Global Family Gatherings

Global Family Gatherings God's Standards (Matt 5:14-16)

IKUMBUKE SIKU YA SABATO UITAKASELeo tutaanza kidogo kuangalia mambo yahusuyo Sabato. Tutaangazia mambo yafuatayo..Sabato...
21/06/2026

IKUMBUKE SIKU YA SABATO UITAKASE

Leo tutaanza kidogo kuangalia mambo yahusuyo Sabato.
Tutaangazia mambo yafuatayo..
Sabato ni nini?
Ilianzia wapi?
Lengo lilikuwa ni nini?
Leo ina maana gani?

Tumetua mstari pendwa wa Kutoka 20:8
[8]Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.

Neno Sabato ni neno la Kiebrania *SHÂBATH*.

Kwa kutumia kanuni za kuchambua maandiko, (THE LAW OF FIRST MENTION) yaani neno liliandikwa au kutajwa wapi kwa mara ya kwanza kabisa... limeandikwa na Musa kwenye kitabu chake cha Mwanzo 2:1-3
[1]Basi mbingu na nchi zik**alizika, na jeshi lake lote.
[2]Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; AKASTAREHE siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.
[3]Mungu akaibarikia siku ya saba, AKAITAKASA kwa sababu katika siku hiyo Mungu ALISTAREHE, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.

Maneno *AKASTAREHE* na *ALISTAREHE* ni neno la Kiebrania shâbath...

Neno hili limetajwa zaidi ya mara 70 katika Biblia Agano la Kale.. Hivyo ni neno lililotumika sana.

Neno hili shâbath lina maana ya Kuacha (to cease) au kusababisha iache (to cause to cease).. mara nyingine hutumika kuonyesha kupumzika SI K**A ALAMA ya KUCHOKA bali kuacha kufanya jambo au kusababisha jambo LIISHE AU LIKAMILIKE.

_it's resting NOT from being tired but SIMPLY because it is finished, complete or DONE_

Neno UITAKASE ni neno la Kiebrania pia *qâdash* lenye maana ya kuifanya iwe safi au kutenga kwa kusudi maalum au kuifanya iwe maalum.

Neno IKUMBUKE na lenyewe ni neno la Kiebrania *zâkar* lenye maana ya kutafakari, kufikiria jambo, kulitilia maanani au kukumbushia jambo (recall)..

Musa aliandika maelezo yake kwenye Kutoka 20:8-11
[8]Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
[9]Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
[10]lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
[11]Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

Kwa hiyo kusema IKUMBUKE SABATO anamaanisha ITAFAKARI SABATO, FIKIRIA JUU YA SABATO...

Musa alirudia pia kwenye Kumbukumbu la Torati 5:12-15
[12]Ishike siku ya Sabato uitakase, k**a BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru.
[13]Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
[14]lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng’ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako ye yote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile k**a wewe.
[15]Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa BWANA, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.

Kwa muktadha wa maandiko haya ya juu.... MTU HATAKIWI KUFANYA CHOCHOTE ZAIDI YA KUKUMBUKA AU KUITAFAKARI..

Kutokana na Mwanzo 2:1-3, Mwanadamu anatakiwa kufanya kazi moja tu KUTAFAKARI YALE AMBAYO MUNGU AMEYAFANYA.

Sasa twende taratibu hapa..

Neno shabbâth ni kitenzi (KUPUMZIKA AU KUSTAREHE) na nomino yake ni menûchâh ambayo maana yake ni PUMZIKO, STAREHE AU RAHA.

Tuangalie kidogo maeneo ambayo shabbâth imetumika...

Kutoka 16:30
[30]Basi hao watu wakapumzika kwa siku ya saba.

Neno la Kiswahili KUPUMZIKA ni sawa na KUSTAREHE.. kumbuka Mwanzo 2:1-3

Kutoka 31:17
[17]Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika.

Angalia Zaburi 95:11
[11]Nikaapa kwa hasira yangu
Wasiingie RAHANI mwangu.

👉MENÛCHÂH

Mbali na Zaburi imeonekana pia kwenye Kumbukumbu la Torati 12:9
[9]kwani hamjafikilia bado katika RAHA na urithi akupao BWANA, Mungu wako.

Isaya 11:10
[10]Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na MAHALI pake PA KUPUMZIKA (MENÛCHÂH) patakuwa na utukufu.

A place of REST. Menûchâh.
Isaya 28:12
[12]ambao aliwaambia, Hii ndiyo RAHA yenu, mpeni raha yeye aliyechoka; huku ndiko kuburudika; lakini hawakutaka kusikia.

Sasa turudi kwenye tafsiri ya Maandiko ya Musa, k**a umesoma kitabu changu cha AKAANZA KUTOKA MUSA utagundua kuwa Musa hakuwa anaandika matukio ya kihistoria lakini alikuwa anaandika habari za Kristo na Wokovu wake kwa kutumia matukio hayo..

Angalia alivyosema Yesu mwenyewe, Yohana 5:39-40,45-47
[39]Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.
[40]Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima.
[45]Msidhani kwamba mimi nitawash*taki kwa Baba; yuko anayewash*taki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi.
[46]Kwa maana k**a mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu.
[47]Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?

Maandiko aliyokuwa anayataja hapa ni maandiko wa Musa ambayo tumeona swala la SABATO likitajwa.

Pia alirudia kusema kwenye Luka 24:25-27
[25]Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!
[26]Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?
[27]Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.

Kwa hiyo Yesu alichambua vitabu vya Musa na manabii habari za kufa na kufufuka kwake.

Kisha akahusisha habari hizo na ukombozi wa mwanadamu au msamaha wa dhambi. Hii ni kwenye Luka 24:44,46-47
[44]Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.
[46]Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;
[47]na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.

Kwa hiyo MUSA NI MHUBIRI WA INJILI KWA NJIA YA MATUKIO YA KIHISTORIA.

Hivyo itatusaidia kuangalia vizuri alichokiandika Musa kwenye kitabu cha Mwanzo, na vitabu vyake vilivyofuata pamoja Zaburi na vitabu vya manabii k**a ambavyo tumeona hapo juu SABATO ikizungumziwa.

Kuna maagizo ya kutosha juu ya kuikumbuka SABATO UITAKASE kwenye vitabu vya Musa.

Hebu tujikite katika maeneo ambayo tulianzia hapo juu (Mwanzo, Kutoka na Kumbukumbu la Torati).

Kutoka 20:8-11
[8]Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
[9]Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
[10]lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
[11]Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

Tena hapa,

Kumbukumbu la Torati 5:12-15
[12]Ishike siku ya Sabato uitakase, k**a BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru.
[13]Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
[14]lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng’ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako ye yote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile k**a wewe.
[15]Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa BWANA, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.

Hapa amehusisha pia safari ya kutoka Misri (Ukombozi).

Musa alianzia Mwanzo 2:1-3
[1]Basi mbingu na nchi zik**alizika, na jeshi lake lote.
[2]Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.
[3]Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.

Mambo haya ni ya MSINGI SANA.

Mwanadamu anaambiwa ASIFANYE KWA SABABU MUNGU AMESHAFANYA.

AKUMBUKE (ATAFAKARI) TU ALICHOKIFANYA MUNGU.

Ina maana kazi ya ukombozi, Mungu amemaliza.. kazi ya mwanadamu ni kutafakari au zaidi tukisema ni KUAMINI TU.

Kumbuka kwenye uchambuzi wa kitabu cha Mwanzo tuliona ya kuwa Mbingu na Nchi ni lugha ya Musa ya Muunganiko wa Mungu na Mwanadamu aka Ukombozi au kuwa roho moja naye au Uzima wa Milele.

Nimesema inahitaji tu kuamini? Ndiyo. Wasioamini hawakuingia katika SABATO.

Angalia, Zaburi 95:10-11
[10]Miaka arobaini nalihuzunika na kizazi kile,
Nikasema, Hao ni watu waliopotoka mioyo,
Hawakuzijua njia zangu.
[11]Nikaapa kwa hasira yangu
Wasiingie rahani mwangu.

Mbali na Musa kuhangaika kuwaelezea bado hawaku "SHABBÂTH" na hivyo hawakuingia kwenye MENÛCHÂH..

Maneno ambayo mwandishi wa kitabu cha Waebrania aliyarudia na kuyaelezea..

Waebrania 3:7-11
[7]Kwa hiyo, k**a anenavyo Roho Mtakatifu,
Leo, k**a mtaisikia sauti yake,
[8]Msifanye migumu mioyo yenu,
K**a wakati wa kukasirisha,
Siku ya kujaribiwa katika jangwa,
[9]Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima,
Wakaona matendo yangu miaka arobaini.
[10]Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki,
Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa;
Hawakuzijua njia zangu;
[11]K**a nilivyoapa kwa hasira yangu,
Hawataingia rahani mwangu.

Kwa hiyo inawezekana walikuwa wanasherehekea k**a sherehe ya kawaida badala ya kutafakari kazi ya Ukombozi ulio katika Kristo Yesu.

Angalia anavyoelezea tena. Waebrania 4:1-3
[1]Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.
[2]Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile k**a hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.
[3]Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha ile; k**a vile alivyosema,
K**a nilivyoapa kwa hasira yangu,
Hawataingia rahani mwangu:
ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Angalia maneno SISI TULIOAMINI, tulioamini siku? Hapana. Kazi tuliyoutafakari au kazi ya ukombozi.

Kwa hiyo kwenye maandiko (AGANO LA KALE) IKUMBUKE SABATO ILI UITAKASE ni sawa na kusema AMINI ALICHOKIFANYA MUNGU NA KUKIMALIZA.

Angalia mwandishi wa kitabu cha Waebrania anavyomalizia hapa.. Waebrania 4:8-10
[8]Maana k**a Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye.
[9]Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu.
[10]Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, k**a vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake.

Kwa hiyo, Uumbaji wa Mbingu na nchi na jeshi lake lote ni lugha ya picha ya Ukombozi wa mwanadamu,
Wayahudi kutoka Misri kwenda Kanaani ni lugha ya picha ya Ukombozi pia..

Ndiyo maana baada ya kufika kule bado Daudi aliimba Zaburi ya 95:11.. wasioamini (hapo wamefika Kanaani) anawaambia hawataingia katika RAHA yake.

Ndiyo maana mwandishi wa kitabu cha Waebrania anaonyesha tena HILI SI PUMZIKO/STAREHE ya MWANADAMU SIKU YA JUMAMOSI AU JUMAPILI bali MUNGU KUMALIZA KAZI YAKE KABISA na MWANADAMU ANATAKIWA KUIAMINI HIYO KAZI TU.

Sasa inakuwaje RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU? Ni kwa sababu wao ndiyo wanaokombolewa, wao ndio wanufaika wa KAZI HIYO YA UKOMBOZI!.

Hawakushindwa kuingia kwa sababu waliabudu Jumapili 🤣

🪚Waebrania 4:6
[6]Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,

KUASI KWAO. WALIASIJE? Kwa sababu UGUMU WA MIOYO.
Waebrania 4:7
[7]aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; k**a ilivyonenwa tangu zamani,
Leo, k**a mtaisikia sauti yake,
Msifanye migumu mioyo yenu.

UGUMU WA MIOYO ni sawa na Moyo Mbovu, na ni kufanyeje? Ni KUTOKUAMINI KAZI YA UKOMBOZI WA YESU KRISTO.

Waebrania 3:12
[12]Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai.

USIPOAMINI, UNAJITENGA NA MUNGU, NA UNAKUWA UMEPOTEA MAANA KUAMINI KATIKA KAZI YAKE ALIYOKAMILISHA.

Tena asema Yohana 3:17-18
[17]Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
[18]Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

TULIA KATIKA KAZI YA KAMILIFU YA MUNGU KATIKA KRISTO,

HUKO HUPOTEI, NI KUAMINI TU.
MUNGU ANASEMA AMEMALIZA.

WEWE UKO KWENYE RAHA IKIWA UMEAMINI.

Hii sasa ndiyo RAHA YA MILELE. Hausubiri ufe, Mungu anakupa uzima wa MILELE kwa KUAMINI TU.

Yohana 10:28
[28]Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.

Aliyeahidi ni MWAMINI,
Yafaa umwamini,
Atakupa uzima wa milele siyo wa kitambo unaokuja na kupotea.. ni wa milele.

Ameahidi ya kwamba akikupa HUTAPOTEA KAMWE..

Wala hakuna mtu (pamoja na wewe) atakayempokonya katika mkono wake.

MUNGU NI MWENYE NGUVU..

HALELUYA.

Ap Shemeji Melayeki
Global Family Gatherings
"God's Standards"
+254 714 548 565

SIKU ZOTE, NAMSHUKURU MUNGU/NIKIWAKUMBUKAUkiangalia msisitizo wa Maombi katika maandiko matakatifu utashangaa sana. Nyar...
08/06/2026

SIKU ZOTE, NAMSHUKURU MUNGU/NIKIWAKUMBUKA

Ukiangalia msisitizo wa Maombi katika maandiko matakatifu utashangaa sana. Nyaraka zenyewew zimejawa na lugha ya kumaanisha MWENDELEZO USIOKATIKA siyo PUSH (Pray Until Something Happens) bali ni PA (Pray Always). Hakuna namna utakaa kwenye nyaraka na kujiona sawa siku ikapita bila kuomba. Hili ni jambo la msingi sana, ndiyo maana msisitizo wake ni KUENDELEA KUOMBA SIKU ZOTE AU WAKATI WOTE.

Angalia msisitizo huu..

1 Wakorintho 1:4 Namshukuru Mungu SIKUZOTE kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu;

Namshukuru Mungu SIKUZOTE kwa ajili yenu…. Siyo wiki iliyopita nilimshukuru Mungu. Kumbuka kushukuru ni sehemu ya maombi.. angalia hilo hapa…

Wafilipi 4:6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno KWA KUSALI NA KUOMBA, PAMOJA NA KUSHUKURU, haja zenu na zijulikane na Mungu

Yaani KWA KUSALI NA KUOMBA, PAMOJA NA KUSHUKURU… huko mbele utaona mtiririko wa kuomba na kushukuru zikitajwa maraningi pamoja. Angalia na hapa…

2 Wathesalonike 1:3 Ndugu, imetupasa KUMSHUKURU Mungu SIKUZOTE kwa ajili yenu, k**a ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.

Umeona? Imetupasa KUMSHUKURU Mungu SIKUZOTE kwa ajili yenu

Alipoendelea kuandika akasema..

2 Wathesalonike 1:11 Kwa hiyo TWAWAOMBEA NINYI SIKUZOTE, ili Mungu wetu awahesabu kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu;

Angalia hapa…. TWAWAOMBEA NINYI SIKUZOTE. Mstari wa 3 alisema… Imetupasa KUMSHUKURU Mungu SIKUZOTE kwa ajili yenu.

Kwa hiyo alikuwa anaendelea kuandika namna anavyoshukuru na kuwaombea kwa wakati mmoja.

Mstari wa 13 anarudia tena…

2 Wathesalonike 2:13 Lakini IMETUPASA SISI KUMSHUKURU MUNGU SIKUZOTE KWA AJILI YENU, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;

Angalia haya maneno.. IMETUPASA SISI KUMSHUKURU MUNGU SIKUZOTE KWA AJILI YENU. Usisahau msisitizo… KUWAOMBEA NA KUSHUKURU KWA AJILI YAO NI AGENDA YA SIKU ZOTE.

Kwenye Wafilipi 1:3-4

NAMSHUKURU Mungu wangu kila NIWAKUMBUKAPO, SIKUZOTE kila NIWAOMBEAPO ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha,

Kwenye waraka wake kwa Wafilipi, Paulo anaaonyesha kuwa anashukuru kwa ajili ya waamini walioko Filipi, hiyo namna yake ya kuwakumbuka… na anachofanya ni KUWAOMBEA wakati anasema hizo sala zake SIKU ZOTE..

Huu mtindo, Paulo anautumia pia kwa Filemoni. Angalia hapa..

Filemoni 1:4 NAMSHUKURU Mungu wangu SIKUZOTE, nikikukumbuka katika MAOMBI yangu;

Anamshukuru Mungu (bila shaka ni kwa ajili ya Filemoni k**a anavyofanya kwa waamini wengine hapo juu) akimkumbuka katika maombi yake.

Angalia mtiririko huu.

>Anamkumbuka

>Anamshukuru Mungu kwa ajili ya waamini

>Anawaombea..

Tuendelea na waraka wake kwa Wakolosai. Angalia Wakolosai 4:2-3 DUMUNI SANA katika KUOMBA, mkikesha katika KUOMBA huku na SHUKRANI; MKITUOMBEA na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,

Angalia msisitizo wa Paulo tena DUMUNI SANA katika KUOMBA, mkikesha katika KUOMBA huku na SHUKRANI; MKITUOMBEA..

Akiandika waraka wake kwa kanisa la Roma.

Warumi 12:12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; KATIKA KUSALI, MKIDUMU;

KATIKA KUSALI, MKIDUMU, maana yake bila kuacha.. Je, inatofauti na SIKU ZOTE? AU KILA SIKU? La! Hasha.

Kwenye Matendo ya Mitume walipoanza kutekwa na mambo ya kijamii juu ya kugawa mahitaji kila siku wakaona si vyema kuacha KUDUMU kwenye mambo ya msingi k**a kuomba, wakawachagua viongozi ili WADUMU kwenye kuomba. Angalia hapa..

Matendo ya Mitume 6:4 na sisi TUTADUMU katika KUOMBA na kulihudumia lile Neno.

Mitume walisema.. Sisi TUTADUMU katika KUOMBA..

Akimwandikia Timotheo mwanaye katika Imani, Paulo anaandika..

2 Timotheo 1:3 NAMSHUKURU Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, k**a vile NIKUKUMBUKAVYO wewe DAIMA, katika KUOMBA kwangu USIKU NA MCHANA.

Angalia msisitizo tena…

>Namshukuru Mungu

>Nikukumbukavyo wewe DAIMA.

>katika kuomba kwangu USIKU NA MCHANA.

Msisitizo wenye nguvu sana.

Sasa kwa Waraka wake kwa Waefeso anaandika..

Waefeso 6:18 kwa SALA ZOTE NA MAOMBI mkisali KILA WAKATI KATIKA ROHO, mkikesha kwa jambo hilo na KUDUMU katika KUWAOMBEA watakatifu wote;

Tuangalia na msisitizo wa maelekezo ya Paulo juu ya maombi.

>Mkisali KILA WAKATI

>Na KUDUMU KATIKA KUWAOMBEA watakatifu.

Tofauti na sehemu nyingine… ameonyesha namna ya kuomba haya yote.. KUMWOMBEA FILEMONI, KUMWOMBEA TIMOTHEO, KUOMBEA KANISA ZIMA… Wakolosai, Waefeso, Wakorintho… angetumia mtindo gani kuomba kundi lote hili?

Amesema _mkisali KILA WAKATI KATIKA ROHO_ kusali/kuomba katika Roho ni kuombaje?

Angalia Yuda anavyoandika..

Yuda 1:20 Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,

Ametaja pia namna hiyo… na kuomba katika Roho Mtakatifu..

Kwenye waraka wa kwanza kwa Wakorintho Paulo alielezea hili hapa..

1 Wakorintho 14:14-15

Maana nikiomba kwa LUGHA, ROHO yangu HUOMBA, lakini akili zangu hazina matunda. Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia.

Anasema nikiomba kwa LUGHA, ROHO yangu HUOMBA, kwa hiyo KUOMBA KWA ROHO ni KUOMBA KWA LUGHA.

Kwa hiyo namna ya kudumu, kuomba kila wakati, kwaombea watakatifu, kuwaombea viongozi wako wa kiroho, pamoja na kumshukuru Mungu kwa ajili yao ni KUOMBA KWA LUGHA.

Yape maombi kipaumbele,

Yawe sehemu yako ya kila siku,

Dumu,

Siku zote,

Kila wakati.

LEO UNAOMBA/UTAOMBA?

Ap Shemeji Melayeki
Global Family Gatherings
“God’s Standards”

Mtu ALIYEKETISHWA PAMOJA na KRISTO anapiga picha na mwanasiasa mwenye mapepo.. halafu kwa ujasiri anaandika "Nimeketishw...
06/06/2026

Mtu ALIYEKETISHWA PAMOJA na KRISTO anapiga picha na mwanasiasa mwenye mapepo.. halafu kwa ujasiri anaandika "Nimeketishwa pamoja na wakuu".. hiyo Biblia yako umebakiza hatua chache ufungie mandazi. 😆 Mtu ambaye unatakiwa kumsaidia aje kwenye ufalme unaodumu milele wewe unasifia wakuu wa giza.. LAITI UNGEJIONA WEWE ULIVYO KATIKA KRISTO ungewaonea huruma wakuu wa ulimwengu huu.. ungeanza kuomba fursa ya kuwahubiria Injili.. JIOMBEE WEWE!...
—Global Family Gatherings
"God's Standards"

Paulo anashangaa sana kizazi hiki ambacho hakijui thamani ya Imani yao katika Kristo. Siku moja Paulo aliwekwa mbele ya ...
06/06/2026

Paulo anashangaa sana kizazi hiki ambacho hakijui thamani ya Imani yao katika Kristo. Siku moja Paulo aliwekwa mbele ya Baraza lenye viongozi k**a Mfalme Agripa, Festo, Bernike, maliwali na viongozi wa mji... alijikita kuchambua maandiko na kutaka kuwashawishi waamini habari za Mateso, Kufa na Kufufuka kwa Yesu Kristo pamoja na matokeo yake. Lakini wewe ukimwona mtu mwenye cheo kikwapa kinatoka jasho. Ndiyo maana unatakiwa kujiombea...
— Global Family Gatherings
"God's Standards"

Ujasiri ni signature ya mwamini. Dalili ya kwamba ufunuo wa Kristo umeathiri akili yako ni aina ya ujasiri unaoupata. Pe...
06/06/2026

Ujasiri ni signature ya mwamini. Dalili ya kwamba ufunuo wa Kristo umeathiri akili yako ni aina ya ujasiri unaoupata. Petro aliyekuwa mwoga anasimama mbele ya baraza na kukataa vitisho vyao kuhusu Injili ya Yesu. Alisema kabisa mbele yao "Amueni mnachotaka maana sisi hatutaacha kusema".. Wewe umetishiwa tu na mama "nakupa laana" sijui nani kakuambia 'nisikuone tena' ghafla umeanza kuishi k**a mtumwa. Unajifichajificha. Unamuonea Kristo aibu? Wewe ukishikiwa panga, injili si bye bye? 🤔 JIOMBEE.
— Global Family Gatherings
"God's Standards"

Hapa Tanzania tunabembelezana ili kuhubiri Injili. Tunapeana mpaka sambusa lakini wapi? 😆 unamwambia mtu njoo hubiri kwa...
06/06/2026

Hapa Tanzania tunabembelezana ili kuhubiri Injili. Tunapeana mpaka sambusa lakini wapi? 😆 unamwambia mtu njoo hubiri kwa njia ya nyimbo anakwambia bila Tshs 5M siwezi kuja. Mwenzako anaenda uwanja wa vita ili kuwahubiria waasi... Mwenzako anaenda India mahali wanapochinja wakristo akahubiri Injili. Wengine wako Sudan porini wanatafuta mpenyo ili wawafikie watu kwenye mazingira magumu. Sisi tutajitetea na nini? Kwa nini umeacha kuhubiri? WHY?
— Global Family Gatherings
"God's Standards"

04/06/2026

Ukiambiwa kuna mtu amekufa kwa ajili ya dhambi zako unakasirika.. ulitaka akuue wewe kwa ajili dhambi zako?

— Global Family Gatherings
"God's Standards"

04/06/2026

Huwezi kutenganisha maisha ya huduma na maombi.. ni sawa na kujitahidi kuwa hai bila kupumua. Huduma inakuwa nusu kaputi k**a huombi. Itahema kwa tabu. Ikiwa unapenda kumtumikia Bwana Yesu... usiweke maombi pembeni. Usiwe na hekima izidiyo maombi. Maombi ni hekima ya Mungu. TUOMBE.

— Global Family Gatherings
"God's Standards"

Si msalaba tu bali msalaba wa katikati.  Si msalaba tu wa katikati bali aliyeko juu ya huo msalaba. Yesu aliungana na we...
26/05/2026

Si msalaba tu bali msalaba wa katikati. Si msalaba tu wa katikati bali aliyeko juu ya huo msalaba. Yesu aliungana na wenye dhambi katikati ya dhambi zao, wakijitahidi kulipia makosa yao. Mmoja akaona msalaba wa Yesu kuwa wokovu.. Mwingine akaudharau.. akafa kwenye jitihada zake. Na hakusaidika. Wewe unashikilia jitihada zako au unaitazama kazi ya Mwokozi? Yesu anataka kukutakasa uko busy unajitakasa. Anataka kukuhesabia haki bure uko busy kulipia dhambi zako. Ukishachoka sema usaidiwe...

— Global Family Gatherings
"God's Standards"

22/05/2026

UFAHAMU JUU YA UPENDO WA MUNGU UNATUFUNDISHA KUJITOA KWA AJILI YA WENGINE..

Address

Sinza
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Global Family Gatherings posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Global Family Gatherings:

Shortcuts

Share