14/08/2026
๐๐ ๐๐๐๐ผ ๐ผ๐๐ผ๐๐๐๐๐๐ผ๐๐๐๐ผ ๐ฝ๐ผ๐๐ผ๐๐ผ ๐ผ๐๐ผ ๐๐ผ๐๐๐ผ๐๐ผ ๐๐ผ ๐๐๐ผ๐๐๐๐๐๐ผ ๐ฝ๐ผ๐๐ผ๐๐ผ ๐๐๐๐๐
๐๐๐๐:
Matendo ya Mitume 19:11,13,15-16
[11]Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida;
[13]Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.
[15]Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani?
[16]Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.
Jina la Bwana libarikiwe.
Maandiko matakatifu yanaelezea namna Mtume Paulo alivyofanya miujiza, Ishara na Ajabu nyingi kupitia Jina la Yesu Kristo. Watu wengi walioshuhudia matukio haya walijawa na mshangao, wengine nao walijaribu kuiga, miongoni mwao ni;
Wana saba wa kuhani wa kiyahudi aliyeitwa Skewa ambao walijaribu kuamuru pepo k**a alivyofanya Paulo ghafla wakajikuta wamevamiwa na kushambuliwa na hao pepo.
Tunaweza kujifunza kitu hapa kwamba,
Si kila mtu anaweza kuamuru pepo atoke na akakutoka.
Si kila Mtu anaweza kukemea pepo atoke naye akatii.
K**a ingekuwa hivyo basi hakuna Mtu angekuwa anateswa na nguvu za giza maana pepo wanakemewa kila siku na hakuna mabadiliko. Kumbe basi si kila Mtumishi ni Paulo wengine ni wana wa Skewa.
Vivyo hivyo si kila Mtu anaweza kuamuru baraka zikujilie na zikaja.
Si kila Mtu anaweza kukuwekea mikono, akatamka baraka nazo zikakujilia.
K**a ingekuwa hivyo basi hakuna mtu angekuwa anaishi maisha ya laana hapa duniani kwasababu kila jumapili tunatamkiwa baraka huko makanisani kwetu na bado tunaishi k**a waliolaaniwa.
Kila mara tumekuwa tukiambiwa ubarikiwe lakini hatuoni badiriko kwenye maisha yetu,
Tazama mikono ya Mtume Paulo jinsi ilivyokuwa inaachilia nguvu za Mungu;
Matendo ya Mitume 19:6-7
[6]Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.
[7]Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili.
Tazama baada ya mtume Paulo kuwawekea mikono hao wanaume kumi na mbili, Roho Mtakatifu akawajilia juu yao wakaanza kunena kwa lugha na kutabiri.
Je mimi na wewe ni mara ngapi tumewekewa mikono na watumishi wa Mungu na bado hakuna kilichobadilika kwenye maisha yetu?
Tafakari na uchukue hatua.
Shalom Shalom.......
๐ฌ๐๐
๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐ ๐ญ๐๐๐๐๐๐๐ (๐ด๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐ฉ๐๐๐๐๐) ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐
๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐ ๐๐ ๐ด๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐๐.
ยฎ๏ธ ๐ณ๐๐๐๐๐๐๐ ๐ฎ๐๐๐๐๐
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐@๐๐๐๐๐.๐๐๐
+๐๐๐ ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐