14/05/2026
Alhamdulillah, tumefanikiwa kufanya kipindi chetu cha “Mafunzo kutoka ndoa ya Imam Ali (a) na Bibi Fatima (a)” kilichowasilishwa na Dr. Mohamed Shabbir Nathoo.
Katika kipindi hiki tulijifunza kuwa ndoa yenye mafanikio hujengwa juu ya msingi wa imani, upendo, heshima, subira na ushirikiano. Kupitia maisha ya Imam Ali ibn Abi Talib (a) na Fatima al-Zahra (a), tuliona mfano bora wa familia iliyojengwa kwa taqwa, uadilifu na kujali haki za kila mmoja.