Saints Blessed Church SBC

Saints Blessed Church SBC Teaching the Word of God through Christ Jesus our Lord under the influence of the Holy Spirit. We partner with you for your progression in Joy.

Transforming and comforming men to the image and likeness of God through the revelational knowledge of Christ.

11/02/2026
28/07/2025

Yesu NI Bwana.

13/07/2025

AMEN

Shalom Abba Baba ni series ambayo inafafanua juu ya Ubaba wa Mungu na Mpango wake wa milele katika maisha ya mwanadamu.N...
30/06/2025

Shalom

Abba Baba ni series ambayo inafafanua juu ya Ubaba wa Mungu na Mpango wake wa milele katika maisha ya mwanadamu.

Ni maarifa ambayo yanamimina hekima katika utambulisho wa Mwamini na ushirika wake pamoja na uungu, kadhalika ikiweka wazi mamlaka ya mwamini katika ushirika huo wa kushangaza alionao na Mungu.

Ni somo muhimu kwa ukuaji wa Kiroho, ni msingi wa ufunuo wa Mungu katika maandiko matakatifu.

Ni neno limeelezwa katika uwazi kiasi cha kwamba matokeo yake ni Kristo kutukuzwa na Mwamini kujengwa ndani ya Kristo.

Unaweza kusikiliza somo hili, pia unaweza kupakua na usikilize mara kwa mara.

https://t.me/Mungupamojanasi/73

Baba amekubariki sana.

16/02/2025

Nguvu ya Sala

Ukisha fahamu, thamani ya sala,
Hutakoma tena, kuomba daima.
Ni nuru ya moyo, faraja ya roho,
Kilicho na nguvu, kushinda mahojo.

Katika dhoruba, ni ngao imara,
Hutuliza mawimbi, huleta fanaka.
Ukiwa na huzuni, au na furaha,
Sala ni mlango, wa neema tele.

Ukisha fahamu, thamani ya sala,
Hutakoma tena, kuomba daima.

Word | Spirit | TansformationWhen the Word is taught in Simplicity and Clarity, the Spirit is given a free flow and the ...
26/11/2024

Word | Spirit | Tansformation

When the Word is taught in Simplicity and Clarity, the Spirit is given a free flow and the transformation will be evident in the life of the hearer.

Join us today as we navigate through the *“TANGIBILITY OF FAITH“*

The Right hand of fellowship in rejoicing.
Miracle, Signs and Wonders abound in the name of Jesus.
The glory of His mighty display in simplicity and saints edified in the same.

The SPIRIT says COME.

Zaburi 118:25[25]Ee BWANA, utuokoe, twakusihi; Ee BWANA, utufanikishe, twakusihi. Moyo wa mwanadamu una kiu na shauku ya...
27/10/2024

Zaburi 118:25
[25]Ee BWANA, utuokoe, twakusihi;
Ee BWANA, utufanikishe, twakusihi.

Moyo wa mwanadamu una kiu na shauku ya wokovu, moyo huu unalia ukihitaji wokovu.

Moyo wa mwanadamu unahitaji nini?

Unahitaji kufanikishwa.

Moyo unajua kuwa Bwana ndiye aokoaye, afanikishaye. Kwahiyo hitaji la moyo linaitwa kumsihi Bwana aokoe na kufanikisha.

Mungu ameweka tamaa ndani ya moyo wa mwanadamu, tamaa hiyo ni juu ya Bwana, awe na uhitaji ambao utoshelevu wake ni Mungu mwenyewe.

Warumi 8:22
[22]Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa.

Paulo anaeleza kuwa viumbe vyote vinaugua, vina shauku ndani ya mioyo yao, kuna shauku ndani yako ya kushibishwa, vina njaa na kiu ya kula na kunywa kutoka kwa Bwana.

Kuugua huku Yesu anakuita "mavuno ni mengi"

Luka 10:2
[2]Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.

Mavuno haya ni wale wanaopatikana kila mji na kila mahali. Ni kila kiumbe katika nchi.

Bwana anautazamaje ulimwengu?

Mavuno ni mengi.

Ulimwenguni unafanyaje?

Unaugua.

Kwanini ulimwengu unaugua?

Kuugua kwa ulimwengu ni kwasababu wanahitaji kuvunwa na Bwana.

Bwana anavunaje?

Anapeleka watenda kazi.

Luka 10:1
[1] Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.

Kila mahali, mji alipokusudia kwenda mwenyewe, aliwatuma watenda kazi.

Watenda kazi wanaenda kufanyaje?

Kuvuna mavuno yaliyo mengi.

Yesu anawatazamisha wanafunzi wake kuwa kila mji na kila mahali waone mavuno ni mengi. Kila watakayekutana naye waone ya kuwa Bwana ana haja naye kwa maana ndani ya moyo wake kuna kuugua kunakohitaji msaada kutoka kwa Mungu.

Zaburi 107:20
[20]Hulituma neno lake, huwaponya,
Huwatoa katika maangamizo yao.

Itaendelea…

Address

Segerea
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 18:15 - 19:30
Tuesday 18:15 - 19:30
Wednesday 18:30 - 19:30
Thursday 18:15 - 19:30
Friday 17:15 - 19:30
Saturday 15:00 - 18:00
Sunday 08:30 - 13:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Saints Blessed Church SBC posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Saints Blessed Church SBC:

Share