Holy Spirit Connect

Holy Spirit Connect Kujifunza Neno
Kukua Kiroho
Uhusiano na Roho Mtakatifu
Maombi

JIFUNZE KUMWELEZA MUNGU SHIDA ZAKOSisi wanadamu ni wazuri kueleza shida zetu au matatizo yetu kwa wanadamu. Lakini sio w...
03/08/2026

JIFUNZE KUMWELEZA MUNGU SHIDA ZAKO

Sisi wanadamu ni wazuri kueleza shida zetu au matatizo yetu kwa wanadamu. Lakini sio wazuri kueleza shida zetu au matatizo yetu kwa Mungu.

Tunachotakiwa kufanya k**a wakristo ni kujifunza kueleza mambo yetu kwa Mungu, na sio kwa wanadamu.

Kuna faida nyingi sana za kupeleka shida zako kwa Mungu kuliko kupeleka kwa wanadamu.

Ukipeleka shida zako au matatizo yako kwa wanadamu, kesho utazikuta shida zako mtaani au kwenye mitandao wakikucheka na kukukebehi. Lakini ukizipeleka kwa Mungu, Mungu atazipokea na kukupa majibu ya maombi yako.

Hana alipopitia changamoto ya uzao wa tumbo, alipeleka shida yake kwa Mungu na Mungu alimjibu na kumpa haja ya moyo wake.

Mpendwa, kwa Mungu kuna majibu ya maombi yetu. Tupeleke shida zetu kwa Mungu peke yake; Kwa maana kwake kuna majibu.

"Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa."
Mathayo 7:7

Ubarikiwe sana.

Innocent Morris
+255652796450 (WhatsApp)

MSTARI WANGU WA WIKI"Usiogope, wewe hutaaibika. Usiogope aibu, wewe hutaaibishwa."Isaya 54:4a NENLeo ni siku ya jumapili...
02/08/2026

MSTARI WANGU WA WIKI

"Usiogope, wewe hutaaibika. Usiogope aibu, wewe hutaaibishwa."
Isaya 54:4a NEN

Leo ni siku ya jumapili ambayo ipo maalum kwa ajili ya ile programu yetu ya kushika mstari moja katika wiki. Unachotakiwa kufanya leo ni kuandaa mstari wako alafu utauandika kwenye kikaratasi ambacho utatembea nacho kila sehemu ukiushika huo mstari na kuuweka kichwani na moyoni.

Pia utakuwa ukiukiri huo mstari wako kwa sauti utakapo amka asubuhi nausiku utakapo taka kulala, unaweza kuukiri pia wakati wowote utakao taka. Kukiri neno la Mungu kutaleta matokeo makubwa sana katika maisha yako.

Usiwasahau watoto wako wa andikie mstari wao na uwe unakiri nao kila jioni mnapo kuwa pamoja. Hii itajenga kitu kikubwa sana katika familia yako. Hata k**a hawawezi kusoma basi jitahidi kuwasomea. Pia k**a una mume/mke au mpenzi mnaweza kuwa na mstari mmoja na mkawa mnapata muda ambao mtakuwa mkiukiri huu mstari kwa pamoja na kuurudia rudia. Itajenga kitu cha msingi sana katika uhusiano wenu. Uhusiano wenu unajengwa na msingi wa neno la Mungu. Jenga moyo wako na familia yako katika msingi wa neno la Kristo. Moyo wako na familia yako itakuwa imara siku zote.

K**a utaupenda mstari ambao mimi nitautumia huo hapo juu unaweza kuutumia pia. Lakini k**a utakuwa na mstari wako umeandaa itakuwa ni jambo njema sana ukishare na sisi hapa ili k**a mtu akiupenda mstari wako aweze kuutumia katika wiki hii.

"Maana ni vizuri kuyahifadhi ndani yako, hali yakithibitika pamoja midomoni mwako."
Mithali 22:18

Mpendwa, ukimpenda Mungu utalishika neno lake na Mungu atakupenda. Na Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu watakuja kufanya makazi ndani yako.

"Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake."
Yohana 14:23

Hii programu ni kwa ajili ya kujaza neno la Mungu ndani ya mioyo yetu na katika akili zetu na kulitendea kazi neno lake.

Unaweza kushare na watu wengine programu hii.

Ubarikiwe sana

Innocent Morris
+255652796450 (Whatsapp)

Page yetu ya shuhuda

01/08/2026

MAOMBI YA MWEZI WA NANE - Innocent Morris

31/07/2026

USIKU WA MAOMBI 31/07/2026 by Innocent Morris

Instagram Page: holyspiritconnect
page: Holy Spirit Connect

Contact: +255652796450 (WhatsApp)

Instagram Link:
/holyspiritconnect

Facebook Link:
/holyspiritconnect

YouTube Link:
/holyspiritconnect
, , , , , , , Innocent

OMBA SIKUZOTE - Innocent Morris"Imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa."Luka 18:1Ubarikiwe sana.Innocent...
31/07/2026

OMBA SIKUZOTE - Innocent Morris

"Imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa."
Luka 18:1

Ubarikiwe sana.

Innocent Morris
+255652796450 (WhatsApp)


ROHO MTAKATIFU ATAKUWA PAMOJA NAWE KATIKA SHIDA KUKUSAIDIAYesu ameahidi anasema "Sitawaacha ninyi yatima."(Yohana 14:18)...
29/07/2026

ROHO MTAKATIFU ATAKUWA PAMOJA NAWE KATIKA SHIDA KUKUSAIDIA

Yesu ameahidi anasema "Sitawaacha ninyi yatima."
(Yohana 14:18), bali "Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele." (Yohana 14:16).

Roho Mtakatifu ni Msaidizi wetu, yupo pamoja na wewe katika kila hali. Kwenye raha yupo pamoja na wewe, kwenye shida yupo pamoja na wewe.

Mungu anasema "Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza."
Isaya 43:2

Hata ukiwa katika moto, Yeye atakuwa pamoja nawe hata kuacha. Hata k**a unajihisi uko peke yako, tambua kwamba Roho Mtakatifu yupo pamoja nawe.

Shadraka, Meshaki na Abednego walitupwa katika tanuru la moto, lakini Bwana hakuwaacha. Bwana alikuwa pamoja nao (Danieli 3:19). Haijalishi adui atakutupa katika tanuru gani la moto, Roho Mtakatifu hatakuacha; atakuwa pamoja nawe kwa maana Yeye ni Msaidizi wetu.

Roho Mtakatifu atakusaidia hadi ufike pale ambapo Mungu anataka ufike. Wakati wa shida atakupa furaha, atakupa amani na atakupa utulivu.

Tunahitaji tuwe karibu sana na Roho Mtakatifu ili aweze kutusaidia katika kila eneo la maisha yetu. Tunaposhindwa tumwambie Yeye, kwamba Roho Mtakatifu hapa siwezi kwa nguvu zangu, nisaidie, naye atakusaidia.

K**a kuna eneo unajiona ni dhaifu, mwambie Roho Mtakatifu, kwamba Roho Mtakatifu katika eneo hili, mimi ni dhaifu, naye atakusaidia. Atakupa nguvu ya kushinda udhaifu huo.

Ni ngumu sana kuishi maisha ya ukristo pasipo Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ndiye atakayetuwezesha kuishi maisha ya utakatifu na uaminifu. Roho Mtakatifu ndiye atupaye nguvu za kushinda kila changamoto ambazo mkristo anakutana nazo.

Tunatakiwa tujiachilia kwa Roho Mtakatifu. Tunatakiwa tuwe karibu naye kuliko kitu kingine chochote duniani. Roho Mtakatifu akawe furaha yetu, Roho Mtakatifu akawe tumaini letu, Roho Mtakatifu akawe kila kitu kwetu.

MAOMBI:
"Ee Roho Mtakatifu, ninakupenda sana. Wewe ndio kimbilio langu na msaada wangu. Unishike mkono pale ninaposhindwa, unitie nguvu pale nilipo dhaifu. Unipe amani pale ninapokosa amani, unipe utulivu pale ninapokosa utulivu katika jina la Yesu Kristo. Amina"

Ubarikiwe sana.

Innocent Morris
+255652796450 (WhatsApp)

28/07/2026

AMINI TU - Innocent Morris

"Yote yawezekana kwake aaminiye."
Marko 9:23

Ubarikiwe sana.

Innocent Morris
+255652796450 (WhatsApp)

MAOMBI YA LEOOmba maombi haya kwa imani ukimaanisha.Ubarikiwe sana.Innocent Morris+255652796450 (WhatsApp)
27/07/2026

MAOMBI YA LEO

Omba maombi haya kwa imani ukimaanisha.

Ubarikiwe sana.

Innocent Morris
+255652796450 (WhatsApp)

26/07/2026

SUNDAY NIGHT SERVICE 26/07/2026 - Innocent Morris

Contacts: +255652796450 (WhatsApp)

Instagram Page: holyspiritconnect
page: Holy Spirit Connect
Contact: +255652796450 (WhatsApp)

Instagram Link:
/ holyspiritconnect

Facebook Link:
/ holyspiritconnect

YouTube Link:
/ holyspiritconnect , , , , , , , ,

Address

P. O. Box 65409
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Holy Spirit Connect posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share