KMT Tambani Msongora

KMT Tambani Msongora MATHAYO 28:19

IBADA YA CHRISTMAS SIKU YALEO TAREHE  25/12/2025
25/12/2025

IBADA YA CHRISTMAS SIKU YALEO TAREHE 25/12/2025

23/11/2025

WAKATI WA KUABUDU KWENYE IBADA YA LEO TAREHE 23/11/2025

IBADA YA LEO TAREHE 23/11/2025 HAKIKA MUNGU NI MWEMA.
23/11/2025

IBADA YA LEO TAREHE 23/11/2025 HAKIKA MUNGU NI MWEMA.

LEO KWENYE IBADA YA LEO KULIKUWA NA SHUKRANI YA WAZALIWA WA MWEZI WA KUMINA MOJA MUNGU AWATUNZE MMALIZE MWAKA SALAMA.
23/11/2025

LEO KWENYE IBADA YA LEO KULIKUWA NA SHUKRANI YA WAZALIWA WA MWEZI WA KUMINA MOJA MUNGU AWATUNZE MMALIZE MWAKA SALAMA.

FAIDA ZA KIFO CHA YESU MSALABANIMsalaba ni nini?Msalaba ni adhabu ya kifo ya kutundikwa juu ya mti mpaka kufa na kila al...
12/04/2024

FAIDA ZA KIFO CHA YESU MSALABANI

Msalaba ni nini?

Msalaba ni adhabu ya kifo ya kutundikwa juu ya mti mpaka kufa na kila aliyeangikwa juu ya mti alilaniwa.
Kumbu 21:22-23 “ikiwa mtu ametenda dhambi impasayo kufa,akauawa,akauawa,nawe ukamtundika juu ya mti;mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti lazima utamzika siku iyo hiyo;kwani aliyetundikwa amelaniwa na Mungu asije akatia unajisi katika nchi yako akupayo BWANA Mungu wako,iwe urithi wako.

Agano Jipya
Msalaba ni nguvu ya MUNGU IOKOAYO.

1wakoritho 1:18 “Kwa sababu neno msalaba kwao wanaopotea ni Upuzi,bali kwetu sisi tunaokolewa ni nguvu ya Mungu.

Kwa hiyo thamani ya wokovu wetu imetokana na msalaba nje ya msalaba kusekuwa na wakovu


ZABURI 14:2,3,7 “Toka Mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu ,Aone k**a yuko mtu mwenye akili,Amtafutaye Mungu Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja,Hakuna atendaye mema,La! Hata mmoja.Laiti wokovu wa Israeli utoke katika sayuni!BWANA atawarudisha wafungwa wa watu wake;Yakobo atashangilia, atafurahi.

Mathayo 27:45,46,50,51-53. “Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa.Na k**a saa tisa,Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akasema,Eloi,Eloi,lama sabakthani?Yaani Mungu wangu ,mbona unaniacha?Naye Yesu akisha kupaza sauti tena kwa nguvu,akaitoa roho yake.Na tazama ,pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini,nchi ikatetemeka,miamba ikapasuka,makaburi yakafunuka;ikainuka miili mingi Ya watakatifu waliolala,nao wakiisha kutoka makaburini mwao,baada ya kufufuka kwake,wakaingia mji mtakatifu,wakawatokea wengi.

TUANGALIE FAIDA ZA KIFO CHA YESU MSALABANI

1:Msalaba ulilipa adhabu ya dhambi ya Mauti na Kutupatanisha na Mungu.
Mwanzo 3:9,24 ” Bwana Mungu akamwita Adamu,akamwambia uko wapi?Basi akamfukuza huyo mtu,akaweka makerubi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni na upanga wa moto uliogeuka hukona huko kulinda njia ya mti wa uzima.

Kumbuka kila mmoja alipwasa kulipwa mauti k**a mshahara wa dhambi zetu.
Warumi 6:23 “kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti;bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Warumi 5:10 “kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake;zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.

Warumi 5:17 “Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja,zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema,na kile kipawa cha haki,watatawala katika uzima kwa yule mmoja,Yesu Kristo.

Zaburi 130:3-4 “BWANA k**a ungehesabu maovu,Ee Bwana,nani angesimama?Lakini kwako kuna msamaha ili wewe uogopwe.
Je bado kwenye maisha yako ni mauti ipi inayokusumbua wakati Yesu amerejesha uzima.

Somo litaendelea................................

Mwl. Samwel Wambura
Prayer &Deliverance Ministry Page
KMT- Tambani Msongora.
March,29,2024.



KARIBU TUENDELEE NA SOMO JE UNALIISHI  KUSUDI LA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO.Efeso 1:11 "Na ndani yake sisi nasi tulifanywa...
02/04/2024

KARIBU TUENDELEE NA SOMO JE UNALIISHI KUSUDI LA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO.
Efeso 1:11 "Na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake".

Mimi na wewe tulichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi Lake ili tuje tulitumikie kusudi Lake sio letu au la wazazi wetu au la mtu awaye yeyote.

Mungu anafanya kila kitu kwa shauri(Kusudi) au kwa kushauriana na mapenzi Yake.
Yapo mapenzi maalum na mahususi ya Mungu katika maisha ya kila mmoja wetu.
Utendaji wa Mungu maishani mwetu hutegemea sana mapenzi Yake hayo

Marko 3:35 “Kwa maana mtu ye yote atakayefanya mapenzi ya Mungu.huyo ndiye ndugu yangu,na umbu langu,na mama yangu.

1Yohana 2:17 “Na dunia inapita na tamaa zake,bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.

Yohana 9:31
Mungu huwasikia wanaotenda mapenzi yake.
Ufunuo 4:11
kila kilichopo dunia ni kiliumbwa kwa Mapezi ya Mungu.

Matendo 13: 36. “Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu”

Lipo (kusudi) shauri la Mungu ambalo Daudi aliishi kulitumikia na alipomaliza bibilia inasema akalala pamoja na babaze.
Mafanikio ya kila mmoja wetu machoni pa Mungu yanapimwa ni kwa kiasi gani tuliliishi kusudi la Mungu kwa ajili yetu.

Somo litaendelea..........................

Mwl.Samwel Wambura
Prayer & Deliverance Ministry Page.
KMT-MVULENI TAMBANI MSONGORA.
April 2,2024.

HAPPY BIRTH DAY TO ME,Ninaposherekea siku yangu ya kuzaliwa naomba pia ujifunze kitu KARIBU.SIKU MBILI ZA MUHIMU KABISA ...
01/04/2024

HAPPY BIRTH DAY TO ME,
Ninaposherekea siku yangu ya kuzaliwa naomba pia ujifunze kitu KARIBU.
SIKU MBILI ZA MUHIMU KABISA KATIKA MAISHA YAKO NI SIKU AMBAYO UMEZALIWA NA SIKU AMBAYO UNAGUNDUA KWANINI ULIZALIWA NA UTAKAPO ANZA KURISHI KUSUDI LAKO LA KUJA DUNIANI."
Matendo 13: 36. “Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu”
MUNGU AKUBARIKI

KARIBU SANA TUMUABUDU MUNGU NA TUOMBE ILI YESU ANAPOFUFUKA TUANZE MAISHA MAPYA NA YA MILELE.
29/03/2024

KARIBU SANA TUMUABUDU MUNGU NA TUOMBE ILI YESU ANAPOFUFUKA TUANZE MAISHA MAPYA NA YA MILELE.

KARIBU KWENYE IBADA YA LEO YA WAGENI KMT TAMBANI TAREHE 3/3/2024.
03/03/2024

KARIBU KWENYE IBADA YA LEO YA WAGENI KMT TAMBANI TAREHE 3/3/2024.

03/03/2024

TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA WAGENI WATATU KWENYE IBADA YA WAGENI KMT TAMBANI TAREHE 3/3/2024 NA KATI YAO WAWILI WAMEKUBARI KUJIUNGA NA KANISA LETU TUMETIMIZA UTE MKUU MATHAYO 28:19.

02/03/2024

Address

Tambani, Msongora, Dar Es Salaam CC
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when KMT Tambani Msongora posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share