Jesus Cares Church Tanzania

Jesus Cares Church Tanzania Touching Lives Transforming Communities

KARIBU JESUS CARES CHURCH.Karibu kwenye makusanyiko yetu, mahali tunapokusanyika kumwabudu Mungu, kujifunza Neno la kwel...
07/09/2026

KARIBU JESUS CARES CHURCH.

Karibu kwenye makusanyiko yetu, mahali tunapokusanyika kumwabudu Mungu, kujifunza Neno la kweli na kujengwa katika Kristo.

Kila Juma Pili
JCC Midizini

Saa 1:30 Asubuhi — Kusanyiko la Kwanza (Kiingereza)

Saa 3:00 Asubuhi — Bible Study

Saa 4:00 Asubuhi — Kusanyiko la Pili (Kiswahili)

Karibu sana Njoo na rafiki yako. Tunakungojea kwa furaha.

05/09/2026

Ushuhuda wa huduma ya matibabu bila malipo inayoendelea Hapa Jesus Cares Church.

Bado hujachelewa, huduma inaendelea karibu na wewe pia upate huduma kwa ajili ya afya yako.
Yesu anajali afya yako

05/09/2026

Hii ilikuwa siku ya kwanza (Jana) ya zoezi la utoaji wa huduma za matibabu na elimu ya afya bila malipo, Zoezi hili linaendelea tena leo katika viwanja vya kanisa hapa makao makuu ya JESUS CARES CHURCH (JCC) - Midizini, barabara ya Wazo-Madale.

Yesu anajali kuhusu afya yako na jambo kubwa zaidi Yesu anajali kuhusu hatima ya roho yako.
Karibu tena leo uhudumiwe kimwili na kiroho.

Zoezi la utoaji wa huduma za matibabu na elimu ya afya bila malipo linaendelea katika viwanja vya kanisa hapa makao maku...
04/09/2026

Zoezi la utoaji wa huduma za matibabu na elimu ya afya bila malipo linaendelea katika viwanja vya kanisa hapa makao makuu ya JESUS CARES CHURCH (JCC) - Midizini, barabara ya Wazo-Madale.

Yesu anajali kuhusu afya yako na jambo kubwa zaidi Yesu anajali kuhusu hatima ya roho yako.
Karibu uhudumiwe kimwili na kiroho.

03/09/2026

*NI BURE! NI BUREE! NI BUREEE! *

Tunawaletea GOSPEL MEDICAL MISSION 

 Tarehe 4–5
Karibuni wote kupata huduma mbalimbali BURE kabisa

Huduma zitakazotolewa:
 Kumwona Daktari, vipimo na dawa
 Ushauri wa afya na kisaikolojia
 Ushauri wa kiroho
 Elimu ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukizwa yanayotokana na mtindo wa maisha na lishe
 Madaktari bingwa wa macho watakuwepo
Madaktari bingwa wa meno watakuwepo

HUDUMA ZOTE NI BURE

Usikose. Mlete ndugu, rafiki na jirani yako.

02/09/2026

Mambo mengine hayatoki kwa kulalamika au kutumia akili za kibinadamu bali yanatoka kwa MAOMBI.

​Walipowaweka Paulo na Sila gerezani, hawakukata tamaa. Walipoomba usiku wa manane, misingi ya gereza ilitikisika na milango ikafunguka.

​Hauwezi kutoka kwenye hiyo changamoto k**a hutaki kuomba. Amsha maisha na nguvu ya maombi ndani yako leo.

01/09/2026

Kuna nyakati katika safari ya wokovu ambapo mambo huwa magumu, majaribu huongezeka na moyo unaweza kuchoka. Lakini katika nyakati hizo, usikimbie kutoka kwa Mungu kimbilia katika maombi.

Maombi ndiyo mahali tunapopata nguvu mpya, tunapotiwa moyo, tunapata hekima ya kuendelea na kujengwa upya ndani yetu. Kuna vita ambavyo hatuvishindi kwa nguvu zetu, bali kwa kukaa mbele za Mungu katika maombi.

*Usiache kuomba *

01/09/2026

Men with Mission Day 2026 Recap

Lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana (Yoshua 24: 15)

Kukusanyika pamoja ni sehemu muhimu ya maisha yetu ya imani. Tunapokutana, tunapata nafasi ya kumwabudu Mungu pamoja, ku...
31/08/2026

Kukusanyika pamoja ni sehemu muhimu ya maisha yetu ya imani. Tunapokutana, tunapata nafasi ya kumwabudu Mungu pamoja, kusikia Neno, kujengana na kutiana moyo katika safari yetu ya kumfuata Kristo.

Jana tulikutana tena k**a waamini na kufurahia ushirika pamoja, huku tukisherehekea kwa namna ya pekee Sikukuu ya Wanaume tukimshukuru Mungu kwa wanaume wanaosimama katika familia, kanisa na jamii, na kuwaombea waendelee kukua katika Kristo na kutimiza nafasi yao kwa uaminifu.

Kuna furaha katika kuwa pamoja. Kuna nguvu katika kukusanyika. Kuna baraka katika kusimama pamoja k**a familia ya Mungu.

Karibu sana kwenye sikukuu ya Wanaume (JCC) siku ya kesho hapa kanisani Jesus Cares.Karibu tumsifu Mungu Pamoja, tujifun...
29/08/2026

Karibu sana kwenye sikukuu ya Wanaume (JCC) siku ya kesho hapa kanisani Jesus Cares.

Karibu tumsifu Mungu Pamoja, tujifunze pamoja na tuwe na ushirika k**a familia ya Kristo
Mwalike ndugu, jamaa na rafiki yako tufurah pamoja

Men With Mission Day 2026🔥🔥

Address

Midizini, Mivumoni (Barabara Ya Wazo-madale)
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jesus Cares Church Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Jesus Cares Church Tanzania:

Shortcuts

Share