Efatha Church Matunda

Efatha Church Matunda we connect people to Jesus Christ our saviour through media. He is the way the truth and the life

UKIRI WA SIKU. NAIBARIKI JUMAMOSI YANGU. Mimi sifi kwa magonjwa au ajali wala kwa mapenzi ya yule mwovu ama ya wanadamu....
05/09/2026

UKIRI WA SIKU.

NAIBARIKI JUMAMOSI YANGU.

Mimi sifi kwa magonjwa au ajali wala kwa mapenzi ya yule mwovu ama ya wanadamu. Nitamaliza Safari yangu Salama na nitafikisha Umri ambao BWANA amenipangia ili Atukuzwe!!! Na Nitahesabu Mapato yangu huku nikimshangilia BWANA.

YESU ni Mzuri.

UKIRIKatika jina la Yesu Kristo, Kusanyiko la Mwaka huu la KUTENDA MAPENZI YA MUNGU litakuwa la maajabu na miujiza kulik...
04/09/2026

UKIRI

Katika jina la Yesu Kristo, Kusanyiko la Mwaka huu la KUTENDA MAPENZI
YA MUNGU litakuwa la maajabu na miujiza kuliko makusanyiko mengine.
Tunatangaza ulinzi na usalama, hali nzuri ya hewa, ukamilifu wa miundombinu,
uwepo wa Mungu na kila aliyekusudiwa kufika atafika, kwenye kusanyiko.
AMEN.

MCHUNGAJI ; LABANI LUTUFYASOMO: MAANDALIZI YA KUKUTANA NA BWANA KUPITIA KUSANYIKO LA WANA WA MUNGU-kukusanyika ni agizo ...
04/09/2026

MCHUNGAJI ; LABANI LUTUFYA
SOMO: MAANDALIZI YA KUKUTANA NA BWANA KUPITIA KUSANYIKO LA WANA WA MUNGU

-kukusanyika ni agizo la Mungu, Mungu anapowakusanya watoto wake anakuwa na NENO , agizo kwa ajili yao
Mungu anapotaka tukusanyike ni kwa faida yetu maana ana jambo JIPYA kwa ajili yetu
SWALI: Je Mungu anapokuita kwenye KUSANYIKO lake UNAKUWA umejiandaa kwa namna gani? Hakuna msafiri ambaye haandai safari yake na sisi tuna safari yetu ya kwenda mbele za Baba yetu wa Mbinguni ni kwa namna gani tumejiandaa ili turudi na ushuda? Kila anayesafiri anaporudi baada ya safari yake anakuwa na ushuhuda .
Mithali 16:1
Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu;
Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.

Jukumu la kuandaa moyo wako ili Bwana aweze kukupa HAZINA zake ni la kwako mwenyewe si la mchungaji au mtumishi yoyote qnayesimama mbele Yako . Mtumishi wa Mungu inawezekana akanyimwa kufunuliwa Yale unayopita nayo ila wewe unajua yake unayoyapitia na Mungu mwenyewe,huu ni wakati wa kumwambia Baba ninaenda mahali AMBAPO unasema kasema na mimi kuhusu maisha yangu naenda mahali unapojibu kanijibu mimi kuhusu mambo yangu ,uandae moyo wako vizuri kupokea matakatifu ya Mungu aliye Baba Yako

Kutoka 19:10
BWANA akamwambia Musa, Enenda kwa watu hawa, ukawatakase leo na kesho, wakazifue nguo zao,

-usijishughurishe na mambo mengi katika KIPINDI HIKI CHA maandalizi kwa ajili ya KUSANYIKO yatakuchelewesha andaa moyo wako .

Pata muda wa kutafakari je ni yepi yanayokuhmiza ,ni yepi yanayokusononesha ni ugonjwa ,ni KUKOSA kipato,ni ndoa ni WATOTO nenda mbele za Baba MWAMBIE Baba mwaka huu ninapoenda mahali pale AMBAPO Kuna uwepo wako mkubwa najiungamanisha na madhabahu ile ili na mimi nirudi na ushuhuda wangu .

UKIRI WA SIKU. NAIBARIKI IJUMAA YANGU. Nafurahi katika BWANA, maana BWANA wa Mabwana, NENO yuko ndani yangu, na Mimi nda...
04/09/2026

UKIRI WA SIKU.

NAIBARIKI IJUMAA YANGU.

Nafurahi katika BWANA, maana BWANA wa Mabwana, NENO yuko ndani yangu, na Mimi ndani Yake; maadui zangu wote wapo chini ya Miguu yangu, hakuna cha kunishinda. Mimi ni Mshindi.

Asante YESU

UKIRI WA SIKU. NAIBARIKI ALHAMISI YANGU. Nafurahi katika BWANA; kwangu hakutapungua Kicheko, Furaha, Tafrija, Karamu na ...
03/09/2026

UKIRI WA SIKU.

NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.

Nafurahi katika BWANA; kwangu hakutapungua Kicheko, Furaha, Tafrija, Karamu na Utele, maana NENO yuko ndani yangu. Mimi Nimebarikiwa na BWANA.

Asante YESU.

02/09/2026
UKIRI WA SIKU. NAIBARIKI JUMATANO YANGU. Katika BWANA nakula NENO, katika BWANA natafakari NENO, katika BWANA natamka NE...
02/09/2026

UKIRI WA SIKU.

NAIBARIKI JUMATANO YANGU.

Katika BWANA nakula NENO, katika BWANA natafakari NENO, katika BWANA natamka NENO; Katika BWANA Mimi ni Hodari, katika BWANA Mimi nina Nguvu, katika BWANA Mimi ni Mmiliki, katika BWANA Mimi ni Mtawala, katika BWANA hakuna cha kunishinda.

YESU ni Mzuri.

UKIRI WA SIKU. NAIBARIKI JUMANNE YANGU. Familia yangu itasonga mbele haiwezi kurudi nyuma. Kwetu kutakuwa Kwema, hakutak...
01/09/2026

UKIRI WA SIKU.

NAIBARIKI JUMANNE YANGU.

Familia yangu itasonga mbele haiwezi kurudi nyuma. Kwetu kutakuwa Kwema, hakutakuwa na magomvi wala magonjwa wala vifo, wala ukata. Maisha yetu yatakuwa Mazuri kwa kuwa Tumebarikiwa na BWANA.

Asante YESU, Wewe ni Mzuri BWANA.

KARIBU KATIKA MWEZI WA SEPTEMBA — JIANDAE KUUONA UTUKUFU WA MUNGU KATIKA UKAMILIFU WAKE…….WELCOME TO THE MONTH OF SEPTEM...
01/09/2026

KARIBU KATIKA MWEZI WA SEPTEMBA — JIANDAE KUUONA UTUKUFU WA MUNGU KATIKA UKAMILIFU WAKE

…….

WELCOME TO THE MONTH OF SEPTEMBER- GET READY TO SEE GOD’S GLORY IN ITS FULLNESS

30/08/2026

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Matunda posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share