Believers Community Church

Believers Community Church We are committed to teach, preach the word in clarity and precision. Heralding the Lordship of the word, demonstrating the influence of the spirit

IFAHAMU, BELIEVERS COMMUNITY CHURCH (BCC)Dhamira yetu ni kufundisha na kuhubiri NENO la Mungu ulimwenguni kote; yaani ka...
24/01/2026

IFAHAMU, BELIEVERS COMMUNITY CHURCH (BCC)

Dhamira yetu ni kufundisha na kuhubiri NENO la Mungu ulimwenguni kote; yaani katika kila taifa, kila lugha na kabila, kila eneo, tamaduni, bara na kila sehemu ya dunia.

Kwa hiyo, tumejitoa kufundisha hivi, kwa kuwaandaa, kuwatengeneza na kuwahamasisha waamini waweze kuingia katika uhalisia, ukomavu, na huduma iliyo katika Kristo Yesu; yaani huduma ya NENO. Tunafanya hivi kwa msisitizo mkubwa kww habari ya uhalisia wa kiumbe kipya katika ukombozi.

Tunajitahidi kufundisha na kuhubiri injili hii yenye mtazamo wa Kristo, kwa udhihirisho halisi wa ishara, ajabu na miujiza; yaani, utendaji wa kiungu uliobeba miujiza.

Believers Community Church ni huduma yetu ya kanisa, ambapo kwa uthabiti tunamfunza(kumtengeneza) na tunamkuza mwamini ili aweze kupokea na kuhudumu dhamira hii kwa ufanisi mkubwa, katika kuhakikisha tunafanya uwasilishaji wa mara kwa mara kuhusu maono yetu kwake.

Tunabaki kuona dunia YOTE ikijaa maarifa ya utukufu wa Mungu, k**a vile maji yanavyoifunika bahari (Habakuki 2:14).

—Believers Community Church
“Making your life count”

Mwamini yeyote yule anapaswa awe chini ya uangalizi katika kanisa la mahali kwa sababu kanisani ni mahali pekee ambapo m...
24/12/2025

Mwamini yeyote yule anapaswa awe chini ya uangalizi katika kanisa la mahali kwa sababu kanisani ni mahali pekee ambapo malighafi(mwamini) inachakatwa kuwa bidhaa adhimu ifaayo kuingia sokoni( mwamini aliyefunzwa vizuri huduma). KANISA LA MAHALI ni mpango wa milele wa Mungu katika ukombozi. Kanisa la mahali ni karakana au kiwanda kinachotengeneza bidhaa inayoitwa mwamini anayetenda kazi ya huduma yaani awe mtendakazi katika nyumba ya Mungu asilimia mia moja. Lakini pia kanisa la Mahali ni Shule kwa sababu inawaweka waamini darasani kwa ajili ya mafunzo ya huduma. Ukuaji wa kiroho unaanzia katika kanisa la mahali.Ni sehemu ambayo itashepu mtindo wa maisha yako ili ufuate mpango wa Mungu hata katikati ya dunia hii mbovu.
Tukiangalia wanafunzi na mitume katika kanisa la kwanza huduma zao zilizaliwa katika kusanyiko la watakatifu.

Tumwangalie stefano kwenye matendo ya mitume sura ya 6 na 7 ambaye alikuwa shemasi katika kanisa la mahali alifunzwa neno la Mungu vizuri akaishia kumhubiria sauli na wengine wengi sana kabla ya kifo chake.

Matendo 6:3
[3]
Basi ndugu, *chagueni watu saba miongoni mwenu,* walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili;

Paulo na Barnaba kabla ya kutumwa na kanisa kwenda kuhuburi Asia walipokea mafunzo katika kanisa la mahali lililokuwa Antiokia.

Matendo 13:1
[1]
Na huko *Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba,* na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na *Sauli* .

Timotheo kabla ya kuchukuliwa na paulo alikuwepo katika kanisa la mahali lililopo Listra na alishuhudiwa vema na watakatiku katika kanisa kwa sababu ya mwenendo wake mzuri

Matendo 16:1-3
[1]
Basi akafika Derbe na Listra, na *hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo,* mwana wa mwanamke Myahudi aliyeamini; lakini babaye alikuwa Myunani.
[2]
*Mtu huyo alishuhudiwa vema na ndugu waliokaa Listra na Ikonio.*
[3]
*Paulo akamtaka huyo afuatane naye,* akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni Myunani.

Mtindo kamili wa uanafunzi tunaona unaanzia katika kanisa la mahali.Ni katika kanisa la mahali tunafunzwa jinsi ya kutenda kazi ya huduma kwa ubora.Ni katika kanisa la mahali tunajifunza namna ya kuenenda kwa upendo na kuwatumikia watakatifu wengine. Ni katika kanisa la mahali tunapokea marekebisho,maonyo na maelekezo maalumu ya namna bora ya kutenda kazi ya huduma. Ni katika kanisa la mahali utaratibu maalumu wa jinsi ya kutimiza mpango wa Mungu juu ya maisha yetu unawekwa kwa uwazi.
Kuwa chini ya uangalizi wa kanisa la mahali inakusaidia kuwa na uwajibikaji wa machaguzi yako kila siku. Tii mamlaka iliyopo hapo.Fuata maelekezo ya mahali hapo.Watumikie watakatifu wengine mahali hapo. Katika nia yako vaa vazi la utumishi na kuwatanguliza wengine. Jifunge unyenyekevu wakati wote hata katikati ya sifa na pongezi kutoka kwa wanadamu unabaki na mtazamo kwamba wengine ni bora kuliko nafsi yako.
Kanisa la mahali ni nguzo ya lazima na muhimu kwa kila mwamini kujizoeza UPENDO KWA VITENDO,UNYENYEKEVU KWA VITENDO NA KUHESABU MAISHA YAKO KILA SIKU KWA VITENDO. Mambo haya ni rahisi zaidi kujizoeza ukiwa katikati ya watakatifu wengine katika kanisa la mahali. Mpango wa Mungu taangia mwanzo imekuwa ni kanisa na si mtu mmoja mmoja. Ndio maana kuna maelekezo ya kutoacha kukusanyika k**a ilivyodesturi ya wengine. Tunadumu katika hili siku zote.

Biblia inarecord kwamba wale watu 3000 waliookoka siku ya pentekoste walikuwa wakidumu katika ushirika na watakatifu wengine

Matendo2:42
[42]
*Wakawa wakidumu* katika fundisho la mitume, na *katika ushirika* , na katika kuumega mkate, na katika kusali.

Jipate katika kusanyiko la watakatifu katika kanisa la mahali. Tumika hapo. Fikia mahitaji ya kanisa na watakatifu wengine hapo. Tii na heshimu uongozi wa mahali hapo. Pokea maelekezo kutokea hapo.
Baada ya hapo subiria matokeo yanayoshikika na utendaji wa neema ya Mungu katika maisha yako.
Umewezeshwa!

—Believers Community Church
"Making your life count "

Namna unavojiona na kujitambulisha katika nia yako ni muhimu zaidi kuliko ulimwengu unavojaribu kukutambulisha. Siku uli...
23/12/2025

Namna unavojiona na kujitambulisha katika nia yako ni muhimu zaidi kuliko ulimwengu unavojaribu kukutambulisha. Siku ulipomwamini Yesu utambulisho wako ulibadilika katika roho yako. Kilichobaki ni mwamini kuchukua hatua za makusudi za kuvaa utambulisho mpya katika kiuno cha nia yake. Paulo anawaambia warumi wamvae Kristo. Namna gani wanamvaa ameelezea katika mistari ya juu ni kwa KUENENDA KATIKA UPENDO.
Warumi13:14

Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.

Mungu ni pendo. Injili ya kristo pia msukumo ulionyuma yake ni upendo. Ndicho kilichofanya Yesu aje kutuokoa. Paulo anawaambia wafilipi Yeye alikuwa Yu sawa na Mungu ila aliacha Comfort zone akaja kutuokoa. Hamasa kubwa inayotuchochea sisi k**a waamini ni UPENDO ndicho kiungo kinachotufanya tuache Comforts zetu na kushiriki mateso yake katika kuufikia ulimwengu. Si kitu kipya wala si kitu kigeni ni asili ambayo tumeirithi kutoka kwa Baba yetu.
Wafilipi 2:5-7
[5]:
Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;

ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushik**ana nacho;
[7]
bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;

Aliacha comfort akaja akatufia
Warumi 5:8
[8]
Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

K**a alivyotoka tunatoka tunashiriki mateso yake
Wafilipi3:10

ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na *ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;*

Unaacha comfort UNASHIRIKI MATESO YAKE. Namna gani unashiriki? Ni katika mchakato wa kuhubiri injili hata katikati ya upinzani na kuwahudumia watakatifu katika kanisa la mahali. Tuna msukumo huu wa mateso ndani yetu ambao umejengwa katika nguzo imara inayoitwa upendo. Ninaweza kushiriki mateso yake, unaweza kushiriki mateso yake, tunaenda tena leo, TUNATOKA TENA LEO na katika kutoka nguvu za Mungu zitalithibitisha
lile neno tulihubirilo.

Marko 16:20
[20]
*Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote* , Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.

Walishiriki mateso yake tunashiriki mateso yake KWA KUTOKA.

Huu ni utambulisho wetu. Hii ni kweli ya kiumbe kipya pia. AMEN.

—Believers Community Church
"Making your life count "

Address

Makumbusho
Dar Es Salaam

Opening Hours

Saturday 12:00 - 15:00
15:00 - 18:00
Sunday 08:30 - 13:00
15:00 - 18:00

Telephone

+255656566610

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Believers Community Church posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Believers Community Church:

Shortcuts

Share