01/07/2020
UKIMYA WA MUNGU
Ukimya ni hali ya kutokuongea,kusema au kupiga kelele.
Ni ile hali ya kutokupata mafunuo,ndoto,au kusikia sauti yoyote kutoka kwa Mungu.
Kipindi hiki cha ukimya ,huwa kina wafadhaisha wengi haswa waombaji na watu wanaopitia kwenye magum,hudhani k**a Mungu hasikii ,au hajibu na kuona kuwa Mungu amewaacha kabisa.
Tukikumbuka umbali Wa Agano LA kale mpaka agano jipya (malaki hadi mathayo).
Ni miaka *400* ambayo Mungu alikaa kimya..
Katika kipindi hiki hakukuwa na unabii wala mtume yeyote..ni kipindi cha ukimya.
Ila tunajifunza kitu katika ukimya huo..kuwa alikuwa akifanya maandalizi juu ya ujio Wa Yesu ulimwenguni.Hapa aliandaa watu,mahali na njia ya Yesu kupita ili iwe rahisi kueneza injili kwa watu wote.
Yamkini unaweza kuona kimya kwenye mambo yako,kazi,ndoa ,biashara ,na mipango yako,usifadhaike mpendwa Mungu anaandaa surprise kwa ajili yako.
Mambo ya msingi kuelewa pale unapohisi Mungu amekaa kimya kwako.
▪️ *Amini uwepo Wa Mungu* (Trust God's Presence in your life)
Ukimya Wa Mungu hauna maana eti kuwa Yeye hayupo, kukaa kimya hakuna maana ya mhusika hayupo...
Mathayo1:23, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Kuja kwa Yesu duniani,kulibeba maana hiyo kubwa sana,yakuwa Mungu yupo pamoja nasi, *hatuachi ,wala hatatuacha* mda wote yupo Pamoja nasi.
"So don't be depressed but feel the presence of God in any situation that you're, because Our Lord Jesus will not forsake us even in a single breath."
Trust him with all your heart.
▪️ *Mungu anaandaa mpango mzuri kwa ajili ya maisha yako*
Wakati Wa huzuni ,ni wakati ambao unahisi upo peke yako,ila nataka nikwambie kuwa ndo wakati Mungu anaandaa kicheko kwa ajili yako..
Mungu siku zote ,Yeye ni bora ,hatua (process) zake zinaweza kuwa ngumu au zenye maumivu ,lakimi hatima yake ikawa nzuri zaidi.
Yer 29:11, Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.*
Pengine Israel walipokuwa utumwani Babeli walilia ,wakizani wapo pekee yao,na kujua kuwa habari yao ndio mwisho utumwani.
Maana waliona k**a Mungu amewanyamazia...hata k**a kulikuwa na manabii Wa uongo wakitoa nabii zisizotimia.
Lakini Mungu kupitia nabii wake,anaawaambia yakuwa siku zenu za mwisho zitakuwa njema..maana yake, *Mungu alikuwa akiiandaa hatima ya kila mmoja wao*
Mungu anaandaa hatima yako.
"Trust God's process ,He is preparing your destiny for good."
▪️ *Kaa tayari kupokea*
"Get ready to receive"
Usitoke katika uwepo Wa Mungu kwa sababu ya kelele za watu,eti Mungu wako amenyamaza.
Kaa tayari kupokea uliyoyaomba.
"God is going to break that silent soon and with a big surprise to you"
Huu ndo mda Wa kumsikiliza Mungu kwa makini sana na ndo mda Wa kuendelea kuomba sana..
*Soma neno lake ,jifunze,tafakari neno lake*
*Yer 33:3 Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.*
Endeleea kuita,endelea kuomba atakujibu kwa majira yake.
Mungu akubariki. Uwe na mwanzo mwema Wa mwezi Julai 2020.
Imeandaliwa na Mtumishi Ditrick Milinga
Kutoka Sikari-Kitunda,DSM.