Goshen Ministries International

Goshen Ministries International Kusudi kubwa la Page hii ni
(1) Kuwakamilisha watakatifu,
(2) Kazi ya Huduma itendeke
(3)Tatu Mwili wa Kristo ujengwe, (4) Kuufikia umoja wa Imani

22/09/2019

SAFARI YA KUMILIKI
Neno la Msingi:
Kumbukumbu 2:24
“Ondokeni, mshike safari yenu, mvuke bonde la Arnoni; tazama, nimemtia Sihoni Mwamori mfalme wa Heshboni mkononi mwako, na nchi yake; anzeni kuimiliki, mshindane naye katika mapigano.

Watu wengi hawaelewi juu ya safari ya kumiliki inavyokuwa. Wanafikiri baada ya kuambiwa juu ya ahadi fulani ya mafanikio au unabii fulani wa mafanikio basi kumiliki hayo kutakuja "automatic" bila kutoa jasho lolote wala jitihada zozote binafsi, huko ni kujidanganya. Safari ya mafanikio ni Safari ndefu ya kuvuka mabonde, kupanda na kushuka vilima na milima. Hakuna kitu chochote ya kumiliki ambacho utakipokea kwa mteremko hata k**a neno la Mungu limesema kuhusiana na hicho.

Kumbukumbu 2:1-3
“Ndipo tukageuka, tukashika safari yetu kwenda jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu, k**a alivyoniambia BWANA; tukawa kuizunguka milima ya Seiri siku nyingi. BWANA akanena, akaniambia, Mlivyouzunguka mlima huu vyatosha; geukeni upande wa kaskazini.”

MAANA YA KUMILIKI
Kumiliki ni kutawala vitu fulani k**a nyumba, mashamba, mali n.k.
Mmiliki ni mtu anayemiliki vitu k**a nyumba, mashamba, mali n.k.

Mithali 8:15-16
“Kwa msaada wangu wafalme humiliki, Na wakuu wanahukumu haki. Kwa msaada wangu wakuu hutawala, Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia.”

Kumbukumbu 1:8
“Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao.”

SAFARI YA KUMILIKI
Safari ya kumiliki ina mambo mengi ya kuyafanya na kufuatilia. Ili uone kumiliki kunafanyika katika maisha yako lazima ufahamu kwamba kumiliki ni Safari. Safari inachukua muda, umbali, nguvu, uelekeo, utofauti wa mazingira, hali ya hewa, uono wako n.k.

Kumbukumbu 2:24-25
“Ondokeni, mshike safari yenu, mvuke bonde la Arnoni; tazama, nimemtia Sihoni Mwamori mfalme wa Heshboni mkononi mwako, na nchi yake; anzeni kuimiliki, mshindane naye katika mapigano. Hivi leo nitaanza mimi kutia utisho wako na kuhofiwa kwako juu ya watu walio chini ya mbingu kila mahali, watakaosikia uvumi wako, na kutetemeka, na kuingiwa na uchungu kwa sababu yako.”

I. Ahadi
Biblia ni kitabu kilichojaa ahadi za Mungu kwetu watoto wake. Mungu ameahidi kutumilikisha mambo mengi katika maisha yetu. Uzuri wa Mungu hasemi uongo kile ambacho amekisema at akitimize bila shaka. Mungu alitoa ahadi juu ya Taifa la Israeli la kumiliki nchi NJEMA, PANA iliyojaa MAZIWA na ASALI. Lakini katika hiyo nchi kulikuwa na watu wanaoimiliki. Mataifa makubwa ambayo ukilinganisha na Taifa la Israeli wal ionekane ni watu wasio na uwezo tens walikuwa wachache.

Kutoka 3:7-8
“BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.”

II. Mipango
Ahadi yoyote lazima iambatane na mipango mikakati wa kutaka kutimia kwa ahadi hiyo. Mpango unasaidia kutembea katika malengo ambayo umejiwekea. Macho yako yanatakiwa kuangalia mpango ambao huko mbele yako.

Mithali 16:1, 3
“Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.
Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika.”
‭‭
Usiache macho yako kuangalia mpango wako ulionao. Usiruhusu kutoka katika lengo lako ambalo unaloliendea. Uwe king'ang'anizi katika kile ulichokipanga.

Mithali 4:25
“Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.”
‭‭
III. Ondoka/Chukua hatua
Kuondoka ni kuchukua hatua ya kutoka hapo ulipo na kwenda kwenye hatua nyingine kuelekea ndoto au mpango wako. Hauwezi kumiliki ikiwa hautakubali mabadiliko chanya katika maisha yako.

Wafilipi 2:13
“Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.”
‭‭
IV. Shika Safari
Kushika Safari ni kuendelea kutembea katika mpango wako wa kumiliki bila kuangalia mazingira yanayokuzunguka. Mazingira yanaweza kukukatisha tamaa lakini wewe endelea kushika Safari yako.

Mwanzo 13:17-18
“Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo. Basi Abramu akajongeza hema yake, akaja akakaa kwenye mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea BWANA madhabahu huko.”

Waebrania 11:8-10
“Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, k**a katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.”

V. Vuka Bonde
Kuna wakati wa kuvuka bonde. Siyo kila wakati ni tambarare kwingine kuna bonde la kulivuka. Unapoelekea kumiliki kuna wakati unatakiwa uvuke bonde. Bonde inaweza ikawa ni kukosa mtaji, Ada ya shule, kukosa msaada kwa watu wako wa karibu, kuumwa au kuuguliwa n.k.

Zaburi 23:4
“Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.”‭‭

VI. Mtambue Adui aliyek**ata nchi yako
Lazima uweze kumtambua Adui yako. Yule ambaye ameshikilia Uchumi au Afya yako. Adui ambaye amekamta kitu chako cha kukimiliki.

Mathayo 13:24-25
“Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.”

VII. Shindana na Adui
Ukishamfahamu adui hautakiwi kumchekea Bali ushindane naye katika mapigano. Unajua ni roho ya umaskini au roho ya kukurudisha nyuma kimaendeleo au ni roho ya chuma ulete ni lazima ushindane nayo hadi kieleweke.

Luka 11:21-22
“Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama; lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang’anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.”


VIII. Anza kumiliki
Kumiliki kunaanzia ndani ya nafsi yako. Unaanza kuona mafanikio, baraka, ushindi ndani ya nafsi kabla ya kuona kiuhalisia. Maadui unawaona wamekwishaachia baraka zako.

Mithali 23:7
“Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.”
‭‭
Hesabu 14:6-9
“Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. Ikiwa BWANA anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye BWANA yu pamoja nasi; msiwaogope.”

Bishop Emmanuel Mbagwile (+255 715 136868)
‭‭

09/07/2019

KUIOMBEA NDOTO YAKO
Habakuki 2:1-2
“Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu. BWANA akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma k**a maji.”
‭‭
Ndoto yoyote haiwezi kutimia pasipo maombi ya kina. Ili ndoto tuliyonayo iweze kutimia inahitaji kuiatamia katika maombi. Baada ya kuku kutaga mayai anachokifanya ni kuyaatamia yale mayai hadi siku za kutotolewa vifaranga zitakapotimia. Wakati kuku anaatamia mayai yake kinywa chake huwa na sumu ya kuwadhuru maadui wanaotaka kuharibu mayai yake.

1. NDOTO NI NINI?
Ndoto ni ule mpango au kusudi ulilonalo ndani ya moyo wako. Ni lengo ambalo unataka liweze kutimia katika maisha yako. Ni kitu ambacho unachokiona ndani ya nafsi yako. Kile unachokiona ndivyo kitakavyokuwa.

Mithali 23:7
“Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.”

Yeremia 1:11
“Tena neno la BWANA likanijia, kusema, Yeremia, waona nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi.”

2. KUIOMBEA NDOTO YAKO
Ni muhimu sana kuiombea ndoto yako kwa kuwa adui hafurahii kutimia kwa ndoto hiyo. Usifikiri kwamba ukiwa na mpango au lengo zuri litaenda tu kwa kuwa ni la Mungu. Kitu kzuri chochote cha mwana wa Mungu hukabiliwa na upinzani kutoka kwa adui. Kwahiyo mtu wa Mungu ni lazima uchukue muda mrefu kuiombea ndoto uliyo nayo.

‭Kila ndoto kubwa inahitaji maombi makubwa (mengi). Upinzani kwenye ndoto kubwa ni mkubwa vile vile.

1Wakorintho 16:9
“kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.”
‭‭
Anna binti Fanueli alichukua muda mrefu kuiombea ndoto yake ya kuzaliwa kwa Yesu. Alitumia muda mwingi wa maisha yake katika kuiombea ndoto kubwa ambayo aliipata kutoka kwa Mungu. Ndiyo maana baada ya kutimia kwa ndoto yake alimshukuru Mungu na kuwaelezea wengine juu ya yeye aliyezaliwa. Ndoto ikitimia unamshukuru Bwana.

Luka 2:36-38
“Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.”

3. JINSI YA KUIOMBEA NDOTO YAKO
‭I. Mkabidhi mipango yako (ndoto)
Mithali 16:3-4
“Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika. BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.”

‭‭Kila ndoto uliyo nayo inatakiwa uikabidhi kwa Mungu kwa njia ya maombi. Mipango ya kazi unamkabidhi Muajiri Mkuu kwanza kabla haujaenda kwenye ofisi yeyote ile.

II. Mkumbushe juu ya mipango yako (ndoto)
Isaya 43:26
“Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.”

Ni wajibu wako kumkumbusha Mungu kuhusiana na ndoto yako. Mungu ameweka utaratibu wake wa kutaka kukumbushwa juu ya yale unayoyahitaji kutoka kwake. Usipomkumbusha na yeye anakaa kimya.
‭‭
III. Omba bila kukata tamaa
Luka 18:1
“Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.”

Endelea kuomba bila ya kukata tamaa hata k**a kunaonekana kuchelewa. Labda unaomba kazi na nafasi yako yuko mtu mwingine anatakiwa aondolewe pale halafu upachikwe wewe k**a ilivyokuwa kwa Malkia Esta, Vashti malkia afanye kosa na kuondolewa kwenye nafasi ya umalkia halafu Esta awekwe mahali pake.

IV. Ombea ndoto yako kwa IMANI
Yakobo 1:5-6
“Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni k**a wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.”

Maombi yako yanatakiwa yachanganyikane na Imani. Unaweza ukaomba sana lakini hauna imani hapo unakuwa unajaza maji katika debe lililotoboka. Ombea ndoto yako kwa Imani.
‭‭
Bishop Emmanuel Mbagwile (+255 715 136868)

‭‭

30/04/2019

BARAKA ZA KUWEKA NADHIRI NA KUIONDOA
Neno la Msingi:
Zaburi 76:11
“WEKENI NADHIRI, MKAZIONDOE Kwa BWANA, Mungu wenu. Wote wanaomzunguka wamletee hedaya, Yeye astahiliye kuogopwa.”
‭‭
Watu wengi hawafahamu nguvu na baraka za kuweka nadhiri mbele za Mungu. Kila mmoja wetu akipata ufahamu juu ya somo hili ataweza kuziona baraka za Mungu katika maisha yake. Kuweka nadhiri mbele za Mungu ndiyo sadaka kubwa na yenye nguvu ya kufanya mambo ya kushangaza katika maisha yetu.

I. NADHIRI NI NINI?
Nadhiri ni sadaka ya hiari ambayo mtu ameihaidi kwa kinywa chake. Nadhiri ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako kwamba utafanya jambo fulani. Nadhiri ni ahadi ambayo mtu ameiahidi kwamba atafanya au atatoa. Mtu anapokuwa katika taabu fulani na akaamua kutamka maneno ya ahadi mbele za Mungu kwamba akitolewa katika taabu hiyo atatenda jambo fulani kwa Mungu hiyo ni nadhiri.

Zaburi 66:13-14
“Nitaingia nyumbani mwako na kafara; NITAONDOA kwako NADHIRI zangu; Ambazo midomo yangu ilizinena; Kinywa changu kikazisema nilipokuwa taabuni.”

Mwanzo 28:20-21
“Yakobo AKAWEKA NADHIRI akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu.”

II. KUWEKA NADHIRI
Kuweka Nadhiri ni kitendo cha mtu kuahidi kutoa sadaka ya hiari kwa kinywa chake. Kuweka nadhiri mbele za Mungu ni kutoa ahadi kwa kinywa chako juu ya sadaka ya hiari ambayo utaitoa siku fulani zinazokuja. Kwa kawaida ukishaweka nadhiri usiwe mlegevu kuiondoa kwakuwa ukichelewa inakuwa ni dhambi kwako uliyoiweka.

Kumbukumbu 23:21-23
“Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako. Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitakuwa dhambi kwako. Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri BWANA, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.”

Hesabu 30:2
“Mtu ATAKAPOMWEKEA BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; ATAFANYA sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.”

Ukishaweka nadhiri umekwishaweka hauwezi kusema sikuweka, Bali hiyo nadhiri itakuwa juu yako wakati wote hadi uiondoe.

Zaburi 56:12
“Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu; Nitakutolea dhabihu za kushukuru.”

III. MADHARA YA KUTO-KUONDOA NADHIRI
Chochote kile kilicho kizuri kina baraka zake na madhara yake. Yapo madhara tunayoyapata pale ambapo hatuziondoi nadhiri zetu ambazo tuliziweka mbele za Mungu.

i). Kufanya dhambi
Mtu ambaye haondoi nadhiri yake anafanya dhambi. Kwenye Arusi na mambo mengine anatoa ahadi lakini kwa Mungu haondoi tayari mtu huyo yuko dhambini.
Kumbukumbu 23:21-23
“Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.

ii). Kuwa kwenye laana
Asiyeondoa nadhiri aliyoiweka anajiingiza mwenyewe katika laana. Ukiona mambo hayaendi lazima ujiangalie wewe binafsi k**a huko na shida hiyo.
Malaki 1:14
“Lakini na alaaniwe mtu mwenye kudanganya, ambaye katika kundi lake ana mume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema BWANA wa majeshi, na jina langu latisha katika Mataifa.”
‭‭
iii). Kuwa mpumbavu
Tusipoondoa nadhiri tunahesabika kuwa ni wapumbavu mbele za Mungu. Ukiwa unaomba juu ya baraka kinachoonekana ni mpumbavu anaomba baraka.
Mhubiri 5:4-5
“Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri. Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe.”

IV. BARAKA ZA KUONDOA NADHIRI ULIYOIWEKA
Baraka tele zinamsubiri mtu yeyote ambaye ataweka nadhiri na kuiondoa nadhiri hiyo kwa wakati wake. Muda ni muhimu sana katika kuziondoa nadhiri zetu ambazo tuliziweka mbele za Mungu.

Zaburi 22:25
“Kwako zinatoka sifa zangu Katika kusanyiko kubwa. Nitaziondoa nadhiri zangu Mbele yao wamchao.”

Zaburi 116:14
“Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA, Naam, mbele ya watu wake wote.”

Ziko baraka nyingi zilizoko katika kuziondoa nadhiri lakini hapa tutaziangalia chache.

i). Bwana atasikia maombi yako
Unapotimiza nadhiri yako, Bwana atasikia kila ombi ambalo utakalomuomba lililo katika mapenzi yake.
Mhubiri 22:27-28
“Utamwomba yeye naye atakusikia; Nawe utazitimiliza nadhiri zako. Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako.”
‭‭
ii). Njia zako zitakuwa na Mwanga
Njia kuwa na Mwanga maana yake hautatembea katika giza bali nuru itamulika kila unalolifanya na kulielekea. Mikosi na balaa haitakuwako.
Mhubiri 22:27-28
“Utamwomba yeye naye atakusikia; Nawe utazitimiliza nadhiri zako. Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako.”

iii). Malengo yako yatafanikiwa
Kila lengo ulilonalo katika maisha litafanikiwa kwa kuwa umeonyesha UAMINIFU kwa Mungu kwa kutimiza nadhiri zako.
Mhubiri 22:27-28
“Utamwomba yeye naye atakusikia; Nawe utazitimiliza nadhiri zako. Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako.”

iv). Kuokolewa siku ya mateso
Mtu anayeondoa nadhiri kwa wakati wake huokolewa siku ya mateso inapofika kwenye hema yake.
Zaburi 50:14-15
“Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye juu nadhiri zako. Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.”
‭‭
Yona 2:9-10
“Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa BWANA. BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.”

‭‭v). Asiyefaa hatapita juu yako
Shetani na maajenti wake hawatapita na kuharibu maisha yako na familia yako. Uharibifu utakuwa mbali nawe.
Nahumu 1:15
“Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.”
‭‭
"Ukiyajua hayo ni HERI WEWE ukiyatenda"

Bishop Emmanuel Mbagwile (+255 715 136868)

12/04/2018

NENO LA KRISTO LIKAE KWA WINGI- II
Neno la Msingi:
Wakolosai 3:16
“NENO LA KRISTO NA LIKAE KWA WINGI NDANI YENU katika HEKIMA YOTE, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.”
‭‭
Nyakati tulizonazo ni nyakati za hatari ambazo watu wengi hawatapenda kukaa katika Neno la Mungu la kweli bali katika madanganyo matupu. Na wengine watajipatia waalimu makundi makundi wa kutaka kufundishwa yale mambo wanayoyataka wao. Jambo linalofundishwa likiwa tofauti na matakwa yao hulipiga kijembe NENO hilo.

4. FAIDA ZA NENO LA MUNGU
Ziko faida nyingi ambazo tunazozipata katika kulifanya Neno la Mungu kukaa ndani yetu. Zifuatazo ni faida chache ambazo tumeziainisha katika somo hili.

I). Huongeza Imani ndani yetu
Imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa kupitia Neno la Kristo. Iwapo hatuna Imani au Imani zetu ni dhaifu tunaweza kuongezeka kukua katika imani kwa kusikia Neno la Mungu.

Warumi 10:17
‭“Basi imani, chanzo chake ni KUSIKIA; na kusikia huja kwa NENO LA KRISTO.”

II). Husababisha Baraka maishani
Tunapochukua hatua ya kusikia na kulishika Neno la Mungu tunaachilia baraka za Mungu katika maisha yetu. Kila kitendo cha wewe kuweza kusikia Neno la Mungu iwe ni Kanisani, Redioni, Television au Mahali popote huachilia kiasi cha baraka kwetu.

Luka 11:28
“Lakini yeye alisema, Afadhali, HERI WALISIKIAO NENO LA MUNGU na KULISHIKA.”

III). Silaha dhidi ya Adui yetu
Adui yetu mkuu watu wa Mungu ni Shetani. Shetani ni kiumbe cha kiroho ambacho tutaweza kukishinda tukiwa tumeliweka Neno la Mungu kwa wingi ndani yetu. Neno linatajwa k**a UPANGA wa roho.

Waefeso 6:17
“Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na UPANGA WA ROHO ambao ni NENO LA MUNGU;”

IV). Husafisha maisha yetu
Maisha yetu katika wokovu husafishwa kupitia Neno la Mungu. Hakuna namna yoyote ya kuwa safi mbele za Mungu bila ya Neno la Mungu. Wewe unayesoma somo hili ukiwa unaishi maisha machafu ya dhambi lazima ujifahamu kwamba hauna Neno la Mungu ndani.

Yohana 15:3
“Ninyi mmekwisha kuwa SAFI kwa sababu ya lile NENO nililowaambia.”

V). Hutuponya na kututoa katika maangamizo
Magonjwa yoyote yale ambayo tunayokutana nayo katika maisha yetu inawezekana kuponywa kupitia Neno la Mungu na kiasi cha Imani kinachohusiana na tatizo ulilonalo. Tafuta Neno linalohusiana na changamoto unayoipitia na kulitafakari Neno hilo ili upate uvumbuzi wa tatizo lako.

Zaburi 107:20
“Hulituma NENO LAKE, HUWAPONYA, Huwatoa katika MAANGAMIZO yao.”

VI). Hutuwezesha kutokutenda dhambi
Tunapoliweka neno la Mungu moyoni tunakuwa na uwezo wa kutokutenda dhambi. Iko tofauti ya kuliweka Neno la Mungu KICHWANI na kuliweka MOYONI. Ukimuona mtu anatenda dhambi na anasema analijua Neno sana, ujue huyo ana neno kwenye kichwa chake (head knowledge) lakini moyoni hakuna Neno la Mungu. Mtu anaweza kufaulu vizuri katika Bible Knowledge lakini akawa hajaokoka na ni mtenda dhambi wa kawaida kwa kuwa maarifa hayo yako kichwani hayako moyoni.

Zaburi 119:11
“MOYONI mwangu nimeliweka NENO LAKO, NISIJE NIKAKUTENDA DHAMBI.”

VII). Linatujenga kiroho na kutupatia Urithi wetu
Tunahitaji kujengeka kiroho ni kwa kuliweka Neno la Mungu kwa wingi ndani ya mioyo yetu.

Matendo 20:32
‭“Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa NENO LA NEEMA YAKE, ambalo laweza KUWAJENGA na KUWAPA URITHI pamoja nao wote waliotakaswa.”

5.‭ JINSI YA KULIWEKA NENO LA MUNGU NDANI YETU
I). Kusikia Neno la Mungu
Ni muhimu sana KUSIKIA Neno la Mungu. Tunaweza kuliweka Neno la Mungu kwa wingi wetu pale tunaporuhusu masikio yetu kusikia. Huu ni mlango mkubwa sana wa kuliweka Neno la Mungu.

Kumbukumbu 28:1
“Itakuwa UTAKAPOISIKIA sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;”

Tunalisikia Neno la Mungu kupitia watumishi wake wanadamu ambao Mungu amewaweka kwa ajili yetu kwa kusikiliza mahubiri ya moja kwa moja au kupitia vyombo vya kisasa vya kusikia iwe ni Redio, Simu n.k.

1 Wathesalonike 2:13
“Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu MLILOLISIKIA kwetu, mlilipokea si k**a neno la wanadamu, bali k**a neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.”

II). Kulisoma Neno la Mungu
Yeyote anayetenga Muda wake kulisoma Neno la Mungu lazima ataziona baraka. Haitoshi kusoma Neno la Mungu kanisani tu bali tunapokuwa majumbani kwetu ni muhimu sana kusoma Neno la Mungu tena na tena.

1 Timotheo 4:13
“Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika KUSOMA na kuonya na kufundisha.”
‭‭
III). Kulitafakari Neno la Mungu
Kutafakari ni kufikiria kwa kina juu ya jambo fulani. Unafikiria kwa kina zaidi juu ya mambo uliyojifunza na mambo unayoyapitia ili kupata ufumbuzi kupitia Neno ambalo umejifunza. Kila anayelitafakari Neno kwa namna hiyo anapokea baraka kupitia hilo Neno.

Mithali 16:20
“ATAKAYELITAFAKARI NENO atapata mema; Na kila amwaminiye BWANA ana heri.”

IV). Kulitii Neno la Mungu
Tunatakiwa kulitii Neno la Mungu baada ya kulisikia, kulisoma na kulitafakari. Hili Neno liendelee kukaa ndani yetu tunatakiwa kulifanyia kazi.

‭Zaburi 119:9
‭“Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa KUTII, akilifuata NENO LAKO.”

‭Bishop Emmanuel Mbagwile (+255 715 136868)

12/04/2018

NENO LA KRISTO LIKAE KWA WINGI - I
Neno la Msingi:
Wakolosai 3:16
“NENO LA KRISTO NA LIKAE KWA WINGI NDANI YENU katika HEKIMA YOTE, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.”
‭‭
Nyakati tulizonazo ni nyakati za hatari ambazo watu wengi hawatapenda kukaa katika Neno la Mungu la kweli bali katika madanganyo matupu. Na wengine watajipatia waalimu makundi makundi wa kutaka kufundishwa yale mambo wanayoyataka wao. Jambo linalofundishwa likiwa tofauti na matakwa yao hulipiga kijembe NENO hilo.

1. MAANA YA NENO
Biblia imeletwa kwetu katika Lugha kuu mbili ambazo ni Kiebrania(Hebrews) na Kiyunani(Greek). Pia kuna baadhi ya maneno ya Kiaramu (Aramaic). Neno la kiyunani "lógos" (log'-os) lina maana ya neno lolote lililosemwa, kutamkwa au kuandikwa. Neno la kiyunani "rhema" hili ni neno maalum kwa mtu maalum kwa kusudi maalum na kwa wakati maalum.

Yohana 15:7
“Ninyi mkikaa ndani yangu, na MANENO YANGU YAKIKAA NDANI YENU, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”
‭‭
Neno linaloleta matokeo ni "rhema" lakini lazima usikie "logos" ili upate rhema. Petro alipoambiwa na Yesu "NJOO" lilikuwa ni Neno maalum kwa ajili ya yake kwa wakati ule na ndiyo maana aliweza kutembea juu ya maji. Wewe ukilichukua Neno hilo na ukaenda Ferry au Kigamboni na ukataka kutembea juu ya maji kwa kuwa Petro alitembea "tutakuzika".

Mathayo 14:28-29
“Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Akasema, NJOO. Petro akashuka chomboni, AKAENDA KWA MIGUU JUU YA MAJI, ili kumwendea Yesu.”
‭‭
2. SIFA ZA NENO LA MUNGU
Kuna sifa nyingi ambazo Neno la Mungu limezibeba ila hapa tutaangalia chache katika hizo

I). LINA UWEZO WA KUUMBA
Neno la Mungu lina uwezo wa kufanya uumbaji. Ulimwengu huu tunaouona uliumbwa kupitia Neno la Mungu. Tumbo la Sara lilikuwa limekwisha kufa lakini kupitia Neno la Mungu ulifanyika uumbaji hata Sara akaweza kuzaa akiwa na umri wa miaka 90. Kila kilicho kufa katika maisha yako Neno la Mungu laweza kufanya uumbaji.

Waebrania 11:3
“Kwa imani twafahamu ya kuwa ULIMWENGU ULIUMBWA kwa NENO LA MUNGU, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.”

II). LIMEHAKIKISHWA
Kuhakikishwa maana yake ni uhakika. Hakikishwa linatokana na neno "hakika" Neno la Mungu limethibitishwa kwa vipimo vyote vya kimbingu. K**a halijatimia katika maisha yako mwenye tatizo siyo Mungu ila wewe mpokeaji.

Mithali 30:5
“Kila NENO LA MUNGU LIMEHAKIKISHWA; Yeye ni ngao yao wamwaminio.”

III). LASIMAMA MILELE
Mambo yote yatapita Bali neno la Mungu lenyewe litadumu milele. Kile alichokisema Mungu lazima kitatimia tu. Vizazi vitapita bali Neno litasimama.

Isaya 40:8
“Majani yakauka, ua lanyauka; Bali NENO LA MUNGU wetu LITASIMAMA MILELE.”

Zaburi 119:89
Ee BWANA, NENO LAKO LASIMAMA IMARA mbinguni hata milele.”

IV). LINA NGUVU, LINA UKALI NA LINACHOMA
Neno la Mungu lina nguvu ya kufanya chochote katika maisha yetu. Lina nguvu ya kumbadilisha mtu aliyeshindikana. Lina ukali na linachoma. Tuwe Tayari kusikia Neno ambalo litazungumza juu ya maisha yetu. Tukubali lituchome ndani ya mioyo yetu ili tubadilike.

Waebrania 4:12
“Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.”

‭‭V). NI UZIMA
Neno la Mungu ni uzima. Neno hili lina sifa ya uzima ndani yake. Kuna uzima wa milele na uzima katika afya ya kimwili ndani ya neno la Mungu.

Wafilipi 2:16
“mkishika NENO LA UZIMA; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure.”

VI). NI ROHO
Neno la Mungu ni roho. Maneno mengine hayana "ROHO" ndani yake tofauti na Neno la Mungu. Kila alichozungumza Kristo kina Roho wake ndani yake.

Yohana 6:63
“Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni ROHO, tena ni UZIMA.”

3. MADHARA YA KUTOKUPATA NENO LA MUNGU MAISHANI
K**a tunavyoona kuna madhara mtu anayoyapata kwa kutokula chakula cha kimwili vivyo hivyo kwa yule ambaye ni mtoto wa Mungu hupata madhara kwa kwa kutokupata chakula cha kiroho ambacho ni Neno la Mungu. Kuishi na kukua kwetu kiroho kunategemeana sana na aina ya chakula cha kiroho tunachokipata kila siku.

Mathayo 4:4
“Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu HATAISHI KWA MKATENDA TU, ila kwa kila NENO litokalo katika kinywa cha Mungu.”

Kiroho chetu kinahitajika kupata chakula kila siku ili tuweze kukua kiroho. Ili tusife kiroho Neno la Mungu ni muhimu sana kwako.

Tutaendelea..............

‭Bishop Emmanuel Mbagwile (+255 715 136868)

05/04/2018

JE! KUANGALIA PICHA ZA NGONO NI DHAMBI?
Neno la Msingi:
Zaburi 101:3
“SITAWEKA mbele ya MACHO yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.”

Watu wengi wameanguka katika mtego huu wa Ibilisi na kujikuta wakifanya mambo ya "AIBU" wanapokuwa sehemu zao za Siri iwe ni chumbani au bafuni. Wanaume wamejikuta wakipiga punyeto (Ma********on) na Wanawake wakijisaga ( wanatumia mikono yao na viungo vyao vingine k**a njia ya kujikidhi hali zao za tamaa mbaya waliloziamsha wao wenyewe).

Haipaswi kamwe kuwa hivyo. Biblia inasema tusiyachochee wala kuyaamsha "mapenzi" mpaka yatakavyoona yenyewe (Wimbo ulio bora 2:7, 3:5). Naomba tufuatane pamoja kwenye somo hili muhimu sana ambalo litakuweka huru mbali na "utumwa wa fikra za kingono"

1. MAANA YA PICHA ZA NGONO
Neno PICHA ni kivuli cha mtu, watu, kitu n.k. PICHA si kitu halisi bali ni kivuli chake. Unaweza ukapewa PICHA ya mtu lakini usifahamu urefu wake au ni mfupi kiasi gani lakini sura yake ukawa umeiweka katika kumbukumbu yako.
NGONO ni kitendo cha mtu, watu kufanya kitendo cha kujamiana (Tendo la Ndoa) na pia ni ile hali ya kuwa uchi wa mnyama. Kuangalia picha za ngono ni kitendo cha kuangalia watu wakifanya Matendo ya kujamiana iwe kwa njia ya asili, kinyume na maumbile au kufanya na wanayama. Kitendo hicho huleta kuchochea tamaa ya miili kiasi ambacho watu wengine hufanya mambo ya "AIBU" katika nyumba zao (Warumi 1:24-28).

PICHA za NGONO zimeenea kila mahali kwa sasa, kwenye simu yako unaweza ukakutana na "uchafu" wa namna hiyo. Wahindi wao picha za ngono huziita "kachumbali" na unaweza ukamkuta Mhindi amekaa na familia yake anaangalia "kachumbali" wanadai inanogesha utamu wanapofika kitandani. Huko ni kujidanganya Mungu hakumletea Adamu PICHA ya NGONO bali alimletea mke ambaye watashirikiana naye kwenye Tendo Takatifu (Mwanzo 2:18, 21-25).

Wakati mmoja Mfalme Daudi wakati watu wake wa vita wamekwenda vitani yeye akawa yuko ghorofani anaangalia "PICHA LIVE" ya NGONO mwanamke alikuwa akioga matokeo yake yakawa ni kufanya kitendo chenyewe na kuamua kumuua mume wa Bathsheba.

2Samweli 11:2-27
“Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?”...........

Kile kitendo cha Daudi "kuona" lilikuwa kosa kubwa la kiufundi katika akili yake likamchanganya. Ndivyo ilivyo kwa PICHA ZA NGONO lazima ukiangalia upate "UKICHAA" wa muda ukajikuta umeng'ang'ania sabuni au ndizi ukiwa unapiga punyeto. Ni aibu sana sana mtu mwenye heshima zako k**a wewe labda wewe ni meneja, mkurugenzi, mtu mwenye Elimu yako ya maana unakutwa unaangaika sabuni, godoro au toy la jinsia ya kiume.

2. JE! KUANGALIA PICHA ZA NGONO NI DHAMBI?
Kuangalia picha za ngono "NI DHAMBI" kwa herufi kubwa. Katika Sheria ya Musa ilikuwa mtu anahesabika kuwa ametenda dhambi pale ambapo atakutwa akifanya kitendo hicho au kukiwa na mashahidi wawili au watatu atatakiwa kuhukumiwa sawasawa na Sheria husika. Kwenye dhambi ya uzinzi mtu alitakiwa apigwe mawe hadi afe sivyo kwa Sheria ya Kristo yenyewe inazungumzia juu ya kitendo cha "kutamani" tu unahesabika kuwa umefanyika DHAMBI (Mathayo 6:27-29, Waebrania 10:28). Tamaa mbaya ni dhambi k**a dhambi nyinginezo.

Kwa kawaida tamaa huja na ile tamaa huchukua mimba na baadaye huzaa dhambi (Yakobo 1:13-16). Kitendo cha kuangalia picha za ngono hupofusha "FIKRA" nzuri za mtu alizonazo. Mawazo machafu uanza kutawala katika ubongo wako hadi "USHUSHE" huo mzigo ulioko kwenye viungo vyako vya uzazi. Ahaaa ni hatari aiseeee. Wewe unayengalia picha za ngono K**a ndiyo starehe yako unaiharibi nafsi yako "unakuwa zezeta wa akili"

Biblia inasema "taa ya Mwili jicho na jicho lako likiwa safi mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa bovu mwili wako wote utakuwa na giza.."(Mathayo 6:22-23). Kwa wale wanandoa ni "MWIKO" kutumia picha za ngono ili kunogesha kufanya Tendo la Ndoa. Wewe mume unaye hapo "chombo" unakiona "live" na kimethibitishwa na Mungu mwenyewe sasa hiyo mipicha ya nini? Kila kiungo Mungu alikiweka kwa ajili ya kusudi maalum k**a ni mdomo kwa ajili ya kuongea na kupitisha chakula na si kunyonya sehemu za Siri za mwenzi wako. Mungu ameweka sehemu ya "haja kubwa" kwa ajili ya kutolea uchafu uliotengenezwa na tumbo na si kiungo kingine kiende kukoroga "zege" hilo huo ni uchafu(Ufunuo 22:10-15).

Warumi 1:26:27
“Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.”
‭‭
3. JINSI YA KUSHINDA DHAMBI YA KUANGALIA PICHA ZA NGONO
PICHA ZA NGONO zinavutia sana kuziangalia ila zina maangamizo makubwa sana katika maisha yako. Lazima ufikie mahali kukata shauri ndani ya Moyo wako kuambatana na Mungu. Kusudi kubwa la shetani kuachilia mambo yake ya NGONO kwenye mitandao ili apate wafuasi wengi zaidi. Hakuna kitu unachoweza kukifanya katika simu za Android wengine wasikitambue. Kila unalolipitia na kuliangalia kwa Siri siku ya siku litaletwa hukumuni na Mungu mwenyewe (Warumi 2:16, Mhubiri 12:14)

USHAURI WAKIVITENDO:
I) Yatie Nuru macho yako - Zaburi 13:3, 19:8 -
Yaruhusu macho yako yaingiziwe nuru na Yesu. Chukua muda wa kutosha kuingiza PICHA zinazomhusu Mungu zaidi. Angalia wahubiri mbalimbali.

II) Tazama mambo ya Adili(mema) - Zaburi 17:2-3 -
Kuna nguvu kubwa sana tunapokuwa tunaangalia mambo mema. Vipindi vizuri vya neno la Mungu. PICHA zinazojenga siyo zinazoharibu fikra zetu.

III) Kumuomba Mungu afumbue macho yako - Zaburi 119:18, 146:8- Maombi ni muhimu ili kufanya macho yako kuona kusudi la Mungu na Kutambua uwepo wa shetani katika PICHA ZA NGONO.

IV) Weka maneno ya Mungu Mbele za macho yako - Mithali 4:20-21
Wakati wote soma neno la Mungu kupitia kifaa chochote cha ki-electronic ili uweze kumjua Mungu zaidi.

V) Macho yako yatazame Mbele - Mithali 4:25-27
Kutazama Mbele maana yake uwe na maono. Maono ni PICHA au TASWIRA ya Mbele ya maisha yako. Yeremia aliulizwa unaona nini naye akasema "anaona ufito wa mlozi" anaona kitu kizuri (Yeremia 1:11-12).

VI) Pendezwa na njia za Mungu - Mithali 23:26
Kuanzia sasa anza kupendezwa na njia za Mungu katika maisha yako. Acha kuzifuata njia zako katika kuufurahisha mwili wako wa PICHA zisizofaa.

VII) Tafuta watumishi wa Mungu ili wakufundishe - Isaya 48:17, 30:20-21
Kuna mambo ambayo yanatupa shida katika maisha yetu ni vizuri kuwaona waalimu ili watusaidie jinsi ya kutoka katika mtego huo.

VIII) Omba rehema na neema ya Yesu - Waebrania 4:16
Tunahitaji neema ya Mungu ili kushinda Hali hiyo ya kupenda KUANGALIA PICHA ZA NGONO na pia kufunguliwa kutoka katika vifungo hivyo vya pepo wa tamaa na mahaba.

Mungu atakubariki ukipeleka ujumbe huu kwa wengine

Bishop Emmanuel Mbagwile (+255 715 136868)

Address

Ubungo Extenal
Dar Es Salaam
32575

Telephone

+255765411119

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Goshen Ministries International posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Goshen Ministries International:

Share