Efatha Church Kinondoni

Efatha Church Kinondoni Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Efatha Church Kinondoni, Religious organisation, Bunju Usalama Dar es Salaam, Dar es Salaam.

Hii ni page ni maalumu kwa ajili ya huduma za kiroho ambazo zinatolewa na Kanisa la Efatha Mkoa wa ki-efatha Kinondoni hususani kituo cha Bubujiko kinachoongozwa na Mchungaji Kiongozi Erwin Herman Mahundi.

Karibu Ibada ya mkesha Leo tarehe 5/6/2025Karibuni watu wote
04/06/2026

Karibu Ibada ya mkesha
Leo tarehe 5/6/2025
Karibuni watu wote

03/06/2026
*SIKU YA ISHIRINI NA SABA YA KUFUNGA NA KUOMBA*Tunamshukuru Mungu kwa neema yake katika safari hii ya kiroho. Leo ni sik...
27/05/2026

*SIKU YA ISHIRINI NA SABA YA KUFUNGA NA KUOMBA*

Tunamshukuru Mungu kwa neema yake katika safari hii ya kiroho. Leo ni siku ya kutulia mbele zake, kutafuta uso wake na kusikiliza sauti yake kwa undani zaidi.

Usikate tamaa katika maombi, maana Mungu huwajibu wale wanaomtafuta kwa moyo wa kweli. Endelea kusimama katika imani, ukijua kwamba Mungu anaendelea kufanya kazi katika maisha yako.

Zaburi 27:8 (SUV) “_Uliposema, Nitafuteni uso wangu, moyo wangu umekuambia, Bwana, uso wako nitautafuta._”

NENO LA SIKUNa, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la EfathaTAREHE: 26/05/2026SOMO: FUATA NJIA ZA MAONO YA ...
26/05/2026

NENO LA SIKU

Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha

TAREHE: 26/05/2026

SOMO: FUATA NJIA ZA MAONO YA MOYO WAKO

Njia za moyo wa mtu huja kwa kuwaza na kusema, atakuwa na vitu vizuri au atafanya hivi na vile. Anapozingatia kwa bidii njia za moyo wake, ndipo hufikia matarajio yake.

Mtu anaporuhusu moyo wake ufurahi, hutengeneza njia ndani yake na huanza kuziona. Moyo wenye furaha, mara zote huleta kitu kizuri katika mawazo ya mtu na hilo wazo huwa jema kwa ajili ya ubaadaye wake.

Maisha yenye maana ni mtu kuishi kwa matarajio ya maono yake ambayo husababisha apate majibu kutoa wa MUNGU. Kadri mtu anavyotamani kuona ubaadaye wake, ndivyo MUNGU anavyokamilisha maono yaliyo ndani yake.

Maono huhitaji utekelezaji ili yatimie, maana Biblia inasema “Imani bila matendo imekufa”. Umakini wa kutekeleza maono ni jukumu la mtu mwenyewe na MUNGU huangalia hilo ili afanikishe.

SIKU YA ISHIRINI NA TANO YA KUFUNGA NA KUOMBA.Tukiwa katika siku ya ishirini na tano, tunashuhudia uaminifu wa Mungu amb...
25/05/2026

SIKU YA ISHIRINI NA TANO YA KUFUNGA NA KUOMBA.

Tukiwa katika siku ya ishirini na tano, tunashuhudia uaminifu wa Mungu ambao hauyumbi. Tumefika hapa si kwa nguvu zetu, bali kwa rehema zake zisizokoma.

Tunaendelea kusimama katika nafasi ya maombi, tukitafuta uso wa Mungu kwa bidii na unyenyekevu. Kadri tunavyokaribia mwisho wa safari hii ya kiroho, tunatambua kuwa kila siku imekuwa mbegu ya imani, uvumilivu na ufunuo wa neema.

Tumemuona Bwana akizidi kutujenga na kutubadilisha. Tunaendelea kumsihi Bwana azidi kuimarisha mioyo yetu, atupe kuona mbele kwa macho ya imani na kutufanya tayari kwa yote anayotarajia kutoka kwetu.

Isaya 40:31 (SUV) “bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa k**a tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”

24/05/2026

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 24/05/2026

18/05/2026

NDOTO

Address

Bunju Usalama Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Kinondoni posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Efatha Church Kinondoni:

Share