Tanzania Adventist Media Channels

Tanzania Adventist Media Channels (Tanzania Adventist Media Channels)Ni Taasisi ya Vyombo vya Habari... Inayomilikiwa na Kanisa la Wa Adventista Wasabato Tanzania.

Sabato Njema, Kwako na Familia Yako.
24/03/2023

Sabato Njema, Kwako na Familia Yako.

   with    SADAKA MAALUM🙏🏾|Sabato hii ya tarehe 11/3/2023, ni sabato maalum ya kutegemeza mpango mkubwa wa upanuaji wa h...
11/03/2023

with

SADAKA MAALUM🙏🏾|
Sabato hii ya tarehe 11/3/2023, ni sabato maalum ya kutegemeza mpango mkubwa wa upanuaji wa huduma za radio zetu za Rock FM, Morning Star Radio na Adventist World Radio (AWR).

Shiriki mbaraka huu kwa kutoa sadaka yako kuwa mbaraka kwa wengi. Waweza kuiwasilisha sadaka kwa mhazini wa kanisa mahalia au kupitia TigoPesa LipaNamba (6025197) jina ni Tanzania Adventist Media Channels au CRDB A/C 0150452883000. Mungu akubariki sana🙏🏾.


Yesu Anakuja! JIHUSISHE
📍Mbeya Mjini SDA

  MFIKIE MTOTO UUFIKIE ULIMWENGUby Bulengela AncoBMkutano wa Idara ya Huduma za Watoto ulioandaliwa  kwa ushirikiano wa ...
27/06/2018



MFIKIE MTOTO UUFIKIE ULIMWENGU
by Bulengela AncoB

Mkutano wa Idara ya Huduma za Watoto ulioandaliwa kwa ushirikiano wa Majimbo makuu yote mawili, umehitimishwa tarehe 26 June 2018, ambapo wajumbe zaidi ya 170 wamepatiwa mafunzo ya Malezi ya Watoto, Kuendesha masomo ya Kiungo Cha Neema, ufundishaji ulio hai, kukuza imani, kuwahusisha Watoto katika kujifunza, ni baadhi tu ya Masomo. Tutarajie maboresho na ufanisi toka kwa waalimu hawa.

Baadhi ya sentensi makini;

"Watoto wenye umri wa Miaka 12 wanapoonyesha wamekuwa wakristo na kutaka kubatizwa wasizuiwe, wabatizwe endelea kuwafundisha, ukiwazuia wakagairi itakuwa ngumu kuwarejesha tena" Mr. Yusto E. Mwano- (NTUC)

"Tuwalinde Watoto wetu wasisikilize, kutazama na kujaribisha kila kitu kisicho katika wakati sahihi na Wala kwenda sehemu za starehe"; WAVULANA sikia "usichongechonge penseli yako itaisha kabla ya mtihani"; WASICHANA sikia usifungue soda yako asubuhi gesi itaisha kabla ya sherehe, maana sherehe ni jioni" Pr. Eli Mchome

"Na tukomeshe unyanyasaji kwa Watoto wetu katika Mambo ya kiroho, tuwapatie viti wasikae chini, tusiwape wadogo zao kuwabeba/kuwalea darasani, wapewe mazingira Bora na zana za kujifunzia; Darasa liwe angalau watoto watatu. Tuwalinde" Mrs Hodia Mtani - mkurugenzi Jimbo dogo la kusini mwa Tanzania (SHC)

"Na tuwekeze kwa Watoto sasa maana wakati fulani hatutakuwepo; wao ndio watalitegemeza Kanisa la Mungu" Pr. Mariam Samo - Mkurugenzi Jimbo kuu la kaskazini mwa Tanzania NTUC

"Wengine wameonekana kukimbizana na Watoto wao ili kuwaadhibu; Usimkimbize mtoto K**a kuku, ili kumwadhibu, umitaka kumk**ata kuku dondosha mahindi msululu Hadi kwenye Banda k**ata Chinja. Sikia msubiri mtoto atakuja kwenye Banda/nyumbani ndipo shughulika naye", Ndege ni wako manati ya nini?" Mrs. Devota Shimbe - Mkurugenzi Jimbo dogo Mashariki na Kati (ECT)

Kuwafundisha kwa jinsi iliyohai kutawafanya Watoto kuelewa haraka na kuuhisi upendo wa Mungu kwao. Mrs Neema Erasto M. Mkurugenzi Jimbo dogo la Kusini Mashariki mwa Tanzania (SEC).

Ni Busara kutambua utofauti si wa umri tu Bali tukitambua tofauti ya Kizazi na Kizazi, itasaidia kuleta mlingano wa urithishaji wa elimu, ujuzi na ufahamu. Mrs. Ruth Eyembe - Mkurugenzi Jimbo kuu la Kusini mwa Tanzania (STUM)

Pongezi Vongozi wa Majimbo Makuu ni Miriam Shamo (NTUC) na Mrs. Dr. Ruth Eyembe (STUM)

  "MFIKIE MTOTO UUFIKIE ULIMWENGUHizi mada ni makini kwa ajili ya ulezi wa watoto, kuelewa program ya  "Kiungo cha Neema...
21/06/2018



"MFIKIE MTOTO UUFIKIE ULIMWENGU

Hizi mada ni makini kwa ajili ya ulezi wa watoto, kuelewa program ya "Kiungo cha Neema" (Y. Mwamo); "Kuwalinda watoto Dhidi ya Unyanyasaji" (Mrs Hodia Mutani); kutambua makuzi ya watoto (Mrs. Devota Shimbe). Hiki ni kionjo toka katika mkutano wa Idara ya Huduma za watoto Unioni ya kaskazini na Kusini mwa Tanzania. Mkutano huu katika kanisa la Unyanhae Singida umeanza leo tarehe 21 - 26 June 2018.

Tanzania Adventist Media Channels (TAMC) imepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mchungaji Msafiri Yohana kilichotok...
19/06/2018

Tanzania Adventist Media Channels (TAMC) imepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mchungaji Msafiri Yohana kilichotokea tarehe 15 June, 2018.

TAMC inakumbuka mchango wake katika utumishi ndani ya Kanisa la Waadventista wa Sabato pamoja na maneno yake ya mwisho aliyozungumza na wasikilizaji wa Morning Star Radio mwezi march 2018; *" Zamu yetu ya Utumishi imekwisha, kuishi zaidi ya miaka 88 ni zawadi na rehema toka kwa Mungu, tunajua tutalala mioyoni mwetu tunalo tumaini lililo kuu ".* (Tazama video fupi akiimba)

Pr. Msafiri Yohana amelitumikia kanisani k**a Mwalimu, Mchungaji wa mtaa, mkurugenzi katika ngazi ya Field kisha kustaafu akiwa mwenyekiti wa iliyokuwa Field ya Magharibi mwa Tanzania (sasa ni West Tanzania Conference).

Tunatoa pole na kuomba faraja za Roho Mtakatifu ziwe kwa familia, ndugu, jamaa na kanisa katika kipindi hiki cha maombolezo.

Tunasubiri kwa shauku asubuhi ya ufufuo kwa kuyaenzi mambo mema aliyoyafanya katika siku za uhai na utumishi wake.

Imetolewa na Mkurugenzi TANZANIA ADVENTIST MEDIA CHANNELS

https://youtu.be/NGCveiL68OM

https://youtu.be/u2PbMtVYpzY

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Adventist Media Channels posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Tanzania Adventist Media Channels:

Share