaveri walikuwa Roma kwa Kupewa Kibali rasmi cha Shirika lao Jipya, zamani hizo Mfalme wa Ureno alimwomba Mtakatifu Inyasi apeleke Mapadre wa Shirika lake Kuhubiri Injili katika India.

Fransisko Ksaveri akatumwa kwenda huko pamoja na Mapadre wawili wengine katika Mwaka 1541 Alijipakia na kushuka baada ya miezi kumi na mitatu, katika pwani ya Goa(India)huko Fransisko aliizungukia nchi yote akiwakusanya Watoto na Watumwa ili waje kufundishwa naye Katekisimu akisaidiwa na mkalimali.

Watu wengi hawakukawia kuongoka Miaka miwili baadaye alihamia sehemu ya kusini ya India akiwafundisha hasa Wavuvi wa Pwani na Visiwani dini ya Yesu Kristo, alitenda miujiza mingi hata aliwafufua watu wange na walipoona mwujiza huo walitaka kubatizwa.

Baada ya kuwapatia wenyeji wa huko Mapadre alisafiri tena akafika katika Ufalme wa Trevankor (srilanka) dini katika visiwa vya Moluk, Amboins na Ternate akapata Wakristo wapya wengi alitengeneza Katekisimu ndogo katika lugha ya Ki-Malayan.

Mwaka 1549 alishuka katika Pwani ya Japan ambamo alikaa kwa muda wa miaka miwili, makasisi wao walimchongea kwa Mfalme na hatimaye wakamfukuza katika nchi yao alirudi Goa lakini hakukaa sana, kwani alitamani kupeleka Injili katika nchi ya china.

Alipofika Kisiwani Sanchian akaugua, wakamwacha huko Mreno mmoja alimhurumia akampokea kibandani mwake alikufa Disemba 2, mwaka 1552 katika kisiwa cha sanchian huko china katika muda wa miaka kumi mmisionari huyu aliwabatiza watu wengi ajabu miezi miwili na nusu baada ya kufa kwake waliukuta mwili wake haujaoza bado, ingawa alizikwa katika chokaa isiyozimka kusudi upate kuteketea upesi, ukapelekwa kwa heshima kubwa huko Goa (India) ambako umehifadhiwa hadi hii leo.

Nirahisi kuzitaja na kuziorodhesha nchi alizokuwa amefanya kazi, bali siyo rahisi sana kupata picha halisi ya uzito wa shughuli zile nyingi alizozifanya wakati wa miaka ile kumi na mmoja tangu aondoke Ulaya, mbali na safari mbili za kwenda Japan kutoka India na baadaye kuvuka bahari kuelekea kisiwa cha Sanchian alizifanya safari zake kwa miguu akitembea kilometa nyingi katika hali ya uchovu, Ugonjwa, ugumu wa kazi na kadhalika kweli Mtakatifu Fransisko alikuwa ni mtu hodari sana aliyesukumwa na Upendo wake kwa Bwana ili utawala wake uzidi kuenea mioyoni mwa watu na watu wengi zaidi wapate kumpenda na Kumtumikia.

Katika Barua mojawapo aliyomwandikia mkuu wake Mtakatifu Inyasi alisema Tangu nifike hapa sijapumzika nimekitembelea kila Kijiji nikawaosha Watoto wote wasiobatizwa bado kwa maji Matakatifu hivyo kuna Idadi kubwa sana ya Watoto niliwaondolea dhambi ya asili Watoto hawaniachii nafasi ya kusali breviary kula usingizi kabla ya kuwafundisha.

Lakini walau sala fulani hapo nimepata kungโ€™amua kwamba Ufalme wa mbinguni ni kwa ajili ya hao,
Mtakatifu Fransisko Ksaveri alitajwa Mtakatifu Mwaka 1622 na Mwaka 1927 aliwekwa kuwa Mlinzi wa Wamisionari popote Duniani siku ya leo yafaa sana kuwaombea kwa maombezi ya Mtakatifu Fransiko Ksaveri wale wote wenye kujitahidi kulitangaza kwa namna yoyote ili neno la Mungu.

MTAKATIFU FRANSISKO KSAVERI PADRE UTUOMBEE.

Watambue pia viongozi wa TMCS 2023/2024WILLIAM MEGABE MWENYEKITI,AMOSI LIMBU MAKAMU MWENYEKITI,PENDO M***A  KATIBU, LIGH...
03/12/2024

Watambue pia viongozi wa TMCS 2023/2024
WILLIAM MEGABE MWENYEKITI,AMOSI LIMBU MAKAMU MWENYEKITI,PENDO M***A KATIBU, LIGHTNESS MUNISHI MAKAMU KATIBU, ELIZABETH MADUU MTUNZA HAZINA

๐Ÿ™
03/12/2024

๐Ÿ™

Asante Mungu wangu kwa kunilinda usiku, nimeamka salama. Nakushukuru ninakutukuza na kukuabudu, Ee Bwana nijalie siku hii iwe njema kwangu roho na mwili. Amina
www.radiomaria.co.tz

๐Ÿ™
02/12/2024

๐Ÿ™

02/12/2024

LEO DISEMBA 2 TUNAYAKUMBUKA MAISHA MTAKATIFU BIBIANA, MFIADINI(363)

Hatujui kwa hakika matokeo ya kufa kwake Biiana, ila katika Karne ya tano Wakristo wa Roma(Italia) walikuwa na Kanisa la Mfiadini Mtakatifu Bibiana inasemekana kwamba alizaliwa Roma katika Ukoo wa Watu wenye Cheo na Heshima, lakini jambo lililo muhimu zaidi ni kwamba asili ya Ukoo huo ilikuwa ya Kikristo kwa kuwa Wazazi wake Flaviano na Dafrosa walikuwa wafiadini walioteswa na kuuawa na Yuliano aliyekuwa mkana Dini.

Wazazi wake walipokufa yeye na dada yake Demetria walinyangโ€™anywa mali zao zote. Walijaribiwa kwa mabembelezo na vitisho na liwali wa mji ili waiache Imani yao ya Kweli lakini wakiwa hodari na Imara, waliuchukia upotovu wa liwali huyo.

Taarifa zinasema kwamba Demetria, alipofariki liwali alimpeleka Bibiana kwa Mwanamke Mwasherati ilimradi ampevushe na kuuharibu Ubikira wake, lakini hakufaulu hata kidogo, kinyume chake Mwanamke yule alipouona Uthabiti wa Bibiana aliongoka naye akawa Mkristo.

Liwali aliposikia hayo aliingiwa na ghadhabu akatoa Amri Bibiana avuliwe nguo Wamfunge mikono na Miguu wampige Fimbo, Alipigwa hata na kazimia Mwisho akakata Roho na mwili wake ulitupiwa mbwa nao hawakuugusa.

Wakristo walikuja wakauzika Mwili huo kwa Heshima, alikufa Mwaka 363 wakati wa mateso yaliyoenezwa na Kaisari Yuliano Mkana Dini.

MTAKATIFU BIBIANA MFIADINI UTUOMBEE.

15/11/2024

Dhambi ni chukizo mbele za Mungu

Address

Morogoro Road
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tmcs lita morogoro posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share