NCC Outreach

NCC Outreach Kauli Mbiu:
REACH OUT TO STUDENTS AND RESHAPE THEIR DESTINIES BY THE WORD OF GOD

New Creation in Christ Outreach, kwa kifupi NCC-Outreach ni Huduma ambayo imejikita katika kuwafikia WANAFUNZI WA SEKONDARI kwa MAFUNDISHO yatokanayo na Neno la Mungu. Kwenye page hii, utapokea Neno la Mungu linalohusiana na UPONYAJI KILA SIKU, kwa kusudi la kufungua ufahamu wako juu ya UPONYAJI, lakini pia kwa mtu atakaye kuwa tayari, atapata nafasi ya kuombewa ugonjwa wowote ule - Unaotibika hos

pitali au usiotibika; au vifungo vya kipepo au addiction ya kitu chochote - Na Mungu atamuhudumia na kumponya.

Sasa Unaweza kujipatia Mafundisho Ya Mwalimu Francis Langula Ambaye ni mbeba Maono wa Huduma Ya New Creation in Christ K...
08/05/2026

Sasa Unaweza kujipatia Mafundisho Ya Mwalimu Francis Langula Ambaye ni mbeba Maono wa Huduma Ya New Creation in Christ Kupitia Application Ya Neno App.
Francis Langula
Mwl. Francis M. Langula

08/05/2026

Sasa Unaweza kujipatia Mafundisho Ya Mwalimu Francis Langula Ambaye ni mbeba Maono wa Huduma Ya New Creation in Christ Kupitia Application Ya Neno App.
Mwl. Francis M. Langula Francis Langula

08/05/2026

Shalom Watu wa Mungu!!!

Kutokana na Ukuaji wa Huduma na Uhitaji wa Kuifikia Jamii kiupana kwa Njia za Kidigitali

Huduma Ya New Creation in Christ (NCC) inapenda kukufahamisha kuwa Tarehe 06th May .2026

INAZINDUA RASMI New Creation in Christ (NCC) Digital Library ambayo ni APPLICATION YA "NENO APP" Ambayo Itapatikana kwenye vifaa vya kidigitali vyote (SIMU NA COMPUTER)

KATIKA APPLICATION YA NENO APP UTAJIPATIA:-

🎞️ Mahubiri kwa njia ya picha mjongeo [Videos]
🎙️Mahubiri kwa njia ya sauti [Podcast]
📃Masomo Mafupi ya Maandishi
📖 Vitabu kwa njia ya Nakala laini (Softcopy)
📂Ripoti za utendaji wa Huduma ya NCC-OUTREACH

Na Mengine mengi

Fuatilia Video na Tangazo linalofuata kujua namna ya kupata APPLICATION au BONYEZA www.nenoapp.com

Umebarikiwa
Mbeba Maono Huduma Ya NCC
Francis Langula Mwl. Francis M. Langula

08/05/2026

Shalom Watu wa Mungu!!!

Kutokana na Ukuaji wa Huduma na Uhitaji wa Kuifikia Jamii kiupana kwa Njia za Kidigitali

Huduma Ya New Creation in Christ (NCC) inapenda kukufahamisha kuwa Tarehe 06th May .2026

INAZINDUA RASMI New Creation in Christ (NCC) Digital Library ambayo ni APPLICATION YA "NENO APP" Ambayo Itapatikana kwenye vifaa vya kidigitali vyote (SIMU NA COMPUTER)

KATIKA APPLICATION YA NENO APP UTAJIPATIA:-

🎞️ Mahubiri kwa njia ya picha mjongeo [Videos]
🎙️Mahubiri kwa njia ya sauti [Podcast]
📃Masomo Mafupi ya Maandishi
📖 Vitabu kwa njia ya Nakala laini (Softcopy)
📂Ripoti za utendaji wa Huduma ya NCC-OUTREACH

Na Mengine mengi

Fuatilia Video na Tangazo linalofuata kujua namna ya kupata APPLICATION au BONYEZA www.nenoapp.com

Umebarikiwa
Katibu NCC-OUTREACH
KNY Huduma

IlI.HISTORIA YA HUDUMA (KUUNDWA KWA HUDUMA)Huduma ya NCC - Outreach ilianza rasmi kuwafikia wanafunzi Mwaka 2024, ambapo...
01/05/2026

IlI.HISTORIA YA HUDUMA (KUUNDWA KWA HUDUMA)
Huduma ya NCC - Outreach ilianza rasmi kuwafikia wanafunzi Mwaka 2024, ambapo Seminar ya kwanza ya wanafunzi ilifanyika Mkoani Mwanza Tarehe 20.04.2024; na kufuatiwa na Seminar zingine 6 mikoa mingine tofauti. Mpaka sasa, 2026, Huduma imeifikia mikoa 8 nchini Tanzania na kuhudumia shule Zaidi ya 140 Mbeba Maono wa huduma hii ni Mwalimu Francis Langula ambaye kwa kushirikiana na timu ya viongozi waratibu, walimu walezi na wabia wa huduma wamefanikiwa kugusa wanafunzi wengi nchini Tanzania Huduma huwafikia wanafunzi kwa namna Mbili:
1. Semina ya Ndani ambayo
Huhusisha kuwakusanya wanafunzi sehemu moja.
2. Semina ya nje ambayo huhusisha kuwatembelea wanafunzi mashuleni
kwao.

II.Matawi ya Huduma ya New Creation in Christ na Majukumu yake.
01/05/2026

II.Matawi ya Huduma ya New Creation in Christ na Majukumu yake.

I.MAELEZO JUU YA NCC OUTREACHVew Creation in Christ Outreach, kifupiNCC - Outreach, ni Sehemu ya hudumaya New Creation I...
01/05/2026

I.MAELEZO JUU YA NCC OUTREACH
Vew Creation in Christ Outreach, kifupi
NCC - Outreach, ni Sehemu ya huduma
ya New Creation In Christ (NCC)
inayojihusisha na Kuwafikia na
kuwahudumia Wanafunzi. Kwa sasa NCC
⁃ Outreach imejikita Zaidi katika
kuwafikia wanafunzi wa Sekondari, na
vyuo vya kati kwa kiasi kidogo. Huduma
ya NCC - Outreach inawafikia wanafunzi
kwa mafundisho ya semina
yanayowasaidia wanafunzi kujitambua,
kutambua kusudi, kujitunza kimaadili, na
Kumjua Mungu, lakini pia hugawa bure
vitabu kwa baadhi ya wanafunzi
wanaompa Yesu Maisha kulingana na
vitabu vilivyopatikana

UNIONYESHE NJIA ZAKO, NIPATE KUKUJUAMoja ya sababu kubwa ya watu wengi kutokuona utendaji wa Mungu wa kudumu ni ile hali...
01/08/2024

UNIONYESHE NJIA ZAKO, NIPATE KUKUJUA

Moja ya sababu kubwa ya watu wengi kutokuona utendaji wa Mungu wa kudumu ni ile hali ya kutaka mambo yatokee haraka haraka bila kukubali au kupitia mchakato.

Namanisha kutaka sana MATENDO ya Mungu na sio NJIA ZA MUNGU.

Ni kweli Mungu anayo MATENDO (MIUJIZA) lakini utendaji wake wa kudumu ni wa KIMCHAKATO (njia) zaidi; au naweza kusema msingi wa utendaji wa Mungu ni kupitia MCHAKATO na sio MATUKIO/MATENDO/MIUJIZA... Naamini ukiendelea kusoma mpaka mwisho utanielewa vizuri.

Watu wengi hupenda BIG RESULTS NOW (MATOKEO MAKUBWA SASA AU HARAKA), lakini hawapendi KUFUATA AINA YA MAISHA (LIFESTYLE) AMBAYO ITAZALISHA MATOKEO YA KUDUMU...

Angalia hili andiko utanielewa zaidi 👇👇

Zaburi 103:7
[7]Alimjulisha Musa NJIA ZAKE,
Wana wa Israeli MATENDO YAKE.
He made known his ways unto Moses, his acts unto the children of Israel.

Hilo andiko limetaja vitu viwili:-
1. NJIA ZA MUNGU
2. MATENDO YA MUNGU

Sasa Mungu anavyo vyote, MATENDO na NJIA, lakini hufanya kazi na waliokubali NJIA zake na sio wanaotafuta matendo yake tu...

Ukipewa MATENDO unaanza kushangilia (to celebrate immediately), lakini ukipewa NJIA hauishangilii muda huo bali UNAANZA KUIENDEA kwa umakini...

Kwa mfano, Mtu anayepewa gari, amepewa matendo, anaanza kuliendesha lakini anayepewa WAZO LA BIASHARA NA NAMNA YA KUIFANYA AMBAYO MWISHO INAWEZA KUMPATIA MAGARI, huyo hataanza kushangilia na kuendesha gari, bali atajikuta ANATAKIWA KUWA COMMITTED KWENYE BIASHARA ALIYOPEWA WAZO...

Mwanzoni mwenye matendo ni k**a amepata zaidi, lakini baada ya muda mwenye njia ndio atakuwa na matokeo ya kudumu...

Ukipewa gari haujui namna ya kupata hela ya mafuta na service, hiyo furaha ya gari ni ya muda tu, lakinj, Ukipewa njia ikakufikisha kupata gari, kulihudumia haiwezi kuwa changamoto...

Mfano huo ni mzuri sana kutusaidia kujua tofauti ya NJIA ZA MUNGU NA MATENDO YA MUNGU...

LINAPOKUJA SUALA LA NJIA, MTU HUJULISHWA, HUONESHWA, HUFUNDISHWA, NA ZAIDI SANA MTU UHUSISHWA KATIKA MCHAKATO, LAKINI MATENDO HUTENDEWA NA KUPOKEA...

Matendo ya Mungu sio lazima yamuhusishe mtendewa...

NJIA INAHITAJI WATU COMMITTED, K**A HAUTAAMUA KUWA COMMITTED NA MUNGU HUWEZI KUJULISHWA NA KUHUSISHWA KATIKA NJIA ZA MUNGU... HUWEZI KUPEWA STRATEGIES (MBINU)...

NJIA NI KWA AJILI YA MARAFIKI, NJIA NI USHIRIKA NI PARTNERSHIP

ANGALIA MAOMBI YA MUSA👇👇

Kutoka 33:13
[13]Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, UNIONYESHE NJIA ZAKO, NIPATE KUKUJUA, ili NIPATE NEEMA mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako.

Neema ya kwanza ilimpa Musa nafasi kumuendea Mungu na hapa anaitumia nafasi hiyo kumuomba Mungu AMUONYESHE NJIA ZAKE... Hapa Musa alishaona MATENDO YA MUNGU YA KUTOSHA TU, LAKINI ANAOMBA MUNGU AMUONYESHE NJIA ZAKE...

Halafu anasema MATOKEO YA NJIA ZA MUNGU NI KUMJUA MUNGU ndio maana anasema "nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, UNIONYESHE NJIA ZAKO, NIPATE KUKUJUA"...

Kisha anaendelea kusema "ili NIPATE NEEMA MBELE ZAKO"

Hii Neema ya pili sio Neema ya kwanza, Neema ya kwanza ilimpa nafasi Neema ya pili ni matokeo ya KUTEMBEA KATIKA NJIA ZA MUNGU NA KUMJUA MUNGU ZAIDI...

Sasa hapa kwenye Neema tusiingie ndani, titapaongelea Mungu akitupa nafasi... Tuendelee na NJIA ZA MUNGU

Kumbe matendo ya Mungu hayatoshi kumfanya mtu kumjua Mungu...

Unapaswa kufahamu kwamba, MUNGU akikutendea hataki uweke kituo hapo, anataka UMUENDEE KUMTAFUTA ZAIDI ILI AKUONYESHE NJIA ZAKE NA UPATE KUMJUA ZAIDI...

NJIA NI MATOKEO YA MAHUSIANO IMARA NA MUNGU... NA MAHUSIANO SIO TUKIO NI MCHAKATO, NJIA NI MCHAKATO

Njia ZINATAFUTWA, ZINADAIWA, ZINAOMBWA... Hutazijua NJIA ZA MUNGU ikiwa HAUTAWEKA UHITAJI KUANZIA MOYONI MWAKO (YOU SHOULD PRESS A DEMAND FOR HIS WAYS)...

Usitulie kwa kidogo (matendo), tafuta NJIA... Do not settle for less

NJIA ZA MUNGU ZITAKUPELEKEA KUMJUA MUNGU NA KUMJUA MUNGU ZAIDI KUTAKUPEKEKEA KUZIJUA ZAIDI NJIA ZAKE NA HAPO NDIPO UKUAJI UENDELEVU KATIKA MUNGU UTATOKEA

Watu wengi UKIMUONA ANAOMBA NI KWA SABABU ANATAFUTA MATENDO YA MUNGU, NI KWELI MUNGU ANAWEZA AKAKUONYESHA MATENDO YAKE UKIOMBA, LAKINI UKIISHIA KWENYE MATENDO YA MUNGU, BAADA YA MUDA UTARUDI KUWA EMPTY NDANI YAKO NA HATA UTAJIKUTA UNERUDI NYUMA WAKATI UNAJUA WAZI MUNGU ALIKUTENDEA...

Kutendewa Matendo mengi hakumkuzi mtu kiroho wala hakumpia mtu kumjua Mungu (aliyeyatenda hayo), na Hilo ndio liliwakuta Wana wa Israeli, walikuwa wanatendewa muujiza, wanafurahia sana lakini baada ya muda wanarudi nyuma, kwa sababu WALIPATA MUUJIZA LAKINI HAWAKUWA NA MAHUSIANO NA MTENDA MIUJIZA...

Kila utendewapo muujiza, usiweke kituo, bali uchukue k**a WITO WA KUMJUA MUNGU ZAIDI... Hii ndio sababu maandiko yanaiita miujiza ni ISHARA (SIGNS)... ISHARA MAANA YAKE ZINAONYESHA MAHALI FULANI... ISHARA SIO MWISHO (SIGNS ARE NOT DESTINATION)

SIGNS ARE NOT TARGET, OUR TARGET IS GOD

ACHA KUFANYA VITU (KUFUNGA, KUOMBA, KUJIFUNZA, NK) KWA AJILI YA KUPATA KITU (MATENDO), ANZA KUFANYA KWA AJILI YA KUMJUA MWENYE VITU...

Kuanzia leo ACHA KUFANYA VITU KWA AJILINYA ISHARA, ANZA KUFANYA VITU KWA AJILI YA MWENYE ISHARA, KWA AJILI YA KUMJUA MUNGU...

Paulo anasema "ILI NIMJUE YEYE" Wafilipi 3:10
Musa anasema "Unionyeshe NJIA ZAKO NIPATE KUKUJUA"
Yesu anasema "Na uzima wa milele ndio huu, WAKUJUE WEWE"

HIKI NDIO KILIO NA SHAUKU YA MOYO WANGU, "MUNGU NIPE KUKUJUA WEWE ZAIDI NA ZAIDI, UNIONYESHE NJIA ZAKO NIPATE KUKUJUA"

Mungu akupe ILE SHAUKU YA KUTOKA NDANI YA KUZIJUA NJIA ZAKE NA KUMJUA YEYE, AMBAYO NDIO ITAKUWA DRIVING FORCE YA KILA UNACHOKIFANYA...

HII ITAPELEKEA KUMJUA MUNGU NA NJIA ZA MUNGU, ITAIMARISHA MAHUSIANO YAKO NA MUNGU NA WAKATI HUO HUO UKIENDELEA KUFURAHIA MATENDO YA MUNGU KWA KUDUMU SIO KWA MATUKIO...

Ayubu 22:21
[21]Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;
Ndivyo mema yatakavyokujia.
Acquaint now thyself with him, and be at peace: thereby good shall come unto thee.

Zaburi 63:1-2
[1]Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
NAFSI YANGU INAKUONEA KIU,
MWILI WANGU WAKUONEA SHAUKU,
Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.
[2]Ndivyo NILIVYOKUTAZAMA KATIKA PATAKATIFU,
NIZIONE NGUVU ZAKO na UTUKUFU WAKO.

Umebarikiwa



Mwl. Francis M. Langula
WhatsApp: +255754711247
TELEGRAM:

26/03/2024

Address

TABATA KINYEREZI
Dar Es Salaam
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NCC Outreach posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to NCC Outreach:

Share