24/12/2024
TUKIO :RETREAT CAMP YA KUFUNGA MWAKA 2024 NA KUFUNGUA MWAKA 2025
UJUMBE: KUINUKA KWA WAOKOZI- OBADIA 1:21
TAREHE : 26TH DECEMBER - 31TH DECEMBER 2024
SABABU 20 KWA NINI USIKOSE RETREAT CAMP HII YA KUFUNGA MWAKA, DESEMBA 26 , 2024 HADI DESEMBA 31, 2024?
1. Ni mahali pa NENO
Neno la kubadilisha maisha yako litatoka kwenye vinywa vya watumishi wa Mungu 12 walio kwenye picha hii
2. Ni mahali pa UPAKO WA ROHO MTAKATIFU
Kila mmoja wa watumishi hawa wa Mungu amelipa gharama na anao Upako juu yake ambao unapaswa kunufaika nao ukija
3. Ni mahali pa kupokea NEEMA KUU ZA MUNGU walizobeba hawa watu wa Mungu
Kila mmoja wa WANENAJI anazo neema kadhaa zinazofanya kazi KIPEKEE MAISHANI MWAKE na kwenye HUDUMA yake, unakosaje?
4. Ni mahali pa KUKUTANA USO KWA USO na watu hawa WAKUU wa Mungu na kuwekewa mikono au kushauriwa au kupewa NENO BINAFSI kutoka kwa BWANA!
5. Ni mahali pa kukutana na watu wa kizazi chako wenye neema mbalimbali kwenye maeneo tofauti waliokuja kunolewa, kuchongwa na kuachiliwa kwenda kuligeuza taifa letu na dunia yetu!
6. Ni mahali pa kubadilishana na Mungu changamoto, matatizo, shida na magumu uliyonayo k**a ilivyokuwa Shiloh kwa Anna, au birika la Bethzatha kwa yule kipofu- It is a place for a personal encounter with God!
7. Ni mahali pa kujifunza KANUNI ZA UKUU zilizowasaidia WANENAJI kuwa hapo walipo na kisha wataziachilia ziingie maishani mwako kwa MATAMKO au kukuwekea mikono!
8. Ni mahali pa kuja kupata watu sahihi wa KUAMBATANA nao kwenye maisha, huduma, taaluma na kesho yako! Watu wanaokuja RETREAT wote hawana mpango wa kuwa wa KAWAIDA kwenye taifa hili, wanataka kutikisa DUNIA YAO, huku ndipo pa kupata marafiki wa maana wanaokwenda mbali k**a wewe!
9. Ni mahali pa kuja kuandika MALENGO NA MIPANGO YA MWAKA UJAO NA MAISHA YAKO YAJAYO, kisha kupata muda mwingi kuiombea na kuikabidhi mikononi mwa Bwana Yesu, unaachaje kuja?
10. Ni mahali pa kuja ku-refresh baada ya mwaka mzima wa MAFANIKIO au CHANGAMOTO, ili kukusanya nguvu za Mungu za kuuendea mwaka 2023 ukiwa safi na makini!
11. Ni mahali pa kuamsha ari na shauku yako ya kufanya mambo makubwa kwa ajili ya Mungu na dunia yako, maana utakutana na watu watakaokupa changamoto na utajiona k**a unacheza na haufanyi kitu bado na MAISHA YAKO! You need inspiration of the Spirit to go to next level.
12. Ni mahali pa kukupa dira na mwelekeo wa mwaka wako 2025, ukiwa hapa Mungu atakupa hekima, na tutakuongoza kuweka malengo na mipango inayofikika na inayopimika, utakayoikamilisha mwaka ujao kwa bidii na imani!
13. Utatambua KUSUDI LA MUNGU JUU YA MAISHA YAKO! Mahali hapa huwezi kuja na usirudi umejua cha kufanya na maisha yako, haiwezekani -Matendo 13:1-5
14. Mahali hapa utafunguliwa jumla toka DHAMBI zote ambazo ulikuwa unahangaika kuziacha kwa nguvu zako bila mafanikio!
15. Mahali hapa utafunguliwa toka kila TABIA SUGU ambazo zimekuwa zikikuharibia mambo mengi kwenye maisha yako!
16. Mahali hapa utapata malezi na maongozi ya kiroho, vipawa na karama ulizobeba ili usiishie njiani!
17. Mahali hapa utajazwa na Roho Mtakatifu na KUGEUZWA KUWA MTU MWINGINE
18. Mahali hapa utakuwa umepata mapumziko sahihi ya mwisho wa mwaka, ili uuanze mwaka 2025 ukiwa mpya, bora na asiyezuilika!
19. Mahali hapa yale uliyokuwa unayasoma kwenye Biblia k**a Ishara, miujiza, karama za Roho Mtakatifu utaviona vikifanyika live k**a kwenye Mathayo, Marko, Luka, Yohana na Matendo ya Mitume!
20. Unaweza kukutana na mwenzi sahihi wa maisha huku kwa wale ambao hamjaoa au kuolewa, na wenye NDOA huku ndipo honeymoon pa kuja kuchaji upya NDOA ZENU!
UNAWEZA KULIPA ADA KWA AKAUNTI HII MAALUM YA RETREAT CAMP
ACC: 015C690443302
JINA: ABC GLOBAL RETREAT CAMP
BENKI: CRDB BANK
(Tunza risiti)