Bethel Deliverance Center

Bethel Deliverance Center Bethel Deliverance Center ni Madhabahu ya Kiagano inayojibu kwa Moto

MISSION:
To provide believers with a full deliverance of their spirit, minds, and physical so as to help their community national and international wise by accomplishment of the saints in the body of CHRIST.

HERI YA MWAKA MPYA 2026 TUNAOUTARAJIA, TUKIJALIWA.Wakolosai 3:23-24.Tulichokianzisha kwa gharama kubwa tutakilea kwa dha...
29/12/2025

HERI YA MWAKA MPYA 2026 TUNAOUTARAJIA, TUKIJALIWA.

Wakolosai 3:23-24.

Tulichokianzisha kwa gharama kubwa tutakilea kwa dhamira kubwa. Tutafanya hivi tukijua kwamba kuanzisha jambo kubwa ni ujasiri lakini kuliendeleza ni uwajibikaji.

Ndugu zangu, Ujumbe wangu wa Mwaka Mpya tunaoutarajia ni huu:

Hatuanzishi vitu ili baadaye tuje tuviachie vififie na hatimaye kufa kwa kuvitelekeza. K**a hilo lingekuwa lengo letu tangu mwanzo, basi tungejiuliza kwa dhati: Kwa nini tulitumia muda wetu, nguvu zetu, na rasirimali zetu za thamani kuvianzisha? Ukweli ni mmoja—hakuna anayepanda mbegu akiwa na matumaini ya kuvuna majivu.

Tulianzisha haya mambo kwa sababu tuliona thamani yake. Tuliona mustakabali wake. Tuliona namna ambavyo yangeweza kukua, kustawi, na kuwa baraka kwetu sisi na kwa wengine. Ndani ya kila hatua ya mwanzo kulikuwa na ndoto, matumaini, na imani kuwa juhudi zetu hazitakuwa bure.

Changamoto njiani hazipaswi kuwa sababu ya kukata tamaa, bali ziwe kumbusho la kwa nini tulianza. Kila kitu chenye thamani hupitia misukosuko kabla hakijaimarika. Ni wajibu wetu kusimama imara, kurekebisha pale panapohitaji kurekebishwa, na kuendelea kusukuma mbele hata pale panapochosha.

Tusikubali vile tulivyovianzisha kwa gharama kubwa vife kwa sababu ya uzembe, woga, au kukosa umoja. Badala yake, tushikane, tushirikiane, na tuvilee kwa bidii mpya. Kwa kufanya hivyo, si tu kwamba tutavihifadhi, bali tutaviona vikikua na kuleta matunda ambayo yatakuwa fahari yetu sote.

Huu ni wakati wa kuchagua—kuacha au kuendeleza.

Mimi nimechagua kuendeleza. Mwenzangu, ndugu yangu, umechagua lipi?

TWAA TENA! Tawi la Mzabibu Unaozaa!

Hali nikijaa shukrani za neema kwa 2025, nakutakia wewe pamoja nami mwaka 2026 wenye heri na mibaraka ya kushangaza! Amina.

Pastor Innocent Kapenda
Man of Grace

SIKUKUU YA VIJANA - BETHEL“Saved by Grace” — Waefeso 2:8–92026 - Tumechagua kuendeleza bila kuchoka, tukisimama imara ka...
28/12/2025

SIKUKUU YA VIJANA - BETHEL
“Saved by Grace” — Waefeso 2:8–9

2026 - Tumechagua kuendeleza bila kuchoka, tukisimama imara katika imani, tukimtumikia Kristo kwa bidii na uaminifu.

Vijana wa Mungu, tuendelee kung’aa na kuishi neema tuliyopewa!

26/08/2023
Its a great honor to inivite you to  this sunday Service , WORSHIP with Us at BDCT_KinyereziI was happy when they told m...
13/05/2023

Its a great honor to inivite you to this sunday Service , WORSHIP with Us at BDCT_Kinyerezi

I was happy when they told me to go to the Lord's house
______________________________
Nalifurahia waliponiambia twende nyumbani mwa Bwana



Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bethel Deliverance Center posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share