Alain Morisho Ministries

Alain Morisho Ministries Mafundisho ya NENO LA MUNGU
UNABII na UDHIHIRISHO WA NGUVU ZA MUNGU.
“Mafundisho yabadilishayo maisha”
“Nguvu ifunguayo hatma”

Mpendwa, wakati tunakaribia mwisho wa mwezi huu, leo tena nakuja na Habari kutoka kwa Mungu! Je kuna hali au kitu kimeku...
05/04/2026

Mpendwa, wakati tunakaribia mwisho wa mwezi huu, leo tena nakuja na Habari kutoka kwa Mungu! Je kuna hali au kitu kimekumeza? Je umebanwa kwenye eneo fulani la maisha toka siku nyingi? Je uko mahali pa giza hauoni njia ya kutoka? Mungu anataka kusema na hiyo hali ili ikuachie! Fanya k**a Yona, omba bila mashaka ukiwa na imani! Usikate tamaa! Mungu ni Bwana juu ya kila kitu duniani! Akisema lazima hiyo hali itii neno la Mungu! Kwa hiyo uwe tayari kutoka, Bwana ananena na samaki ili akutapike; atapike ndoa yako, atapike cheo yako, atapike watoto wako, atapike pesa yako, nk.

Fanya maombi haya:
Mungu, nena na samaki ili atapike baraka zangu zote kwa jina la Yesu Kristo !!!

Christ in Us, Hope of Glory

Sijui wapi umeanguka lakini utainuka tena,usikubali kubaki chini. Biashara imeanguka? utainuka tena, kazi imeanguka? uta...
04/04/2026

Sijui wapi umeanguka lakini utainuka tena,usikubali kubaki chini. Biashara imeanguka? utainuka tena, kazi imeanguka? utainuka tena, uzao umeanguka? utainuka tena, nk. Umuamini Mungu kukuinua tena. K**a wewe ni mwenye haki, usinung’unike, inuka tu na kila kitu Kitanunu!

Fanya maombi haya:
Mungu uniinue tena kwa jina la Yesu Kristo !!!

Christ in Us, Hope of Glory.

Nataka niseme hivi kuendelea kwa vita kusikusumbue, maadui zako wakiamua kuendelea kukupiganisha hata usiangaike, wakifa...
03/04/2026

Nataka niseme hivi kuendelea kwa vita kusikusumbue, maadui zako wakiamua kuendelea kukupiganisha hata usiangaike, wakifanya hivyo ni kwa hasara yao wenyewe !

Mungu akisimama upande wako vita vitaendelea lakini wewe utastawi na wao watadhoofika ! Ujiandae kuona wanaokupinga kudhoofika, wale wote waliokusumbua miaka yote hii, umefika wakati wako wa kustawi na wao kudhoofika !

Fanya maombi haya:
Mungu pamoja na vita vyote naomba unipe kustawi na adui zangu wadhoofike kwa jina la Yesu Kristo !!!

Christ in Us, Hope of Glory

Msamaha! Msamaha ni muhimu! Unaweza kuwa na sababu za msingi, za maana na za kweli za kutokusamehe mtu. Inawezekana hata...
02/04/2026

Msamaha! Msamaha ni muhimu! Unaweza kuwa na sababu za msingi, za maana na za kweli za kutokusamehe mtu. Inawezekana hata huyo mtu hajaomba msamaha kwako, hata hajatambua makosa yake.

Pamoja na haya yote, unatakiwa kusamehe tu! Samehe mpendwa, maana usiposamehe, wewe pia Mungu hatokusamehe. Na Mungu asiposamehe makosa yako, hali yako itakuwa mbaya kabisa. Kwa hiyo kwa faida yako mwenyewe, uwasamehe watu!

Fanya maombi haya:
Leo nafungua moyo wangu ili kusamehe walionikosea kwa jina la Yesu Kristo !!!

Christ in Us, Hope of Glory.

MWEZI WANGU WAKUCHAGULIWA=> Mwezi huu wa nne wa mwaka 2026, Mungu amedhamiria akupe kibali. k**a Mungu alivyomchagua Dau...
01/04/2026

MWEZI WANGU WAKUCHAGULIWA

=> Mwezi huu wa nne wa mwaka 2026, Mungu amedhamiria akupe kibali. k**a Mungu alivyomchagua Daudi na chaguo lile likabadilisha maisha ya Daudi kabisa, na wewe Mungu anataka kukuchagua na anataka uchaguliwe. ni mwezi wa chaguo la Mungu kuonekana maishani mwako, lakini ni mwezi wa watu kukukubali na kukuchagua wewe kwa kila fursa, na nafasi za baraka.

=> K**a ulikua unakataliwa, unaachwa, hautambuliki na unasahauliwa. mwezi huu ndio mda wa kukataa hizo hali. Ukijua na kuamini kwamba Bwana mwenyewe amekuchagua na ameamuru watu wakuchague ili upate nafasi mpya

Kiri baraka hizi juu ya mwezi wako :
1. Mda wa kukataliwa umekwisha, ni mwezi wa Bwana kunichagua na kunipa kibali.
2. Kila roho ya kukataliwa na kutokuchaguliwa imeshindwa na kuondolewa.

3. kila siku ya mwezi huu imeletwa ili nichaguliwe na kuinuliwa.

4. Bwana mwenyewe ananichagua na anasababisha mimi kuchaguliwa mwezi huu.

5. Ninakiri nitamaliza mwezi huu nikiwa nimechaguliwa kupata nafasi mpya

Ninatangaza baraka hizi juu yangu kwa jina la Yesu Kristo!!!

Christ in Us, Hope of glory.

Naongea na mtu mmoja tu siku ya leo, rudi utii Mungu alichokuambia! Kuna mwingine anasema mbona ni jambo dogo tu, naumia...
31/03/2026

Naongea na mtu mmoja tu siku ya leo, rudi utii Mungu alichokuambia! Kuna mwingine anasema mbona ni jambo dogo tu, naumia kivipi? Inatupasa kumtii Mungu kwa makubwa na madogo.

Mungu anasema ni dogo kweli lakini usipomtii kwa haka kadogo utaumia vibaya! Yani nakuomba tii kile Mungu alichosema k**a alivyosema, usijaribu kubadilisha, utaumia tu! Usijaribu kutumia udanganyifu, kupaka makosa yako make-up , Mungu hadanganyiki, utaumia mpendwa!
Nasema tena tii sauti ya Mungu, Mungu hataki uumie!

Fanya maombi haya:
Mungu ninaamua kukutii, nisiumie kwa jina la Yesu Kristo !!!

Christ in Us, Hope of Glory.

Mpendwa, kiburi sio kitu kizuri, tena ni sumu kabisa ! Unapoona kiburi kinakaribia, fahamu kabisa kwamba aibu haipo mbal...
30/03/2026

Mpendwa, kiburi sio kitu kizuri, tena ni sumu kabisa ! Unapoona kiburi kinakaribia, fahamu kabisa kwamba aibu haipo mbali ! (Sio mimi nasema, Biblia imesema). Endapo kiburi kinaanza kuinuka moyoni mwako kumbuka aibu haipo mbali. Tujitahidi kukataa kiburi na kuelekeza mioyo yetu kwenye unyenyekevu, tutapata heshima zaidi. Usidanganyike mpendwa ukiipa nafasi kiburi, utaaibika kwa namna moja au nyingine. Uwe makini !

Fanya maombi haya:
Nakataa roho ya kiburi kwa jina la Yesu Kristo !!!

Christ in Us, Hope of Glory

Ndugu,leo Bwana amekuletea neno la marejesho na badiliko! Bwana yuko tayari kukusimamisha upya, kuziba palipobomoka, na ...
29/03/2026

Ndugu,leo Bwana amekuletea neno la marejesho na badiliko! Bwana yuko tayari kukusimamisha upya, kuziba palipobomoka, na kujenga upya kila kitu maishani mwako! Uamini neno hili na kumtegemea Bwana na utaishi miujiza na maajabu!

Fanya maombi haya:
Mungu baba, ninaamini na kukiri kwamba huu ni mda wa marejesho, kujengwa na kusimama upya kwa jina la Yesu Kristo !

Christ in Us, Hope of Glory

Kumbukeni! Biblia leo inakumbusha jambo lililojitokeza mwanzo ili tukumbuke. Tukumbuke nini? => Dhambi inamchukiza Mungu...
28/03/2026

Kumbukeni! Biblia leo inakumbusha jambo lililojitokeza mwanzo ili tukumbuke. Tukumbuke nini? => Dhambi inamchukiza Mungu! Mungu anahukumu dhambi. Mungu anatuma moto kuteketeza watenda dhambi sasa hivi na kwa hukumu ya milele.

Kwa hiyo tusisahau kuna moto wa milele lakini pia kuna moto unaoweza kuwaka mda wowote ule maishani mwetu sasa hivi tukiwa tunacheza kwenye dhambi. Na k**a hukumu haijatukuta ni kwamba Mungu anatupa mda wa kutubu. Kwa hiyo, tutubu kabla moto haujawaka na kabla moto wa milele haujakaribia.

Fanya maombi haya:
Mungu, samehe dhambi zangu na uniondolee hukumu kwa jina la Yesu Kristo !!!

Christ in Us, Hope of Glory.

Watu wengi wanajituma sana kwenye kazi zao ila ikifika kwenye mambo ya Mungu wanakuwa wavivu; wavivu kwenda kanisani, wa...
27/03/2026

Watu wengi wanajituma sana kwenye kazi zao ila ikifika kwenye mambo ya Mungu wanakuwa wavivu; wavivu kwenda kanisani, wavivu kusoma Biblia, wavivu kuomba, wavivu kutoa sadaka, wavivu kumtumikia Mungu, nk.

Matokeo ya hayo yote ni kuwa watu ambao hawamjui Mungu na wanakuwa watu wasio na matunda. Ndugu bidii unayotumia kutafuta pesa, tumia zaidi kumtafuta Mungu! Vitu vya kiMungu viwe kwako na viwe kwa utele upate kumjua Yesu na kuzaa matunda!

Fanya maombi haya:
Nataka niwe mtu anayetoa matunda kwa sababu ya kumjua Bwana Yesu, nisiwe mvivu ila nijae tele na nitoe matunda kwa jina la Yesu Kristo !!!

Christ in Us, Hope of Glory.

Nataka tu nikutaarifu au nikukumbushe kwa mujibu wa maandiko haya kwamba muovu yupo kazini tayari! Usizubae, ulimwengu m...
26/03/2026

Nataka tu nikutaarifu au nikukumbushe kwa mujibu wa maandiko haya kwamba muovu yupo kazini tayari! Usizubae, ulimwengu mzima umeshaanza kusongwa na kuendeshwa na nguvu ya kuasi.

Na K**a haijatawala kabisa ni kwa sababu bado inazuiliwa hadi Mungu atakapoondoa walio wake! Kwahiyo tunatakiwa kukesha na kuambata sana na Mungu tusije tukapotea!

Fanya maombi haya:
Mungu uniepushe na ushawishi wote wa nguvu ya uovu utendayo kazini ulimwenguni kwa jina la Yesu Kristo !!!

Christ in Us, Hope of Glory

23/03/2026

Wiki hii Bwana anasema na wewe, PANDA! Mungu ameshaweka kila kitu mbele yako, Mungu ameshamaliza, kazi ni kwako kutenda kwa imani. kataa ile roho ya kufadhaika inayokufanya kuangalia nyuma kila saa, inakuchelewesha.

Kataa roho ya uoga inayokuzuia usithubutu kupiga hatua, inayosababisha hata akili yako isifikirie kwenda kumiliki. inuka leo maana wiki hii kuna mlango na njia mbele yako KUPANDA na KUMILIKI. Mungu wako anasema mda umefika, kila kitu kipo tayari, nenda na uanze kupiga hatua utauona mkono wa Bwana wiki hii!

Fanya maombi haya:
1. Ninaondoa roho ya hofu inayonikwamisha
2. Ninaondoa roho ya kufadhaishwa inayonichelewesha
3. Alichokinena Mungu juu ya maisha yangu kitatokea
4. wiki hii ninapanda viwango na kutamalaki vya kwangu

Ninatangaza baraka hizi juu yangu kwa jina la Yesu Kristo!!!

Christ in Us, Hope of Glory

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Wednesday 17:00 - 19:00
Friday 17:00 - 19:00
Sunday 09:00 - 12:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Alain Morisho Ministries posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Alain Morisho Ministries:

Share

Category