23/05/2024
*AMRI YA BWANA WETU.*
*Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Mathayo 28:19.*
⏯️ Ndivyo Yesu alivyowapatia wanafunzi wake utume wao. Alifanya maandalizi kamili kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hiyo, na akajitwika jukumu la kuifanikisha. Ili mradi walitii neno Lake, na kufanya kazi katika uhusiano Naye, hawangeweza kushindwa. Nendeni kwa mataifa yote, Aliwaamuru. Nendeni mbali zaidi kwenye makazi ya watu... Fanyeni kazi kwa imani, kwa maana nitakuwa pamoja nanyi siku zote.
⏯️ Utume wa Mwokozi kwa wanafunzi unawajumuisha wote wanaoamini. Unajumuisha wote wanaomwamini Yesu Kristo hadi mwisho wa wakati. Ni kosa la kufisha kufikiri kuwa kazi ya kuongoa roho inawahusu tu wachungaji waliowekwa wakfu. Wote ambao uvuvio wa mbinguni umewajia wanawekwa amana kwa injili. Wote wanaopokea uzima wa Kristo wanawekwa wakfu ili kufanya kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wenzao. Kanisa lilisimikwa kwa ajili ya kazi hii, na wale wanaochukua viapo vyake vitakatifu wanaahidiwa kuwa watendakazi pamoja na Kristo.
⏯️ Tunapaswa kuwa mikondo iliyowekwa wakfu, ambayo kwayo maisha ya mbinguni yanapaswa kutiririka kwa wengine. Roho Mtakatifu anapaswa kuhuisha na kulivuvia kanisa lote, akisafisha na kuimarisha mioyo. Wale ambao wamezikwa pamoja na Kristo katika ubatizo wanapaswa kuinuka katika upya wa uzima, wakitoa uwasilishaji hai wa maisha ya Yesu... Umewekwa wakfu kwa kazi ya kufanya injili ya wokovu ifahamike. Ukamilifu wa mbinguni unapaswa kuwa nguvu yako.
🔘 *Wakati fulani Duke wa Wellington alikuwepo wakati ambapo kikundi cha wanaume Wakristo kilikuwa kikijadili uwezekano wa kufaulu katika jitihada za umisionari miongoni mwa wapagani. Walitoa wito kwa kiongozi huyo kusema ikiwa kwa maoni yake juhudi k**a hizo zinaweza kuthibitisha mafanikio kulingana na gharama. Yule askari mzee akajibu: "Waheshimiwa, ni nini mipango yenu ya kazi? Mafanikio sio swali la wewe kujadili. K**a ninalisoma agizo lenu vizuri, linasema, 'Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.' Waheshimiwa, tiini agizo lenu la kazi."*
*MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA.*
🙏🙏🙏🙏