27/04/2024
ROHO INA NAFASI GANI KATIKA AKILI ZA BINADAMU? SOMA MAKALA YOTE TAFADHALI.
(Nukuu kutoka katika kitabu cha, Kuwa na uwezo mkubwa Kiakili).
Kwa kweli katika mambo ya kusoma na kuchunguza kuhusu uumbaji wa Mungu, kuna mengi ya kujifunza. Kwani hata ukimtafakari tu binadamu jinsi alivyoumbwa huwezi kummaliza kwa mara moja, nadhani itachukua muda mwingi sana kujua jinsi alivyoumbwa na jinsi anavyofanya. Kuhusu roho. Roho ni sehemu moja inayoweza kutawala maamuzi ya mwili iwapo hiyo roho ikishinda vita vya mwili. Mwili una akili zake ambazo ni tofauti na roho. Haya ni kwa mujibu wa maandiko matakatifu.
Wagalatia 5:16.17. Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
Andiko la hapo juu linasema, mwili na roho zimepingana au zinatofautiana maamuzi. Ikiwa na maana kuna matakwa ya roho na matakwa ya mwili.
Katika andiko la Wagalatia 5:16.17 Inataja habari ya kuongozwa na Roho, Ikiwa na maana kuongozwa na Roho wa Mungu. Lakini chakuzingatia hapo ni kwamba Roho au roho, zote zinatabia ya kuongoza. Ikiwa na maana hata roho ya binadamu ina sifa ya kuongoza maamuzi ya mwili, au huulazimisha mwili kufanya ambacho roho ya binadamu imekusudia. Kwa kifanya.
Mara nyingi roho ndio inayotegeneza aina ya mtu. Roho ndio ina picha halisi ya kiumbe kuwa ni cha aina gani. Ili kupata aina ya kitu tunahitaji aina ya roho. Na ili kupata aina ya mtu au watu, tunahitaji aina ya roho. Roho ndio inayotengeneza tofauti ya hiki na hiki. Roho ndio inayotengeneza aina ya vizazi (Kabila)
Mithali 30:11.14. Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao; Wala hawambariki mama yao. Kuna kizazi cha watu walio safi machoni pao wenyewe; Ambao hawakuoshwa uchafu wao. Kuna kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka k**a nini! Na kope zao zimeinuka sana. Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni k**a visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.
Hapo imetaja aina ya vizazi (Binadamu) na tabia zao, sisi binadamu k**a unavyoona mbenu za vitu mbalimbali ambazo hata k**a ni mmea wa aina moja lakini utatofautiana na mwingine kwa kitu fulani au sifa fulani nasi vivyo hivyo. Yesu aliongea kuhusu tabia za kizazi (Roho za kurithi kutoka kwa mababa na mama).
Mathayo 12:34. Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.
Kwa hiyo inaonyesha wazi kuwa kuna tabia nyingine zinatokana na roho za familia au kabila. Yesu amesema tena kuhusu roho za kurithi,
Mathayo 12:39 Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.
Yesu alikitaja kizazi kibaya cha zinaa kinatafuta ishara, Ikiwa na maana ni uzao wenye roho ya uovu, hao hutenda si kwa sababu walifundishwa bali wanatenda kwa sababu ndani yao kuna roho inayowaongoza kutenda uovu hata k**a hawataki. Kuna matendo ndani ya mtu wakati fulani sio maamuzi yake bali ni roho aliyozaliwa nayo ndio inaamua nini afanye au asifanye au awe na tabia gani.
Akili kubadilishwa kwa kuvamiwa na pepo wachafu(roho chafu, shetani).
Kuna ukweli mkubwa kuwa mtu anaweza kubadilishwa akili zake mara tu mtu huyo akivamiwa na mapepo (Majini). Sayansi ya kiroho inathitisha kuwa, pepo anapomuingia mtu, na sehemu muhimu anayoikimbilia ni kwenye akili za mtu.
2 Wakorinto 4:3.4. Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
Andiko hili linasema kuwa mungu (Shetani) wa dunia hii hupofusha watu fikira zao. Ikiwa na maana mtu akiingiwa na roho chafu, ile roho chafu itapofusha fikira au akili za mtu, ili akili zake huyo mtu zisifanye kazi k**a inavyohitajika, badala yake akili za kipepo zianze kufanya kazi kwa kuchukua nafasi ya akili halisi ya binadamu mwenyewe. Yaani akili ya roho chafu ndio inakuwa tabia na muonekano wa yule mtu.
Uthibitisho wa jinsi roho chafu (Mapepo) zinavyobadilisha akili za mtu.
Luka 8:27.35 Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini. Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese. Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana amepagawa naye mara nyingi, hata alilindwa kifungoni na kufungwa minyororo na pingu; akavikata vile vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo. Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia. Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni. Basi, hapo palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilisha mlimani; wakamsi- hi awape ruhusa kuwaingia wale. Akawapa ruhusa. Pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, nalo kundi lilitelemka gengeni kwa kasi, wakaingia ziwani, wakafa maji. Wachungaji walipoona lililotokea walikimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka kwenda kuliona lililotokea, wakamwendea Yesu, wakamwona mtu yule aliyetokwa na pepo ameketi miguuni pa Yesu, amevaa nguo, ana akili zake; wakaogopa.
Kwa mijibu wa andiko la hapo juu, tumeona mtu ambaye alikuwa amechanganyikiwa akili, alikuwa kichaa na alikuwa mtu hatari sana mwenye tabia za ajabu sana, alikuwa uchi alikuwa na nguvu mno. Lakini kwa mujibu wa maandiko, hali hiyo imesababishwa na mapepo yaliyokuwa ndani ya huyo mtu (Sio tu kuwa ndani ya mtu, bali yalikuwa kwenye akili zake kichwani mwake).
Ni wazi kuna matendo au tabia ndani ya binadamu sio za kawaida, bali ni za kipepo. Wakati fulani mtu akili zake zinaweza kuwa sio za kawaida au anakuwa na matendo ya ajabu, lakini hiyo inatupasa kujua kuwa sio akili za kawaida za huyo mtu.
Kuna ukweli mwingi sana kuhusu pepo wabaya kuingilia mfumo wa akili za binadamu na kuutumia k**a atakavyo na muhusika asijue k**a afanyacho sio yeye.
Labda katika mambo ya mitandao kuna watu wajanja wanaweza au wanautaalamu wa kuingilia akaunti ya mtu katika mtandao maarufu kwa Kingereza ni (Hackers), tafsiri yake kwa kingereza ni a person who uses computers to gain unauthorized access to data.)
Aanapoingilia akaunti ya mtu mwingine anaitumia k**a yeye ndiye mwenye akaunti, na mara kadhaa wanaweza kuposti vitu vya ajabu ajabu hata watu wakashangaa baadae ndipo mwenye akaunti atagundua kuna mtu mwingine anaitumia akaunti yake bila ya kujua amefanyaje hadi akaiingilia akaunti hiyo.
Katika ulimwengu wa roho pia kuna uingiliaji wa kihalifu ambao pepo wabaya hufanya kwa ajili ya upotosha watu na kuwavuruga. Nadhani mwanzilishi wa wahalifu wa kimtandao (Hackers) atakuwa ni shetani. Maana shetani yeye ndiye aliye kuwa (Hacker) wa kwanza kwa kuingilia uhusiano wa binadamu na Mungu na kuuharibu. Leo haya k**a marudio ya matendo ambayo shetani aliyafanya na anaendelea kuyafanya.
Katika sayansi hii ya kiroho, shetani anaweza akazini kupitia mtu kwakutumia akili za mtu, anaweza akaiba, anaweza akaua, anaweza akawa kiburi kupitia mtu, anaweza akawa mkatili sana kupitia mtu, anaweza akawa shoga, anaweza akawa mbakaji, anaweza akawa mchawi, anaweza akawa mtumiaji pesa vibaya hata bila ya kuzihurumia, anaweza akawa mlevi mbwa, (Shetani) yeye anakuwa nyuma ya hayo matukio lakini haonekani yeye bali ataonekana yule binadamu anayetumiwa na shetani hata bila ya yeye kujua.
Huduma ya shetani ni uwalimu wa uongo.
Kazi kubwa ya shetani ni kuwa mwalimu mdanganyifu, tangu Edeni alifanya huduma ya kufundisha uongo.
Mwanzo 3:1.7. Hivyo shetani kazi yake nikuwafanya watu wajifunze mambo ya kuwapotosha, au kuwapoteza au kupoteza hata malengo yao mazuri kupitia udanganyifu wa shetani. Kazi ya shetani ni kumshawishi mtu aamue mambo yatakayompoteza.
Roho za kurithi na uhusiano wake kiakili.
Mtu anapozaliwa katika familia fulani yenye roho fulani, mara nyingi yule mtoto atachukua hali (Akili) ya ile roho ya familia. Ikiwa na maana kuwa, ni kitu cha kuzaliwa nacho sio cha kujifunza.
Anaweza akazaliwa na ujuzi, au ujinga, au utambuzi, au hekima, au ukatiri, au roho mbaya, au uongo, au wizi, au uzinzi, au umalaya wa kuzaliwa.
Kuna matendo ya kujifunza na matendo yaliyoumbika ndani ya mtu tangu kuzaliwa kwake. Mtu atazaliwa na kile kinachofanana na familia yake.
Ndio maana kwa mfano mtu akiwa malaya au mzinzi lakini ule uzinzi sio wa kuiga bali ni wa familia, kuacha kwake ni vigumu sana, na anaweza akazini k**a mbwa au akafanya umalaya k**a hajipendi. Hiyo ni wazi huyo sio malaya wa kufundishwa bali ni malaya wa kuzaliwa nao.
Kwa hiyo basi, kuna ukweli mkubwa kuhusu roho za kurithi kutawala akili za kizazi kitakachozaliwa.
Roho ya taifa/nchi (Spirit of nation), mji, kijiji, eneo, mtaa.
Kila taifa lina roho yake inayotenda kazi, na kila mji una roho yake inayotenda kazi, na kila kijiji au eneo au mtaa lazima kuna roho yake inayotenda kazi katika eneo hilo, na ndio inayoamua watu wawe na mtazamo gani au akili gani.
Huwezi ukawa na akili kupita akili ya taifa lako, au mji wako au kijiji chako au mtaa wako. Na iwapo utajaribu kuwa na akili zaidi ya akili ya mahali husika hilo eneo litakuangamiza au utaishi kwa shida sana.
Na ndio maana kuna umuhimu sana wa kiongozi wa juu awe na roho na akili sahihi, ili nchi iwe na akili kubwa. Niliwahi kwenda taifa fulani, nikagundua kuwa hilo taifa lina roho ya uzinzi sana, nilishawahi kwenda mahali fulani nikagundua hilo eneo kuna roho ya ulevi. Ikiwa na maana k**a utaishi eneo hilo (K**a huna nguvu ya Mungu au neema ya Mungu) nguvu ya ulevi au uzinzi au ujinga itakuvuta uwe sawa na lile eneo.
Jinsi ya kutoka.
1. Njia ya kutoka ni kuzaliwa mara ya pili (Kuokoka), kwa kumuamini Yesu kristo k**a Bwana na mwokozi wa maisha yako, yeye ana uwezo wa kuwafanya wale waliomuamini kuwa watoto wa Mungu.
Yohana 1:12.13 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, kwa Mungu.
Yohana 3:3.7 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
Biblia inapotaja umuhimu wa kuzaliwa upya(mara ya pili) bila shaka, ina maanisha imetambua kuwa bila ya mtu kubadili aina ya uzaliwa, au kizazi, au roho ya familia ni vigumu kumpende- za Mungu. Au imebaini kuwa asili ya kuzaliwa ni tatizo kubwa katika mtazamo wa binadamu. Bila shaka mtu hawezi kujitoa alipokwama kabla ya kujitoa kwenye tope la kale(asili)
2. Kujifunza kuhusu ukweli huu kuhusu roho zinavyoweza kumiliki akili, na kuweka mpango mkakati wa kuzikataa, na kutafuta mabadiliko.
3. Maombi. Wakati fulani ni vigumu kujitoa katika nguvu za roho za asili yoyote, iwe kuzaliwa, ukoo, au kabila, au taifa pasipo maombi ya kuvunja hizo roho za asili.
4. Maombi kwa ajili ya kuivunja roho ya taifa. 2. Nyakati 7:14
2 Timoseo 2:2.
Kuagiza kitabu au manunuzi ya jumla na rejareja wasiliana nasi kwa 0717528272 /0788170367 / 0755528965.