Scripture Union Tanzania

Scripture Union Tanzania SERVING CHILDREN,YOUTH TO TRANSFORM FAMILIES AND WHOLE COMMUNITY

20/07/2026

Kongamano la Watoto katika Kanisa la Filadelfia Nzuguni
Dodoma,
Scripture Union Tanzania kanda ya kati wakifundisha katika kongamano la watoto,

watoto walijifunza kuhusu kujidhibiti, wakihimizwa kujizula kutenda mabaya na kuchagua kufanya' mema katika maisha yao ya kila siku, Lengo lilikuwa kuwajengea maadili mema, tabia njema, na msingi imara wa kumcha Mungu.

"Mwenye kujitawala ni hodari kuliko autekayė mji"
Mithali 16:32

16/07/2026

Neno la Mungu linaendelea kuwafikia wanafunzi wa Mbeya High School, likiwajenga katika maadili mema, kumcha Mungu na kufanya maamuzi yenye hekima. Kupitia ushirika, maombi na mafundisho ya Biblia, wanafunzi wanatiwa moyo kuishi maisha yanayomtukuza Mungu na kuwa taa katika jamii.

"Mwanzo wa hekima ni kumcha BWANA." Mithali 9:10

15/07/2026

Kubadilisha Maisha kwa Neno la Mungu

Neno la Mungu lina nguvu ya kuleta mwanga, kujenga tabia njema na kuelekeza maisha katika njia ya haki. Kupitia huduma za Scripture Union of Tanzania, tunaendelea kuwafikia watoto, vijana na familia kwa mafundisho ya Biblia, ukuzaji wa maadili na uanafunzi unaobadilisha maisha.

Karibu tushirikiane kueneza mwanga wa Kristo katika jamii zetu.

"Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu." Zaburi 119:105

08/07/2026

Hongera Wanafunzi wa Kidato cha Sita Hosteli ya Scripture Union Tanzania! 🎓

Tunamshukuru Mungu kwa mafanikio yenu katika matokeo ya Kidato cha Sita. Bidii yenu, nidhamu, maombi na kujituma vimezaa matunda. Tunawatakia kila la heri katika hatua inayofuata ya masomo na maisha.

Je, unatamani kusoma katika mazingira yanayokupa utulivu wa kujifunza, kukuza maisha ya kiroho, na kukuwezesha kufanya vizuri kitaaluma?

Karibu Hosteli ya Scripture Union Tanzania mahali penye mazingira bora ya kujifunza, malezi ya kiroho, maombi, ushauri, na msukumo wa kufikia ubora wa kitaaluma.

📌Jiunge nasi na ujenge msingi imara wa mafanikio ya kiroho na kielimu.

Hongera tena wahitimu wetu, na karibu wanafunzi wapya!


#ᴠɪʀᴀʟᴠɪᴅᴇᴏ

07/07/2026

🇹🇿 Heri ya Sabasaba!

Sabasaba ni ukumbusho wa fursa, ubunifu na maendeleo ya Taifa. Tuchangie kwa bidii, uadilifu na kumtegemea Mungu katika kila tunachofanya ili kujenga Tanzania yenye maadili na matumaini.

"Mkabidhi Bwana kila ufanyalo, naye atayathibitisha mawazo yako." Mithali 16:3

Tunawaombea baraka tele katika biashara, kazi na familia zenu.

Mungu ibariki Tanzania. 🇹🇿

Salama kutoka kwa mkurugenzi wa Kimataifa wa Scripture Union Scripture Union International Salamu kwa Jumuiya zote za Um...
05/07/2026

Salama kutoka kwa mkurugenzi wa Kimataifa wa Scripture Union Scripture Union International

Salamu kwa Jumuiya zote za Umoja wa Kujisomea Biblia (Scripture Union) duniani!

Ni furaha kubwa kwangu kuwatumia salamu zangu za dhati kila mmoja wenu. Asanteni kwa uaminifu wenu katika kuwahudumia watoto, vijana, na familia katika jamii mnazozihudumia.

Nawatia moyo kuendelea kusimama imara katika utume wenu wa kuhamasisha ushiriki na Neno la Mungu, mkisaidia watu wasilisome tu Biblia, bali pia walipende Neno la Mungu, walielewe, na kuliishi kila siku.

Tunapoendelea kushiriki Maandiko kwa uaminifu, na iwe watoto, vijana, na familia wengi zaidi wamjue Mungu binafsi, wampende kwa moyo wote, wakue kiroho, na wapate uzoefu wa nguvu za Yesu Kristo zinazobadilisha maisha.

Asanteni kwa kujitoa kwenu, maombi yenu, na huduma yenu ya uaminifu. Bwana awatie nguvu na kuwatia moyo mnapoendelea kufanya wanafunzi na kuleta tumaini kupitia Neno Lake.

Mungu azibariki kwa wingi Jumuiya zote za Umoja wa Kujifunza Biblia tunapoendelea kumtumikia pamoja kwa utukufu Wake.

Kwa salamu za upendo na maombi,

Monika
Mkurugenzi wa Kimataifa, Scripture Union

30/06/2026

Masomo waliyojifunza watoto katika programu ya Bible engagement.

Kutibu majeraha ya ndani; Kuwasaidia kujenga moyo wa msamaha, uponyaji wa kihisia na kumtumaini Mungu.

Marafiki; Kuwafundisha umuhimu wa kuchagua marafiki wenye tabia njema wanaowahamasisha kufanya yaliyo mema.

Usafi wa mwili na roho; Kuwajengea utamaduni wa usafi pamoja na maisha ya utakatifu yanayompendeza Mungu.

Tunaamini watoto wanaofundishwa maadili na Neno la Mungu leo, hukua kuwa watu wenye tabia njema na msingi imara wa maisha ya baadaye.





24/06/2026

Tulipata nafasi ya kumtembelea mzee wetu Eliapenda Chuwa katika makazi yake ya Mbokomu, Moshi. Ilikuwa ni wakati wa baraka na furaha kubwa, ambapo alifurahi sana kutuona na kututumia salamu nyingi za upendo na shukrani kwa wana UKB.

Ziara k**a hizi huimarisha upendo, umoja na mshik**ano wetu, huku zikitukumbusha umuhimu wa kuwathamini na kuwajali wazee wetu. Pia hutupatia fursa ya kujifunza kutoka katika uzoefu wao na kuwafariji kwa uwepo wetu.

Tunaendelea kumwombea afya njema, amani na nguvu zaidi katika Bwana.

ScriptureUnionOfTanzania #

Address

Kalenga Street Upanga Dar Es Salaam Tz
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Scripture Union Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Scripture Union Tanzania:

Shortcuts

Share