12/04/2019
BWANA YESU ASIFIWE NAPENDA TUELEWE MAANA AU TAFSIRI YA MANENO YA BIBLIA TUKIANZA NA NENO• Nzige.
Jamii mbalimbali za panzi wanaohama katika makundi makubwa. Katika Sheria ya Musa, walionwa kuwa safi na wangeweza kuliwa. Makundi makubwa ya nzige yanayotafuna kila kitu kokote yanakopita na kusababisha uharibifu mkubwa, yalionwa kuwa pigo.—K*t 10:14; Mt 3:4.
O
• Omeri.
Kipimo cha vitu vikavu kilichokuwa sawa na lita 2.2, au sehemu moja ya kumi ya efa. (K*t 16:16, 18)—Angalia Nyongeza B14.
P
• Pakanga.
Vijiti vya mimea mbalimbali vyenye ladha chungu sana na harufu kali inayovutia. Pakanga hutumiwa kwa njia ya mfano katika Biblia kufafanua matokeo machungu ya uasherati, utumwa, ukosefu wa haki, na uasi imani. Katika Ufunuo 8:11, “pakanga” humaanisha kitu kichungu chenye sumu, kinachoitwa pia absinthe.—Kum 29:18; Met 5:4; Yer 9:15; Am 5:7.
• Paradiso.
Bustani maridadi, au shamba lililo k**a bustani. Paradiso ya kwanza ilikuwa Edeni, ambayo Yehova aliwatayarishia wanadamu wawili wa kwanza. Yesu alipokuwa akizungumza na mmoja wa wahalifu waliotundikwa kando yake kwenye mti wa mateso, alidokeza kwamba dunia itakuwa paradiso. Katika andiko la 2 Wakorintho 12:4, ni wazi kwamba neno hilo linarejelea paradiso ya wakati ujao, na katika Ufunuo 2:7, linarejelea paradiso ya kimbingu.—Wim 4:13; Lu 23:43.
• Pasaka.
Sherehe ya kila mwaka iliyofanywa siku ya 14 ya mwezi wa Abibu (baadaye mwezi huo uliitwa Nisani) ili kuadhimisha ukombozi wa Waisraeli kutoka Misri. Iliadhimishwa kwa kumchinja na kumchoma mwanakondoo (au mbuzi), na kumla kwa mboga chungu na mikate isiyo na chachu.—K*t 12:27; Yoh 6:4; 1Ko 5:7.
• Patakatifu Zaidi.
Chumba cha ndani zaidi katika hema la ibada na hekaluni, ambamo sanduku la agano liliwekwa; panaitwa pia Patakatifu pa Patakatifu. Mbali na Musa, ni kuhani mkuu peke yake aliyeruhusiwa kuingia Patakatifu Zaidi, naye angeweza kuingia humo siku moja tu katika Siku ya kila mwaka ya Kufunika Dhambi.—K*t 26:33; Law 16:2, 17; 1Fa 6:16; Ebr 9:3.
• Patakatifu.
Chumba cha kwanza kikubwa zaidi katika hema la ibada au katika hekalu, nacho ni tofauti na chumba cha ndani zaidi, yaani, Patakatifu Zaidi. Katika hema la ibada, Patakatifu palikuwa na kinara cha taa cha dhahabu, madhabahu ya uvumba ya dhahabu, meza ya mikate ya wonyesho, na vyombo vitakatifu; katika hekalu, mahali hapo palikuwa na madhabahu ya dhahabu, vinara kumi vya taa vya dhahabu, na meza kumi za mikate ya wonyesho. (K*t 26:33; Ebr 9:2)—Angalia Nyongeza B5 na B8.
• Pazia.
Kitambaa kilichofumwa kwa njia maridadi na kutariziwa kwa michoro ya makerubi ambacho kilitenganisha Patakatifu na Patakatifu Zaidi katika hema la ibada na pia hekaluni. (K*t 26:31; 2Nya 3:14; Mt 27:51; Ebr 9:3)—Angalia Nyongeza B5.
• Pembe za madhabahu.
Sehemu zilizochomoza k**a pembe kwenye kona nne za madhabahu fulani. (Law 8:15; 1Fa 2:28)—Angalia Nyongeza B5 na B8.
• Pembe.
Neno hili linarejelea pembe za wanyama, ambazo zilitumiwa k**a vyombo vya kunywea, vyombo vya mafuta, vyombo vya wino na vipodozi, na ala za muziki au za kutoa ishara fulani. (1Sa 16:1, 13; 1Fa 1:39; Eze 9:2) “Pembe” hutumiwa mara nyingi kwa njia ya mfano kumaanisha nguvu na ushindi.—Kum 33:17; Mik 4:13; Zek 1:19.
• Pentekoste.
Sherehe ya pili kati ya sherehe tatu kuu ambazo wanaume wote Wayahudi walipaswa kusherehekea kule Yerusalemu. Neno Pentekoste, linalomaanisha “(Siku) ya Hamsini,” ndilo neno linalotumiwa katika Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo kurejelea Sherehe ya Mavuno au Sherehe ya Majuma inayotajwa katika Maandiko ya Kiebrania. Sherehe hiyo ilifanywa siku ya 50 kuanzia Nisani 16.—K*t 23:16; 34:22; Mdo 2:1.
• Pete ya muhuri.
Aina ya muhuri uliovaliwa kwenye kidole au kutiwa kwenye kamba, na huenda ulivaliwa shingoni. Pete hiyo ilikuwa ishara ya mamlaka ya mtawala au ofisa. (Mwa 41:42)—Tazama MUHURI.
• Pigo.
Katika Maandiko ya Kiebrania, kwa kawaida neno hili linamaanisha tauni, ugonjwa, au adhabu ya msiba kutoka kwa Yehova. Katika Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo linamaanisha kupiga kwa kiboko au mjeledi wenye vifundo au ncha kali.—Hes 16:49;Yoh 19:1.
• Pima.
Kipimo cha urefu kinachotumiwa kupima kina cha maji, ni sawa na mita 1.8 (futi 6). (Mdo 27:28)—Angalia Nyongeza B14.
• Pimu.
Kipimo cha uzito na pia bei ambayo Wafilisti walitoza ili kunoa vifaa mbalimbali vya chuma. Mawe kadhaa ya kupimia uzito yaliyopatikana katika machimbo ya vitu vya kale katika nchi ya Israel yana konsonanti za kale za Kiebrania za neno “pimu”; kwa wastani yana uzito wa gramu 7.8, ambao ni karibu theluthi mbili za shekeli.—1Sa 13:20, 21.
• Porneia.—
Tazama UASHERATI.
• Purimu.
Sherehe ya kila mwaka iliyofanywa siku ya 14 na ya 15 katika mwezi wa Adari. Inaadhimishwa ili kukumbuka jinsi Wayahudi walivyokombolewa ili wasiangamizwe katika siku za Malkia Esta. Neno pu·rimʹ ambalo si la Kiebrania linamaanisha “kura.” Sherehe ya Purimu, au Sherehe ya Kura, iliitwa hivyo kwa sababu ya tendo la Hamani la kupiga Puri (Kura) ili kuamua siku ambayo angetekeleza njama yake ya kuwaangamiza Wayahudi.—Est 3:7; 9:26.
R
• Rahabu.
Jina linalotumiwa kwa njia ya mfano katika kitabu cha Ayubu, Zaburi, na Isaya (si mwanamke Rahabu anayetajwa katika kitabu cha Yoshua). Katika kitabu cha Ayubu, muktadha unafunua kwamba huyu Rahabu ni mnyama mkubwa sana wa baharini; katika maandiko mengine mnyama huyu mkubwa sana wa baharini anatumiwa kufananisha Misri.—Ayu 9:13; Zb 87:4; Isa 30:7; 51:9, 10.
• Rehani.
Kitu kinachomilikiwa na mkopaji ambacho anampa mkopeshaji ili kumhakikishia kwamba atalipa mkopo. Kitu hicho kiliitwa pia dhamana ya mkopo. Sheria ya Musa ilikuwa na maagizo yaliyohusu rehani ambayo yaliwalinda maskini na raia wa taifa hilo ambao hawakuwa na mtetezi.—K*t 22:26; Eze 18:7.
• Roho takatifu.
Kani ya utendaji isiyoonekana inayotumiwa na Mungu kutimiza mapenzi yake. Ni takatifu kwa sababu inatoka kwa Yehova, ambaye ni safi na mwadilifu kwa kiwango cha juu zaidi, na kwa sababu ndiyo njia anayotumia Mungu kutimiza mambo matakatifu.—Lu 1:35; Mdo 1:8.
• Roho waovu.
Viumbe waovu wa roho wasioonekana wenye nguvu zinazozidi za wanadamu. Kwa kuwa wanaitwa “wana wa Mungu wa kweli” katika Mwanzo 6:2 na “malaika” katika Yuda 6, hawakuumbwa wakiwa waovu; badala yake, walikuwa malaika waliojifanya wenyewe kuwa maadui wa Mungu kwa kutomtii katika siku za Noa na kujiunga na Shetani katika kumwasi Yehova.—Kum 32:17; Lu 8:30; Mdo 16:16; Yak 2:19.
• Roho.
Neno la Kiebrania ruʹach na neno la Kigiriki pneuʹma, ambayo kwa kawaida hutafsiriwa kuwa “roho” yana maana kadhaa. Yote mawili yanarejelea kitu ambacho macho ya wanadamu hayawezi kuona na huthibitisha kuwapo kwa nguvu inayotenda. Maneno hayo ya Kiebrania na Kigiriki hutumiwa kurejelea (1) upepo, (2) nguvu ya uhai inayotenda ndani ya viumbe walio duniani, (3) nguvu za msukumo zinazotoka katika moyo wa mfano na kumfanya mtu aseme na kutenda mambo kwa njia fulani, (4) maneno yaliyoongozwa na roho yanayotoka katika chanzo kisichoonekana, (5) Mungu na viumbe wa roho, na (6) nguvu za utendaji za Mungu, au roho takatifu.—K*t 35:21; Zb 104:29; Mt 12:43; Lu 11:13.
S
• Sabato.
Neno hili linatokana na neno la Kiebrania linalomaanisha “kupumzika; kukoma.” Ni siku ya saba katika juma la Kiyahudi (ilianza Ijumaa baada ya jua kutua mpaka Jumamosi baada ya jua kutua). Siku nyingine za sherehe katika mwaka ziliitwa pia siku za