Mwalimu Yona Ministry

Mwalimu Yona Ministry kristo Yesu asema" hubirini kuwa ufalme wa mbingun i umekaribia"

lengo la page hii ni kutaka kujua ile kweli nayo ituweke huru Yesu aliangiza kuwa mnapo hubiri injili na mseme kuwa ufalme wa Mungu umekaribia na si kuhusu mali,utajiri, upako.n.k...amen

30/05/2025
Nguvu za Mungu ni kubwa na kuu kuliko nguvu za viumbe vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.Uweza wa Mungu haufananishw...
30/05/2025

Nguvu za Mungu ni kubwa na kuu kuliko nguvu za viumbe vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
Uweza wa Mungu haufananishwi na jambo lolote lile,

Mamlaka ya Mungu ni kuu kuliko zote, kila mamlaka inatii mbele za Mungu. Na mamlaka hizo zote zinatii mbele za Yesu.
"Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani." (Mathayo 28:18)

Ndiyo maana tukilitaja jina la Yesu ufalme wa shetani unatii na kituacha huru.
Tukilitaja jina la Yesu maombi yetu yanajibiwa kwa kwa ukamilifu bila kikwazo chochote,
"Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya." (Yohana 14:13-14)

Mungu anachotaka ni mtu kumwamini tu bila kuwa na shaka yoyote ile.
K**a watu wote wangemwamini Mungu kwa moyo wote bila kusita sita, hakika wasingehangaika na vitu vya ajabu ambavyo havina msaada wa kiroho, ambavyo ndani yake kuna utapeli wa hali ya juu na kuangamiza roho za watu.

Mungu ni mwenye nguvu, mamlaka na uweza, hakuna linaloshindikana kwake, kila jambo linalowezekana ni Imani tu ndiyo inayotakiwa.
Mungu akubariki sana.

Mwl. Lazaro Zakaria

30/05/2025

*ROHO MTAKATIFU HAWEZI KUKAA PAMOJA NA MAPEPO.*

Palipo Roho Mtakatifu hapawezi kukaa pepo wa aina yoyote ile, ni sawa na giza lisivyoweza kustahimili palipo na nuru.

Palipo Roho Mtakatifu pana Mungu pia, hivyo Mungu hawezi kuchangamana na mapepo kwa wakati mmoja kwa mtu mmoja.

2 Wakorintho 6:16.
" Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; k**a Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu."

Hapana mapatano yoyote kati ya Mungu na mapepo, Hivyo Roho Mtakatifu akiingia kwa mtu ni lazima mapepo yampishe maana yeye ni Mtakatifu hakai pamoja na uchafu, yeye ana nguvu kuliko mapepo kwasababu Yesu na Mungu mwenyewe wanakuwa mahali hapo.

Hivyo basi haiwezekani mtu aliyeokoka akampokea Roho Mtakatifu akaendelea kuwa na mapepo, na maombi yakifanyika kanisani au mahali popote pale akawa anaanguka mapepo.

Ukiona hali hiyo kunakuwa kuna tatizo kwa mtu huyo.
1. Hajampokea Roho Mtakatifu ndani yake, hivyo hana nguvu ya kuzuia mapepo kumwingia.
2. Ana maisha ya mchanganyo ya dhambi yanayotoa nafasi kwa mapepo kumwingia. Hajaamua sawasawa kumwamini Yesu na kuacha dhambi na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.
3. Hajafundishwa kuhusu Roho Mtakatifu, kazi zake na namna ya kumpokea, hivyo anabaki kuwa ni mtu tegemezi kwa wengine.

Mtu akishamwamini Bwana Yesu, akatubu dhambi ni lazima ampokee Roho Mtakatifu na kujazwa nguvu zake kila mara na aishi maisha ya kumpendeza Mungu ili kusiwe na nafasi ya tena ya kuingiwa na mapepo.
Mungu akubariki sana.

Mwl. Lazaro Zakaria

JARIBU LINAPOMPATA MTU, TAMBUA MAMBO YAFUATAYO.1. Siyo kwamba Mungu anakuwa amemwacha, bali anakuwa amezuia majaribu yal...
30/05/2025

JARIBU LINAPOMPATA MTU, TAMBUA MAMBO YAFUATAYO.

1. Siyo kwamba Mungu anakuwa amemwacha, bali anakuwa amezuia majaribu yale ambayo k**a yangempata basi mtu asingebaki salama, bali lingemwangamiza kabasa.

2. Pia Mungu hawezi kuliacha jaribu lidumu kwa muda mrefu bali kuna wakati ukifika, Mungu atamfanyia mlango au namna ya kutoka kwenye jaribu.

3. Endelea kumwamini Mungu kuwa ana uweza mkubwa juu ya kila jambo linalokuja mbele yako. Ukimtumaini atakuvusha, ukimwacha utapotea kabisa.

4. Shetani anaweza kutumia nafasi hiyo kudhoofisha imani yako kwa kukuletea maneno na mawazo mwengi sana kuwa utumie njia zisizo sahihi kulitatua jaribu hilo. Ukimsikiliza anakumaliza kabisa kiroho na hata kimwili pia.

Hivyo ni muhimu kuendelea kuwa na imani kwa Mungu kuwa yupo pamoja na wewe, pamoja na majaribu yote hayo yeye anabaki kuwa Mungu mkuu anayeweza kukuokoa katika hatari yoyote.
Mungu akubariki sana.

Mwl. Lazaro Zakaria

Address

Chukwani
Dar Es Salaam

Telephone

+255711450583

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mwalimu Yona Ministry posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Mwalimu Yona Ministry:

Share