True Light Church Tlc

True Light Church Tlc TRUE LIGHT CHURCH (TLC)
MAHALI: TEGETA KWA NDEVU, TANZANIA. KANISA LIKO MKABALA NA JENGO LA GDBP

Bwana Yesu asifiwe.Kanisa la True Light Church Dar es salaam tunaomba kipekee kukukaribisha kwenye semina ya Maalumu ya ...
03/04/2026

Bwana Yesu asifiwe.

Kanisa la True Light Church Dar es salaam tunaomba kipekee kukukaribisha kwenye semina ya Maalumu ya Pasaka ambayo itafanyika siku ya Ijumaa pamoja na Jumapili .

Mtumish wa Mungu Askofu Lotha Laizer kutokea Arusha atakuwa mgeni akifundisha na kuombea watu kwenye semina hii.

Kwenye semina hii Mtumishi wa Mungu atakufundisha NAMNA DAMU YA YESU INAVYOWEZA KUKUSAIA KUTOKA KWENYE VIFUNGO VYA SHETANI.

Watu wengi hawajui Namna Damu ya Yesu inavyoweza kuwasaidia kumshinda shetani na Kila njama zake .

Ufunuo wa Yohana 12:11
[11]Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
And they overcame him by the blood of the Lamb, and by the word of their testimony; and they loved not their lives unto the death.

Semina hii itafanyika Ijumaa ya Pasaka tarehe 3/4/2026 Kuanzia saa kumi jioni na Jumapili ya Pasaka Kuanzia saa nne Asubuhi .

Ni siku mbili tu za KUJUA Siri za rohoni za Namna ya Kumshinda Shetani na Njama zake .

Kwenye semina hii tutakuwa na Waimbaji mbalimbali wakiongozwa na Wana wa Asafu .

Nikuombe popote ulipo USIKOSE kwenye semina hii muhimu .

WAALIKE WATU WENGI KADIRI UWEZAVYO .

Wako ,
Prophet AJ Mazengo
Mchungaji Kiongozi
True Light Church _Worldwide .
MAWASILIANO 0716854881

JESUS IS ALIVE COME AND SEE

TAARIFA MUHIMU KWA WASHIRIKA WA KANISA LA TRUE LIGHT CHURCH -DSMKanisa likiwa na Roho ya Maombi litakuwa tu na Roho ya U...
23/03/2026

TAARIFA MUHIMU KWA WASHIRIKA WA KANISA LA TRUE LIGHT CHURCH -DSM

Kanisa likiwa na Roho ya Maombi litakuwa tu na Roho ya Uamsho. Maombi na Uamsho vyote hutokana na Roho huyo huyo mmoja, Roho Mtakatifu.

Kanisa la True Light Church Dar es salaam kupitia Idara ya Maombi wanakukaribisha kwenye Maombi ya Mfungo wa siku mbili .
Maombi haya yataanza kesho Jumanne tarehe 24/03/2026 mpaka jumatano tarehe 25/03/2026.

Niwaombe washirika wote wa kanisa la True Light Church Dar es salaam Kuanzia kesho tutakuwa na Mfungo wa Siku mbili wa masaa 12.

Kila siku saa 11:00 JIONI tunakutana kanisani kuomba Kwa pamoja .

Tutakuwa tukimlilia Mungu tumalize Mwezi huu wa tatu tukiwa salama na tuanze Mwezi tukiwa salama .
Na kuombea kilele Cha week ya Wanawake ambacho kitahitimishwa jumapili Kwa Kongamano kubwa la Wanawake wote wanaopatikana Katika MJI WA DAR ES SALAAM.

Wako ,
Mkurugenzi wa IDARA ya Maombi
Minister Isaya Jerome
True Light Church Dar es salaam
Mawasiliano 0690399511

Kupitia Kwa .
Mwenyekiti WA IDARA ya Maombi
Minister Anna Masawe
True Light Church Dar es salaam
Mawasiliano.0676723695

Coordinator IDARA ya Maombi
Minister Mary adidas
True Light Church Dar es salaam
Mawasiliano 0678648358

26/02/2026

Bwana Yesu asifiwe.
Kipekee Naomba kukukaribisha kwenye KONGAMANO LA WATUMISHI WA MUNGU WOTE TANZANIA .Kongamano hili linaenda Kwa jina la FLYING WITH WINGS MINISTERS CONFERENCE ambalo litafanyika jumapili hii tarehe 01/03/2026 Kuanzia Saa Nane Mchana kwenye Kanisa la True Light Church _Tegeta Kwa Ndevu Darajani.

Kongamano hili litahudhuriwa na Wazee wa zamani ,Mababa zetu wa Sasa na Kizazi kipya ambacho ndiyo kinachipukia na kinaandaliwa kuchukua kijiti .Niwaombe Wazee wetu Mababa Askofu ,Mitume , Manabii , Wainjilisti , Wachungaji,Walimu , Viongozi wa Makanisa na Watumishi wote wa Mungu mnaopatikana kwenye mji wa Dar es salaam na nchi ya Tanzania kuhudhuria Kongamano hili la siku Moja .

Haya ni Majira ya Kanisa la Tanzania kusimama pamoja Kwa ajili ya ufalme wa Mungu na kazi yake .

Tutakuwa na muda mzuri wa Kujifunza Neno la Mungu Kwa kina zaidi .K**a una kiu ya kuacha alama Kwenye uso wa nchi uliyopewa uimiliki Usipange kukosa .

Wako ,
Prophet AJ Mazengo
True Light Church World wide
MAWASILIANO Vd 0769684881 Tg 0716854881

KWA GARAMA YOYOTE USIKOSE

Kanisa la True Light Church Tlc  _Dar es salaam. linakuKaribisha kwenye Ibada maalumu ya UKOMBOZI WA FAMILIA .Mara nying...
21/02/2026

Kanisa la True Light Church Tlc _Dar es salaam. linakuKaribisha kwenye Ibada maalumu ya UKOMBOZI WA FAMILIA .
Mara nyingi adui hupambana na Msingi wa Familia Kwa sababu familia ndiyo lango la kutengeneza watu imara na watakaokuwa na matokeo Katika kizazi husika .

JUMAPILI hii Mtumishi wa Mungu ambaye amekuwa baraka katika ardhi ya Tanzania na nje ya Tanzania Bishop Lotha Laizer atatufundisha NAMNA UNAVYOWEZA KUINUA FAMILIA YENYE MISINGI IMARA na atafanya Maombi ya ubarikio Kwa familia yako Kwa ajili ya Mwaka 2026

Mara nyingi Adui hupambana na Familia na Uzao wa FAMILIA na hatma za wanafamilia .

Musa alipitia vita Katika umri wake mdogo .Yesu alikutana na vita Katika Mwanzo wake mdogo .
Samson alikutana na upinzani Katika Mwanzo wake mdogo.

K**a mkono wa Mungu usiposimama na wewe pamoja na Familia yako Kuna baraka ambazo Mungu amezikusudia Kwako na familia yako lakini hazitakaa zidhihirike katika macho ya nyama.

Ungana nasi Kwenye Ibada maalumu ya Familia Kwenye kanisa la True Light Church_Tegeta Kwa Ndevu Darajani.
Ibada hii itaanza saa tatu na nusu Asubuhi .

Wasiliana nasi Kwa Voda 0769684881 Tigo 0716854881

Wako,
Prophet AJ Mazengo
True Light Church (TLC)

Jesus is Alive ,Come and See

13/02/2026

POPOTE ULIPO KWENYE MJI WA DAR ES SALAAM

Karibu Jumapili hii kwenye USIKU WA NIMPENDAYE KATIKA KWELI
Usiku huu ambao ni maalumu kwa wale wapendanao na wampendao Kristo umeandaliwa na Idara ya Vijana ya kanisa .

Kwenye siku hii kutakuwa na keki maalumu ya KUMBUKIZI YA MIAKA KADHAA YA NDOA kwa Wana ndoa wazamani na wapya .

Tunaomba popote ulipo jiandae na MWANDAE na Mwenzako .

Wale mlioko single msiwaze itakuwaje yamkini Bwana akawa na JIBU lako siku hiyo na Yeye aliyezifanya mbingu atakushangaza .

Wazee wenzangu karibu tuungane na Vijana ili kuwatia akili ili wajue yawapasayo kutenda

NI JUMAPILI HII KUANZIA SAA KUMI NA MBILI JIONI

Ukibaki Nyumbani ni Kwa Hasara yako.

Kipekee Nikukaribishe kwenye Ibada maalumu ya SHOW ME YOUR GLORY(NIONYESHE UTUKUFU WAKO jumapili kuanzia saa tatu na nus...
24/01/2026

Kipekee Nikukaribishe kwenye Ibada maalumu ya SHOW ME YOUR GLORY(NIONYESHE UTUKUFU WAKO jumapili kuanzia saa tatu na nusu Asubuhi .

Ibada maalumu ya kumsihi Mungu atuonyeshe utukufu wake kwenye maisha yetu .K**a Kuna mahali tumekuwa tukitembea bila majibu kwenye Ibada ya kesho Bwana atatupatia majibu ya Yale tumeyatamani Kwa muda mrefu .

Naamini Mungu atasimama katikati yetu na kujitukuza kwetu .

JE NI ENEO GANI UNATAMANI KUUONA UTUKUFU WA BWANA ?
🔴 Mahusiano na Ndoa
🔴Biashara
🔴Kazi
🔴Familia
🔴Kuponywa
🔴Kufunguliwa kutoka kwenye minyororo ya Giza
🔴Kuinuka kimaisha

Mungu atakuwepo kwenye Ibada ya Jumapili hii kutuonyesha utukufu wake .

Naomba waalike Watu kadiri uwezavyo wasikose Ibada hii ya baraka .Na sambaza taarifa hizi kwa Watu wote .

Wako,
Prophet AJ Mazengo
True Light Church_Worldwide

Familia ya True Light Church(TLC) tunapenda kuwapa pole  Ndugu zetu watanzania na Familia ambazo walipoteza Ndugu zao na...
04/11/2025

Familia ya True Light Church(TLC) tunapenda kuwapa pole Ndugu zetu watanzania na Familia ambazo walipoteza Ndugu zao na Wapendwa wao .Faraja ya Mungu iwe nanyi katika kipindi hiki na Mungu ayakumbuke machozi yenu
Tunaamini Haki huinua taifa;
Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.

Karibu kwenye SIKU TANO za maombi ya KUFUNGA NA KUOMBA.SIKU TANO MAALUMU ZA KUPOKEA UPAKO WA OMEGA Ni Kuanzia  jumatatu ...
01/07/2025

Karibu kwenye SIKU TANO za maombi ya KUFUNGA NA KUOMBA.

SIKU TANO MAALUMU ZA KUPOKEA UPAKO WA OMEGA

Ni Kuanzia jumatatu tarehe 30/06/2025 mpaka ijumaa tarehe 4/07/2025 ya week hii.

Kila jambo lenye mwanzo mwema lazima liwe na mwisho mwema
Na mojawapo ya eneo unaweza kupata mwisho mwema ni kupitia kumlilia Mungu ili aachilie mema kwenye maisha yako kupitia kufunga na kuomba.

Ndani ya siku hizi Tano tutakuwa tukimuomba Mungu atupe UPAKO WA KUWA NA MWISHO MWEMA NDANI YA MWAKA HUU WA 2025 KWA MIEZI SITA ILIYOBAKI

Siku hizi Tano za maombi ni maalumu kwa ajili ya Kuomba MKONO wa Mungu uende nasi katika MIEZI sita iliyobaki.

Mtumishi wa Mungu Musa alimlilia Mungu ili aende Pamoja naye katika njia yake ili maisha yake yafanikiwe katika siku alizokuwa anaziendea .

Kutoka 33:15
[15]Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa
And he said unto him, If thy presence go not with me, carry us not up hence.

Hata sisi tunatamani kumuona Mungu akienda Pamoja nasi katika MIEZI sita iliyobaki ndiyo maana tumetenga siku HIZI Tano za kuomba na kufunga .

Tunakutana kanisani kuomba kuanzia saa kumi na Moja jioni Kila jioni.

TAMBUA MUNGU HAWEZI KUFANYA KITU CHOCHOTE KWENYE MAISHA YAKO HATA K**A ANAKIJUA MPAKA UMUOMBE
Mathayo 7:7-8
[7]Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;*

[8]kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa

MWALIKE NA MWENZAKO AMBAYE HANA TAARIFA HIZI

Imetolewa na
Ofisi ya Mchungaji Kiongozi
Prophet AJ Mazengo
True Light Church -Worldwide
MAWASILIANO 0716-854881

Ungana nasi kwenye Ibada ya kesho ya ufungulivu na uponyaji .Je Kuna jambo Gani kwenye maisha yako unahisi haliendi sawa...
20/07/2024

Ungana nasi kwenye Ibada ya kesho ya ufungulivu na uponyaji .
Je Kuna jambo Gani kwenye maisha yako unahisi haliendi sawa na linahitaji Mkono wa Bwana wa uponyaji na ufungulivu ?
Kesho Neema ya Mungu ya kutusaidia kutoka kwenye Kila udhaifu na Kila ugonjwa itakuwa katikati
yetu .
Ni pale pale MJI WA BWANA Tegeta Kwa Ndevu Darajani mkabala na jengo la GDBP.

17/07/2024

Naomba kipekee kukukaribisha kwenye Ibada MAALUMU ya kumshukuru Mungu Kwa mwaka mmoja WA Huduma ya True Light Church Tlc Tawi la Dar es salaam .
Tunakiri kuwa Mkono wa Bwana ndiyo uliotubeba mpaka kufikia hatua hii .

Yapo mengi tuliyoyapitia mengine yalikuwa ya kutuangamiza lakini mkono wa Bwana ulisimama nasi kututetea .
Mungu alituinulia jeshi la watu ambao walijitoa usiku na Mchana Kwa ajili yetu.

Hakika Mungu amekuwa Baba ,Mpenzi na rafiki kwetu .

Tarehe 4/8/2024 ndiyo Siku yetu Maalumu ya kupeleka shukrani zetu za pekee mbele za Bwana na kiti chake Cha enzi Kwa yote aliyotutendea tangu tumeingia katika Mji huu wa Dar es salaam na kumjengea Madhabahu.

K**a si Bwana kuwa pamoja nasi hatungekuwa lolote Wala chochote.Ule mkono uliotusaidia kuwa hapa ndiyo tunaulilia tena utupeleke katika vimo na Viwango vikubwa ambavyo tusingeweza kwenda Kwa akili na nguvu zetu .

Address

Tegeta Kwa Ndevu
Dar Es Salaam
DARESSALAAM_

Telephone

+255716854881

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when True Light Church Tlc posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to True Light Church Tlc:

Share