30/08/2026
Nehemia 8:10 “Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.”
Furaha ya Bwana inapokuja ndani yako inakupa nguvu, inakupa kuwa hodari na shujaa kwa nini? Kwa sababu kile ulichokula ndicho kinachokupa furaha, kipi hicho? Neno la Mungu linakupa furaha, na ni nguvu yako. Unapopata hiyo furaha inakupa nguvu na wepesi.
Zaburi 51:12 “Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.”
Nini maana ya furaha ya wokovu? Unapokula Neno la Mungu ambalo ni mkate wa uzima linakupa furaha. Roho ya wepesi ni nini? Ni kujua namna ya kufanya mambo kwa haraka na kwa wakati pasipo kupoteza majira yaliyowekwa. Kwa maana kuna muda wako wa kuanzisha biashara, kujenga au kuanziasha jambo fulani sasa kwa wewe kulijua Neno litakupa furaha na hiyo furaha itakusaidia kufanya mambo kwa wepesi na kwa wakati sahihi.
Yohana 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.”
Kwa kulifahamu Neno unakuwa unatenda katika haki na ukamilifu, kwa nini Neno lina nguvu namna hii? Neno lina nguvu ili kukufanya wewe uwe mshindi katika kila eneo la maisha yako.
Neno la Mungu lina maeneo saba ya muhimu sana:-
1. Ukilielewa Neno kamwe hauwezi kuwa masikini,
2. Neno ni mkate wa uzima: linatupa nguvu,
3. Neno ni mwanga wa miguu yetu;
Zaburi 119:105 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.”
Soma Neno, tafakari neno, kula neno, tamka Neno, kwa namna unavyofanya hivyo ndivyo unaruhusu neno likae ndani yako, namna unavyotenda na kukiri neno ndivyo linakaa ndani yako na kuanzia hapo kila utakachokitenda kitakaa kwa nini? Kwa sababu neno linakuwa ndani yako.
©Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira