Sili ya uhai ndani ya damu ya Yesu

Sili ya uhai ndani ya damu ya Yesu sili ya uhai ndani ya damu ya Yesu

21/05/2022

Bwana Yesu asifiwe kanisa neema ya Kristo iwe juu yetu na leo tena

Tumepata muda mwingine wa kutafakali neno la Mungu

Somo: matendo ya miujiza

Muujiza ni jambo ambalo linatendeka kupita uwezo wa mwanadamu

Yesu alipoamliwa kuja duniani alitenda miujiza mingi sana kwa wanadamu mujiza wa uponyaji, promotion,safari,ajira nk ni haki ya kila aliyendani ya ufalme wa Mungu kila ambaye alikabidhiwa ktk mikono ya Yesu na akatii sheria ya ufalme basi huyo ni mtoto wa Baba yani Mungu

Yesu alitenda miujiza mingi kila mahali hii ni kutudhibitishia kuwa ni haki yetu kupona au kupokea miujiza hunaaja ya kutafuta bali unayo inajalisha sana nini unaamini
Mathayo 13:58_
Marko 6:2_

Ukiwa mtoto wa Mungu hunahaja ya kulilia mujiza sababu ni sehemu ya maisha yako

Mathayo15:27_ sisi hatufananishwi na mwanamke mkananano mwenye kuomba makombo bali sisi tunasema na jambo linatokea

Yesu anamjibu nilitumwa kwa nyumba ya Israel yani watoto wa Mungu mama mkananayo anaonekana akimwomba Yesu uponyaji na Yesu anamwambia haukuja kwaajiri ya mtu asiye mtaka Mungu wala kufata sheria ya Mungu inaonyesha mama huyu alikuwa haamini mambo ya Mungu sasa kwasababu ya uhitaji anamfata Yesu na kuomba hata masalia ya uponyaji sasa wewe k**a ni mtoto wa Yesu unaaja ya kuomba makombo? Tizama tofauti kubwa sana hii

Kuchelewa kupokea mujiza
Yapo mambo yanayo tufanya tuchelewe ktk kupokea muujiza
_tunaenda kwa Yesu tukitaka kupata kwa haraka mahitaji Yetu
_kuto kuamini kwetu Yesu alimwambia binti jipe moyo mkuu mathayo 9:22
_ kuishi maisha yasiyo na toba kutokwenda ktk sheria ya Bwana (kutokutii)

17/05/2022

Shalom wapendwa ktk Bwana ninamtukuza Mungu kwaajili yako
Leo Mungu ametupa nafasi nyingine ya kutafakali neno lake ( Mungu wetu ni waupendo)

SOMO: mharibifu
MWANZO-1:26 Mungu anasema tumfanye mtu kwa mfano wetu lakini sio mfano tu akatawale kila kitu hakika Mungu wetu anatupenda sana

Wakati Mungu wetu anatuwazia mema mharibu anawaza kuharibu baraka hii ya mfano wa Mungu kumiliki

Ukiwa mfano wa Mungu magonjwa hayatakuwa juu yako, umaskini, kudhalauliwa,ajari nk

Ukiwa mtawala hutatawaliwa na magojwa, kutengwa nk

Mharibu muda wote huwaza kupotosha baraka za Mungu na kuweka majuto mharibu ukimwachia nafasi hata kidogo atahakikisha anaharibu kila kitu ukisoma kitabu cha ayubu utaona mharibu anavyo dodosha mate kwa kutaka kuharibu kilakitu cha ayubu

Ukisoma pia Ufunuo utaona shetani anafanya vita na uzao wa mwanamke mharibu anafanya kila mbinu kuharibu furaha ya mwanadamu

Chakufanya tujifunze kuwa waombaji wafanya vita ktk nyakati zote ili kumshida adui haijarishi nini unapitia kwasasa juwa kina mwisho ukitaka maombi yako ndio majibu ya tatizo lako tuombe bila kukoma yote yanawezekana amen

15/03/2022

Bwana Yesu asifiwe watoto wa mfalme Yesu Kristo natumai umzima hapo ulipo

Napenda tukumbushane jambo moja la umuhimu na la msingi ktk maisha yetu

Ktk karne na karne tumeona tukipata mafundisho mengi ya namna ya kuenenda ktk kumtii Kristo na zaidi ya hayo kuushika ufalme wa Mungu, nina shaka mahala sijui k**a mafundisho haya tunayachukulia kuwa ni sehemu ya maisha yetu Au tunaenenda kimazoea tu

Yesu anasema utafuteni kwanza ufalme wake unapoutafuta ufalme unapaswa kuushikilia kuishi ndani yake pamoja na sheria zake

Ukisoma waefeso 2 anasema tulikuwa wafu kwa kufuwata kawaida ya ulimwengu inamaana wote wafatao tabia ya ulimwengu huu mitindo au mwenendo mzima wa maisha ya dunia ni wafu mbele za Bwana

Lakini sasa ukifuwata sheria za ufalme wa Mungu ni lazima ukubari kubadilika unaishi ktk hìi dunia lakini tabia inakuwa ya ufalme wa Mungu ukubari kuacha, kutii na mambo mbalimbali utakayo amliwa kufanya na ufalme wa Mungu Je tupotayari kuacha tabia na mwenendo wa dunia hii au tupotayari kuishi kimazoea wokovu wa vuguvugu na baridi? Kuulidhisha mwili ktk tabia za dunia na mwisho wa siku tuishie jehanamu? Uamuzi ni wako na uchaguzi pia

07/02/2022

NAWASALIMU KTK JINA KUU LA YESU KRISTO

Ningependa tujifunze pamoja jambo hili ktk biblia ufunuo 12: 7 na kuendelea inaeleza kwamba kuna vita ilifanyika mbinguni kisha ibilisi na malaika ambao sasa wanaitwa mapepo ambao waliasi enzi yao walitupwa hapa duniani na ni mwenye ghadhabu kubwa sana na mwanadamu sasa onahii

Shetani ni mwelevu sana japo anaghadhabu akienda kwa mtu hutumia njia ambayo hutamgundua kuwa niyeye
Jambo la muhimu kujuwa njia anazotumia kuja kwako hapo utashinda na zaidi sana kupata msaada wa Roho ya Mungu yani ROHO MTAKATIFU

Mbinu zake: anaweza kwenda kwa mtu kwa kumtumia mtu au watu, anaweza pia kutumia mawazo yako ukaona unachowaza ni sawa kumbe mawazo yamesha ingiliwa na adui, mazingila yanayo kuzunguka, watu unaowaheshimu na kuwasikiliza sana na nyingine nyingi tu kumbuka yeye ni roho so tegemea mambo mengi kutoka kwake muda mwingine hata kutumia maandiko

Mfano: mathayo 4:1_11 hapa shetani anamjaribu YESU kwa kutumia maandiko sasa kwakuwa YESU alikuwa anajuwa maandiko alimjibu ipasavyo na shetani akamwacha Yesu

Nataka nikwambie nini! maisha yamezungukwa na ghadhabu ya ibilisi wala hatatamani hata siku moja ufanikiwe kwachochote wala kupatana na yoyote angali yupo duniani

Kuna wakati unaweza kugombana na ndugu, wafanyakazi wenzako, watu wa dhamani, majirani ukajuwa ni hawo kumbe unasemezana na adui bila wewe kujua adui anaweza kukusemesha kupitia mtu usipokuwa na hekima ya kuhukumu mambo unaweza kuona Mungu amekwacha siku zote lazima uwe mwelevu k**a nyoka usiwe na hasira za haraka jambo lolote linalokutokea mbele yako jifunze kulipa muda bila kujari ukubwa wake jifunze kuhojiana na Mungu yeye atakwambia chanzo cha tatizo ni nini hapo utakuwa umemshinda adui, adui shetani humfanyia mtu mambo ya kukera sana kuhakikisha hakupi muda wa kungoja kwa maumivu ya jambo hilo na wewe sasa kwanzia leo badilika jifunze kutoa muda, kuomba, na kuhojiana na Mungu juwa sana maandiko maana ndio silaha pekee ya kupiga ghadhabu ya shetani

Ukiri
Kwa jina la Yesu kwanzia leo nakataa kutawaliwa na hasira ya shetani juu ya chochote nazivuwa roho za hasira ziletazo hasara, mauti ,magomvi na machukizo bali leo natoa nafasi kwa Yesu kunifundisha namna ya kutenda kwa Jina la Yesu amen

23/12/2021

Nikusalimu ktk jina la Yesu Kristo rafiki wa fb
Nichukuwe nafasi hii kukutia moyo wewe unaye pitia magumu ktk hali yoyote ile nikwambie tu Yesu hajakuacha bado anakupigania hata sasa kwakuwa bado unapumua
Ngoja nikupe shuhuda hii siku moja nilipata simu kutoka kwa marafiki kuwa niombe nao kwahabari ya ugonjwa uliokuwa ukiwasumbua nikauguwa moyoni na kumwomba Mungu kwaajiri yao
K**a unavyo juwa Mungu anajibu akaniambia mimi ninawajuwa watu wangu niliposikia hivyo tu nikawaambia marafiki zangu kuwa wakazane kuutafuta uso wa Mungu na kumlingana Bwana zaidi ya hayo wajifunze juu ya mambo yake namtukuza Mungu kwaajiri yao maana walitii na kufanikiwa kwa hatuwa kubwa sana
Mwanadamu yoyote aliye tembea ktk sheria ya Mungu anapopitia magumu ya kushindikana na wanadamu yeye anao uwezo wa kuvuka kwanini? Mwanzo 1:26
Mungu alimfanya mtu kwa sula yake kisha akampa kibari cha kutawala ktk uso wa nchi hivyo unao uwezo wa kusemesha au kuamulu kikakutii kwakuwa wewe ni mtawala Mungu alifanya hivyo makusudi kwakujuwa yupo ibilisi mwenye kupenda madalaka ya kuwamiliki wanadamu sasa ni muda wako wa kujuwa mamlaka uliyonayo simama amulu jambo litakuwa kwa jina la Yesu

22/10/2021

Nipende kuchukuwa nafasi hii kuwasalimu ktk jina la Yesu

SOMO: HOFU YA MAUTI
__TUJIFUNZE KITU WAPENDWA JUU YA MAUTI
MAUTI NI NINI?_ NI roho inayo weza kuvaa umbo na kuingia ndani ya mnyama,mtu au vitu ikilenga kuua kuondoa uhai au kukiondosha hicho kitu ktk ulimwengu wa kuonekana kwahivyo roho hii ikiingia ndani ya mtu, biashara au mnyama inaleta mauti hivyo ni roho kamili ambayo inaweza kutembea, na kwenda mahala kwa nia ya kuleta umauti

Ufunuo 20:14 inasema mauti na kuzimu ikatupwa kumbe mauti ni kitu kabisa ambacho kinaweza kuchukuliwa na kutupwa

Ufunuo 6:8 anasema akaona mauti amepanda farasi kumbe mauti pia inauwezo wa kusafiri juu ya chochote na kuleta umauti (kupanda gari,mnyama,biashara nk)

Sasa tuhame ili tujifunze jambo kubwa la kujifunza wanadamu tumekuwa na hofu kubwa sana juu ya roho ya mauti tena haswa pale inapotaka kuleta matokeo yake ktk mali, biashara, mifugo na hata kwa wanadamu

Muda huwo ni muda ambao mwanadamu hupoteza tumaini kabisa hata la kumkumbuka Mungu
Kuna wanadamu walio wengi wakiona wamefikia ktk hali ya kupoteza hukimbilia kwa waganga kupata majibu ya uzima wao hii humchukiza sana Mungu

2WAFALME 1:1_7 mfalme ahazia alipoanguka kwenye chumba chake juu mpaka chini gholofani akaanza kuumwa yeye aliamuwa kuwatuma wajumbe wake kwenda kwa baal_ zebubu mungu wa eklon kujuwa kwamba atapona ugojwa wake au laa hiyo yote ni sababu ya hofu ya kukosa majibu kuwa atapona au laa na kusahau kuwa yupo Mungu wa kumuliza nasi miungu na kujikuta anapoteza uhai wake baada ya watumishi wake kukutana na nabii njiani na kuwaambia wale watumwa nendeni mkamwambie atakufa kwanini anaenda kuuliza kwa miungu? ndivyo ilivyo ktk baadhi ya maisha ya wengine ugonjwa unapomwingia mtu akikosa majibu hospital ataenda kwa waganga kuuliza nani kaniloga au kwanini naumwa au biashara ikifa atataka kujuwa chanjo lakini sio kwenda kumuliza Mungu bali ni waganga

Nataka nikwambia kwamba mauti akishaamuliwa kuingia ndani ya chochote hata ufanye nini huwezi kuikimbia sababu ilishaelekezwa kuja kwako

Lakini jambo la ajabu kwa Mungu kuna wakati nafasi ipo ya kumkumbusha juu ya yale uliyotenda ktk huu ulimwengu na akaghaili juu ya mauti kuondoa uhai wako
Isaya 38:1_7 mfalme Ezekia alipewa ujumbe wa mauti yake ila yeye alikumbuka kumlilia Bwana yani Mungu sababu alijuwa hata afanye nini atakufa bora kumlilia aletaye pumzi na kumkumbusha juu ya mambo aliyofanya hapa duniani mpaka kuongezewa muda wa kuishi
Jambo kubwa la kujuwa mwanadamu, hofu ya mauti isichukuwe nafasi ktk maisha yako ktk chochote hata k**a umeona huwezi tena mgeukie Mungu na Hojiana naye na usiende kuuliza kwa mwanadamu maana na yeye yupo chini ya Mungu

Yeremia 17:5 inasema amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu

Aombi yangu Bwana aondoshe hofu ya mauti ktk family zetu biashara zetu kwa watoto wetu na vitu vyote na tuwe majasili k**a simba amen

14/08/2021

NINAWASALIMU KTK JINA LA YESU

SOMO: ULINZI WA MIMBA

__MLINZI WA KWANZA WA MIMBA NI MUNGU
KISHA WANAFATA WAZAZI (MAMA) MWENYE MIMBA

__VIPENGELE HIVI NI MUHIMU SANA KUVIFUWATA SABABU NDANI YAKE VINA UJUMBE NA MAELEKEZO

:ULINZI WA MUNGU (mathayo 1:18_25

__UKITIZAMA KTK KUTUNGWA MIMBA KWA YESU UTAONA MUNGU NDIO ANAANZA KUONGEA KWA HABARI YA MPANGO MZIMA WA MIMBA YA YESU MPAKA KUZALIWA KWAKE HATA KUTOA JINA LA MTOTO, MUNGU NDIYE MLINZI WA KWANZA WA MIMBA ILI MPANGO WAKE UTIMIE KTK UUMBAJI WAKE ADUI ALIANZA KUTAFUTA ROHO YA MTOTO MAPEMA SANA

:ULINZI WA WAZAZI (MAMA)
__MZAZI NI MLINZI 2 BAADA YA MUNGU KUTIMILIZA MAAGIZO YA MUNGU NA YALE ANAYOYAONA KWA KUONYESHWA NA MUNGU AU KWA KUONYWA MZAZI ASIPOFANYA HAYO ANAARIBU MPANGO MZIMA WA MISHENI YA MUNGU

MFANO: WAAMUZI 13:2_14
UNAONA MANOA NA MKE WAKE WANAMUULIZA MALAIKA KWA HABARI YA MTOTO, NI KAZI GANI HASWA MTOTO HUYU ATAIFANYA AKIZALIWA? NA BAADA YA KUAMBIWA WALIISHI KTK HAYO MPAKA MTOTO ALIPO ZALIWA NA KUKUWA.

SWALI? NI WAZAZI WANGAPI WAMEFANYA K**A ALIVYOFANYA MKE WA MANOA? ULISHAWAHI KUMUULIZA MUNGU KWA HABARI YA JINA LA MWANAO AU UMEKUWA UKILITHISHA MAJINA WATOTO WAKO?
UKISOMA PALE JUU UTAONA MUNGU ANAMWAMBIA MARIAM UTAZAA MTOTO NA JINA UTAMWITA YESU/ EMMANUEL YANI MAANA YAKE MUNGU PAMOJA NASI HATIMA YA MTU IPO KTK JINA UNALOMWITA MTOTO WAKO ULIMWITE JINA MTOTO KULINGANA NA MAZINGILA MAGUMU UNAYOPITIA BARI MWITE JINA KULINGANA NA MAAGIZO ULIYOPEWA NA MUNGU.

__MAMBO YA KUTIZAMA NA KUCHUKUWA HATUWA
YAPO MAMBO MENGI WAMAMA YANAWAPATA WAKATI WA MIMBA MABADILIKO YA MWILI, NDOTO ZA USIKU MBAYA NA NZURI, VITISHO VYA NDUGU AU MUME , MATIZAMO YA MIZIKI ISIYO NA MAADILI NA MOVIE POTOFU ZA KUTISHA nk HIVYO NI VITU MUHIMU SANA KUWANAVYO MAKINI MAANA ADUI ANAWEZA KUTUNIA K**A SILAHA KUPANDA MBEGU YA HASARA KWA MTOTO AKIWA TUMBONI
NA UNAPOZAA MTOTO UNASHANGAA TABIA YA MTOTO INAKUWA TOFAUTI KABISA NA WATOTO WENGINE

WAKATI YESU YUPO TUMBONI MUNGU NA WAZAZI WAKE WALIJITAHIDI SANA KUMWEKA KTK NJIA NZURI NA KUMWEPUSHA NA HATARI ZOTE HATA KUFIKA HATUWA YA KUZALIWA MAHALA PASIPO STAHILI MTU KUZALIWA HIYO YOTE NI KUKILINDA KITUKUFU, NA WEWE MZAZI NI NAFASI YAKO KUMLINDA MTOTO ALIYE TUMBONI KWA GHALAMA ZAKO ZOTE
MKULIMA ANAPOPANDA MAZAO HUWA MAKINI SANA KTK MBEGU KUHAKIKISHA KILICHO ALDHINI KIKO SALAMA HAKISHAMBULIWI NA MDUDU WA AINA YOYOTE

ELIZABETH WAKATI ANAMBIMBA MARIAM alipomsalimu TU KITOTO KIKALUKA TUMBONI MWAKE NI DHAILI KWAMBA WATOTO WANASIKIA SAUTI YA NJEE NA MAMBO YANAYO ENDELEA NJEE MAASI YETU NA MAZURI YETU LUKA 1:44
MAMA UNAPOOTA MABAYA KWA MTOTO ALIYE TUMBONI USINYAMAZE KIMYA UNAPASWA KUOMBA ILI KUTIMIZA MPANGO WA MUNGU UNAPOONA VITU VIBAYA MFANO MOVIE NA MIZIKI ISIYO NA UTUKUFU USITIZAME MAANA KWA KUTIZAMA ADUI ANAPANDA MBEGU MBAYA KWA MTOTO
AMKA OMBAA KWAAJIRI YA KILA MBEGU ANAYOPANDA ADUI WAKATI WA MIMBA AU USINGIZINI

UKILI
_ SEMA BABA KTK JINA LA YESU KUANZIA SASA NINAJIOSHA KWA DAMU YA YESU NIWE SAFI MWILI NA ROHO YANGU PAMOJA NA MWANANGU HUYU ALIYE TUMBONI NINA HARIBU KILA MBEGU MBAYA AMBAYO ADUI AMEIPANDA KUPITIA NDOTO, MANENO,MIZAA, MOVIE MBAYA KWA MTOTO WANGU NINAHARBU KWA JINA LA YESU NAONDOA MAUTI ALIYOPANDA ADUI NDANI YA TUMBO LANGU NAPANDA UZIMA KWA JINA LA YESU AMEN

01/07/2021

Shalom wana fb
Kuna watu husema kuwa uponyaji wa magonjwa ulikuwa kipindi cha Yesu tu na sasa hakuna uponyaji

Nataka nikwambie tu k**a upo hapa na unasoma hii post na unaamini kuwa Yesu alitundikwa msalabani akachomwa mkuki, akawekewa taji ya miba
mathayo27:29
__kule tu kuamini teali ni uponyaji wa kwanza juwa kuwa matukio hayo yote yanamaana ktk ulimwengu wa roho
Ktk torati damu haswa ilitumika kuleta upatanisho kati ya mtu na Mungu lakini pia damu huleta uhai ndani ya mtu ndomaana damu ikimwishia mtu mauti huingia kwa mtu

Hivyo basi Yesu ni damu ya uhai alikufa ili leo afanyike uhai kwa mtu anaye hitaji uhai afya ,ulinzi ,akili,kazi,elimu,uzaonk

Damu hiyo ya Yesu alipochomwa mkuki ubavuni ilichuluzika mpaka alidhini Inalia inadai kisasi kwa watu wake, itumie damu ya Yesu kuleta upatanisho kati ya mtu na mtu au nchi na nchi
Mfano:
Agano la kale utaona damu ya habili ilivyokuwa inalia alidhini baada ya kutendewa Hiyana na ndugu yake kaini sasa sembuse ya Yesu Yesu alitendewa mabaya kushinda habili mwanzo 4:8

Ukili
Ktk jina na la Yesu nakataa udhaifu ndani ya mwili wangu naluhusu uzima ndani yangu kwa damu ya Yesu

Mathayo11:28 imeandikwa njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha
Natoka kwenye mizigo ya magonjwa ya kifamilia najiunganisha na uhai ndani ya Yesu Kristo amen
Krbu inbox kwa ushauri zaidi

30/06/2021

__Habari ya muda huu watu wa dhamani
__Leo tuangalie habari ya Yona na Mungu
Mungu alipoona maovu yamezidi ktk mji wa ninawi
Akatazama ktk nchi nani nitamtuma, akamtuma yona
Aende akapige kelele ktk huwo mji kuwa waache maovu laasivyo atawaangamiza woye Yona 1:1_

HAPA KUNA JAMBO LA KUJIFUNZA
1. dhambi ya mtu,kitu au nchi huwa inazidi mpaka kumfikia Mungu mbinguni
2. Mungu humtuma mtu sio Yoyote bali yule anayeweza kufanya hilo jambo
3.Mungu huchungulia duniani na kutizama mambo yanavyo endelea
4. Mungu hutumia chochote kufanikisha anachotaka ( samaki na yona Bahalini) yona alipogoma kwenda anapotakiwa kwenda alitupwa bahalini kisha kimezwa na samaki
__Hivyo basi unapaswa kutafakali mimi nikiwa duniani nimeagizwa mangapi kufanya na sijafanya yanayo mhusu Mungu?
__Ukisha jiuliza maswali hapo juu unapaswa kujuwa pia Mungu hutumia chochote kufanikisha anachotaka k**a mwanadamu anagoma kufanya
K**a unauhitaji wowote ktk maisha yako au mwili wako fanya kwanza ya Mungu na yeye afanye yakwako

15/05/2019

Hallo watu wote natumai mmeamka salama kabisa lipo jambo naweza kushare na wewe unajuwa ktk maisha tuliyo nayo yapo mengi maudhi lakini mema ya kuhesabu inafika mahala unakata tamaa na kuongea mengi lakini nataka nikufundishe kitu ujuwe namna ya kutumia kinywa hatak**a unamagumu kiasi gani usitamke neno lolote ambalo litasababisha kuaribu engine yako yani mwili wako maisha ya mwanadamu inategemea Sana anawaza nn anasema nn nikutakie kuwa na siku njema ya kuuzuia ulimi wako

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sili ya uhai ndani ya damu ya Yesu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Sili ya uhai ndani ya damu ya Yesu:

Share

Category