30/08/2026
Unawezaje kupata uhai?
Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Neno ndiyo mkate, ukilisikia Neno la Mungu na ukalipokea ndipo imani inaumbika ndani yako kwa maana hiyo uhai unaumbika ndani yako na Neno linasema “Yote yawezekana kwake aaminiye.”
Sasa je! Kwa nini wewe unakwama k**a unayo imani? Ukiona unakwama maana yake ni kuwa huenda ulionja mkate (Neno la Mungu) haujalila na ndiyo maana kwako hakuna uhai kwa maana k**a ulikula huo mkate (Neno la Mungu) wewe utakuwa hai na kila ulichonacho kitakuwa hai.
Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”
Watu gani wanaruhusa ya kuomba? Yohana 10:9 “Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.”
Yule ambaye anaruhusa ya kuomba ni yule ambaye amekubali kukaa ndani yake mzima mzima, je unaingiaje ndani yake mzima mzima? Kwa namna unavyolifahamu Neno, namna unavyolifahamu neno ndivyo unavyoingia kwake.
1 Yohana 1:1-4 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu)… ”
Ukifikia mahali pa kulijua Neno la Mungu ndipo imani inaumbika ndani yako na uzima unaumbika kwako pia; hapo ndipo furaha inaanza. Tunapozungumzia furaha ya Bwana tunazungumzia uhakika wa kujua kile kilichopo mbele.
©Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira