Kwaya ya Mt. Sesilia - Mavurunza

Kwaya ya Mt. Sesilia - Mavurunza Huu ni ukurasa rasmi wa Kwaya ya Mt. Sesilia (inayohudumu ibada ya misa ya 3 kila jumapili) katika k

02/10/2022

Tumsifu Yesu Kristo ndugu mpendwa, ninakukaribisha kwa moyo mkunjufu kutembelea kurasa zetu za kwaya katika mitandao mbalimbali ya kijamii k**a Youtube na Facebook ili uweze kupata taarifa mbalimbali za kwaya yetu na matukio mbalimbali ya uinjilishaji.
Sanjari na hilo ningependa kukuomba ewe rafiki wa kwaya yetu kuungana kwa pamoja na kwaya yetu katika safari yake ya Hija kuelekea MWANZA mwezi huu wa OCTOBER kwa kadiri utakavyoweza kujaaliwa.
Hija hii niya muhimu sana kwa kwaya na tungependa tuungane sote kwa hali na mali tusafiri pamoja ili kutimiza lengo la safari yetu ya kiimani. Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwenu kwa sala na kwa namna yoyote ile mtakavyoweza kujaaliwa.
Mwenyezi Mungu na awabariki

Tumsifu Yesu Kristo!Karibu utazame video ya wimbo wetu unaojulikana kwa Jina la "Lakini Wewe Bwana" utunzi wake Mwl. Ven...
05/07/2020

Tumsifu Yesu Kristo!

Karibu utazame video ya wimbo wetu unaojulikana kwa Jina la "Lakini Wewe Bwana" utunzi wake Mwl. Venant Mabula, unapatikana kwenye album yetu mpya inayoitwa SIFA NA ENZI.

Note: Ili kujipatia album hii, tupigie kupitia namba zilizopo kwenye kasha la album k**a linavyoonekana kwenye profile.

Usisahau ku LIKE, COMMENT & SUBSCRIBE Channel yetu.

Kwaya: Mtakatifu Sesilia. Parokia: Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili - Mavurunza. Wimbo: Lakini Wewe Bwana Mtunzi: Venant Mabula Album: Sifa na Enzi Mche...

Tumsifu Yesu Kristo!Karibu utazame wimbo huu unaoitwa "MIMI NA YESU ulioimbwa na Kwaya ya Mt. Sesilia -  Mavurunza" na u...
15/06/2020

Tumsifu Yesu Kristo!

Karibu utazame wimbo huu unaoitwa "MIMI NA YESU ulioimbwa na Kwaya ya Mt. Sesilia - Mavurunza" na unapatikana kwenye Albu yetu mpya inayoitwa "SIFA NA ENZI".

Usisahau ku Like, Comment, Subscribe & Share.

Mwenyezi Mungu akubariki sana🙏🏾

Kwaya: Mtakatifu Sesilia. Parokia: Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili - Mavurunza. Wimbo: Mimi na Yesu Mtunzi: Peter Mboye Album: Sifa na Enzi. ...

Tumwimbie Bwana....!Karibu utazame video ya wimbo mmojawapo uliomo kwenye album yetu mpya inayoitwa SIFA NA ENZI.NB: Usi...
08/06/2020

Tumwimbie Bwana....!

Karibu utazame video ya wimbo mmojawapo uliomo kwenye album yetu mpya inayoitwa SIFA NA ENZI.

NB: Usisahau ku Like, Comment, Subscribe & Share.

Kwaya: Mtakatifu Sesilia. Parokia: Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili - Mavurunza. Wimbo: Mungu Wetu Astahili Kusfiwa. Mtunzi: David B. Wasonga. Mcheza Ki...

29/05/2020

MTAKATIFU GERMANO WA PARIS-ASKOFU(496-576).

Germano alizaliwa katika nchi ya Ufaransa, mwaka 496. Askofu wake alipoona ni mtoto mtii na mwenye bidii kwa mambo ya imani, alitambua kuwa ni mteule wa Mungu. Alimwuliza k**a angependa kuwa Padre. Kijana Germano akajibu kuwa, hiyo ndiyo hamu ya moyo wake. Basi, Germano akaingia Seminari, na baada ya kuhitimu majiundo Kasisi, mwaka 530, akapewa daraja Takatifu ya Upadre. Baada ya muda mfupi, akawa Abate wa Monasteri ya Mt. Simforiani.
Padre Germano aliishi maisha magumu ya kujinyima na kujitesa, akafanikiwa kuwarudisha wadhambi wengi katika kundi.
Sifa take ilianza kuvuma kuwa ni mtu wa fadhila kuu, mwenye huruma na mapendo kwa masikini na wagonjwa. Aidha, Mungu alimjalia karama nyingi. Habari zake zikaenea hadi mjini Paris huko Ufaransa, mji alipoishi Mfalme wa nchi, aitwaye Shildebert.
Askofu Eisebius wa Paris alipoiaga dunia, Mfalme Shildebert pamoja na watu wa mji mzima wa Paris, walimtaka Padre Germano awe Askofu wao mpya. Basi, Germano akapewa daraja ya Uaskofu wa Paris. Lakini aliendelea aliendelea na maisha yake ya kujishusha na unyofu wa moyo. Nyumba yake daima ilijaa masikini na wagonjwa. Alikula chakula na masikini kila siku. Hakuacha mazoea yake magumu ya kuutumikisha mwili wake. Mchana kutwa aliutumia kwa kazi zake k**a Askofu, na usiku aliutumia katika kusali.
Askofu Germano akiwaona masikini njiani, aliwaleta nyumbani kwake na kula nao chakula. Siku za kuhubiri neno la Mungu Kanisani, alionesha ujasiri wake wa kunena kwa ufasaha, huku akipinga upuuzi wa dunia, dhuluma na dhambi zote. Aliwaongoa watu wengi, hata viongozi wa watu waliigeuza mienendo yao mibaya, wakafuata ushauri wake. Mfalme mwenyewe aliguswa sana na maisha ya Askofu Germano, hata naye akayaiga.
Siku moja, Mfalme Shildebert alimpa fadha nyingi Askofu Germano ili awagawie masikini. Askofu Germano alipokwisha kuwagawia masikini, akazihesabu na kuona zimebaki nusu. Alienda nazo kwa Mfalme ili amrudishie, akisema, "Leo sikuwapata masikini wengi, hivyo, hapa ninakurishia fedha zilizobaki". Mfalme akamjibu:"Hasha, sitatwaa fedha nilizokwishazitoa. Ziweke hadi utakapopata nafasi ya kuzitumia; na k**a hazitatosha nitatoa zingine, wala sitachoka kutoa". Mfalme akamwita wake, akamwambia achukue vyombo vya fedha na dhahabu na mikufu ya thamani, ampelekee Askofu Germano.
Watu wa Paris na wa miji iliyoko kando kando yake, walimwona Germano k**a baba yao; na ni kweli alikuwa zaidi ya baba na mama kwao. Mwenyezi Mungu alimpa hekima na uwezo wa kuwaongoza na kuwafaa watu. Vifaa vyake vilikuwa na nguvu ya pekee. Watu walikuwa wakivichukua kwa imani: nyasi za kitandani mwake, nyuzi za vitambaa vya kanzu yake, au nyaraka alizoziandika, ili wapate kuwaponya maradhi yao.
Mwenyezi Mungu alimjalia kipawa cha kutenda miujiza. Alipotoka nje akisha kusali Kanisani, wagonjwa na walemavu mbali mbali walimngoja njiani wakiwa wamejipanga mistari miwili, ili apate kupita kati yao na kuwawekea mikono vichwani mwao, wapate kupona. Mfalme Shildebert alipougua na madaktari wake kushindwa kumtibu, Germano alimwombea na kumwekea mikono na kumponya. Mfalme Germano aliongoka kabisa kwa sala zake na akaanzisha Taasisi nyingi za kidini na kupeleka fedha nyingi kwa Askofu Germano kwa ajili ya masikini.
Askofu alipokuwa na umri wa miaka 80, alitambua siku ya kuiaga dunia imekaribia. Hivyo aliandika katika jalada na akalitundika juu ya kitanda chake, ili apate kuliona kila siku, asije akasahau kujiandaa.
Askofu Germano aliiaga dunia mwaka 576, terehe 28 Mei.
Mtakatifu Germano wa Paris, Askofu, utuombee kwa Mungu ili imani yetu iendane na matendo yetu. Amina.

Tuzidi kuomba huruma ya Mwenyezi Mungu ili atuepushe na kutukinga dhidi ya janga hili la virusi vya Corona (COVID-19)
23/04/2020

Tuzidi kuomba huruma ya Mwenyezi Mungu ili atuepushe na kutukinga dhidi ya janga hili la virusi vya Corona (COVID-19)

Wimbo: Yesu njoo utuokoe' Kwaya: Mt. Sesilia Mavurunza. Album: Nimefungua vitabu vyote.

Askofu mkuu Novatus Rugambwa, ateuliwa kuwa Balozi huko Samoa!Askofu mkuu Novatus Rugambwa alizaliwa tarehe 8 Oktoba 195...
19/04/2020

Askofu mkuu Novatus Rugambwa, ateuliwa kuwa Balozi huko Samoa!

Askofu mkuu Novatus Rugambwa alizaliwa tarehe 8 Oktoba 1957 Jimbo Katoliki la Bukoba nchini Tanzania. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 6 Julai 1986. Akajiunga na utume wa kidiplomasia mjini Vatican hapo tarehe 1 Julai 1991. Tarehe 6 Februari, 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, akamteuwa na kuwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu hapo tarehe 18 Machi 2010.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu mkuu Novatus Rugambwa kuwa Balozi mpya wa Vatican kwenye Kisiwa cha Samoa. Ataendelea pia kuwa Balozi wa Vatican kwenye Visiwa vya Marshall, Kiribati, Nauru na Tonga. Ataendelea pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini New Zealand, Fiji, Palau na Mwakilishi wa Kitume kwenye Bahari ya Pacific. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Novatus Rugambwa alizaliwa tarehe 8 Oktoba 1957, Katika Jimbo Katoliki la Bukoba nchini Tanzania. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre mikononi mwa Askofu Nestorius Timanywa kunako tarehe 6 Julai 1986. Akajiunga na utume wa kidiplomasia mjini Vatican hapo tarehe 1 Julai 1991.
Baada ya kufanya kazi mbali mbali katika Balozi za Vatican, kunako tarehe 28 Juni 2007 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa XVI akamteuwa kuwa Katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la shughuli za kichungaji kwa ajili ya wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi maalum. Ilikuwa ni tarehe 6 Februari, 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, akamteuwa kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Angola, Sao Tome na Principe na kuwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu na Kardinali Tarcisio Bertone, aliyekuwa Katibu mkuu wa Vatican kwa wakati ule hapo tarehe 18 Machi 2010. Na tarehe 5 Machi 2015 akateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Honduras. Na kunako tarehe 29 Machi 2019, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican huko New Zealand na mwakilishi wa kitume kwenye visiwa vya Bahari ya Pacific. Tarehe 17 Aprili 2020 amemteuwa kuwa Balozi wa Vatican kwenye Kisiwa cha Samoa. https://www.vaticannews.va/sw/vatican-city/news/2020-04/askofu-mkuu-novatus-rugambwa-balozi-kisiwa-samoa.html

MASOMO YA MISA - APRILI 19, 2020.DOMINIKA YA 2 YA PASAKA, MWAKA AWIMBO WA MWANZO: 1Pet 2:2K**a watoto wachanga waliozali...
19/04/2020

MASOMO YA MISA - APRILI 19, 2020.
DOMINIKA YA 2 YA PASAKA, MWAKA A

WIMBO WA MWANZO:
1Pet 2:2

K**a watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu, aleluya.

SOMO 1
Mdo 2:42 – 47

Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume.
Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote k**a kila mtu alivyokuwa na haja.
Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, walimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 11:2 – 4, 13 – 15, 22 – 24 (K) 1

(K) Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele.

Israeli na aseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
Mlango wa Haruni na waseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele. (K)

Ulinisukuma sana ili nianguke;
Lakini Bwana akanisaidia.
Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu,
Naye amekuwa wokovu wangu.
Sauti ya furaha na wokovu
Imo hemani mwao wenye haki. (K)

Jiwe walilolikataa waashi
Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Neno hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni ajabu machoni petu.
Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana,
Tutaishangilia na kuifurahia. (K)

SOMO 2
1 Pet. 3 – 9

Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu; tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu. Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya Imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.
Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; ili kwamba kujaribiwa kwa Imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufufunuliwa kwake Yesu Kristo. Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu, katika kuupokea mwisho wa Imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO
Yn. 20:29

Aleluya, aleluya,
Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadfiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.
Aleluya.

INJILI
Yn. 20:19 – 31

Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana.

Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; k**a Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.

Walakini mmoja wa wale Thenashara, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu. Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo.

Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati akasema, Amani iwe kwenu. Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kole chako, uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu; wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye. Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.

Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa; ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini na uzima kwa jina lake.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Tamko Rasmi Kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).  kuomba huruma yake Mwenyezi Mungu atukinge na kutokomeza...
17/04/2020

Tamko Rasmi Kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

kuomba huruma yake Mwenyezi Mungu atukinge na kutokomeza kabisa virusi vya Corona (Covid-19).

14/04/2020

Kristo Amefufuka, Aleluya Aleluya!




📀
🔥🔥🔥

Address

Parokia Ya Mavurunza, Jimbo Kuu Katoliki La Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kwaya ya Mt. Sesilia - Mavurunza posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Kwaya ya Mt. Sesilia - Mavurunza:

Share