Acts Fellowship Tanzania

Acts Fellowship Tanzania Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Acts Fellowship Tanzania, Dar es Salaam.

KARIBU ACTS FELLOWSHIP TANZANIA-MBEYA.
4:32-34

Acts fellowship Tanzania kwa mkoa wa Mbeya wanapenda kukukaribisha katika huduma za neno la zinazofanyika ndani ya viwanja vya maonesho vya NANENANE MBEYA.

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! David Manzinga, Alfred Mwahalende, Hamad Mbeyale, Mamy De...
10/12/2025

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! David Manzinga, Alfred Mwahalende, Hamad Mbeyale, Mamy De Lwinga Lwinga, Veri Mtela, Sarafu Ya Mwambogo, Juma Mikui, Steven Mpeleta, Kocha Makirita Amani, Rodrick Mwazembe

09/12/2025

UVUMILIVU — NGUVU YA WATU WENYE UTHUBUTU
Mwandishi: Alfred Mwahalende

Uvumilivu ni msingi muhimu katika safari ya uthubutu. Ili kufanikiwa, lazima ujenge uwezo wa kustahimili hali ngumu, kuchelewa kwa matokeo, na changamoto zisizokoma. Mafanikio si tukio la ghafla; ni matokeo ya safari ndefu iliyojaa milima na mabonde, siku za furaha na nyakati za maumivu.

Kila hatua ya uthubutu huja na changamoto zake. Wakati mwingine utawekeza bila kuona matokeo ya haraka. Wakati mwingine utajaribu biashara au mradi na ukakutana na upinzani, ukosefu wa mtaji, lawama, au hata kukataliwa na wale uliotarajia kukuunga mkono. Hata hivyo, kinachokuweka kwenye njia sahihi si nguvu ya mwili, bali ni nguvu ya moyo—uvumilivu.

K**a asemavyo Joyce Meyer, “Uvumilivu si tu kusubiri, bali ni namna unavyojiendesha unapokuwa kwenye kipindi cha kusubiri.” Uvumilivu hukufundisha nidhamu ya muda, utulivu wa maamuzi, na uwezo wa kuona mbali. Mtu mvumilivu hujikita katika maono ya muda mrefu, akijua kuwa kuchelewa si kushindwa.

Faida za uvumilivu ni nyingi. Hukujengea historia ya mapambano yenye ushuhuda wa kusisimua. Hukufundisha namna ya kuhimili vipindi vya upungufu na wingi. Hukuwezesha kukutana na watu sahihi kwa wakati sahihi. Hukufanya kuwa mtu wa kuaminika, mwenye maamuzi ya busara na asiyeongozwa na papara. Na mwisho, hukupa heshima ya kutumia mafanikio yako kwa hekima utakayoyafikia.

Kwa hiyo, ili uwe mtu wa uthubutu wa kweli, jifunze kuwa mvumilivu. Wakati matokeo yanachelewa, endelea kujifunza, kujitathmini na kujiandaa zaidi. Kumbuka, mafanikio makubwa hayahitaji haraka—yanahitaji moyo usiokata tamaa.

NGUVU YA ULIMI BY Mpeli Mwaisumbe
07/12/2025

NGUVU YA ULIMI BY Mpeli Mwaisumbe

Habari!Je umekuwa ukitamani kufanya biashara/Ujasiriamali lakini huna *MTAJI PESA*Kuwa mjasiriamali/mfanyabiashara ni za...
26/09/2025

Habari!
Je umekuwa ukitamani kufanya biashara/Ujasiriamali lakini huna *MTAJI PESA*

Kuwa mjasiriamali/mfanyabiashara ni zaidi ya kuwa na MTAJI WA PESA.

*Zifuatazo ni mbinu za jinsi ya kufanya Ujasiriamali/biashara bila mtaji wa Pesa.*

* #️⃣UWE MWAMINIFU KWA WATU WANAOKUZUNGUKA NA UWATUMIE K**A FURSA.*

* #️⃣FANYA KAZI KWA BIDII*

Onesha juhudi katika utendaji wako, usikwamishwe na mazingira yako, hakikisha shughuli unazozifanya hata k**a ni ndogo unazifanya kwa juhudi na bidii kuu.

* #️⃣KUWA NA WAZO ZURI BUNIFU*

Ukiwa hauna mtaji wa kuanza safari yako ya kijasiriamali jitahidi kuwa na wazo zuri la ubunifu ambalo hata ukiwasilisha kwa wenye pesa wataona sababu ya kuwekeza kwenye wazo hilo.

* #️⃣HAKIKISHA UNAJIJENGEA MTANDAO WA WATU SAHIHI*

Katika Maisha ya kawaida huwezi kufanya jambo lolote zuri bila kuwa na watu sahihi.

Watu sahihi ni watu waliotayari kusema ukweli juu yako, wako tayari kukushauri, wako tayari kuunga mkono juhudi zako.

* #️⃣ONESHA NA KUTUMIA KIPAJI CHAKO*

Kipaji chako ni mtaji tosha kuanza safari yako ya kuelekea mafanikio makubwa, kipaji chako ni biashara, kipaji chako ni kazi.

Tambua vipaji vyako na uone namna ya kuvitumia kukufanikisha katika safari yako.

* #️⃣PENDA KUJITOLEA ILI UPATE UZOEFU NA UPATE WATU SAHIHI*

Unatamani kuanza safari yako ya kijasiriamali lazima utenge muda wa kujitolea kwenye taasisi na makampuni

yaliyopiga hatua ili uweze kujifunza na kupata watu sahihi watakaosimama k**a washauri pindi unapoanza mradi wako au biashara yako.

KWA Ushauri na Elimu wasiliana na
Mwl.Mary Mariki

Mwalimu|Mshauri Katika Fedha na Biashara.
+255 769 743 997

*ALFAKHA COMPANY LIMITED*

Fursa za kiuchumi
26/09/2025

Fursa za kiuchumi

26/09/2025

CHUKUA HATUA LEO. ANZA LEO

#️⃣Haijalisha unapitia hali gani kwa sasa kiuchumi. Haijalisha January ina changamoto nyingi kiasi gani, Sijui una Hali gani kwa sasa? Sijui unawaza Nini kwa Sasa? Sijui uko wapi na unafanya Nini?

Lakini Natamani kusema na wewe neno moja tu
"anza lile wazo lako leo" Anza leo kufanyia kazi mipango yako, hata k**a bado kuna mambo hayajakaa vizuri "anza kwanza"

#️⃣Kitendo Cha kuanza kitakupa nguvu na ishara za kuanza kuyatafuta mafanikio katika Jamabo lako.

✔️ K**a ulipanga mwaka huu kuanzisha biashara yako ama kuanzisha kampuni yako ama kuanzisha taasisi yako, baasi anza zile hatua za awali ambazo zitakuwezesha kwenda hatua ya pili na tatu Zaidi.

#️⃣Wakati mwingine tunashindwa kupiga hatua katika mipango na malengo tunayojiwekea kila mwaka kwa sababu ya kukosa uthubutu wa kuanza kutekeleza mipango yetu.

#️⃣Unapoweka mipango yako hakikisha unakuwa balozi na msimamizi mkuu wa mipango yako, kushindwa au kufanikiwa katika mipango yako inategemea sana nguvu na kipaumbele unachoweka katika mipango yako.

#️⃣K**a uliweka mpango wako wa kuanzisha biashara yako, kuanzisha taasisi yako au kufungua na kusajili kampuni yako nzuri na umeona umekwama kabisa na umekosa msaada wa mawazo kabisa basi hujachelewa na wala usijutie juu ya jambo hilo nitakuwepo kukusaidia hatua kwa hatua.

📞ALFAKHA CONSULTING AGENCY

#️⃣WASILIANA NASI KWA 0758051641/[email protected] kwa kutuma neno NIANZISHE SASA.

26/09/2025

SIYO WOTE WANAOSEMA "HUWEZI" WANAMAANISHA KWAMBA HUWEZI; WENGINE NI WIVU TU

Habari za leo, ndugu msomaji wa makala zangu za hamasa katika hatua za mafanikio katika biashara na ujasiriamali.

Namshukuru sana Mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na nchi. Aidha, napenda kukushukuru sana wewe msomaji wangu na nakuombea Mungu akufanikishe katika mambo yako yote na uwe na kibali kikuu katika kazi zako zote.​

Siyo wote wanaosema "huwezi" wanamaanisha kwamba huwezi kweli kufanikiwa; la hasha. Wengine wanasema hivyo kwa sababu ya wivu tu, wengine kwa sababu hawajui nguvu uliyonayo katika kufikia mafanikio; wengine kwa sababu hawana uelewa na mambo unayofanya; na wengine kwa sababu wana midomo ya kusemea.​

Ukitaka kupiga hatua na kufanikiwa katika maisha yako, acha kuambatana na wakatisha tamaa. Acha kukaa na kuwasikiliza watu wenye lengo la kukukatisha tamaa.​

Pia, katika kupiga hatua ya mafanikio, usisubiri sana watu waseme. Anza kupiga hatua huku ukijifunza kwa waliofanikiwa na kuangalia walifanikiwaje, na pia kujifunza kwa waliofeli ili ujue walifelije.​

Maneno mabaya huzorotesha nguvu ya kupiga hatua. Maneno mabaya yana nguvu kubwa sana katika kukurudisha nyuma kuliko maneno mazuri.​

KWA USHAURI, ELIMU NA UWEZESHAJI KATIKA HATUA YA URASIMISHAJI WA BIASHARA NA HUDUMA TANZANIA

Wasiliana nasi kupitia:​
Forbes

📞 +255 758 051 641
📧 [email protected]

Tutakusaidia kufikia malengo yako na kufanikiwa katika biashara yako.

Address

Dar Es Salaam
00000

Telephone

+255758051641

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Acts Fellowship Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share