SDA .The prophecy of the last days

SDA .The prophecy of the last days I would like to invite all people to this page, so that we can learn about the prophecies of the last days.

[30/09, 2:21 am] +255 782 287 711: KESHA LA ASUBUHI Ijumaa 30/09/2022*KILA MUUMINI ASAIDIE KUENEZA INJILI**Basi Yesu aka...
30/09/2022

[30/09, 2:21 am] +255 782 287 711: KESHA LA ASUBUHI

Ijumaa 30/09/2022

*KILA MUUMINI ASAIDIE KUENEZA INJILI*

*Basi Yesu akawaambia tena akasema, "Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.* Yohana 8:12

📜 Wale wanaomfuata Yesu watakuwa watenda kazi pamoja na Mungu. Hawatatembea gizani, bali wataipata njia ya kweli ambapo Yesu, aliye nuru ya ulimwengu, huongoza njia; na wanapokunja hatua zao kuelekea Sayuni, wakisogea kwa imani, watapata uzoefu angavu katika mambo ya Mungu. Utume wa Kristo unaofahamika kidogo mno, unaeleweka kwa ufinyu mno, uliomwita kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu hadi kwenye fumbo la madhabahu ya msalaba wa Kalivari, utaifungua akili zaidi na zaidi, na itaonekana kuwa katika kafara ya Kristo hupatikana chemichemi na kanuni ya kila utume mwingine wa upendo. Ni upendo wa Kristo ambao umekuwa kichocheo cha kila mfanyakazi wa kweli wa Kimishenari katika miji, mijini, katika barabara kuu na njia za dunia.

📜 Kanisa limepangwa duniani kwa kusudi la umishenari, na ni muhimu sana kuwa kila muumini binafsi wa kanisa awe mfanyakazi mwaminifu pamoja na Mungu, akijazwa na Roho, akiwa na fikra za Kristo, aliyekamilishwa katika huruma ya Yesu Kristo, na hivyo basi akitimia kila juhudi kulingana na uwezo wake aliopewa katika uokoaji wa roho. Kristo anataka kuwa kila mtu ambaye angependa kuitwa kwa jina Lake afanye kazi Yake kuwa ya kwanza na ya juu kabisa, na kushirikiana bila ubinafsi na wajumbe wa mbinguni katika kuwaokoa wale wanaoangamia ambao Kristo aliwafia.

🔘 *Kutumia vibaya nyenzo au mvuto au mtaji wowote wa akili au mwili ukiokabidhiwa ni kumwibia Mungu au kuuibia ulimwengu; kwa maana ni kuzigeuza nguvu kuwa njia nyingine zaidi ya ile ambayo Mungu alipanga kuwa zinapaswa kusonga mbele kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu. Kristo alipokuwa hapa duniani, aliwatuma wanafunzi Wake kuutangaza ufalme wa Mungu katika uyahudi yote, na katika mfano huu alifunua waziwazi kuwa ni jukumu la watu Wake wakati wote kutoa kwa wengine elimu waliyonayo ya njia, ya uzima, na ya kweli. Katika kazi zake zote Yesu alitafuta kufundisha kanisa Lake kwa ajili ya kazi ya umishenari, na idadi yao ilipoongezeka, utume wao ungeenea, hadi hatimaye ujumbe wa injili ungezunguka ulimwengu kupitia huduma zao.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️
[30/09, 4:46 am] Abner Joshua: KESHA LA ASUBUHI

*KESHA LA ASUBUHI* Alhamisi 29/09/2022*HUDUMA ISIYO NA UBINAFSI INAMFURAHISHA KRISTO PAMOJA NA SISI*Tena tusichoke katik...
29/09/2022

*KESHA LA ASUBUHI*

Alhamisi 29/09/2022

*HUDUMA ISIYO NA UBINAFSI INAMFURAHISHA KRISTO PAMOJA NA SISI*

Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. *Wagalatia 6:9*

▶️ Kazi yetu kwa Mungu karibia inaonekana kutokuwa na matunda katika dunia hii. Jitihada zetu za kufanya mema zinaweza kuwa za bidii naza kudumu, hata hivyo huenda tusiruhusiwe kushuhudia matokeo yao. Kwa upande wetu juhudi yetu inaweza kuonekana kuwa bure. Lakini mwokozi anatuthibitishia kuwa kazi yetu imehifadhiwa mbinguni,na kuwa ujazo hauwezi kupungua... Katika maneno ya mtunga zaburi tunasoma: "Ingawa mtu anakwenda zake akilia, azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, aichukuapo miganda yake". Zaburi 126:6

▶️ Na ingawa thawabu kuu ya mwisho inatolewa wakati wa kuja kwa Kristo, utumishi wa moyo wa kweli kwa Mungu huleta thawabu hata katika maisha haya. Vizuizi, upinzani, na uchungu ni mambo yenye kuvunja moyo ambayo wafanyakazi watalazimika kukabiliana nayo. Wanaweza wasione matunda ya mahangaiko yao. Lakini mbele ya haya yote wanapata katika kazi yao malipo yenye baraka.

▶️ Wale ambao wanajisalimisha wenyewe kwa Mungu katika huduma isiyo ya ubinafsi kwa wanadamu wako katika ushirika na Bwana wa utukufu. Fikra hizi huleta utamu wa kazi zote, huimarisha nia, hutia moyo kwa lolote litakalotokea. Wakifanya kazi kwa moyo usio na ubinafsi,wakiwa wamekuzwa kwa kuwa washiriki wa mateso ya Kristo, wakishiriki huruma zake, wanasaidia kuongeza wimbi la furaha yake, na kuleta heshima na sifa kwa jina Lake lililotukuka.

▶️ Katika ushirika na Mungu, pamoja na Kristo, na pamoja na malaika watakatifu wamezungukwa na anga hewa ya mbinguni, anga ambayo huleta afya kwa mwili, nguvu kwa akili, na furaha kwa roho. Wote wanaoweka wakfu mwili, nafsi na roho katika huduma ya Mungu daima watakuwa wakipokea karama mpya ya nguvu za kimwili, kiakili na kiroho. Ugavi usioisha wa mbinguni ni kwa ajili yao. Kristo anawapa pumzi ya Roho Wake mwenyewe, uhai wa uhai Wake. Roho Mtakatifu huweka nguvu zake za juu zaidi kufanya kazi katika moyo na akili.

*TAFAKARI NJEMA SANA*

SOMO LA ASUBUHILEO May 9/2022Malezi Bora na mafundisho Kwa watoto wetuMTAZAMO wa sasa ulimwenguni ni kuwaacha vijana kuf...
09/05/2022

SOMO LA ASUBUHI
LEO May 9/2022

Malezi Bora na mafundisho Kwa watoto wetu

MTAZAMO wa sasa ulimwenguni ni kuwaacha vijana kufuata nia zao wenyewe kwa kawaida. Na k**a wakiwa wakaidi sana katika ujana wao, wazazi husema wataendelea vizuri baadaye kidogo wanapofikisha umri wa miaka kumi na sita au kumi na minane, watayapima mambo wenyewe, na kuacha mazoea yao mabaya, na hatimaye kuwa wanaume na wanawake wenye manufaa. Kosa gani! Kwa miaka mingi humwacha adui kupanda mbegu moyoni; huacha mafundisho mabaya kukua, na mara nyingi jitihada yote ya baadaye itakayofanywa juu ya mtu huyo haitakuwa na mafanikio yo yote.
Shetani ni mwenye hila, fundi hodari, adui mkubwa. Wakati wo wote neno lisilo la akili likisemwa lenye kuwadhuru vijana, liwe kuwasifu mno wasivyostahili au kuwafanya wasichukie sana dhambi fulani, Shetani hulifaidi na kustawisha mbegu mbaya ipate kutelemsha mzizi na kuzaa mavuno mengi. Wazazi wengine wamewaacha watoto wao kuwa na mazoea mabaya, alama ambazo huweza kuonekana siku zote za maisha. Dhambi hiyo ni juu ya wazazi. Watoto hao waweza kujidai ni Wakristo, walakini, bila kazi maalumu ya neema moyoni na pasipo uongofu kamili maishani mazoea yao ya zamani yataonekana katika mambo yote ya maisha yao, na wataonyesha tabia ile ile ambayo wazazi wao waliwaacha kuwa nayo. 1
Yawapasa wazazi kuwatawala watoto wao, kuzisahihisha tamaa zao, na kuwatiisha, ama sivyo Mungu atawaangamiza hao watoto siku ya hasira yake kali, na wazazi wasiowatawala watoto wao hawatakosa kuwa na hatia. Hasa ingewapasa watumishi wa Mungu kuwatawala watu wa nyumba zao wenyewe na kuwaweka chini ya utawala mzuri. Naliona kuwa hawako tayari kuhukumu wala kuamua mashauri ya kanisa, k**a wasipoweza kutawala vizuri nyumba yao wenyewe. Kwanza hawana budi kuwa na utaratibu nyumbani, ndipo maamuzi yao na mvuto wao vitakuwa na matokeo kanisani. 2
Kila mwana na binti angeitwa kutoa habari k**a akikosekana nyumbani usiku. Yawapasa wazazi kujua marafiki za watoto wao na nyumba ya mtu wanamozitumia saa zao za jioni. 3
Akili ya mwanadamu haijagundua zaidi ya kile Mungu ajuacho wala kubuni shauri bora zaiai juu ya namna ya kuwatendea watoto kuliko lile lililotolewa na Bwana wetu. Ni nani awezaye kuelewa vizuri zaidi mahitaji ya watoto kuliko Muumbaji wao?
Ni nani awezaye kuyatilia moyo zaidi mambo yao kuliko Yeye aliyewanunua kwa damu yake mwenyewe? K**a neno la Mungu lingesomwa kwa uangalifu na kushikwa kwa uaminifu maumivu makuu ya roho juu ya tabia zilizopotoka za watoto waovu yangepungua.
Watoto wanayo madai ambayo wazazi wao wapaswa kuyajua na kuyajali. Wana haki ya elimu na mafundisho yatakayowafanya kuwa wenye maana, wanaoheshimiwa na wenye kupendwa na watu hapa kuwapa hali ya tabia ya kufaa kwa jamii ya watu safi na watakatifu baada ya hapo. Vijana wangefundishwa kuwa hali yao ya wakati huu na lle ya wakati ujao pia hutegemea sana juu ya mazoea wanayofanya utotoni na katika siku za ujana. 4
Wanaume na wanawake wanaodai kuheshimu Biblia na kuyashika mafundisho yake hushindwa mara nyingi kutimiza masharti yake. Katika kuwafundisha watoto hufuata tabia zao wenyewe zilizopotoka badala ya mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa wazi. Kukosa kufanya wajibu huo huleta hasara kwa roho za watu maelfu. Biblia imeweka kawaida za malezi bora ya watoto. K**a masharti hayo ya Mungu yangefuatwa na wazazi, tungeona leo jamii ya vijana walio tofauti kabisa wenye kupiga hatua ya juu ya utendaji. Lakini wazazi wanaodai kuwa ni wasomaji wa Biblia na wafuasi wa Biblia wanafanya kinyume kabisa cha mafundisho yake. Tunasikia kilio cha huzuni na maumivu makuu kutoka kwa akina baba na mama wanaosikitikia tabia ya watoto wao, wasifahamu ila kidogo tu kwamba wanajiletea huzuni wao wenyewe na maumivu hayo, na kuwaharibu watoto wao waliopewa na Mungu kwa kutowazoeza watoto wao mazoea mema tokea utotoni. 5
Watoto ambao ni Wakristo wataupendelea upendo na kibali cha wazazi wao wanaomcha Mungu zaidi ya mibaraka yote mingine ya duniani. Watawapenda na kuwaheshimu wazazi wao. Yafaa njia ya kuwafurahisha wazazi wao iwe mojawapo ya mambo makubwa wanayojifunza maishani mwao. Katika zama hizi za uasi, watoto hawajapata mafundisho na malezi bora, hawajui ila kidogo tu wajibu uwapasao kwa wazazi wao. Mara nyingi ndivyo ilivyo, yaani, kadiri wazazi wao wanavyowatendea mema, ndivyo wanavyozidi kutokuwa na shukrani na kutowaheshimu.
Furaha ya wakati ujao ya watoto wao iko zaidi mikononi mwa wazazi. Kazi kubwa ya kuzirekebisha tabia za watoto hawa ni juu yao, mafundisho yaliyotolewa utotoni yatafuatana nao siku zote za maisha yao. Wazazi hupanda mbegu ambazo zitaota na kuzaa matunda ama kwa wema ama kwa ubaya. Huweza kuwafanya wana na mabinti zao kufaa kwa raha ama kwa hali mbaya sana. KN 215.1 - KN 216.5

Address

Mwongozo
Dar Es Salaam

Telephone

+255748692063

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when SDA .The prophecy of the last days posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share