11/07/2026
SOMO: FAHAMU NAMNA MUNGU ANAVYOTAJIRISHA WATU WAKE
I. UTANGULIZI
Tunamuabudu na kumtumikia Mungu tajiri. Vyote ambavyo unaviona na usivyoviona ambavyo ni utajiri ni mali yake
- Hagai 2:8, Zaburi 24:1
Kupitia wokovu tunaunganishwa na utajiri wa Mungu na kufanyika wana - warithi pamoja na Kristo Yesu
- Warumi 8:16-17,
- 2 Wakorintho 8:9
Fahamu kwamba, MUNGU AMEKUKUSUDIA WEWE UWE TAJIRI, ikiwa bado umekumbatia umaskini, basi wewe ndiye umeamua hivyo.
II. NAMNA GANI MUNGU HUTAJIRISHA WATU WAKE?
Mungu ana njia zake ambazo huzitumia kuwaungamanisha watu wake na utajiri wake hapa duniani.
- Isaya 55:8-11.
Unachotakiwa sio kupingana na njia hizo, au kujiwekea mikakati ya kibinadamu, bali:
1. Tafuta kujua njia za Mungu (Zaburi 25:4-5)
2. Jinyenyekeze ukubali Mungu akuongoze (Zaburi 25:9)
3. kuwa mwaminifu kuzifuata njia za Mungu (Isaya 1:19-20, Yoshua 1:8)
Hizi hapa ni njia ambazo Mungu anatumia kutajirisha na kustawisha watu wake:
1.Anakupa maono ya utajiri mkuu
- maono hukufaya kujiona tajiri k**a Mungu anavyokuona
- maono hukupa msukumo wa kuanzisha jambo la kiuchumi
Mwanzo 12:2
- "nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki (kukutajirisha) na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;"
2.Anakubariki ili uwe tajiri
- Baraka yoyote unayopata ni mbegu ya kukutajirisha
- baraka inaweza kuwa elimu, ujuzi, nguvu, kazi, biashara, watu, n.k
Mithali 10:22
- "Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo."
3.Anakupa nguvu ya kupata utajiri (uweza wa kutengeneza utajiri)
- utajiri haupatikani kwa matamanio, unapatikana kwa nguvu za kiroho (3 Yohana 1:2)
- nguvu inaweza kuwa maono, ujuzi, ubunifu, elimu, n.k-
Kumbukumbu la Torati 8:18
- "Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana *ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri;* ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, k**a hivi leo"
4.Anakufundisha na kukuongoza katika njia za kupata utajiri (namna ya kufanya ili uwe tajiri)
- utajiri unazo njia zake. Kwa lugha rahisi utajiri una kanuni zake. *Mungu hukufundisha kuzijua kanuni zake za utajiri* (Yoshua 1:8).
- Mfano wa kanuni hizo ni: utumishi, utoaji, kazi, bidii, n.k
Isaya 48:17
- "BWANA, mkombozi wako,... asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
5.Ameachilia neema maalumu ya kukutajirisha.
- neema ni uwezesho wa kiungu ndani Yako unaokupa uweza wa kufanya mambo kwa namna ya kiungu.
2 Wakorintho 8:9
- "Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake".
6. Anakupa fursa ya kumtumikia ili kuungamanika na utajiri wake
- Kutoka 23:25-26.
Kila fursa ya kumtumikia Mungu ni fursa ya kuungamanika na utajiri wa kiungu,
- utumishi unabariki, baraka hutajirisha
- utajiri hugusa na kufunua moyo wa Mungu, moyo wa Mungu una Siri za mafanikio na utajiri
- n.k
III. MAMBO YA KUZINGATIA
Hivyo, fahamu kwamba:
- utajiri sio dhambi, dhambi ni kutumia njia za kishetani kujitafutia mali na utajiri.
- utajiri sio dhambi, dhambi ni kuufanya utajiri kuwa Mungu wako
UTAJIRI AU UMASKINI: UCHAGUZI NI WAKO
Licha ya kwamba Mungu amekuwekea vyote vinavyohitajika ili uwe tajiri, lakini kuwa tajiri ni hiari na uchaguzi wako mwenyewe.
Mungu anataka na anakushauri uchague kuwa tajiri: wewe na uzao wako
- Kumbukumbu la Torati 30:19.
Ukichagua kupata utajiri wa Kiungu, sharti:
- ukubali njia na maelekezo ya Mungu,
- utii na kutatendea KAZI k**a alivyoelekeza (Yoshua 1:8, Kumbukumbu la Torati 28:1-14)
IV. OMBI MAALUMU
- Baba, naomba neema maalumu ya kuniwezesha kuchukua hatua, kulipa gharama zinazohitajika kuufikia Utajiri ambao umeweka mbele yangu katika jina la Yesu Kristo (Mwanzo 4:1-7).
UBARIKIWE SANA. NAKUONA UKIPAA JUU KATIKA JINA LA YESU KRISTO.
Valley of Life Church