26/12/2021
SOMO: SIKU MOJA
Siku Moja Mwili wangu utakuja Kulala na sitaweza tena kufundisha watu kuhusu Yesu, sitaweza kuhubiri tena habari za Msamaha na Wokovu. Huenda watu watatamani kuisikia sauti yangu, lakini nitakuwa nimekwenda zangu kwa Baba wakati huo mwili wangu ukiwa kwenye jeneza, watoto wangu wa kimwili wakilia, mke wangu akilia, watoto wangu wa kiroho wakilia, wale niliokuwa baraka kwao ndani ya maisha yangu ya Utumishi tangu 2000 watakuwa wakilia. Hata wale ambao leo wanapuuza mafundisho yangu na mahubiri yangu, siku hiyo watanisifia na kusema walinipenda sana. Huku mimi nitakuwa niko zangu kwa Baba namshangaa Paulo Mtume mtu aliyeupindua ulimwengu wa nyakati zake kwa Injili. Nitakuwa namshangaa Daudi kijana aliyewapenda adui zake kuliko watu waliompenda (hili kwangu ni somo gumu kuliko hata kumuua Goliath). Nitakuwa namshangaa wajina wangu aliyempenda kiongozi wake Musa kwa kiwango cha kutokutaka mwingine awe k**a Musa (wewe mwenyewe si unaona vita yako na kiongozi wako ukitaka uonekane upo juu?). Tabia za Daudi na Joshua zitanifanya niwashangae sana bila kusahau uchapa kazi ya Injili wa Paulo Mtume bila kusahau Utoaji wa Ibrahimu utanifanya nae nimshangae.
Ndiyo ipo siku mwili nilionao huu nitaachana nao! Hata k**a kuna watu watalia sana na kutokuamini, lakini ukweli utabaki hivo kwamba nimeondoka na wengine tutaonana kwa Baba. Sijui ni lini? Hiyo ni siri ya Mungu wangu, mimi sijui. Huenda nitapata neema ya kutokuonja mauti, lakini alijuaye hilo ni Mungu pekee.
Kuna mwisho wa maisha yangu k**a kulivyokuwa na mwanzo wa maisha yangu. Hakuna aliyeishi milele baada ya kuzaliwa. Wameondoka watakatifu wa Bwana, wameondoka pia watumishi wa shetani. Kifo hakijawahi kuchagua k**a jinsi ambavyo Mpagani anavyoondoka ndivyo mcha Mungu anavyoondoka. Tofauti yetu ni sehemu ya kwenda tu baada ya kuondoka kwetu hapa duniani.
Kwanini nasema haya? Mpendwa wangu acha niseme na wewe japo kidogo tu, naomba usinichoke kunisoma eti kwa vile andishi ni refu kwa hiyo linaboa. Hapana mpendwa nisikilize japo kidogo tu.
K**a kulivyo na mwisho wa mwaka, ndivyo kulivyo na mwisho wa sekunde, dakika, lisaa, siku, wiki na mwezi. Hakuna kinachodumu hapa duniani. Hata hii Sayari tunayoiishi upo mwisho wake. Lakini upo mwisho wa miisho yote. Swali langu kwako, Je, mwisho wako utakapowadia, siku utapokuwa umelala, huwezi kusema tena, huwezi kuyatenda hayo unayoyatenda leo, UTAKWENDA WAPI? MILELE YAKO ITAISHIA KUWA YA MAHALI GANI? Kumbuka kwamba utakufa na hayo yote yanayokupa KIBURI leo hayatakusaidia kukikwepa kifo. Elimu yako haitakusaidia, wala utajiri wako hautakusaidia. Utazikwa k**a tajiri wa LUKA 16:19,22-31? Au utachukuliwa na Malaika kwenda kwa Baba Mbinguni k**a Lazaro wa LUKA 16:20-22?
Binti ambaye leo kila saa unajiangalia kwenye kioo ukijishangaa namna ambavyo Mungu alivyokuchora kwa ustadi, lakini huo uzuri wako unautumia vibaya kwa kuwa bidhaa inayojiuza. Siku utakapokufa, utakuwa mgeni wa nani? Nazungumza na wewe kijana, ambaye unajiona Handsome, hakuna k**a wewe, unaelimu, unapesa, unausafiri, unakazi, unanyumba ambayo unaitumia k**a danguro kubadilisha wasichana kila uwatakao. Siku utapoondoka maana utaondoka hata k**a hutaki, utakuwa mgeni wa nani? Maisha yako yote, yatakuwa ya kilio na kusaga meno. Utalia kilio chako, kitaonekana k**a ni kilio cha samaki. Hakuna atakayejali kilio chako k**a jinsi ambavyo wewe leo hujali kelele zetu za maonyo juu yako. Nazungumza na wewe Baba ambaye unautumia utajiri wako kulagai watoto wa wenzako, nazungumza na wewe boss ambaye kazini kwako unaitumia nafasi yako kuwanyanyasa watu kingono. Nazungumza na wewe meneja mwajiri unaetaka rushwa. Nazungumza na wewe polisi unaebambikiza watu kesi za uongo! Ipo siku utalala kimyaaaa kwenye sanduku lako. Wakati huo utakuwa ndani ya sanda, pua zako zitakuwa zimewekwa pamba, mdomo wako nao utakuwa umelazimishwa kufumba, wakati huo masikio yako yatakuwa yamewekwa pamba ya kweli tofauti na sasa ulivyoweka pamba hutaki kusikia Injili. Utakuwa mgeni wa nani? Maana utakufa tu. Binti unaejifanya jeuri leo, hutaki kusikia habari za kuokoka, unawaona waliokoka ni washamba, ipo siku utalala moja kwa moja. Jeuri yote, Kiburi chote kitakuisha. Utakuwa mgeni wa nani?
Mtu mwenye hekima, huitafakari kwa kina kesho yake. Kesho yako bora inatengenezwa na leo yako. Watu wengi wapo makini kuitengeneza kesho yao bora katika maisha haya ya kawaida. Ni vizuri kufanya hivo wala sikukatishi tamaa kuiandaa kesho yako bora. Ila nakupa ushauri uliobora pia. Unapokazana kuiandaa kesho yako iliyobora, pia jiandaye kiroho zaidi. Maana maisha yako baada ya kifo yatakuwa ya milele. Urefu wa maisha yako ya sasa unayoyahangaikia ni k**a tone la maji kwenye bahari zote ulimwenguni. Hayafananishwi na milele yote utakayokuja kuiishi. Usidanganywe na mafundisho ya manabii wa uongo wanaosema ukifa sijui ndugu zako watatoa sadaka za kukusogeza mbinguni taratibu. Usidanganywe na wahubiri hao uchwara. Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu. Na pia inasema Mungu hapokei rushwa! Kumbuka tajiri tuliyemwona kwenye LUKA 16:22-31 alikuwa na ndugu ambao wangeweza kutoa sadaka za kumfanya aende mbinguni, lakini Ibrahimu hamwambii hayo wanayokufundisha wahubiri uchwara.
Kumbuka pia Biblia inasema, kila mtu atatoa habari zake mwenyewe. Hutasingizia kwamba viongozi wako wa dini walikufundisha hivo. Utakwenda mahali pa mateso.
Pia usidanganywe na mashetani ambao wanasema Mungu hataihukumu dunia tena. Hao ni mashetani wanaotaka kwenda na watu wengi motoni. Usikubali huo ujinga. Jehanum ya Moto ni halisi na kuzimu pia ni halisi.
Itumie leo yako vizuri kwa kutubu Dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha. Usipotubu, anasema hivi katika kitabu cha UFUNUO 2:16 "Basi tubu; naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu". Ni hiali yako kuzisadiki habari hizi au kutupuuza. Lakini ushauri wangu kwako OKOKA, acha Dhambi.
Bwana Yesu leo anaweza kukupa zawadi ya Boxing day (WOKOVU), Je, upo tayari au bado utaendelea kushik**a na jeuri yako? Naamini hutaendelea na huo upumbavu! Basi naomba unifuatishe sala fupi hii ya toba, na bila shaka utapata Msamaha wa dhambi. Sema "Bwana Yesu, ninakuja kwako. Mimi ni mwenye dhambi, kwa kutenda na kwa kuzaliwa. Natubu dhambi zangu zote, nisamehe uovu wangu wote. Futa majina yangu kwenye vitabu vya hukumu. Andika majina yangu kwenye kitabu cha uzima mbinguni. Ahsante kwa kunisamehe, katika Jina la Yesu, Amina.
Tayari umeokoka, tangu sasa anza kutafuta mafundisho yatakayokufanya uweze kukua kiroho sawa sawa na 1PETRO 2:2.
Sasa tayari umeokolewa, na kwa msaada zaidi wa kiroho, tafadhali nipigie kwenye simu 0767010109.
Mwl Joshua Africa Mwakyusa.
Huduma ya
Huu ndiyo mwandiko wangu mimi mwenye nimekuandikia maonyo haya ya kinabii. Mungu akubariki sana. Unaweza kushare kwenye groups zako ili ujumbe uwafikie wengi.
Barikiwa Sana, na Heri ya Mwaka Mpya 2022