Mwl Ajs Kagulana

Mwl Ajs Kagulana MWL AJS.

KAGULANA, Ni MTUMWA WA KRISTO YESU, ALIYEITWA KUWA MWL, NA KUTENGWA AIHUBIRI INJIRI YA MUNGU kwa mataifa yote

Kwa Mawasiliano zaidi waweza kuwasiliana naye kwa namba zifuatazo,

- 0789 294 126
What'upp No:- 0626 907 270

22/11/2025

Thanks for join,
Na, KARIBU SANA KATIKA UKRASA HUU WA Mwl Ajs Kagulana.

Mwl Ajs Kagulana ni Mwalimu wa neno la Mungu, aliyeitwa na kutengwa ili aihubiri injiri ya Mungu kwa mataifa yote.

Mungu amemjalia k**a si kumpa hekima na uwezo wa kuleta majibu kwenye maisha ya kila siku ya watu.

Hivyo unakaribishwa kwenye baadhi ya vyanzo mbali mbali vya mafundisho yake ambayo kimsingi ni mafundisho ya Kristo.

Ili ukue kiroho, kimwili na kiakili k**a si kiuchumi, Kiufahamu n.k.

Na vyanzo hivyo vya mafundisho haya ni " NAPENDA MAFUNDISHO YA MWL AJS KAGULANA ".

Na group hili la mafundisho haya ya Mwl Ajs Kagulana linapatikana Facebook na vyanzo vingine vya mafundisho haya ni.

EDtv ( Immanuel discipleship) unaopatikana YouTube.

Na hivi punde tutakuletea mafundisho haya muhimu kwa ajiri ya ustawi wako wa kiroho kupitia majukwaa mengine mengi k**a vile Instragram, Tiktok, What'upp Groups n.k.

Na k**a una ushuhuda au changamoto yoyote usisite kuwasilisha nasi kupitia namba

0789294126 au
0626 907 270 ambayo ni namba ya What'upp.

BARIKIWA.

" Kwa maneno hayo yote, na kwa maono hayo yote ndivyo... Apostle Alpharich Crown Josh " ( 2 Samw 7:17 ).Na Mwl Mwl Ajs K...
20/11/2025

" Kwa maneno hayo yote, na kwa maono hayo yote ndivyo... Apostle Alpharich Crown Josh " ( 2 Samw 7:17 ).

Na Mwl Mwl Ajs Kagulana walivyonena na wewe kupitia video hii unayoiona kwenye ukrasa huu.

Na kwenye Channel hii ya EDtv ( Immanuel discipleship) ili kukufanya umtafute Mungu katika siku hizi.

Za Pastor Washokera Erasto Apostle Alpharich Crown Josh na Mwl Ajs Kagulana watu wenye fahamu katika neno na maono ya Mungu juu ya maisha yako.

Ili Mungu akufanikishe k**a si kukufanya uzifikie ndoto zako k**a Yusufu ambazo umeziota kwa miaka mingi.

BARIKIWA na usiache kufuatilia video hii muhimu kwa ajiri ya ustawi wako wa kiroho.

Usisahau ku coment ku lik pamoja naku shar

15/11/2025

Ni,
" ...watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, wenye zana za vita za kila namna... " ( 1 Nyak 12:33 ).

KUMBUKA;
Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama;

" ...Bali ni juu falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho " ( Waefeso 6:12 ).

MAJI YAMEGAWANYIKA KWENYE MAKUNDI MKUBWA MAWILI KIBIBLIA.Kundi la kwanza i/Ni MAJI TU K**A MAJI YA KAWAIDA AMBAYO KIROHO...
13/11/2025

MAJI YAMEGAWANYIKA KWENYE MAKUNDI MKUBWA MAWILI KIBIBLIA.

Kundi la kwanza i/
Ni MAJI TU K**A MAJI YA KAWAIDA AMBAYO KIROHO HUFAHAMIKA K**A MAJI YALIYO CHINI YA MBINGU.

Ambayo watu huyatumia kwa shughuli mbalimbali k**a vile kufua, kujenga kuoshea vyombo.

Au hata kumwangilia bustani k**a alivyofanya Adam pale kwenye bustani ya Edeni.

Na wazo hili unalipata kwenye kitabu hiki cha Mwanzo 1:9 inayosema,

" Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja ili pakavu paonekane; ikawa hivyo " ( Mwanzo 1:9 ).

Haya maji ni maji tu ya kawaida k**a yalivyo maji mengine yote tunayoyatumia kwenye shughuli zetu za kila siku.

K**a vile kwenye kilimo, kwenye kuzalisha umeme n.k. Maana ni maji yaliyo chini ya mbingu.

Au maji yanayofikika au yanayofikiwa na binadamu kwa ajiri ya kuyatumia kwa shughuli zao.

Na kundi la pili ii/ la maji ni MAJI MENGI K**A HAYA YA UFUNUO 17:1 ALIYOYAKALIA K**A SI KUYAKETIA HUYU KAHABA WA UFUNUO 17:1 na UFUNUO 17:15.

Maji haya si maji k**a maji ya kawaida ila humaanisha jamaa au makutano au mataifa ya watu au watu na lugha zao.

Na wazo hili unalipata kwenye kitabu hiki cha Ufunuo 17:15 inayosema.

" Kisha akaniambia, yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha " ( Ufunuo 17:15 ).

Hivyo ni muhimu kujua kuwa si kila mahali Mungu au mwandishi wa kitabu hiki kitakatifu.

Kiitwacho Biblia anapozungumzia maji basi atakuwa anazungumzia maji tu k**a maji ya kawaida.

ila kuna wakati atazungumzia maji mengi au maji k**a jamaa au makutano au mataifa ya watu au watu na lugha zao.

Ndio maana ili kumsaidia mtu huyu wa kitabu hiki cha Ufunuo ambaye ndiye Yohana.

Akamwambia " maji yale uliyoyaona " ni jamaa na makutano na mataifa na lugha si kwa bahati mbaya.

Ila kwa makusudi ili ajue maji yana tafsri mbili (2) katika ulimwengu wa roho. k**a tulivyoona huko juu.

Asije akaenda na tafsiri moja tu na akakosa kupata ujumbe au kile ambacho mungu amekusudia akipate.

Hivyo hata wewe unayesoma ujumbe huu ni muhimu kufahamu kuwa maji yana tafsri kubwa mbili.

Ya kwanza ni maji tu k**a maji ya kawaida au Maji yaliyo chini ya mbingu

Na ya pili ni maji k**a jamaa au makutano au mataifa ya watu au watu na lugha zao k**a tulivyoona kwenye kitabu cha Ufunuo 17:1,15.

Na hii itakusaidia kuelewa vizuri kile ambacho Mungu au mwandishi atakuwa au amekusudia ukielewe kwenye uandishi wake.

BARIKIWA na usiache kufuatilia mafundisho haya muhimu kwa ajiri ya ustawi wako wa kiroho.

Kiroho,MAJI MENGI HUMAANISHA NINI?.Maji mengi (Kiroho au kwa tafsiri ya Biblia) ni jamaa au makutano ya watu au mataifa ...
13/11/2025

Kiroho,
MAJI MENGI HUMAANISHA NINI?.

Maji mengi (Kiroho au kwa tafsiri ya Biblia) ni jamaa au makutano ya watu au mataifa mbalimbali na lugha zao.

Na wazo hili unalipata kwenye kitabu hiki cha Ufunuo 17:1 Na kitabu hiki cha Ufunuo 17:15 inayosema,

" Kisha akaniambia, yale maji uliyoyaona, ( yaani maji mengi ambayo utayaona kwenye kitabu cha Ufunuo 17:1 ).

hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha " ( Ufunuo 17:15 ).

Hivyo unapokutana na neno " maji mengi " kwenye Biblia ni muhimu kufahamu kuwa.

Mungu au mwandishi atakuwa anakusudia au atakuwa anamaanisha jamaa au makutano au mataifa ya watu au watu na lugha zao.

K**a si maji k**a maji tu ya kawaida kulingana na kitabu hiki cha Ufunuo 17:15.

Kwa mawasiliano zaidi waweza kuwasiliana nami kwa namba zifuatazo,

- 0789 294 126 au
What'upp No;- - 0626 907 270.

Na kwa mafundisho mengine mengi k**a haya muhimu kwa ajiri ya ustawi wako wa kiroho.

Usiache kufuatilia mafundisho haya muhimu kupitia ukrasa huu au jukwaa hili la kiroho la Mwl Ajs Kagulana.

Na uwajulishe na watu wengine wengi kuhusu ukrasa huu wa Mwl Ajs Kagulana kwa Ku-share au kwa kuwatag.

ili wapate mambo haya muhimu kwa ajiri ya ustawi wao pia wa kiroho.

BARIKIWA.

NI NINI KIROHO HUPELEKEA WATU KUANGUKA KWENYE MISIBA HATA K**A HAWANA NASABA NA MISIBA HIYO?.Kuna vitu vingi ambavyo hus...
11/11/2025

NI NINI KIROHO HUPELEKEA WATU KUANGUKA KWENYE MISIBA HATA K**A HAWANA NASABA NA MISIBA HIYO?.

Kuna vitu vingi ambavyo husababisha au hupelekea tatizo hili kutokea kwa watu hasa wanapokuwa misibani.

Na moja kati ya kitu hicho ( cha kiroho ) ambacho hupelekea au huchagiza k**a si kufanya kabisa watu waangukuke kwenye misiba ni " ULIMI WA UPOTOFU "

Na wazo hili unalipata kwenye kitabu hiki cha Mithali 17:20 inayosema,

" Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema; Na mwenye ulimi wa upotofu huanguka katika misiba " ( Mithali 17:20 ).

KUMBUKA;-
Si kila anayeanguka kwenye misiba atakuwa na " ...ulimi wa upotofu... " k**a tulivyosoma kwenye kitabu hiki cha Mithali 17:20.

Ila inawezekana pia akawa hana hizo changamoto zingine nyingi ambazo zinaweza kumpelekea mtu kuanguka msibani.

Isipokuwa hii ya " ulimi wa upotofu " ikiwa tu ameanguka kwenye misiba mingi k**a tulivyoona kwenye kitabu hiki cha Mithali 17:20 inayosema,

" ...mwenye ulimi wa upotofu huanguka katika misiba " ( Mithali 20:17 ).

Na k**a atakuwa na tatizo hili basi atahitaji msaada wa kiroho pia nje ya msaada wa kisayansi au msaada wa kidaktari.

Hili atokane na tatizo hilo la kuanguka kuanguka misibani ili isije ikatokea siku kaanguka.

Akaangukia kitu chenye ncha kali au la na akapoteza maisha kabisa hata tukawa na msiba mwingine.

Au msiba ndani ya msiba Na kwa mawasilano zaidi waweza kuwasiliana nami kwa namba zifuatazo.

- 0789 294 126
What'upp No;- - 0626 907 270

Na kwa mafundisho mengine mengi k**a haya muhimu kabisa kwa ajiri ya ustawi wako wa kiroho.

Usiache kufuatilia mafundisho haya kupitia ukrasa huu wa Mwl Ajs Kagulana na Mungu wa mbinguni atakubariki sana.

huu

Hii ni sehemu ya tatu (3) ya mafundisho yetu haya yanayosema " NJIA BORA ZA KIROHO ZA KUONGEZA SIKU NYINGI ZA KUISHI, AU...
06/11/2025

Hii ni sehemu ya tatu (3) ya mafundisho yetu haya yanayosema " NJIA BORA ZA KIROHO ZA KUONGEZA SIKU NYINGI ZA KUISHI, AU MIEZI AU MIAKA N.K. BILA KUTUMIA GHARAMA KUBWA ".

Njia ya tatu (3) ya kiroho ambayo mtu anaweza kuitumia kwa ajiri ya kuongeza siku zake za kuishi.

Au miaka mbali na kufuata maelekezo ya ki-sayansi au maelekezo ya kidaktari, kumcha Mungu na Kumwomba.

Ni " KUWAHESHIMU WAZAZI WAKO ". Na ieleweke kuwa Wazazi wanaweza kuwa wa ki-mwili au wazazi wa kiroho.

Na wazo hili unalipata kwenye kitabu hiki cha K*toka 20:12 inayosema,

" Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Yesu, Mungu wako " ( K*toka 20:12 ).

KUMBUKA;
Sikuzote kuwa, kuwaheshimu wazazi ni muhimu, Na, ni muhimu kwa sababu kunaongeza siku.

K**a tulivyoona kwenye kitabu hiki cha K*toka sura ya 20:12.

Hivyo hata inapotokea mzazi amekosea ( yeye mwenyewe ) bado anahitaji heshima kutoka kwako k**a mzazi .

Na ikitokea hata k**a amekosea k**a alivyokosea Nuhu kwa kunywa pombe.

Na baada ya kunywa pombe na kulewa akavua nguo ( na kutembea uchi mtaa mzima k**a Nuhu ).

Na ukamkosea au ukaacha kumheshimu au kumpa heshima anayostahili k**a mzazi k**a tulivyoona kwenye kitabu hiki cha K*t 20:12.

Kwenye mazingira k**a hayo ( ya baba kuwa uchi ) bado utapata shida tu! Wewe.

K**a alivyopata Hamu ambaye alikuwa ni mtoto wa tatu wa Nuhu.

Na ukimtendea vyema katika mazingira hayo hayo ya utupu k**a kumstiri kwa mavazi n.k.

Basi utapata baraka au matokeo ambayo Mungu ameyakusudia uyapate Kwenye maisha yako.

Utapata matokeo hayo kwa sababu ukuliacha neno la Mungu la Yakobo 2:14-17 lianguke chini.

Ikiwa ni pamoja na kuishi siku nyingi katika nchi ambayo Yesu Mungu wako amekupa kuishi.

K**a ni Tanzania basi utaishi siku nyingi katika nchi hii ya Tanzania na k**a ni South Africa basi utaishi siku nyingi katika nchi hiyo ya South Africa.

Hata k**a kuna changamoto au machafuko ya hapa na pale bado Mungu atakulinda na hata liacha neno lake lianguke chini.

Na hii haina maana kwamba wanaokufa wakati wa machafuko kuwa hawawaheshimu wazazi wao bali kuna sababu nyingi ambazo hupelekea watu kuifariki dunia.

Ambazo hatuwezi kuzizungumza au kuzitaja zote hapa.

BARIKIWA SANA Na usiache kufuatilia mafundisho haya muhimu kwa ajiri ya ustawi wako wa kiroho kupitia jukwaa hili la facebook lenye jina la Mwl Ajs Kagulana.

Hii ni sehemu ya pili (2) ya mafundisho yetu yanayosema " NJIA BORA ZA KIROHO ZA KUONGEZA SIKU NYINGI ZA KUISHI, AU MIEZ...
06/11/2025

Hii ni sehemu ya pili (2) ya mafundisho yetu yanayosema " NJIA BORA ZA KIROHO ZA KUONGEZA SIKU NYINGI ZA KUISHI, AU MIEZI AU MIAKA N.K. BILA KUTUMIA GHARAMA KUBWA ".

Njia ya pili (2) ya kiroho ambayo mtu anaweza kuitumia kwa ajiri ya kuongeza siku zake za kuishi.

Au miaka ni " KUOMBA KWA MUNGU ". Na wazo hili unalipata kwenye kitabu hiki cha Zab 21:1,4 inayosema,

" ...mfalme...alikuomba uhai, ukampa, Muda mrefu wa siku nyingi... " ( Zab 21:1,4 ).

Hivyo mbali na maelekezo ya ki-Sayansi au maelekezo ya kidaktari, na kumcha Mungu k**a tulivyoona kwenye sehemu ya kwanza ya mafundisho haya.

Ni vizuri pia kwa mtu anayetaka kuishi siku nyingi " kuomba kwa Mungu " k**a alivyofanya mfalme huyu wa hiki kitabu cha Zab 21:1-4.

Ili Mungu ampe maisha marefu au muda mrefu wa siku nyingi k**a tulivyoona kwenye kitabu hiki cha Zab 21:1-4

Na kitabu hiki cha Isaya 38:1-5 ambacho waweza kukisoma kwa uelewa mpana zaidi.

Na usisahau kuwa mfalme nje ya kuwa yeye ndiye head of state na head of the government.

Ana daktari wake pia ambaye analipwa na serikali kwa ajiri ya kazi hiyo.

Yaani kuhakikisha kiongozi yupo imara wakati wote kwa ajiri ya kutekeleza majukumu tofauti tofauti ya kitaifa na ya kimataifa aliyonayo.

Lakini pamoja na hayo yote bado mfalme huyu wa hiki kitabu cha Zab 21:1-4.

Na huyu mfalme Hezekiah wa hiki kitabu cha Isaya 38:1-5 walikwenda kwa Mungu kuomba.

Si kwamba madaktari wao hawakuwa na maana ila walijua kuwa madaktari na maelezo ya kisayansi tu hayatoshi.

Hivyo wanamwitaji Mungu pia ili waishi siku nyingi katika nchi na Mungu akawasaidia k**a tulivyoona.

Hivyo kwa wewe unayetaka kuishi maisha marefu au siku nyingi katika nchi.

Ni muhimu kujua kuwa mbali na kufuata ushauri wa kidaktari au wa ki-sayansi.

Ni vizuri pia kumcha Mungu na kumwomba ili upate matokeo mazuri kwenye maisha yako.

Yatakayokufanya uishi siku nyingi katika nchi k**a huyu mfalme wa hiki kitabu cha Zab 21:1-4.

Na huyu mfalme wa hiki kitabu cha Isaya 38:1-5.

BARIKIWA na usiache kufuatilia mafundisho haya muhimu kwa ajiri ya ustawi wako wa kiroho.

Na kwa msaada zaidi au kwa mawasilano zaidi waweza kuwasiliana nami kwa namba zifuatazo.

- 0789 294 126 au
What'upp No; - 0626 907 270.

NJIA BORA ZA KIROHO ZA KUONGEZA SIKU NYINGI ZA KUISHI, AU MIEZI AU MIAKA N.K. BILA KUTUMIA GHARAMA KUBWAKisayansi kuna n...
06/11/2025

NJIA BORA ZA KIROHO ZA KUONGEZA SIKU NYINGI ZA KUISHI, AU MIEZI AU MIAKA N.K. BILA KUTUMIA GHARAMA KUBWA

Kisayansi kuna namna au mitindo fulani ya maisha ambayo huchagiza au inachangia.

Au inamfanya binadamu aishi maisha marefu au maisha ya siku nyingi katika ulimwengu huu tulionao.

Yaani ulimwengu huu wa damu na nyama k**a kula mlo kamili kulingana na mahitaji ya mwili.

Na kuacha kuvuta au kutumia vitu vyenye kemikali k**a tumbaku, bangi, pombe n.k.

Ila kiroho mbali na mambo hayo tajwa hapo juu ambayo yaliwekwa na Mungu pia ili kuwasaidia watu au kuwafanya watu waishi maisha marefu.

Kuna " KUMCHA MUNGU " Na wazo hili unalipata kwenye kitabu hiki cha Mithali 10:27 inayosema,

" Kumcha Yesu kwaongeza siku za mtu; Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa " ( Mithali 10:27 ).

Hivyo ni muhimu kujua kuwa mbali na kufuata maelekezo ya ki- Sayansi au maelekezo ya kidaktari ni muhimu pia " kumcha Mungu".

Na kitendo cha kushika maelekezo ya Daktari tu! k**a kula mlo kamili, kulingana na mahitaji ya mwili wako.

Na kutokumcha Mungu kwa kufanya mambo yasio haki n.k. K*tapelekea siku zako kupunguzwa.

Na Mungu k**a tulivyoona kwenye kitabu hiki cha Mithali 10:27 na kazi yako yote uliyoifanya ya kuujenga mwili ikawa bure.

Hivyo kwa mtu anayetaka kuishi maisha marefu au maisha ya siku nyingi ni muhimu kujua kuwa .

Katika yote hayo ya Kisayansi au ya Kidaktari kuna Kumcha Mungu pia ambaye tunamwabudu kwa dhamiri safi kabisa.

Usiku na mchana kupitia Kristo Yesu, ambaye kwa kweli ndiye hukamilisha mchakato huu wote wa mtu kuishi siku nyingi katika nchi.

BARIKIWA SANA SANA Mtu wa Mungu na usiache kufuatilia mafundisho haya muhimu kwa ajiri ya ustawi wako wa kiroho.

Na kwa mawasilano zaidi waweza kuwasiliana nami kwa namba zifuatazo

- 0789 294 126
What'upp No; - 0626 907 270.

KUMBUKA;" Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu " ( Mithali 11:14 ).BARIKIWA Na usiache...
05/11/2025

KUMBUKA;
" Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu " ( Mithali 11:14 ).

BARIKIWA
Na usiache kufuatilia mafundisho haya muhimu kwa ajiri ya ustawi wako wa kiroho kupitia kipindi hiki cha and .

Kupitia channel yetu ya EDtv ( Immanuel discipleship).

NI NINI MAONI YAKO KWA KIONGOZ ALIE KUTANGULIA ANAWEZA KUA SABABU YA WEWE KUINUKA AMA KUANGUKA Part 2 [ LIFE AND LIADERSHIP ]

Address

Temeke
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mwl Ajs Kagulana posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share