25/08/2020
UTUKUFU MPAKA AIBU (HOSEA 4:7)
~ Maisha ya mwanadamu akiwa duniani yamejawa na mahitaji mengi sana.
~ Mahitaji mengi ya mwanadamu ni kwa ajili ya kuridhisha matamaniyo ya moyo.
~ Moyo ukisharidhika unatabia ya kujisahau/kujidanganya. Yeremia 17:9
~ Mahitaji ya mwanadamu hupelekwa mbele za Mungu k**a maombi.
~ Wapo watu wanamuomba Mungu cheo, nafasi, pesa, kampuni, ndoa, nyumba, heshima n.k.
~ Kuna wakati Mungu hatupi tumuombayo, sawa sawa na maombi yetu, kwa sababu tunaomba vibaya. Yakobo 4:3
~ Kuna wakati Mungu anatupa, yale tunayoyaomba sawa sawa na maombi yetu, kwa ajili ya UTUKUFU wake. Waefeso 3:20
~ Lakini baada ya kupata tunayoyahitaji, baada ya kupata majibu ya maombi yetu, badala ya kumpa Mungu utukufu tunajisahau na kujitwalia wenyewe utukufu. Tunakuwa wajuaji, viburi, kisilani n.k Luka 12:16-19
~ Lakini hicho kinachokufanya ujitwalie utukufu, Mungu anao uwezo wa kukibadilisha na kuwa aibu mara moja. Luka 12:20 & Hosea 4:7
>>> Tumefanya au tulifanya au tunafanya neema ya Mungu ni kubwa kuliko makosa yetu.
>>> Mungu anatutaka tumrudie na kutubu na atatubariki tena kwa utukufu wake. Matendo 3:19
MWISHO WA UTUKUFU WA MWANADAMU NI AIBU
Mtumishi William Michael,
Cornerstone Bible Baptist Church,
Kigamboni, Kisiwani,
Karibuni.