Viwawa Parokia ya Mt. Maurus, Kurasini

Viwawa Parokia ya Mt. Maurus, Kurasini Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Viwawa Parokia ya Mt. Maurus, Kurasini, Religious Center, Kurasini, Dar es Salaam.

Muonekano wa juu wa Parokia ya Mt. Maurus - Kurasini
05/01/2023

Muonekano wa juu wa Parokia ya Mt. Maurus - Kurasini

21/06/2022

Maandamano ya Ekaristi Takatifu, Waamini wa Parokia ya Mt. Maurus - Kurasini.
"Huyu ni Yesu kutoka Mbinguni, kikombe hiki ni amana ya upendo"

Misa hiyo iliongozwa na Mhashamu Anthony Gaspar Lagwen, Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu.

Matukio katika Picha Maandamano ya Ekaristi Takatifu, Waamini wa Parokia ya Mt. Maurus - Kurasini."Huyu ni Yesu kutoka M...
21/06/2022

Matukio katika Picha Maandamano ya Ekaristi Takatifu, Waamini wa Parokia ya Mt. Maurus - Kurasini.
"Huyu ni Yesu kutoka Mbinguni, kikombe hiki ni amana ya upendo"

Misa hiyo iliongozwa na Mhashamu Anthony Gaspar Lagwen, Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu.
Pc:
Cc:

02/08/2021

Usipitwe na KMK GALA katika Kushehekea Miaka 33 ya Uinjilisha ya Kwaya ya Mt. Kizito Makuburi kutoka Parokia ya Mwenyeheri Anuarite, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Katika Shule ya Sekondari ya Loyola Jumapili 08/08/2021 Moto wa Utume utawaka. Jipatie Tiketi Sasa uweze kushuhudia Makuu ya Mungu katika Utume huu wa Uimbaji.

15/02/2021

Kwaya ya Vijana Mt. Yohane Paul II - VIWAWA Kurasini katika Ziara ya Kitume iliyofanyika Parokia ya Mt. Theresia was Mtoto Yesu - Vingunguti.

26/09/2020

Hivi ndivyo UWAKA Parokia ya Mburahati walivyoingia katika Viwanja vya Loyola Secondary School katika Warsha ya UWAKA Jimbo Kuu la Dar es Salaam

Wanaume Katoliki Nguzo Imara Hekalu la Bwana

Ni furaha iliyoje kulelewa katika familia ya Kikristu, inahitajika kuwa muangalifu kufuata maelekezo ya wazazi.  Wazazi ...
11/07/2020

Ni furaha iliyoje kulelewa katika familia ya Kikristu, inahitajika kuwa muangalifu kufuata maelekezo ya wazazi.
Wazazi ni kioo kwa watoto wao na watoto wanaangalia daima kioo hiki ni faraja iliyoje k**a unaweza kusema "Mimi ni Baba au Mama wa mtoto mnyoofu anayempendeza Mungu na watu."

TANZIARaisi wa Radio Maria Tanzania, ndugu Humphrey Julius Kira,  anawatangazia wanafamilia na wapenzi wa Radio Maria, K...
09/07/2020

TANZIA

Raisi wa Radio Maria Tanzania, ndugu Humphrey Julius Kira, anawatangazia wanafamilia na wapenzi wa Radio Maria, Kifo cha Mwanzilishi wa Radio Maria Ulimwenguni, Mzee Emmanuelle Ferrario, ambaye pia ndiye aliyekuwa Raisi wa kwanza wa Radio Maria Ulimwenguni kote, kilichotokea leo, huko nchini Italia.

Taratibu za Mazishi zinafanyika na zitakapokamilika, tutaendelea kuwaletea taarifa kamili kupitia, ukurasa huu na kupitia Radioni pamoja na kwenye mitandao yote ya kijamii ya Radio Maria Tanzania.

Raha ya Milele uumpe eeeh Bwana na Mwanga wa Milele umuangazie Apmzike kwa Amani Amina.

πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™

RIP Babu FerrarioπŸ™πŸ™
www.radiomaria.co.tz

08/07/2020

Misa ya Upadrisho Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Tuiombee Miito Mitakatifu

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhasahamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi ametangaza Parokia Mpya saba na Paro...
07/07/2020

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhasahamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi ametangaza Parokia Mpya saba na Parokia teule moja. Parokia hizi zimetangazwa wakati wa Adhimisho la Upadrisho kwenye Viwanja vya Msimbazi leo hii.

Parokia Mpya zilizotangazwa ni;
1. Parokia ya Goba Kunguru kutoka Parokia ya Mbezi beach.

2. Parokia ya Goba Mwisho kutoka Parokia ya Mbezi mwisho.

3. Parokia ya Kinzudi kutoka Parokia ya Salasala.

4. Parokia ya Tegeta A kutoka Parokia ya Msumi.

5. Parokia ya Utete kutoka Parokia ya Ikwiriri.

6. Parokia ya Stakishari kutoka Parokia ya Kipawa, Parokia ya Ukonga, Parokia ya Kinyerezi na Parokia ya Segerea)

7. Parokia ya Chakenge kutoka Parokia ya Mji mpya Relini.

Parokia Teule mpya.
1. Parokia teule ya Pande Msakuzi.

Mapadre hawa wapya baada ya Upadrisho walipangiwa Parokia ambazo watakwenda kuhudumu, kati yao Mpadre watano ni wa Jimbo...
07/07/2020

Mapadre hawa wapya baada ya Upadrisho walipangiwa Parokia ambazo watakwenda kuhudumu, kati yao Mpadre watano ni wa Jimbo na Mapadre wawili wa Shirika. Mapadre hao saba waliopata daraja la upadre na majukumu waliopangiwa ni hawa wafuatao;

1. Padre Roniston Semeneses amepangiwa kuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Polycarp (Misugusugu) Kuchukua nafasi ya Padre Saimon Shija ambaye amehamishiwa Parokia ya Manzese k**a Msaidizi wa Paroko.

2. Padre Roland Kashaga amepangiwa kuwa Paroko Msaidizi wa Parokia mpya ya Tegeta A

3. Padre Joseph Osmind Luena amepangiwa kuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mwenyeheri Joseph Alamano (Kibada) kuchukua nafasi ya Padre Titus mwami aliyeamishiwa Seminari ya Visiga kuwa Gombera Msaidizi.

4. Padre Alset Wakhaya amepangiwa kuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Epifania (Kijichi) kuchukua nafasi ya Padre John Mallya anayeenda kuwa Paroko Msaidizi Chakenge.

5. Padre Jorge Mirales amepangiwa kuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Martha (Mikocheni).

6. Pamoja na Mapdre wawili wa shirika ambao ni Padre Peter Chami na Padre Samuel Saguti ambao watapangiwa majukumu na wakuu wao kwenye mashirika wanayotoka.

Tuwaombee hawa Mapadre wapya ili wazidi kudumu katika Imani na kuwavuta watu wengi kwa Kristo kupitia maisha yao.

Upadirsho Jimbo Kuu la Dar es Salaam 07/07/2020
06/07/2020

Upadirsho Jimbo Kuu la Dar es Salaam 07/07/2020

Address

Kurasini
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Viwawa Parokia ya Mt. Maurus, Kurasini posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Viwawa Parokia ya Mt. Maurus, Kurasini:

Share